Siasa za Umeme: Kwa vile Umeme wa Stigler's utatosha na ziada kuuza nje. Je, TANESCO kusaini PPA mpya 6 toka kwa 6 IPPs, sio ufisadi mpya wa kisasa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,543
Wanabodi,

Kwa vile hii ni mada technical, yaani ni mada ya kitaalam, naomba kuanza bandiko hili kwa elimu kidogo kwa members wenzangu ambao sio wataalam wa mambo ya power na energy.

Watu wanadhani siasa ni kusimama tuu majukwaani na kupiga domo, issues yoyote yenye impact kubwa kwa taifa ni siasa, hivyo hivyo zozote zinazohusu utilities, maji, umeme, gesi, mafuta, na public transport ni siasa, na kwa nchi zinazotegemea mkate kama chakula kikuu, issue yoyote. ya mkate ni siasa! kuna nchi inayotegemea mkate kama chakula chake kikuu, bei ya mkate ilipanda kwa thumuni tuu!, wananchi waliingia barabarani na serikali ilipinduliwa!. Hivyo issues za Umeme sio habari mchanganyiko ni siasa!

Kwa vile tumeelezwa umeme wa Stigler ukikamilika utatosha na ziada kuuzwa nje!, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani Desemba 14, 2020 akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua umeme wa Megawati 2115 kwa njia ya maji wa Julius Nyerere, amesema inatarajiwa kwa mwaka 2023 mahitaji ya umeme Nchini yakaongezeka kwa zaidi ya mara mbili mpaka kufikia megawati 2,770.

"Leo hii mahitaji kwa siku ni megawati 1,177.20. Kukamilika kwa mradi huu wa Julius Nyerere kutaongeza megawati 3,973 ambazo zitatumika katika shuguli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii hivyo tunahitaji umeme wa kutosha, utakaobaki tutawauzia majirani zetu" amesema Dkt. Kalemani.

Leo asubuhi, nimesoma mahali kuwa Tanesco imesaini mikataba mipya 6 ya PPA (Power Purchase Agreements) koka kwa wazalishaji binafsi IPPs (Independent Power Producers ) wapya 6, ili kununua megawati 19.16 na kuziingiza kwenye gridi ya taifa, ndani ya miezi 18 ijayo, Jee huu sio aina mpya ya ufisadi mpya wa kisasa kama ulivyokuwa ufisadi wa Richmond, Dowans na IPTL?!.

Hebu kwanza jisomee story yenyewe

TANZANIA: TANESCO to buy 19.16 MW of green electricity from six IPPs

By Inès Magoum - Published on December 14 2020 / Modified on December 14 2020

abriendomundo/Shutterstock" data-src="/proxy.php?image=https%3A%2F%2Fwww.afrik21.africa%2Fwp-content%2Fuploads%2F2020%2F12%2Fshutterstock_1464805487-800x400.jpg&hash=051e3b0f7fda1d5f598545cf47a53447" data-lb-sidebar-href="" data-lb-caption-extra-html="" data-single-image="1"> TANZANIE : la Tanesco va acheter 19,16 MW d’électricité verte à six IPP<img src=abriendomundo/Shutterstock" title="TANZANIE : la Tanesco va acheter 19,16 MW d’électricité verte à six IPPabriendomundo/Shutterstock" width="" height="" />

Six Independent Power Producers (IPPs) have just concluded power purchase agreements with the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO). These private companies are developing renewable energy projects in Tanzania with a total capacity of 19.16 MW.​

The state-owned Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is signing power purchase agreements (PPAs) with six independent power producers (IPPs) that are developing several renewable energy projects in Tanzania. TANESCO agrees to purchase 19.16 MW of electricity, under the supervision of the Energy and Water Regulatory Authority (EWURA) of Tanzania.

