Udhaifu wa Tulia Ackson katika suala la kuchana hotuba ya upinzani - Two Wrongs Don't Make it Right!

MTU mwenyewe ameingizwa bungeni kwa kupitia mlango wa nyuma lazima amuabudu na kumtii aliyempeleka hapo inamaana anatekeleza maagizo toka juu .

Somo kubwa sana. Kumbe kiongozi wa serikali aweza kupandikiza mtu wake bungeni na kuufanya mhimili huo kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kwanza kikatiba wa kuwa sauti ya wananchi na kusimamia serikali kwa niaba ya wananchi. Sasa tumeona kwa macho yetu. Wabunge wote bila kujali vyama vyao wanapaswa kukataa hili ni jambo; vinginevyo hakuna sababu ya kuwa na Bunge. Wabunge wa ccm wanadanganyika kuwa chama chao ndiyo chenye serikali lakini wao wenyewe siyo wawakilishi wa wananchì tena. Badala yake wamekuwa wawakilishi wa serikali. Kadhia ya korosho ni mfano hai.
 
Nimeushangaa sana uamuzi wa Dr, Tulia Ackson kuhusu Mbunge wa CCM kuchana hotuba ya upinzani. Tulia, ambaye ni mwanasheria wa kiwango cha PhD, bila aibu ametetea uamuzi wake kwa kutoa kauli kwamba "Vuma hawezi kupelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Bunge kwa kuwa kipindi cha nyuma mbunge wa Bunda (Chadema) Ester Bulaya aliwahi kurusha vitabu bungeni na kuvichana lakini hakupelekwa katika kamati hiyo"

Hivi kweli, Dr wa sheria, anawezaje kutoa kauli kama hii? Kama uongozi wa Bunge la Tanzania umewahi kutuhumiwa kuwa dhaifu, basi kwa kauli hii ya Tulia nasema Bunge linaongozwa na maspika ambao si tu ni dhaifu, bali pia ni wameamua kwa makusudi kujifanya vipofu na mbumbumbu wa uongozi, ili kulinda maslahi ya chama chao CCM.

Kwa kiingereza ninasema kwamba "Tanzania parliament leaders are excessively biased against the opposition, to the extent that most of the time they forget to be clever or intentionally choose to be stupid". Hii ya Tulia ni typical case. Za Ndugai zipo nyingi sihitaji hata kuzitaja. Za wenyeviti wengine wa vikao vya Bunge kama kina Chenge, Zungu nk zinatia hata aibu kuzitaja.

Tulia anachodai hapa ni kwamba, Bunge linaendeshwa kwa mantiki ya jino kwa jino. Ni sawa na refa wa mpira wa miguu ambaye anainyima penati ya wazi timu moja, na ili kusawazisha kosa lake, anainyima timu pinzani penati ya wazi pia.

Well Dr. Tulia, kauli ya kwamba "two wrongs don't make it right" sio ya kitoto. Wahenga waliiweka ili kuwaelimisha watu kama wewe ambao mnasahau kutumia akili na usomi wenu kwa manufaa yenu binafsi au ya chama chenu. Kama Ester Bulaya wa Chadema alifanya kosa na hakuchukuliwa hatua, hilo lilikuwa ni kosa na udhaifu wa uongozi wa Bunge. Lakini sasa udhaifu huo unazidi kuzidishwa pale ambapo Vuma wa CCM anafanya kosa kama la Ester na unaamua kwamba basi na yeye asichukuliwe hatua kama ilivyokuwa kwa Ester Bulaya.

Huo ni udhaifu mkubwa wa uongozi wa Bunge.
What did you expect from that *P@#&P*!H$U*
 
Ni challenge kubwa sana, na sidhani kama kubadili katiba kutaleta suluhisho. Mara kadhaa tumeona katiba ikivunjwa kwa makusudi na bila aibu. Kitu gani kitazuia hilo kutokea hata ikibadilishwa? Sijui ni jinsi gani ya kumfanya Spika asiwe kibaraka wa chama au raisi
 
Niliweka Post ya "imagine mbunge wa upinzani angechana kitabu cha budget serikali"

Nazani unaweza pata jibu
Ngonja tusubili kipindi hiki cha majadiliano, kama kweli Mbunge wa upinzani hatachana hotuba ya waziri wa Fedha.
 
