Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 16,881
- 22,348
Nimerudi mjini ila naona jamaa waliniachia maboksi yangu ya kubeba mengi sana. Kwa hiyo nimekuwa mtoro sana hapa kijiweni siku hizi ili niyapunguze kidogo. Hata hivyo nimeona nitoe duku duku langu kuhusu uchunguzi unaofanywa pale BOT na 'independent company.' Inasemekana kuwa uchunguzi huu unafanywa na kampuni ya kimarekani inayoitwa Ernst Young, lakini ukweli ni kuwa kazi hiyo inafanywa na jamaa mmoja ambaye ni ndugu wa aliyekuwa aliyekuwa waziri wa fedha wakati wa Mkapa. Waziri huyu ndiye aliyemsaidia ndugu yake huyo kupata franchise ya Ernst Young kwa vile alikuwa akipewa tenda nyingi sana za kukagua mahesbau ya serikali. Nina wasiwasi kuwa mtu kama huyo katika mazingira ya utata uliopo kweli atafanya uchunguzi independent. Ndiyo maana nadhani kuwa tunatwanga maji kwenye kinu, jamaa watayeya tukiwa tunawaona hivi hivi tu.
Uchunguzi mzito kama huu unatakiwa kweli ufanywe na kampuni credible, wala siyo hizi kampuni zetu kanyabwoya za mishen town.
Uchunguzi mzito kama huu unatakiwa kweli ufanywe na kampuni credible, wala siyo hizi kampuni zetu kanyabwoya za mishen town.