Among the selected IPPs is Nishati Lutheran Investment, which is implementing a 36-kW hydropower project at the Ijangala Falls in Makete. Similarly, Madope Hydro is implementing the 1.7 MW Madope Hydroelectric Project on the Madope River. Luponde Hydro is also signing a PPA with Tanesco for its Luponde hydroelectric project (9 kW) on the Luhololo River in Njombe. Lung’ali Natural Resources, which is implementing the Maguta hydroelectric project (1.2 MW) on the Lukosi River Falls in Kilolo, will sell its production to the utility.

Commercial operation in 18 months​

The other IPP selected is NextGen Solawazi which is working on a 5 MW hydropower project in the Kigoma Special Economic Zone. SSI Energy Tanzania, which is currently building a 10 MWp solar power plant in Kahama, will also sell its production to Tanesco. According to the public company, the six private companies will have to start marketing their production within 18 months.

In the meantime, TANESCO is developing other electricity projects in Tanzania. In this way, TANESCO is supporting the Tanzanian government’s policy of achieving a 75% electrification rate by 2035. Among its projects is the construction of the Rumakali and Ruhudji hydroelectric power plants which will have capacities of 222 MW and 358 MW respectively. In July 2020, TANESCO selected Multiconsult Norge AS, a Norwegian engineering consulting firm, to provide consulting services for the two projects.

My Take:
Japo mimi ni mwandishi wa habari, na sasa nimeisha staafu rasmi, lakini kwa vile kazi ya uandishi iko kwenye damu, hivyo ikitokea habari inahitaji ufuatiliaji, mimi nitaiweka tuu humu jf, wahariri watakao iona it's newsworthy, watatuma waandishi wao kuifuatilia, au waandishi watakaona ni habari, wataifuatilia, mimi nitakuwa nimetimiza wajibu wangu kwa jamii, ila ikitokea kweli ukawa ni ufisadi mwingine, utakuja kujulikana mwaka 2025 kabla ya uchaguzi ujao, nitakachokifanya ni kuwakumbusha tuu kuwa tulinusa, tukasikia harufu, tukauliza, na hayo ndio matokeo, ila pia, sio kila unaposikia harufu ya ufisadi ni ufisadi, harufu nyingine ni harufu tuu na hakuna ufisadi wowote, vitu vingine ni ukosefu tuu wa transparency, kama zile Bilioni 1.5 kwenye ripoti fulani ya CAG, watu wakadhani ni ufisadi, ikaja kukutikana hakuna ufisadi wowote.