Ustaarabu wa utawala wa sheria ni mfumo unaopendeza watu wote .Kuhalarisha uvunjaji wa sheria bungeni kwa kisingizio cha bunge mwingine aliishawai kufanya hivyo hakuna kilichofanyika ni hoja isiotakiwa .Ni vyema watu wote waheshimu sheria bila tofauti zetu.Wewe mbunge unapofanya jambo lisilotakiwa wananchi wanakuona kuwa hufai hawatatofautisha kuwa wewe huko chama tawala au la
Na ukweli Bulaya hakuchana vitabu wala, bali aliambiwa aondoke ndani ya Bunge na katika kuondoka kwa hasira akazoa vitabu na vingine vikasambaratika na kuangukia distance. Kwa hiyo ya Ester Bulaya haikuwa ya kuchana vitabu bali alivisambaratisha vikaanguka
 
Mimi nimeshangaa sana yani, hii dharau ya Vuma aisee daaah. Upinzani una hali ngumu sana awamu hii kupita wamu zote... This is not right at all.
Mimi naiona kuwa ni ' blessing in disguise' kwani wanaitangazia dunia aina ya siasa zinazoendeshwa Tanzania. Wacha wazidi kujichafua.
 
Ilitakiwa baada ya kutoa kauli iyo mbunge wa upinzani asimame halafu achane ile bajeti ya serikali wanayo ijadili halafu mambo yaendelee
Wapinzani wangefanya hivyo pande zote wangeonekana ni wapumbavu, wacha rekodi zibaki hivyo hivyo kuonyesha nani ni wapumbavu na nani ni waungwana na wastaarabu.
 
Nimeushangaa sana uamuzi wa Dr, Tulia Ackson kuhusu Mbunge wa CCM kuchana hotuba ya upinzani. Tulia, ambaye ni mwanasheria wa kiwango cha PhD, bila aibu ametetea uamuzi wake kwa kutoa kauli kwamba "Vuma hawezi kupelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Bunge kwa kuwa kipindi cha nyuma mbunge wa Bunda (Chadema) Ester Bulaya aliwahi kurusha vitabu bungeni na kuvichana lakini hakupelekwa katika kamati hiyo"

Hivi kweli, Dr wa sheria, anawezaje kutoa kauli kama hii? Kama uongozi wa Bunge la Tanzania umewahi kutuhumiwa kuwa dhaifu, basi kwa kauli hii ya Tulia nasema Bunge linaongozwa na maspika ambao si tu ni dhaifu, bali pia ni wameamua kwa makusudi kujifanya vipofu na mbumbumbu wa uongozi, ili kulinda maslahi ya chama chao CCM.

Kwa kiingereza ninasema kwamba "Tanzania parliament leaders are excessively biased against the opposition, to the extent that most of the time they forget to be clever or intentionally choose to be stupid". Hii ya Tulia ni typical case. Za Ndugai zipo nyingi sihitaji hata kuzitaja. Za wenyeviti wengine wa vikao vya Bunge kama kina Chenge, Zungu nk zinatia hata aibu kuzitaja.

Tulia anachodai hapa ni kwamba, Bunge linaendeshwa kwa mantiki ya jino kwa jino. Ni sawa na refa wa mpira wa miguu ambaye anainyima penati ya wazi timu moja, na ili kusawazisha kosa lake, anainyima timu pinzani penati ya wazi pia.

Well Dr. Tulia, kauli ya kwamba "two wrongs don't make it right" sio ya kitoto. Wahenga waliiweka ili kuwaelimisha watu kama wewe ambao mnasahau kutumia akili na usomi wenu kwa manufaa yenu binafsi au ya chama chenu. Kama Ester Bulaya wa Chadema alifanya kosa na hakuchukuliwa hatua, hilo lilikuwa ni kosa na udhaifu wa uongozi wa Bunge. Lakini sasa udhaifu huo unazidi kuzidishwa pale ambapo Vuma wa CCM anafanya kosa kama la Ester na unaamua kwamba basi na yeye asichukuliwe hatua kama ilivyokuwa kwa Ester Bulaya.

