Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,571
Wanabodi
Preamble: Naunga mkono juhudi zote zinazofanywa na rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli katika kubana matumizi yasiyo ya lazima na badala yake fedha hizo zitumike kuleta maendeleo.
Baadhi ya maamuzi haya ni maamuzi ya zimamoto ambayo yamefanyika ghafla kama uamuzi wa kufuta mialiko ya kuhudhuria tukio la kuzimwa Mwenge wa Uhuru.
Uamuzi huo umefanyika ghafla as if tukio la kuzimwa Mwenge. Wa Uhuru ni tukio la ghafla na limekuja bila taarifa kama lile tetemeko la ardhi Bukoba!, tukio hili lilikuwepo, limepangwa kwa mwaka mzima, mwenge umezungushwa nchi nzima, protocol ya kilele cha sherehe hizo inajulikana mwaka mzima, bajeti ilipangwa, ikapitishwa, madokezo yakaandikwa, fedha zikaidhinishwa, barua za mialiko zikatolewa, fedha zikalipwa, safari zikapangwa, then ghafla at an eleventh hour ndipo inakuja taarifa ya Ikulu kuifuta mialiko hiyo na waliochukua fedha kurudisha! . What a disturbance and inconveniences? . Kulikuwa na udharura gani kuuzuia mialiko hiyo mapema at the planing stage na kuja kuahirisha kwa mtindo wa zimamoto at the last minute?!.
Kuna kitu kinaitwa "A legitimate expectations", mtu akiishajiandaa kwa safari, na unachukua malipo, unakuwa umeishajiondoa nyumbani na kujipanga kisafari safari, tena wengine hata kupanga utalala wapi na bulangeti la aina gani!, wengine husafiri na ndoo, wengine vidumu na wengine watajua mbele kwa mbele alimradi ni safari halali ya kikazi.
Safari kama hiyo inaweza tuu kuahirishwa kama kumetokea jambo ambalo halikutarajiwa "force majeure", lakini safari inapoahirishwa kwa uamuzi tuu wa utashi wa kiongozi bila kutumia sheria yoyote wala kanuni yoyote, then a legitimate expectations zinawataka watumishi waliokwisha lipwa fedha, kurudishwa zile fedha tuu ambazo hazijatumika ambazo ni fedha za maduhuli (imprest) lakini hawapaswi kurudisha zile fedha za masurufu (allowances), hizo ni halali yao kisheria.
Kitu kingine muhimu kupitia sheria mpya ya the right to information, wananchi tunapaswa kuelezwa maamuzi haya ya Zimamoto yameleta tija gani, kiasi gani kimeokolewa na fedha hizo zimefanyia maendeleo gani isije kuwa watu Tunatwanga Maji Kwenye Kinu, kisha tunapongezana kwa uamuzi wa busara.
Lilipoundwa Baraza ndogo la Mawaziri huku makatibu wakuu wakiongezeka, kuna watu tulisema humu tumeongeza gharama za uendeshaji wa serikali badala ya kupunguza, hata baada ya kupungua wafanyakazi hewa na kutoajiri wafanyakazi wapya, wage bill ya serikali bado unazidi kuongezeka badala ya kupungua, ili usije kuwa ni kutwanga maji kwenye Kinu, wananchi tuambiwe kupunguza ukubwa wa serikali tume save kiasi gani, safari za nje tumeokoa kiasi gani,kufuta sherehe za uhuru tumeokoa kiasi gani, na hizi fedha zote zililookolewa ndio zimepelekwa kwenye huduma za jamii kama afya, elimu etc, ili Watanzania tuone tija ya kubana matumizi na sio kubana matumizi huku tukitwanga maji kwenye Kinu.
Wakati tukiendelea kumpongeza rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa maamuzi yake yenye tija kwa taifa letu, tuendelee kumsisitizia kuwa taifa hili linahitaji zaidi kujengwa kwa mifumo imara ya iutendaji, usimamizi, utekelezaji, na tathimini ili kupata mresho hivyo kufanya uwajibikaji na matumizi mazuri ya fedha za umma kwa shughuli zote zisizo na manufaa kwa taifa zikiwemo Mbio za Mwenge, na sherehe nyingine mbalimbali zisizo na tija na maslahi kwa taifa letu zifutwe rasmi kwa waraka na sio kutegemea utashi tuu wa rais. Hili la rais kutoa maagizo kwa waraka, nilishauri hapa
AG, Mshauri Mh.Rais Atoe Maagizo kwa Presidential Decrees Kuyapa Nguvu ya Kisheria
Suala la nini kina manufaa kwa taifa na nini hakina manufaa kitajulikana kwa kupokea mrejesho na you never know taifa letu linaweza kufikia hatua, kwenye kila mpango, kila wizara, kila idara, kila taasisi, kila mradi kila mpango wa maendeleo, tujenge mfumo wa SMART OBJECTIVES, wenye malango mahsusi na mwisho wa siku tunaletewa mrejesho
Mfano tukifanya tathmini ya majukumu ya post za Wakuu wa Wilaya, tutagundua hizi ni post za colonial legacy tuu, yaani post za kikoloni tuu na hazina maana yoyote ukilinganisha na the expenditure na work done kwa sababu Wakurugenzi wa Halmashauri wanatosha sana tuu hivyo gharama za Wakuu Wa Wilaya nazo ni ufisadi tuu, post hizi zikifutwa zitalisaidia sana taifa letu.
Tumefanya miradi mingi, Mkukuta, Mkurabita, Mkuza, Mkumbita, Uhaulishaji fedha, Kilimo Kwanza, etc ambayo huianza kwa mbwembwe sana, lakini hatupewi mrejesho.
JK alikuja na drive ya uchumi wa gesi kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati, takapanga mipango mingi ya matumizi ya gesi, hadi kwenye magari, viwandani hadi majumbani, gesi ndio iwe the main source of power kwa kufikishwa hadi Bagamoyo kwenye ile industrial park na bandari ya Bagamoyo. Magu kaingia, kaja na drive yake ya Tanzania ya viwanda, SGR, ndege, na the source of power sasa sio gesi tena bali ni hydropower, badala ya kuendeleza miradi ya gesi, sasa tunaanza mradi wa Stigler Gorge!, Bandari ya Bagomoyo imesimamishwa!.
JK akaanzisha mchakato wa Katiba mpya, tukatumia mabilioni, Magu kaingia, kwake katiba sio kipaumbele!. Nchi haiwezi kuendeshwa hivi na tukafika, lazima tujenga tabia ya kufanya tathmini na tuletewe mrejesho.
Hongera sana rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchukua maamuzi magumu kulisaidia taifa letu lenye lindi la umasikini uliotopea uliogubikwa na rushwa na ufisadi, maamuzi haya hata yakiitwa ni ya udikiteta, then afadhali ya udikiteta ili taifa liponywe kama kilivyo kidonge kichungu cha dawa au sindano yenye maumivu ndio iponyeshayo lakini tusianzishe miradi kwa kukurupuka, tufanye kwanza upembuzi yakinifu na mwisho tuletewe tathmini.
Nawatakia maandimisho mema ya Nyerere Day hapo kesho.
Wa Salaam
Pasco
Rejea.
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ..