'Uchochezi' wa CHADEMA umefikia kubaya...

'Uchochezi' wa CHADEMA umefikia kubaya...

mlichochea kina mgaya yakapita
mkachochea wanafunzi wa vyuo vikuu yakapita
mkachochea wamachinga wa mbeya mkayamaliza
mmechochea wakulima wa korosho tukawapuuza,bado hamkuchoka mkaendelea kuchochea madaktari na walimu.
Sasa mmefika kubaya kwa kuchochea waislamu wagomee sensa.
Wasira alishawaonya bado hamusikii tu!

Naona sasa hivi mmejikita katika kuwachochea wananchi wa vijijini eti mwaita M4C...hebu tuacheni tupumue kidogo jamani ah!
unakasura kazuri we mama unapatikana wapi nikupigie misele?
 
Mkuu

Kwenye post yako umezingatia vigezo gani kuwapambanisha chadema na waislamu.

Waislamu ni waumini wa dini ya kiislam wakimfuata Mtume mohamad (SAW)

Chadema ni chama cha kisiasa chenye lengo la kushika dola kwa maana ya kuwasimamia na kuwaongoza watanzania

wote (waislam, wakristu, wahindu na wote wasioamini na kuamini) katika kujitawala na kujiletea maendeleo kwa misingi

ya usawa kama ilivyo ndani ya sheria mama KATIBA.


Hivyo chadema ni chama cha kisiasa na si kiimani ndiyo maana kuna Prof Safari, zito na wengineo ambao ni waislamu je hawa nao wanafanya fujo au sio waislamu hao ni chadema?

Nilichomaanisha ni wafuasi wa chadema na wa dini ya kiislam(baadhi)
 
Nilichomaanisha ni wafuasi wa chadema na wa dini ya kiislam(baadhi)

Ok nimekuelewa mkuu.

Lakini tumeshuhudia pia ccm na vurugu kubwa, kupigana -Dar, kupanda majukwaani na bastola-Igunga, kutishiana bastola-Nzega nk.

A. Unawatofautisha vipi hawa na wale waliouwa

1. mwandishi wa habari kule iringa (wauwaji-polisi)?

2. wanachama wa chdema pale arusha (Wauwaji-Polis)?

3. Polisi kule zanzibar (wauwaji uamsho)?

4. Ali zona pale morogoro (wauwaji-Polisi)


B. katika mauaji yote hayo chadema imeuwa wangapi?

Hata vivyo hakuna uhusiano wowote kati ya vurugu zinazoendelea na chama cha chadema. Ukiyajibu maswali hayo hapo

juu vizuri utagundua hilo na kwamba chadema hata siku moja sio chama cha kiimani wala hakihubiri injili au

uislamu
na wala hakifanyi fujo majibu utayapata kwenye maswali hapo juu. (ndiyo sababu nikakuuliza umetumia

vigezo gani? kuilinganisha chadema na uislamu maana kati ya wanachama wazuri wa chadema ni

waislamu)
 
Sasa tena mmeenda wapi ilituwaelimeshe wale wachache wasio ijuwa chadema endeleeni kuhoji bwana..................uda na Kim
 
Tatizo ni kama vile Mch. Msigwa alivyosema bungeni wakati wa mjadala wa bajeti. "kuruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa" "Profesa akisimama bungei ni sawa na mtoto wa darasa la pili".

Matatizo ya nchi hii hayawezi kutatuliwa na watu wenye kusema kwa kujipendekeza kwa walio madarakani ili wapate vijifavour fulani fulani.

Kwa kuyabaini matatizo kiukweli na kuondoa woga ndipo nchi hii itapiga hatua kimaendeleo na kidemokrasia. Waliopo madarakani ndio wametufikisha hapa. HUO NDIO UKWELI. "You guys are tired." Hayo ni maneno ya Msigwa na ninayaunga mkono kwa 100%.

