EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
- Thread starter
- #21
Kwa vile kuna mpango wa DART ambao unahusiana na usafiri wa Jiji la Dar - kazi iliyokuwa imefanywa kisheria na UDA - kwanini UDA haikubadilisha na kuwa hiyo mamlaka mpya ya DART - ikiwa na facilities na mara nyingine ambazo zingeweza kuwa sehemu ya mtaji wake? Kulikuwa na tatizo gani la kuzuia UDA isiwe DART?
Kwa kweli hata mimi nimeshindwa kuelewa. Decisions nyingine huwa zinafanywa mpaka unashindwa kuelewa why they reached such a decision. Mwaka jana waziri Mkuu Pinda, kwa Niaba ya Rais Jakaya Kikwete, akizundua mradi wa mabasi matano yenye dhamani ya sh 500 million ya kubeba wanafunzi yaliyotolewa na CRDB kwa UDA alilitaka shirika la UDA kuwa macho ili lsije likafia mikononi mwao. Kuna mdau alighusia humu JF mwaka jana kuwa kabla ya kutoa huu msaada, UDA waliomba mkopo wa kununua mabasi CRDB wakatoswa. UDA bado ni shirika zuri na kilichotakiwa kufanywa na serikali ni kulifufua hili shirika na kulitumia katika mradi mzima kuboresha usafiri Dar Es Salaam. Badala yake tunaona yale yale ya KAMATA. Kukiwa na shirika moja tu lenye uhakika kusafirisha watu kwenda waendako sijui kama watu wataamua wapande magari yao kwa kila siku.