Huo ni udhaifu mkubwa wa uongozi wa Bunge.
Kwa niaba ya wanyakyusa wote duniani nachukua nafasi hii kuomba radhi sana kwa yanayotendwa na Tulia .

Mutuswege fijo bha tata na bha jubha
 
Mbunge wa CCM Peter Serukamba aliwahi kusema "Fuc.k you" katikati ya mjadala bungeni na hakupelekwa mbele ya kamati.
Tulia hapa anamaanisha ni sahihi kwa mbunge yoyote atakayeamua kutukana bungeni kwa kusema "Fuc.k you" na yataisha tu bila kupelekwa mbele ya kamati
 
Tatizo ni kwamba wapinzani wa nchi hii hawana mbinu za kisiasa.
Walichobaki nacho ni kumponda Magufuli tu kila siku bila kujua kuwa kuna watu wanaponda mema ya nchi hii kwa sababu ya kutaeuliwa kwao na Mh.Rais Magufuli.
Hivi mtu kama Mkuu wa mkoa anayejipatia mahela mpaka anakosa hata wa kumpa na kubaki sasa kugawa magari ,utamwambia nini kuhusu aliyemteua kama sio kutafuta pyuu pyuuu!!

Tulia anasoma upepo na kupima kina cha maji lakini ameona ni kina kifupi na kina mchanga wa kutosha na miamba sio matope hivyo hawezi kuzama .

Wapinzani wana ubinafsi wa kisiasa sana.
Kuna wakati unabaki ukiwashangaa kuwa wanawaza nini kujikwamua na hali ngumu ya kisiasa iliyopo unakosa jibu mana wanabaki kulalamika tu kwenye mitandao.

Wapinzani wafahamu wazi kuwa kwa sasa watu wa kuokoa taiga hili ili liwe na umoja ,upendo,haki na mshikamano ni Viongozi wa dini hasa , Dini zenye mizizi ya imani kama RC ,KKKT ,Anglikana kidogo na Waislam wale wasio chini ya tawi la CCM linaloitwa Bakwata.
Kundi la pili ni la wanasheria wakiwemo Majaji wenye hofu ya Mungu na wanaojua madhara makubwa ya Jaji kupindisha sheria kiimani,kijamii na hata kisiasa.

Mfano mambo kama hayo ni vyema ushshidi ukakusanywa wakaonyeshwa Viongozi wa makundi hayo ili waone wazi kuwa nchi inawasimamia kanuni na sheria wasio waadilifu hata kidogo.

Mtu hawezi kuwa muadilifu kama haogopi sheria. Yani Kwa sasa sheria ni pale mtu anapoamua kumfurahisha bosi wake tu hata kama anamfurahisha kwa kuvunja sheria.

Nimeona mtu mmoja akimtisha mtu kuwa nitakupiga gumi pamoja na kuwa Mimi na mwanamke.
Sasa tujiulize hivi atampiga ngumi kwa sheria gani na ni vipi mtu apigwe ngumi au akwidwe shati adharani na yeye akae kimya tu mana anayempiga ameteuliwa na mkuu kabisa. Hiyo ni hatari sana mana watu wengine ukimdhalilisha anaweza akatoa kisu akakuchoma pale pale na ukawa marehemu bila kujali nini kitamkuta alimradi tu adumishe heshima yake kama mtu mzima kwenye nchi ya kistarabu na kujenga ustarabu wa kesho.

Tulitawaliwa na wazungu kwa sababu walikuja na dharau zao wakitegemea bunduki lakini watu walipozizoea bunduki walizitumia hizo hizo kutafuta Uhuru wao.