Kulaumu CHADEMA kwa kila ovu ni ufinyu wa uwezo wa kufikiri, uvivu wa kutumia akili tulizopewa, na ni ukasuku ambao unakaribia dhambi kwa dini zote. Nchi hii inahitaji ukombozi wa fikra na mitazamo. Katika kijitabu chake kidogo sana" Tujisahihishe", Rais J K Nyerere alilani sana tabia ya kutoa majibu rahisi kwa matatizo makubwa.
 
Huu ni mtazamo wa wavvu wa kufikiri, na umethbitisha hapa jamvini kuwa ww n mvivu wa kufikiri Mwalimu tangu 2007 walitishia kugoma, madaktar tangu 2001 wanagoma. Je ilikuwa ni chadema au kwa sababu chadema wamevunja ngome za magamba. Au n wafanyakazi kuchoka dhuluma kwa sababu wakubwa wanafaidika wao wanaumia.

na kuuunga mkono mkuu, kwasababu haya mambo ya kugoma hayajaanza jana wala juzi yapo kitambo sana. sasa ninashangaa kuskia haya, mmh!! kazi kweli.
 
kwaiyo tukusaidieje kama nahuko wamechochea?

Huku Tabora nasikia nako CHADEMA wamewashawishi TUME YA KUKUSANYA MAONI isifike baadhi ya maeneo (kata) kisa kuna watu wengi wenye uelewa hivyo watasababisha kupinduliwa kwa mkuu wa kaya. maeneo hayo ni pamoja na kata ya Ipuli ambayo ina wastaafu wengi ambao si wazawa wa Tabora.
 
yani hata museme CHADEMA ni wachochezi, ukweli vijana wengi tumechoshwa na siasa uchwala za magamba. CHADEMA ndio kimbilio letu wanyonge, ccmkweli inawenyewe nakushanga wewe au ni mtoto wa KINGUNGE
 
nadhani wananchi wanaanza kutambua kuwa amani inaweza kuvurugwa na ccm kwa kutumia wachochezi amabao ni wanaccm au wenye uhusiano na ccm.
 
Wamechochea UWT kumkamata Mr Farid
Wamechochea CCM kumuangusha Mrs Malecela.
 
'mlichochea' kina mgaya yakapita
'mkachochea' wanafunzi wa vyuo vikuu yakapita
'mkachochea' wamachinga wa mbeya mkayamaliza
'mmechochea' wakulima wa korosho tukawapuuza,bado hamkuchoka mkaendelea kuchochea madaktari na walimu.
Sasa mmefika kubaya kwa 'kuchochea' waislamu wagomee sensa.
Wasira alishawaonya bado hamusikii tu!

Naona sasa hivi mmejikita katika kuwachochea wananchi wa vijijini eti mwaita M4C...hebu tuacheni tupumue kidogo jamani ah!

hebu ona sasa haya ya uamsho na shekh Ponda!

Uda, kajipange upya.....Uamsho na Chadema wapi na wapi.......maji ya kijani uliyokunywa, shauri yako.
 
Uda, kajipange upya.....Uamsho na Chadema wapi na wapi.......maji ya kijani uliyokunywa, shauri yako.


Nasisitiza : Chadema kweli wachochezi;

