UDA yauzwa kwa bei chee, Ofisi zake Zavamiwa

Hivi UDA ilianzishwa na nani na kwa nini? Ni masalio ya serikali ya Mkoloni?..
Wana JF mnajua hii kampuni ya Simon Group nyuma yake yupo nani? Fanyeni uchunguzi mtajua why 51pc ya shares zimeuzwa kwa kiasi hicho na jeuri ya huyo kwanza kwa kuvunja mkataba?na kufanya alofanya.
 
Ukimwambia Pinda au JK watakuwa hawana habari maana wote wako safarini .CCM mnatumaliza hakika mtauza hata ngozi za watanzania sasa .Yaani kila kukicha nij ufisadi na sheria sijui hazipo ? Au ziko kuwabana akina Sugu pekee ?
 
Dr Gaijin(wastahili)

Mawizarani wapo watu wenye akili tena saana, wengine ni wachapa kazi kweli. Tatizo nipale unakuta file lina kimemo juu,pia maslahi ya wazee, hali kama hii, watu wanavaa miwani ya mbao na kuharakisha mwanaharamu apite salama

Nikupe mfano mzuri, kuna wizara moja nyeti tu, kuna mama moja ni mkuu wa kitengo( elimu yake ni kichekesho) hata mtoto wa kidato cha sita anaweza challenge reason capacity yake. Huyu mama ananguvu kuliko katibu mkuu wa wizara, na hata waziri mwenyewe. Kisheria anatakiwa areport kwa katibu mkuu lakini yeye anareport Magogoni moja kwa moja. ma dr, wasomi waliopo hapo wizarani utawalaumu kwa maamuzi yasiyokuwa na tija kwa taifa yanayotendwa na wizara?

Inaiskitisha lakini ndo hali ilivyo

Sijui ni kwanini umeficha jina la hiyo wizara, lakini mimi nafikiria wewe pamoja na hao mabosi wa huyo mama mna-share kitu kimoja.... woga wa kijinga. Hivi kama mtu wewe ni katibu mkuu wa wizara na kuna ofisa chini yako hataki kufanya kazi chini yako, na badala yake anakimbilia magogoni na unakaa kimya tukueleweje? Unaogopa? Unanidhamu? Hujiamini? Mimi nadhani ningekuwa mimi bora niache kazi kuliko kufanywa ndondocha...
 
UDA ilitokana na kubinafisishwa kampuni binafsi ya Dar es Salaam Motor Transport (DMT) na kuzaa UDA na KAMATA. Kampuni ya DMT ilikuwepo tangu enzi hizo za mkoloni halafu ikabinafishwa na utawala wa Mwalimu Nyerere.
Muuliza swali sio kama hajui jibu mama mdogo.... anataka kuwachokoa wale watu wa kundi linaloona vigumu kutamka "baba wa taifa" badala yake wanasema "mzee Nyerere"
 
tatizo decision maker karibu wote wanamiliki daladala. kama kuna taasisi inaweza kusimamia haya mawazo mazuri yanayotolewa kwenye hii post tunaomba ijitokeze kuishindikiza serikali nasi tutakuwa nao bega kwa bega. Yaani nimeipenda sana hii post kiasi kwamba natami ningekuwa mimi ndiye muamuzi mkuu. msongamano mjini ungeisha fasta
mh.....misukule imegeuka binadamu...
 
kuvunja ofisi hata kama UDA na Simon Group wana mkataba tayari ni uhalifu na hawataweza kukaa pamoja wakapatana nilifikiri polisi wangefanya kazi yao ya kumkamata kwa kosa la kuvunja ofisi mambo ya mkataba hayahusiani na polisi.

Mkuu hata mie nimeshindwa kuelewa kwa nini hili halihusiani na polisi. Kuvunja ofisi at least kutakuwa na criminal damage. kwa mantiki hii unaweza kuvamiwa nyumbani na majambazi, unaenda polisi na kuambiwa ukajadiliane na huyo jambazi.
 
Ukimwambia Pinda au JK watakuwa hawana habari maana wote wako safarini .CCM mnatumaliza hakika mtauza hata ngozi za watanzania sasa .Yaani kila kukicha nij ufisadi na sheria sijui hazipo ? Au ziko kuwabana akina Sugu pekee ?

Lawama hizi zinatakiwa zielekezwe kwa wabunge wa Dar, akina Mnyika na Halima Mdee. Mmmekaa kimya tu tuwaeleweje?
Watanzania iko siku tutauzwa hata ngozi zetu sasa
 
Hii ni dhambi ya kuuza uza tu imeingia kwenye damu zao!! Surely this is very shocking news to me! With introduction to transit system, i thought it was the perfect moment ya UDA kufufuka upya!!!

Hivi haya mambo wakakti yanaendelea hivi, ina maan JK na PINDA huwa wametiwa pamba masikioni!! Oooh i get it ni kati ya siri kubwa za vikao vya baraza...

I wonder, wakimaliza kuza kila kitu watahamia kwenye nini?
 