Maswali ni haya.
  1. Kwanza maendeleo yoyote ya ujenzi wa mioundo mbinu wa umeme wa maji, ni maendeleo, endelevu, hivyo wakati Watanzania tukiusubiri huu umeme wa Stigler kuingizwa kwenye gridi ya Taifa, hakuna ubaya kwa Tanesco kuendelea kununua umeme toka kwa wazalishaji binafsi waliopo, kwa vile kuna wazalishaji wengi na mikataba imesimamishwa, kwa nini Tanesco wasiendelee nao na badala yake wanasani mikataba na wazalishaji wapya?. What is so special na hawa wapya, wakati wa zamani wapo, mikataba imesitishwa na wengine wametushitaki kwa kuvunja mikataba yao?
  2. Kama umeme wa Stigler, unatosha, hizi PPA's 6 mpya zinazosainiwa sasa ni za nini?.
  3. Kule nyuma tulivunja mkataba wa Dowans kwa tuhuma za ufisadi wa kulipishwa capacity charge kubwa na Tanesco kununua umeme wa bei juu toka kwa hawa IPPs na kuuza kwa bei ya chini!, Jee this time kwenye hii mikataba mipya jee Tanesco wananunua kwa bei gani per unit na kuuza kwa bei gani, tusije kuwa tunatwanga maji kwenye kinu?
  4. Baada ya kuvunjwa kwa mkataba wa Dowans, tulishitakiwa, tukashindwa kesi, tukadaiwa fidia iliyotwa Tozo ya Dowans, waheshimiwa wetu kule Bunge, wakajiapisha kwa maneno kama "over my dead body!" hatulipi! did you know what happened?....we paid every single cent kimya kimya na umeme ukapandishwa bei, Watanzania wote kwa ujumla wetu, tukafidia. Kitu cha ajabu sana katika hili, kampuni ile ile ya Dowans tuliovunja nayo mkataba, ikajibadili jina kujiita Simbion, mitambo ile ile, capacity charge ile ile, na mkataba ule ule, ikaingia tena mkataba na Tanesco, na tukakawa tunawalipa hadi JPM alipoingia, akaukataa ujinga huu, ndipo mkataba wa Simbion ukasitishwa na mpaka sasa kesi iko mahakamani, sijui tumefikia wapi! Kawa haya ndio mambo ya Tanesco na hizi PPA's zake, vipi hizi PPA's sita mpya are they clean?, transparent?.
  5. Kuna wakati kule nyuma, Tanesco ilikuwa inaelemewa na madeni ya umeme wa hawa PPA's na situation ya Tanesco kwa sasa ikoje hadi kuendelea kununua umeme kwa hawa wazalishaji binafsi, ili Tanesco ipate faida ni lazima inunue kwa bei ya jini na kuuza kwa bei ya juu, sasa kama Tanesco haina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha, kwa nini hao wazalishaji binafsi wasiruhusiwe kuuza umeme wao direct kwa watumia kwa bei ya chini, wananchi ndio wafaidike?.
  6. Japo tunaelezwa Stigler ikikamilika Tanzania tutakuwa na umeme wa kutosha na ziada kuuza nje. Hawa jamaa wanasema "In the meantime, TANESCO is developing other electricity projects in Tanzania. In this way, TANESCO is supporting the Tanzanian government’s policy of achieving a 75% electrification rate by 2035", wakimaanisha huo mwaka 2035, Tanzania ndio tutafikisha 75% ya mahitaji yetu ya umeme!, sasa nani anasema kweli?, jee ni kweli tutajitosheleza na ziada kuuza nje, au tutajitosheleza kwa mahitaji ya sasa kwasabu bado hajaweza ku electrify nchi nzima, hivyo hiyo ziada tutakayouza nje, tutauza huku baadhi ya vijiji vyetu havina umeme kwasababu hatuna miondombinu ya kutosha ku i electrify nchi nzima?. Which is which?.

Paskali
Update
Habari yenyewe

TANESCO yasaini mkataba wa kununua umeme kwa wazalishaji wadogo​

KUSAINI MKATABA KATI YA TANESCO NA WAWEKEZAJI WADOGO

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeingia mkataba wa kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wadogo wa kampuni sita binafsi, utakaoingia moja kwa moja kwenye kwenye gridi ya Taifa na kutumika katika maeneo mbalimbali Nchini.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mikataba kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Meneja Mwandamizi Uwekezaji, Mhandisi Costa Rubagumya alisema wawekezaji hao wamekidhi vigezo kwa mujibu wa kanuni zilizoidhinishwa na EWURA.

"Kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia uendelezaji wa miradi midogo ya kuzalisha umeme, inaitaka TANESCO kuingia mikataba na wazalishaji umeme wadogo kwenye maeneo ambayo gridi ya Taifa bado haijafika", alisema Mhandisi Rubagumya.

Aliainisha vigezo vingine ni maeneo ambayo yanatatizo la umeme mdogo ili kuimarisha ubora wa umeme na kigezo kingine ni maeneo ya usambazaji umeme ambapo njia za umeme za TANESCO ni ndefu hivyo kusababisha upotevu wa umeme.

Mhandisi Costa alizitaja kampuni hizo kuwa ni, Kahama Solar Power Project MW 10.0, Kigoma Solar Power MW 5.0, Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd MW 0.36.

Makampuni mengine ni, Madope Hydropower MW 1.7, Luponde Hydropower MW 0.9 na Maguta Hydropower MW 1.2.

Wakizungumza Kwa niaba ya Wazalishaji wadogo wa umeme, Padre Luciano Mpoma na Nicholas Richardson wameishukuru Serikali kupitia TANESCO kwa kukubali kufanya nao biashara ya umeme.

Waliongeza kuwa safari ilikuwa ni ndefu lakini hatimaye wamekuwa na furaha kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha nishati ya umeme inamgusa kila mwananchi.