Wamechochea moto wa kuwafichua mafisadi kupitia EPA, DOWANS,RICHMOND na kadhalika
Wamechochea moto wa kupiga kelele kuhusu kodi za wananchi zinazotumika ktk safari za rais zisizo na tija
Wamechochea moto wa kufundisha elimu ya uraia mijini na vijijini ambako kwa miaka 5o ya uhuru hawakuwahi kuijua.
Wamechochea moto wa kupambana na rushwa katika taasisi zaote za serikali
Wamechochea moto wa kumpigania mwananchi ili serikali yake iweze kumjali
Wamechochea moto wa kuinyang'anya CCM majimbo yote nchini kupitia vuguvugu la mabadiliko.
Wamechochea moto wa kuwaelewesha wananchi kuhusu utoaji maoni katka mchakato wa kuunda katiba mpya
Chadema ni wachochezi wakubwa.............................Wamechochea na bado wanaendelea kuchochea
Wamechochea moto ili watumishi wa umma kama vile waalimu waongezewe mishahara
Moto umechochewa na Chadema wa kuwaelewesha askari wote umuhimu wa kukipa chama sapoti
Wamechochea moto amani kwa nguvu ya mabadiliko kila kona ya nchi walipokwenda
Wamechochea moto wa "mwenge"kurudi jumba la makumbusho kwani bajeti yake ni kubwa na ni kodi ya mwananchi.
Wamechochea moto wa kusema ukweli bungeni kuliko ilvyowahi kuwa kabla na baada ya uhuru
Wamechochea moto wa kuwafanya vijana wawe na hamasa ya kuipenda siasa na kulitumikia taifa.
Wamechochea moto wa kuwaelewesha watanzania ni kwanini Mwl JK hakuwahi kuvaa suti ya kijani
Wamechochea moto hadi ugali umeiva sambamba na mboga, na kuvifanya kuwa tayari kuliwa kwa pamoja.
Wamechochea moto wa gesi kuibana serikali kutowaibia wananchi mafao yao kupitia kanuni ya 55yrs na 60yrs.
Wamechochea moto wa kuwa wavumilivu hata pale wanapoonewa na serikali bila ya kulalamika.
Wamechochea moto wa kunyakua majimbo sugu ya CCM
Wamechochea moto wa Vua Gamba, Vaa Gwanda, operesheni iliyovunja rekodi ya mafanikio.
Wamechochea moto wa kuukataa udini, na badala yake kutoa tamko kwamba Sheikh Ponda anastahili dhamana.
Moto moto moto moto huu wa CDM umechochewa kwelikweli na wala hautazimika hadi 2015.
Unaweza endeleza aina zote za moto ambazo sikuzitaja...................................!!
 
Huu ni mtazamo wa wavvu wa kufikiri, na umethbitisha hapa jamvini kuwa ww n mvivu wa kufikiri Mwalimu tangu 2007 walitishia kugoma, madaktar tangu 2001 wanagoma. Je ilikuwa ni chadema au kwa sababu chadema wamevunja ngome za magamba. Au n wafanyakazi kuchoka dhuluma kwa sababu wakubwa wanafaidika wao wanaumia.

CDM inaupport MFUMO KRISTO CAF mfumo islam na CCM MFUMO UFISADI
 
UDA dada yangu mpenzi wewe ni mtafiti muhimu sana katika nchi yetu. Zile fedha za utafiti zilizotengwa kwenye bajeti waweza kupata hata nusu yake!

Hivi! ili nionekane CDM lazima niwe mbishi wa kukubali kila kitu wanachosema viongozi wa CDM?' ukiwa na fikra mbadala basi wewe CCM tena unatukanwa kuwa msaliti? tupo zaidi ya milioni 40 . hatuwezi wote kufikiri kama mnanvyotaka.mnaojiita CDM acheni matusi jadilini hoja.Nchi hii ni yetu sote.Ukombozi tunaoutaka ni ukombozi wa fikra mpya.
 
Huu ni mtazamo wa wavvu wa kufikiri, na umethbitisha hapa jamvini kuwa ww n mvivu wa kufikiri Mwalimu tangu 2007 walitishia kugoma, madaktar tangu 2001 wanagoma. Je ilikuwa ni chadema au kwa sababu chadema wamevunja ngome za magamba. Au n wafanyakazi kuchoka dhuluma kwa sababu wakubwa wanafaidika wao wanaumia.

mkuu naona hapa umekurupuka. nahisi hujaelewa hiii thread na ujumbe uliopo. jamaa kaandika kifalsa zaidi. usije ukajikkuta wewe ndio mvivu wa kufikiri na hata kuelewa.
 
Back
Top Bottom