kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 118
- 237
Uchumi wa Tanzania Bara umekua kwa 5.4% ikilinganishwa na makadirio ya 4.7% katika robo ya kwanza ya mwaka huu huku Zanzibar ukikua kwa 5.1% ikilinganishwa na makadirio ya 5.4%. Wachumi waipongeza Serikali ya Rais Samia Suluhu huku wakisema ukuaji huo ni dalili njema inayodhihirisha kuwa nchi imeanza kupona.
Pamoja na hayo katika taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesema pia akiba ya fedha za kigeni imefikia USD 5,092 hadi mwishoni mwa mwezi uliopita, Ukuaji huo wa uchumi umechangiwa na shughuli za kilimo, ujenzi, viuwanda, uchimbaji wa madini na kuimarika kwa shughuli za utalii hali inayoonesha uwezekano wa kufikiwa kwa makadirio ya ukuaji wa uchumi Tanzania Bara na Zanzibar.
Rais wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA), Godvictor Lyimo ameshauri Serikali iwekeze zaidi kwenye kiilimo cha umwagiliaji akisistiza kuwa ndiyo mkombozi wa uchumi wa Tanzania.
Serikali ya Rais Samia Suluhu tayari imeshaanza uwekezaji tayari imekabidhi kwa mkandarasi hekta 3,500 za ujenzi wa bwawa la kilimo cha umwagiliaji la ujazo wa lita milioni 90, kwa TZS bilioni 27, Dodoma. Mradi huo ni kati ya miradi 21 ya umwagiliaji iliyosainiwa mbele ya Rais Samia Suluhu katika Sikukuu ya Nanenane.