Nilifikia mahali nikamkubali sana Ndugai pale alipoamua kupambana na wabunge wakorofi bungeni na akafanikiwa kurejesha heshima ya bunge na akisema mbunge Fulani toka nje mtu anasimama na kutoka mwenyewe . Hili lilikua jambo zuri sana lakini naadae nikagundua kuwa wanaosimamiwa ili watii kanuni ni wapinzani tu lakini CCM wao wanafanya wanavyotaka na hata wakitukana kama Kibajaji wanaongezewa na muda.
Hii inaudhi sana na ikiachwa hivyo iko siku italeta balaa zaidi bungeni. Mana Nadhani kuchana Karatasi iliyoandikwa kwa gharama za walipa Kodi ni kuhujumu uchumi wa nchi. Sio kudharau wapinzani Bali ni kudharau pesa zetu zilizowaweka wote pale.

Hakuna mbunge anayelipwa kwa fedha za chama chake sasa kama tukiamua kuwaacha watumia Chama chao cha CCM ambacho ama kwa uhakika ni chama kisicho na huruma na mtanzania yeyeyote zaidi ya madaraka yao. Ndio maana CCM na serikali kama zilivyokua serikali za kina Sadam Hussein wanakua tayari kutumia majeshi kuwavunja vunja na hata kuwaangamiza wananchi wale wasiowachagua na kuwapa madaraka. Wanajua wapo kwa ajili ya maslahi yao.

Viongozi wa dini wa halali waendelee kusimamia umoja na upendo wa nchi yetu na wasimame kidete kuwaelimisha waumini wao wa kweli ili wakatae vitendo vya kujenga dhulma katika taifa letu ambavyo kwa asili ya mwanadamu ndivyo vinavyovunja amani.
 
Tatizo ni kwamba wapinzani wa nchi hii hawana mbinu za kisiasa. Walichobaki nacho ni kumponda Magufuli tu kila siku bila kujua kuwa kuna watu wanaponda mema ya nchi hii kwa sababu ya kutaeuliwa kwao na Mh.Rais Magufuli. Hivi mtu kama Mkuu wa mkoa anayejipatia mahela mpaka anakosa hata wa kumpa na kubaki sasa kugawa magari ,utamwambia nini kuhusu aliyemteua kama sio kutafuta pyuu pyuuu!!

Mie nadhani tunawalaumu wapinzani isivyostahili. Hakuna nchi ambayo vyama vya upinzani ninashamiri bila kuwa na raisi ambaye ni open minded katika suala la vyama vya upinzani. Angalia kwamba hata USA nchi ambayo ina ukomavu wa kutosha wa kidemokrasia, kuwa na raisi kama Trump ambaye hayuko open minded kuhusu chama cha upinzani cha Democrats inafanya kuwe na mogongano mkubwa kati ya Republicans na Democrats kiasi kwamba Trump anashutumiwa kuigawa nchi.
  • Hitler alifanya hivyo hivyo Ujerumani ya enzi hizo.
  • Kagame Rwanda pia
  • Museveni Uganda naye
  • Sisi wa Misri pia
Unaenda nchi kama Uingereza, Germany, South Afrika, Kenya, Botswana unaona kuwa wamekomaa, wanaelewa maana ya kuwa na vyama vya upinzani bila kuwa na ugomvi navyo usio na tija.

Kwa hiyo la msingi ni kuwa na kiongozi wa nchi mstaarabu ambaye ana burasa, hekima na uelewevu kwamba upinzani katika nchi sio uadui bali unapaswa kuwapo kwa manufaa ya nchi. Hawa wengine, Spika, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Mawaziri, Wabunge ni wafuata upepo tu, wachumia tumbo, uncultured opportunists.
 
Mbunge wa CCM Peter Serukamba aliwahi kusema "Fuc.k you" katikati ya mjadala bungeni na hakupelekwa mbele ya kamati.
Tulia hapa anamaanisha ni sahihi kwa mbunge yoyote atakayeamua kutukana bungeni kwa kusema "Fuc.k you" na yataisha tu bila kupelekwa mbele ya kamati
Mmh, labda siku akiambiwa yeye hivyo ndio atajua ubaya wake, unless anafurahia kusikia mtu akisema hivyo kwa sababu zake binafsi
 
Back
Top Bottom