Uchawi upo jamani tukazane kumuomba Mungu

nganilevanu

Member
Mar 13, 2019
35
70
Kiukweli toka nazaliwa, nilikua nasikia haya mambo ya kurogwa yaan mtu anaamka amechoka mara amechanjwa chale usiku lakini nilikua nafikiri ni story za kufirika, ingawa hata nilipokuwa naishi na wazazi wanasimulia kua wanaota ndoto za ajabu, lakin bado mimi sikuamin haya mambo.

Lakni safari hii yamenikuta mwenyewe.. ipo hivi kunanyumba naishi mimi na mke wangu na mtoto wangu hii nyumba ni yakupanga nimeishi toka mwaka 2019 mpaka sasa huu ni mwaka wa 5 sasa. Hapo nyuma mambo yalikua freshi hakukua na shida yeyote. Lakin kuanzia mwaka huu mwezi wa 3 ndo kimbembe kikaanza mara wife usiku anaota ndoto za ajabu mara mimi ndoto za ajabu. Ikifika saa 7 usiku unasikia kitu kabisa kimetua kwa nguvu kwenye bati , hata usingizi unakata afu iki kipindi nilianza kuogopa mpka panya maana hiki kipindi yanatokea maluweluwe kulikua na panya mkubwa sana anakoloma yaani kama usiku alikuwa anapiga kelele mpaka tukawa tunajifariji kuwa anataka kuzaa lakini wapi maana hakuzaa chochote mpaka mwezi ukaisha.

Nanilihangaika hiki kipindi cha mwezi mzima kumuua huyu panya lakini ilishindikana nilitumia mitego aina kama 4 lakini ilishindikana na huyu panya majirani walikuwa hata hawamuoni mimi nalalamika kuwa kuna panya mkubwa humu ndani. Kumbe anaishia kwangu tu kwa majirani haendi.

Kumbwa kuliko kunasiku ilikua saa 11 alfajiri kumbukumbu zangu nilikua katika ndoto lakni cha ajabu nilipigwa na kitu ambacho mpaka leo sielewi ni nini maana nilishituka nilipiga kelele mke wangu naye akashituka namwambia nimepigwa na kitu nikaamka palepale kabla mkono wangu haujavimba nikawasha taa sikuona chochote.

Lakni baada ya muda mkono wangu ulivimba sana na michubuko kama mitano. Kiukweli sikuweza pata usingizi tena maana tayari kulikua kunapambazuka. Ilipofika asubuhi nikiwajurisha wa zazi wangu maana wapo kijijini. Mama angu nimlokole akaniombea pia akanipa namba ya mtumishi ambae yupo mjini nako ishi mimi anifanyie maombi pia.

Nashukuru mungu ile hali ya usiku kujakitu kwenye bati kikatoweka. Na yule panya akajichanganya tukamuua kwa virungu. Lakin kama mwezi usiku nilikua nakosa usingizi kabsa mimi na simu usiku mpaka asubuhi mpaka nilivokuja kuzoea badae.

Lakini napenda kuwakumbusha ndugu zangu tujitahidi tunavoenda kulala tujitahidi kumuomba mungu alinde maisha yako na ya familia yako maana hii dunia inamambo mengi ya giza ambayo kwa macho yako ya nyama huwezi ona kitu chochote.
 
Fungulia redio station za dini usiku watumishi wanakemea mapepo usiku kucha, wakisikia jina la Yesu limetawala kwako watasepa tu.

Nunuwa chumvi ya mawe hata pakti NNE weka mezani nyingine uvunguni nyingine chini ya mto.

Hizi ndio Simple codes za kuwakimbiza wachawi bila kutumia ndumba.
 
Pole sana mkuu, mda mwingine hauwezi amini kama haijatokea miujiza kama hyo.

Tatizo uko mbali sana na MUNGU, na imani yako bado ipo chini kwani wenye imani ni ngumu mno kusumbuliwa na hvyo viwatu.

Rejea kwenye ibada, funga na kuswali sana na MUNGU atakutakasa.

#Amiin
 
Fungulia redio station za dini usiku watumishi wanakemea mapepo usiku kucha, wakisikia jina la Yesu limetawala kwako watasepa tu.

Nunuwa chumvi ya mawe hata pakti NNE weka mezani nyingine uvunguni nyingine chini ya mto.

Hizi ndio Simple codes za kuwakimbiza wachawi bila kutumia ndumba.
Nishajua Udocta wako ni wanini hongera ..
 
Kiukweli toka na zaliwa, nilikua nasikia haya mambo ya kurogwa yaan mtu anaamka amechoka mara amechanjwa chale usiku lakini nilikua nafikiri ni story za kufirika. ingawa hata nilipokuwa naishi na wazazi wanasimulia kua wanaota ndoto za ajabu, lakin bado mimi sikuamin haya mambo.

