Sandinistas
JF-Expert Member
- Jul 5, 2013
- 2,609
- 1,771
MTU mwenyewe ameingizwa bungeni kwa kupitia mlango wa nyuma lazima amuabudu na kumtii aliyempeleka hapo inamaana anatekeleza maagizo toka juu .
Somo kubwa sana. Kumbe kiongozi wa serikali aweza kupandikiza mtu wake bungeni na kuufanya mhimili huo kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kwanza kikatiba wa kuwa sauti ya wananchi na kusimamia serikali kwa niaba ya wananchi. Sasa tumeona kwa macho yetu. Wabunge wote bila kujali vyama vyao wanapaswa kukataa hili ni jambo; vinginevyo hakuna sababu ya kuwa na Bunge. Wabunge wa ccm wanadanganyika kuwa chama chao ndiyo chenye serikali lakini wao wenyewe siyo wawakilishi wa wananchì tena. Badala yake wamekuwa wawakilishi wa serikali. Kadhia ya korosho ni mfano hai.