Hotuba ya Dkt Tulia yawafuta machozi waombolezaji na kumpa tabasamu Mjane wa Lowassa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,264
9,715
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna jambo ambalo Mwenyezi Mungu kaliweka ndani ya Dkt. Tulia Acksoni Mwansasu, Dada wa Taifa, Msomi Nguli wa Sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini, Spika wa Bunge, na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, ambalo pengine kuna kitu Mungu anakipitishia na amekuwa akimtumia Dkt. Tulia katika kupeleka ujumbe kwa Watanzania. Japo tunaweza tukawa bado hatujafunuliwa bado kwa wakati huu.

Ilikuwa hivi, ndugu zangu, katikati ya simanzi nzito, mawazo mengi, majonzi mazito, maumivu makali na machungu makali mioyoni mwa ndugu, jamii, marafiki na waombolezaji mbalimbali waliohudhuria katika shughuli ya kumsindikiza Hayati Edward Lowassa katika safari yake ya mwisho ya kumpumzisha katika nyumba yake ya milele.

Ikafika zamu ya Bunge kutoa salamu zake za pole kwa familia. Ndipo akaitwa kwa heshima kubwa, Dada wa Taifa ambaye ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Acksoni Mwansasu. Ambapo akainuka haraka kwa staha, adabu, heshima, unyenyekevu, na kujiamini huku akiwa kavalia mavazi ya heshima na staha yaliyompatia nafasi na uhuru wa kutembea vizuri, akaenda mahali palipo maalumu kwa ajili ya kuzungumza.

Akaanza kwa kurejea yaliyozungumzwa na mkuu wa KKKT kwa kurejea katika kitabu cha Ayubu sura ya 14:1 eneo linalosema mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua na kisha hukatwa. Hapa akatoa somo kwa waombolezaji na Watanzania waliokuwa wanafuatilia kupitia TV kuwa pamoja na kuishi siku chache sisi kama wanadamu kuna muda wa kuchanua maua. Je, maua yako yatakuwa ya kunukia na kuvutia wengi au itakuwaje? Akasema ni lazima tujitathmini tuwapo hai juu ya nini tunafanya na tunakuwa watu wa aina gani katika kuchanua kwetu na katika siku hizo chache za kuishi hapa Duniani.

Mwisho ndipo akamalizia kwa kishindo kikuu kilichowatetemesha na kuwafuta kabisa machozi waombolezaji, na kumfanya mjane wa marehemu Lowassa na pamoja na Mheshimiwa Rais waliokuwa wamekaa jirani nyuso zao kutabasamu na kutikisa vichwa kwa faraja kubwa ya moyo waliyoipata kutoka kwenye maneno ya Dkt. Tulia.

Hii ni baada ya Mh. Dkt. Tulia kwa hekima na utulivu mkubwa sana kusema, "Mheshimiwa Rais, salamu za bunge zinatoka katika kitabu cha Wagalatia 6:7." Kinachosema au chenye maneno yanayosema kuwa, "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; akipandacho mtu ndicho atakacho kivuna."

Kwa hakika maneno hayo yakawa kama leso machoni mwa waombolezaji, maana ghafla watu wakajikuta wanaacha kulia na kunyamaza. Ikawa ni kama Mungu aliingia ndani ya Dkt. Tulia na kuamua kuwafuta watu machozi baada ya kuona wamezidiwa na majonzi. Watu wakawa watulivu na wenye matumaini makubwa sana. Ghafla watu wakaona uwepo wa Mungu katikati yao na kupata faraja na tabasamu katika nyuso zao.

Nimeshuhudia mahali nilipo watu wakiwa bize kusoma Biblia kupitia simu zao na wengine wakifunua Biblia kusoma vitabu vya Ayubu na Wagalatia kujisomea kwa undani zaidi. Wengine wakitamani wabatizwe kabisa ili Mungu awe ndani yao na nuru ya Mungu iwaangazie katika maisha yao yaliyosalia hapa Duniani.

Kwa hakika Dkt. Tulia ni nyota na taa iliyowashwa na Mungu mwenyewe. Hakuna mwanadamu awezaye kuizima. Ni mfano wa kuigwa. Mungu ambariki sana Dkt. Tulia. Libarikiwe tumbo lililombeba Dkt. Tulia Acksoni Mwansasu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna jambo ambalo Mwenyezi Mungu kaliweka ndani ya dkt Tulia Acksoni Mwansasu Dada wa Taifa,msomi Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini, speaker wa bunge na Rais wa umoja wa mabunge Duniani,ambalo pengine kuna kitu Mungu anakipitishia na amekuwa akimtumia dkt Tulia katika kupeleka ujumbe kwa watanzania.japo tunaweza tukawa bado hatujafunuliwa bado kwa wakati huu.

