Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,698
- 4,693
Hapana! Mwanzo wa maeelezo yako ni mbaya! Kenya ilikuwa koloni, Tanganyika haikuwa koloni la waingereza. Hizo ndo hadithi mbaya zisizo na uhalisia. Tanganyika ingewezake kuwa kama Kenya wakati haikuwa koloni?Kuna mzee alinisimulia jinsi Tanganyika ilivyopata Uhuru na kuanisha kuwa Uingereza waliamua kutoa Uhuru mezani baada ya kuona Mtiti uliotokea Kenya.Wazungu waliuawa sana na Mau mau.
Wakaona bora watoe tu bure mana wakiacha Tanganyika nayo ikaanza vita watakosa pa kukimbiia .
Kwatika mazungumzo yake yule Mzee aliweka bayana kuwa kwenye Tawala za kuwatawala watu kuna makundi Matano :-
1.Watawala wanakua ndio kundi lililojiweka Juu kabisa Wakifuatiwa na
2. Wakuu wa majeshi
3.Viongozi wa dini wapo katikakati.
4. Wafanyakazi wanafuata .
5. Wakulima ndilo kundi la mwisho kabisa.
Viongozi wa dini wanawekwa katikati ili kusaidia haya makundi mawawili ya chini yaani ya 4 na 5 yapate faraja kwa kupewa maneno mazuri na ya kuwafanya wawe watiifu na kujipa moyo wa imani .
Majeshi kazi yake ni kuyazuia makundi kuanzia la tatu ,la NNE na la Tano wasilifikie kundi la Kwanza.
Kwa ushawishi wa makundi ya viongozi wa dini ni muhimu sana.
Na pia kuhusu kufanya maovu kwao sio sababu ya kuwatenga na harakati za kuleta haki kwenye jamii.
Ikumbukwe kuwa wengi wa watawala na viongozi wa dini ni wamoja na ndio maana hata Chama tawala kinajitahidi kwa namna yoyote kuwa karibu nao.
Migogoro kwenye makundi ya dini Mara nyingi kuna wanasiasa nyuma mana kama nchi iko stable kwenye Katiba na sheria haliwezekani migogoro ikaibuka kwenye miangoni mwa wananchi.
Mfano Migogoro mingi ya KKKT na Bakwata ni kwa sababu ya Ujanja walioutumia mwanzoni wanasiasa na Watawala wa kuwezesha dini hizo kujitoa kwenye Jumuiya pana za kimataifa na kuanzisha taasisi za ndani ambazo zinakua na migogoro ya madaraka madarakani.
Yote ni kuyafanya makundi ya dini yagawanyike ili wasije wakamulika wanasiasa na kuziona dhambi zao.
Dini ni pamoja na dini za asili ndio maana mpaka leo CCM na serikali yake wanaabudu Mwenge kwa maelekezo ya wazee wa mila na mizimu yao.
Na mwenye umekua na mvuto mkubwa sana kwenye jamii kuliko kitu chochote.
Hebu fikiri kama Mwalimu angedharau Maelekezo ya viongozi wa dini za jadi kule Bagamoyo leo hii wengi wangekua wanakosa dili za kukimbiza mwengi na kupiga hela.