Lakni safari hii yamenikuta mwenyewe.. ipo hivi kunanyumba naishi mimi na mke wangu na mtoto wangu hii nyumba ni yakupanga nimeishi toka mwaka 2019 mpaka sasa huu ni mwaka wa 5 sasa. hapo nyuma mambo yalikua freshi hakukua na shida yeyote. Lakin kuanzia mwaka huu mwezi wa 3 ndo kimbembe kikaanza mara wife usiku anaota ndoto za ajabu mara mimi ndoto za ajabu. Ikifika saa 7 usiku unasikia kitu kabisa kimetua kwa nguvu kwenye bati , hata usingizi unakata afu iki kipindi nilianza kuogopa mpka panya maana hiki kipindi yanatokea maluweluwe kulikua na panya mkubwa sana anakoloma yaani kama usiku alikuwa anapiga kelele mpaka tukawa tunajifariji kuwa anataka kuzaa lakni wapi maana hakuzaa chochote mpka mwezi ukaisha.

Nanilihangaika hiki kipindi cha mwezi mzima kumuua huyu panya lakini ilishindikana nilitumia mitego aina kama 4 lakini ilishindikana na huyu panya majirani walikuwa hata hawamuoni mimi nalalamika kua kuna panya mkubwa umu ndani. Kumbe anaishia kwangu tu kwa majirani haendi.

Kumbwa kuliko kunasiku ilikua saa 11 alfajiri kumbukumbu zangu nilikua katika ndoto lakni cha ajabu nilipigwa na kitu ambacho mpaka leo si elewi ninini maana nilishituka nilipiga kelele mkewangu nae akashituka namwambia nimepigwa na kitu nikaamka palepale kabla mkono wangu haujavimba nikawasha taa sikuona chochote
Lakni baada ya mda mkono wangu ulivimba sana na michubuko kama mitano.
Kiukweli sikuweza pata usingizi tena maana tayar kulikua kunapambazuka. Ilipofika asubuhi nikiwajurisha wa zazi wangu maana wapo kijijini. Mama angu nimlokole akaniombea pia akanipa namba ya mtumishi ambae yupo mjini nako ishi mimi anifanyie maombi pia.

Nashukuru mungu ile hali ya usiku kujakitu kwenye bati kikatoweka. Na yule panya akajichanganya tukamuua kwa virungu. Lakin kama mwezi usiku nilikua nakosa usingizi kabsa mimi na simu usiku mpaka asubuhi mpaka nilivokuja kuzoea badae.

Lakini napenda kuwakumbusha ndugu zangu tujitahidi tunavoenda kulala tujitahidi kumuomba mungu alinde maisha yako na
Ya familia yako maana hii dunia inamambo mengi ya giza ambayo kwa macho yako ya nyama huwezi ona kitu chochote.
Nyumba umepanga?kama ndio hama hapo haraka
 
Fungulia redio station za dini usiku watumishi wanakemea mapepo usiku kucha, wakisikia jina la Yesu limetawala kwako watasepa tu.

Nunuwa chumvi ya mawe hata pakti NNE weka mezani nyingine uvunguni nyingine chini ya mto.

Hizi ndio Simple codes za kuwakimbiza wachawi bila kutumia ndumba.
Chukua Rose water + chumvi ya mawe ombea hiyo mix nyunyuzia kila siku kwenye mipaka ya nyumba yako au ndani mwako usiku wakati wa kulala kunywa kifuniko kimoja cha Rose isiyo na chumvi
 
Fungulia redio station za dini usiku watumishi wanakemea mapepo usiku kucha, wakisikia jina la Yesu limetawala kwako watasepa tu.

Nunuwa chumvi ya mawe hata pakti NNE weka mezani nyingine uvunguni nyingine chini ya mto.

Hizi ndio Simple codes za kuwakimbiza wachawi bila kutumia ndumba.
Yaani kama umejua kipindi yamenikuta majanga nilikua nawasha redio za maombi ucku
 
Kwanini huyo Mungu ni mpaka aombwe ndo awalinde? Anakuwa hajui? Au anajua anatakiwa kuwalinda watoto wake ila hataki tu,kama hataki ni ana upendo wote kweli? Alafu huo uchawi na nguvu za giza si kaziumba yeye?(nime assume kwamba uchawi upo),ila kwenye story yako sijaona huo uchawi zaidi ya wenge lako mwenyewe.
 
Fungulia redio station za dini usiku watumishi wanakemea mapepo usiku kucha, wakisikia jina la Yesu limetawala kwako watasepa tu.

Nunuwa chumvi ya mawe hata pakti NNE weka mezani nyingine uvunguni nyingine chini ya mto.

Hizi ndio Simple codes za kuwakimbiza wachawi bila kutumia ndumba.

Upumbavu, I declare interest: Mimi nimeokona, namwamini Yesu, lakini ulichoandika ni upumbavu, Hakuna mahusiano kati ya chumvi na Yesu.
 
Back
Top Bottom