Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 31,449
- 31,763
Aisee... Upupu mtupu..!!! Unataka wasiofunga wakale wapi!? Kwanini imani yako ya kidini unataka kuwashirikisha wasio wa imani yako kinguvu..!??Mbali na kuzuwiwa kwa vyakula kuuzwa mchana wa ramadhani katika baadhi ya maeneo,lakini bado zuio hili halijatendewa haki.
Waislamu tunaamini kwamba ukifunga basi hata ukila ile punje ya karanga tu na ukameza kwa makusudi basi umefungua sio mpaka ule biriani au urojo bakuli zima.
Sasa ni jambo la ajabu sana kuona kuna baadhi ya vyakula eti ruhusa kuuza kama vile..
Ndizi
Karanga
Mapapai
Korosho
Machungwa
Matikiti ambayo mengine yameshakatwa tayari kwa kuliwa.
Maji pia yanauzwa.
Juisi aina zote zinauzwa madukani.
Biskuti zinauzwa madukani.
Na vitu vingine vingi achilia mbali vitu hivyo.
Lakini vyakula vya kupikwa vimezuiwa kabisa na migahawa imefungwa kabisa.
Mimi naona hii haiko sawa kwa sababu orodha ya vyakula nilivyotaja pia mtu akila anafungua kwa hiyo navyo ilikuwa vizuiliwe kuuzwa ama maduka yafungwe kama ambavyo migawaha imefungwa.
Siku za kawaida tunawaona watu wanakunywa maji hadharani hivyo na maji ilikuwa yapigwe marufuku yasiuzwe ama maduka yanayouza maji yafungwe.
Siku za kawwida watu hula hadharani karanga,hivyo na karanga ilikuwa zizuiwe zisiuzwe.
Siku za kawaida watu hula ndizi hadharani hivyo ilikuwa na vibanda vya matunda vipigwe marufuku lakini hawa wauza matunda ndio utawakuta wanalalamika endapo migahawa haifungwi kana kwamba wao hawauzi vyakula.
Na vinywaji vingine vyote vinavyouzwa madukani tunaona kabisa vinywaji hivyo hunywewa katika siku za kawaida.
Hivyo ilikuwa maduka yanayouza vinywaji yafungwe kama ambavyo migahawa imefungwa.
HOJA WANAYOTUMIA.
HOJA:.eti migahawa inauza vyakula vya kula hapohapo yaani wanaandaa ili kiliwe kwa nyakati hizo.
JAWABU : ndizi,embe,korosho,mapapai,na machungwa maji,juisi,biskuti n.k haya yote yapo tayari kuliwa muda wote na wala hayajapigwa marufuku ama kufungwa maduka,hivyo sio sawa na maduka yafungwe pia.
Kama itasemwa kwamba migahawa watu wanakula hapo hapo nddio maana wamezuia basi wangekataza tu kwamba watu wasile migahawani lakini migahawa ipike vyakula,kidoogo ingemake sense japokuwa tungehoji zaidi.
Imagine familia yote imefunga alafu kuna mgonjwa ana vidonda vya tumbo,sasa badala ya mama kusumbuka kupika huku amefunga si angetoa pesa tu kwendakununjua chakula akarahisisha ?
Huu utaratibu uangaliwe upya na kufanyiwa maboresho katika hayo maeneo ambayo taratibu hizo zipo.