Makampuni hayo yanatakiwa kuanza kuiuzia TANESCO umeme ndani ya miezi 18 kuanzia leo Disemba 08, 2020.

Update 2.
Mchango very constructive
 
Hili swala haliitaji hata technical ability kuelewa kwamba kuna ulazima au hakuna ulazima wa Tanesco kuingia huo mkataba.

Kwanza kabisa tukumbuke Nyerere Hydropower inatarajiwa kukamilika 2022 incase of any delay watanzania wanatarajia kunufaika na hizo 2115Mega watss kuanzia mwaka 2022 au 2023 kama itachelewa sana.

Cha kujiuliza wakati tunangoja mradi kukamilika hapa katikati tunaishije???Ndio maana mkataba ukawa 18months tuki expect kabla kufikia 2022 mambo yatakuwa sawa.
 
Matumizi ya umeme wa gas ile tuliyokuwa tunaimbishwa uchumi wa gas kama wendawazimu yameishia wapi?
 
Mataga watakuambia peleka dukuduku lako mamlaka husika

Na ungepeleka sehemu sahihi kweli kama kuna upigaji ungevutwa pembeni na kuulizwa "Paskali kwani unateseka? Hebu shika hii bahasha ya kishika uchumba kisha kesho uje na Vyeti pamoja na CV yako".
 
Upo ukweli P katika bandiko lako hili.

Ni kama mto Ruvu tu, unaona ni kama unanyooka hivi, halafu badaye ni kama unaruudi tena nyuma.

Tanzania ni nchi ya ajabu, kunamahali tunaweza kuamua kupiga hatua, halafu Wakati mwingine mara turudi nyuma tena!
Tatizo la P siku hizi ni kukosa msimamo!! (Unafiki) tulishasema ccm ni majizi!! yeye akaanza kutetea!! leo amekosa teuzi. amekuja na mada ya umeme!! anaweza kuwa sahihi!! lakini watu hawatamuamini tokokana na tabia yake ya kukosa msimamo!!
 
Mkuu, kuudanganya moyo Ni kujiuwa kidogokidogo!!
 
Mkuu Paschal, hao wote ni wazalishaji wadogo sana huwezi walinganisha na IPTL, RICHMOND etc. Baadhi yao MillardAyo amewarusha Sana kwenye mtandao wake. Tanesco inachofanya ni kujaribu kuwa boost watanzania wabunifu walioanza kuunganisha mitambo yao kwenye maporomoko locally na ku supply vijiji vya jirani tena bure mwanzoni.

JPM aliposikia akaamuru wawezeshwe na waingizwe kwenye mpango maalum ili kuwawezesha baadae kufika level za juu zaidi. Hii imefanyika kati ya 2017 - 2019. Ukifatilia kwa ukaribu hizo kampuni zote ni za wazawa tena wa huko ndani ndani. Hili ni jambo la kuishukuru Tanesco na serikali badala ya kulaumu au kutilia shaka.

Hapo hakuna kampuni ya mchina,mhindi wala mzungu hata mmoja. Hao ni wabunifu wa humu humu Tanesco inajaribu kuwainua. Hujiulizi kampuni sita Total supply ni 19.6 MW ?
 
Paskali, kiasi kinachozalishwa na hao 6 IPPs ni kidogo sana na at most kitasaidia kustabilize umeme kwenye local areas zilizo kwenye national grid. Ni kupoteza muda kushupalia hili suala maana pamoja na SG tunahitaji uzalishaji wa umeme uwe ahead ya mahitaji yetu ya ndani ili kuweza kuuza nje na kuvutia wawekezaji. Tumeslishwa matango pori kuwa kila kitu kinachifanywa na private sector awamu hii kuwa ni ufisadi.
 
Kuna mbungi zinachezwa humu nchini ila hatutoboi 2025 bila kuzijua. Uchumi na hesabu haziongopi soon utaona bei ya umeme inapanda ijue mbungi tayari ishachezwa.
 
Back
Top Bottom