Sandinistas
JF-Expert Member
- Jul 5, 2013
- 2,609
- 1,771
Ni challenge kubwa sana, na sidhani kama kubadili katiba kutaleta suluhisho. Mara kadhaa tumeona katiba ikivunjwa kwa makusudi na bila aibu. Kitu gani kitazuia hilo kutokea hata ikibadilishwa? Sijui ni jinsi gani ya kumfanya Spika asiwe kibaraka wa chama au raisi
Uko sahihi kabisa ingawa unaonekana kukata tamaa. Haya mambo siyo magumu kiasi hicho. Huko nyuma Waziri Mkuu na mawaziri waliweza kuwajibishwa na Bunge kutokana tu na utashi wa kisiasa na kikatiba. Utashi huo umepotelea wapi? Kimfumo utashi huo upo pale pale; tatizo ni taasisi za kusimamia utashi huo wa kisiasa na kikatiba. Demokrasia ya kweli ni harakati za muda mrefu. Matatizo haya hayawezi kumalizwa siku moja lakini yanaweza kupunguzwa taratibu. Hata vyama vyetu vya siasa vinapaswa kujifunza na kuboresha mifumo yao. Haikubaliki kiongozi wa chama cha siasa kuwa ndiyo chama. Rasimu ya Warioba ilikuwa iwe mwanzo wa safari hii ya demokrasia ingawa maboresho yanayohitajika ni mengi. Rasimu hiyo kwa mfano ilitenganisha serikali na bunge. Hatua hii ingepunguza uwezekano wa kuwa na kiongozi wa bunge anayepokea maelekezo kutoka nje ya Bunge. Kwa kiasi ilipunguza pia madaraka ya mkuu wa serikali. Lakini bado kuna mambo ya kutazama. Ni pamoja na raia kuwekekewa utaratibu wa kikatiba wa kuchukua hatua pale wanapoonekana katiba inavunjwa. Kadhalika kuwa na mgombea huru kutawaondoleaa wabunge adha ya kuwa watumwa wa vyama vya siasa na kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kusimamia serikali.