Ilikuwa hivi ndugu zangu, katikati ya simanzi nzito , mawazo mengi,majonzi mazito,maumivu makali na machungu makali mioyoni mwa ndugu ,jamii,rafiki na waombolezaji mbalimbali waliohudhuria katika shughuli ya kumsindikiza hayati Edward lowassa katika safari yake ya mwisho ya kumpumzisha katika nyumba yake ya milele.

Ikafika zamu ya bunge kutoa salamu zake za pole kwa familia.ndipo akaitwa kwa heshimu kubwa dada wa Taifa ambaye ni speaker wa bunge dkt Tulia Acksoni Mwansasu. Ambapo akainuka haraka haraka kwa staha ,adabu ,heshima , unyenyekevu na kujiamini huku akiwa kavalia mavazi ya heshima na staha yaliyo mpatia nafasi na uhuru wa kutembea vizuri akaenda mahali palipo maalumu kwa ajili ya kuzungumza.

Akaanza kwa kurejea yaliyozungumzwa na mkuu wa KKKT kwa kurejea katika kitabu cha ayubu hususani eneo linalosema kuwa siku za kuishi mwanadamu aliye zaliwa na mwanamke hapa duniani ni chache nazo zimejaa shida na taabu na kwamba huchanua kama ua .hapa akatoa somo kwa waombolezaji na watanzania waliokuwa wanafuatilia kupitia Tv kuwa pamoja na kuishi siku chache sisi kama wanadamu kuna muda wa kuchanua maua je maua yako yatakuwa ya kunukia na kuvutia wengi au itakuwaje? Akasema ni lazima tujitathimini tuwapo hai juu ya nini tunafanya na tunakuwa watu wa aina gani katika kuchanua kwetu.

Mwisho ndipo akamalizia kwa kishindo kikuu kilicho watetemesha nakuwafuta kabisa machozi waombolezaji na kumfanya mjane wa marehemu Lowassa na pamoja na Mheshimiwa Rais waliokuwa wamekaa jirani nyuso zao kutabasamu na kutikisa vichwa kwa faraja kubwa ya moyo waliyoipata kutoka kwenye maneno ya dkt Tulia.

Hii ni baada ya Mh Dkt Tulia kwahekoma na utulivu mkubwa sana kusema Mheshimiwa Rais salamu za bunge zinatoka katika kitabu cha wagalatia kinachosema au chenye maneno yanayosema kuwa MSIDANGANYIKE akipandacho mtu ndicho ATAKACHO KIVUNA,.

Kwa hakika maneno hayo yakawa kama leso machoni mwa waombolezaji maana ghafla watu wakajikuta wanaacha kulia na kunyamaza.ikawa ni kama Mungu aliingia ndani ya dkt Tulia na kuamua kuwafuta watu machozi baada ya kuona wamezidiwa na majonzi.watu wakawa watulivu na wenye matumaini makubwa sana.ghafla watu wakaona uwepo wa Mungu katikati yao na kupata faraja na tabasamu katika nyuso zao.

Nimeshuhudia mahali nilipo watu wakiwa Bize kusoma biblia kupitia simu zao na wengine wakifunua biblia kusoma vitabu vya ayubu na wagalatia kujisomea kwa undani zaidi.wengine wakitamani wabatizwe kabisa ili Mungu awe ndani yao na nuru ya Mungu iwaangazie katika maisha yao yaliyo salia hapa Duniani.

Kwa hakika dkt Tulia ni nyota na taa iliyowashwa na Mungu mwenyewe.hakuna mwanadamu awezaye kuizima.ni mfano wa kuigwa.Mungu ambariki sana dkt Tulia.libarikiwe tumbo lililo mbeba dkt Tulia Acksoni Mwansasu.
Hatimae mkeka wangu umetick. Nilibeti Luca hawezi kumaliza siku bila kusema chochote humu
 
Utakuwa mpiga debe wake.. uchawa mbaya sana au kwa lugha rahisi njaa ni mbaya sana.
 
MNAJUA KUJIPENDEKEZA KWA KWELI YANI CCM HAMNA JIPYA.ETI HISTORIA YA MAREHEMU MMERUKA KIPENGELE KUHUSU KUGOMBEA URAISI NA ALIKUWA CHADEMA KAMA MPINZANI WA CCM
 
Utakuwa una ufahamu mdogo. Hata unaemsifia atakuwa anakereka na sifa zisizo na maana. Ungekuwa unanisifia Mimi ningekuwa nimeshakupiga stop. Hata machawa maarufu akina Baba Revo na Mwijaku hawasifii kama namna yako
 
Back
Top Bottom