Kwa kweli hata mimi nimeshindwa kuelewa. Decisions nyingine huwa zinafanywa mpaka unashindwa kuelewa why they reached such a decision. Mwaka jana waziri Mkuu Pinda, kwa Niaba ya Rais Jakaya Kikwete, akizundua mradi wa mabasi matano yenye dhamani ya sh 500 million ya kubeba wanafunzi yaliyotolewa na CRDB kwa UDA alilitaka shirika la UDA kuwa macho ili lsije likafia mikononi mwao. Kuna mdau alighusia humu JF mwaka jana kuwa kabla ya kutoa huu msaada, UDA waliomba mkopo wa kununua mabasi CRDB wakatoswa. UDA bado ni shirika zuri na kilichotakiwa kufanywa na serikali ni kulifufua hili shirika na kulitumia katika mradi mzima kuboresha usafiri Dar Es Salaam. Badala yake tunaona yale yale ya KAMATA. Kukiwa na shirika moja tu lenye uhakika kusafirisha watu kwenda waendako sijui kama watu wataamua wapande magari yao kwa kila siku.

Halafu kuna kitu sikielewi; mara kadhaa kila panapotajwa UFISADI hiyo benki kwenye red ni lazima iguswe kuanzia EPA na mauchafu mengine. Niliwahi kuwa na akaunti kwenye hii benki tangu ikiwa na lile jina tukufu la "Benki ya Ushirika na Maendeleo Vijijini" ambalo walilikana baadaye pengine strategically. Tafadhali, unaweza kulisaidia taifa lako, unaweza kuokoa maisha ya kichanga kimoja, n.k. kwa kufunga akaunti yako kwenye hii benki na kumshauri mwenzako/rafiki yako kufanya vivyo hivyo.
 
John Mnyika na Halima Mdee mbona mko kimya? Ama nyie ndo mmeinunua UDA? Mmmshaanza kutuboa sasa
 
Hisa za UDA zingepelekwa kwenye soko la Mitaji. Wananchi wakauziwa baadhi ya hisa. Kwanini kila kukicha maamuzi yako kinyume na matarajio ya wananchi? Tukisema wakoloni weusi ni wabaya zaidi kuliko wakoloni waliotututawala wanadai tuna kasumba ya kikoloni,hatufiki Kanaani.
 
Hawa wote ni wanafunzi wa Hayati Mwalimu!
attachment.php
 
John Mnyika na Halima Mdee mbona mko kimya? Ama nyie ndo mmeinunua UDA? Mmmshaanza kutuboa sasa

hapa unajaribu kukwepesha wajibu. Wenye kuwajibika ni wana CCM wote wa jiji la Dar na viongozi wao kuanzia anayeishi Magogoni. Sera zinazotekelezwa ni za CCM siyo za Chadema na hivyo watu pekee wa kuwauliza, kuwabana ni kina Zungu na wenzao. Tuweke lawama panapostahili. Hawa wapinzani wanachoweza kufanya ni kuzungumza kwa hasira tu na kutoa maneno makali lakini nje ya hapo influence yao is almost haipo. Zaidi watakachofanya ni kutufanya tujisikie vizuri tu jinsi wanavyomwaga hoja na sera mbadala.
 
kweli Tz inarudi nyuma kimaendeleoa badala ya kusonga mbele..kungekuwa na strategy nzuri pia utekelezaji, UDA ingefika mbali na kusaidia sana public transport..nchi hii sijui imelaaniwa?
 
hapa unajaribu kukwepesha wajibu. Wenye kuwajibika ni wana CCM wote wa jiji la Dar na viongozi wao kuanzia anayeishi Magogoni. Sera zinazotekelezwa ni za CCM siyo za Chadema na hivyo watu pekee wa kuwauliza, kuwabana ni kina Zungu na wenzao. Tuweke lawama panapostahili. Hawa wapinzani wanachoweza kufanya ni kuzungumza kwa hasira tu na kutoa maneno makali lakini nje ya hapo influence yao is almost haipo. Zaidi watakachofanya ni kutufanya tujisikie vizuri tu jinsi wanavyomwaga hoja na sera mbadala.

Mzee mwanakijiji habari ya leo?
Nadhani Halima Mdee na Mnyika hawastahili kukaa kimya at least wangeileta hii hoja ijadiliwe mjengoni. Huyo Zungu achana nae kwani hata sielewi kama kichwani ni mzima
 
Mr. Sherrif, hilo ndilo lilikuwa wazo langu pia. Wanachofanya ni ilie ile template ya ufisadi - wanauza cha Taifa ili waingize cha mtummoja mmoja. Yaani wameanza mpango wa transit system halafu wanauza UDA! Kwanza nimeona sitaki kuamini lakini siwezi kushangaa kabisa kuwa ni kweli. Huwa nauliza kwanini hawabinafsisi Ikulu?

Nadhani kiutendaji ikulu iko mikononi mwa wawekezaji. Tukitoka hapo wataichua yote
 
Washaona dili la darts wanajipanga kuiondoa uda na kuingia wao. Tuwagomee kwa migomo cdm mpo huku ndio kwa kuelekeza maandamanao kama hamna pesa semeni tutachanga ili mradi uda isiuzwe ina magari bomba kuliko haya ya wamiliki binafsi wakipewa darts wanauwezo pia.
 
Back
Top Bottom