Uchawi uchawi uchawi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,298
33,083
ucha.jpg

MWANAMKE huyu ambaye hakufahamika jina lake amekutwa katika mazingra haya jana alfajiri maeneo ya Ilomba Jijini Mbeya akiwa kama alivyozaliwa, Inadaiwa kuwa mwanamke huyu ni mmoja wa wanafunzi wa chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU).

Wananchi walikusanyika katika eneo alipokutwa mwanamama huyu ambapo inadaiwa kuwa alikuwa akiwanga nyakati za usiku lakini akakutana na wababe wa Ulozi mitaa hiyo ndipo aliposhindwa kuendelea na ulozi wake na kujikuta akikosa nguvu na kushindwa kuendelea na safari yake ya ulozi hadi alipokutwa asubuhi kweupee!!!

Inaelezwa kuwa eneo hilo ni maarufu kwa kukamata watu wanaoingia anga hizo kwa ajili ya kufanya ugagula ambapo miezi michache iliyopita mtoto mdogo wa kike naye alibambwa akitaka kufanya ulozi na kukutwa na umati wa watu kabla ya kufanya ulozi wake.

Mwanamke huyu aliokolewa na askari polisi ambao walimchukua moja kwa moja hadi kituoni kwa ajili ya kuhifadhiwa ili asipate madhara zaidi.Jitihada za kukutana na uongozi wa chuo kikuu cha TEKU zinaendelea ili kujua kama mwanamke huyu alikuwa ni mwanafunzi wa chuo hicho kama inavyoelezwa na watu ama la.

Mbeya Yetu: UCHAWI UCHAWI UCHAWI

Wabongo mumezidi imani za kishirikina Mtu akiwa yupo uchi basi ni Mchawi njooni huku ulaya muone Wazungu

wanavyotembea Uchi mutasema hawa Wazungu wote ni wachawi? Ahhhhh mimi nimechoka na tabia za Kibongo

Tembeeni muone watu wanavyoishi jamani Wabongo nyie amkeni............ Acheni Usingizi........... Huy mwanamke

anaweza kuwa ni mgonjwa wa akili basi akitembea uchi mtasema ni Mchawi ahhhhhhhhhhhhh Wabongo ndugu Amkeni....
 
Ashukuru aliachiwa uhai. Hali hii inaashiria kutojitambua baada ya ulevi mwingi wa pombe na madawa ya kulevya. Pia pengine kakutwa na wahuni wakamfanyia vibaya. Naanini alipelekwa hosiiptali kwa uchunguzi. Ikiwa ni mwanafunzi wa chuo hatua za kinidhani zichukiwe dhidi yake kwa kudhalilisha chuo husika.
 
Mh! Kuna walevi wa utamaduni wa Ulaya humu wanadhani kutembea uchi ni jambo jema hivyo wanakupigia debe. Mama yako anatembea uchi? Ulaya watu tumeenda na wengine wameenda tangu 1930s-40s msibabaishe watu kutuaminisha kuwa kutembea uchi deal. Waje Ulaya kuangalia watu wanavotembea uche halafu iweje? Ala!
 
mimi mwenyewe nilikuepo kwenye tukio hili kwa taarifa tu huyu mdada hakuwa mchawi bali ni mgonjwa wa akili aliondoka kwao usiku wa manane na kukutwa kwenye nyumba ya mtu ambayo ipo karibu na soko linaitwa mwambene kata ya Ilomba mbeya wakazi wa eneo hilo walijua mchawi bali alikuwa mgonjwa baada ya majirani na ndugu zake kuthibitisha hilo na ameitimu TEFILO KISANJI UNIVERSITY 2008/2011 Kilichopo mkoani mbeya.
 
Afu mzizimkavu nikuulize, hivi ukichana newel vizuri na kujipaka lotion na perfume, ukienda kuwanga itagoma? Manake naonaga picha za wachawi wanakuwa hawajachana nywele na wamepaukaaa
 
Afu mzizimkavu nikuulize, hivi ukichana newel vizuri na kujipaka lotion na perfume, ukienda kuwanga itagoma? Manake naonaga picha za wachawi wanakuwa hawajachana nywele na wamepaukaaa
Itagoma kuwanga kuna sheria zake Sio kila Mtu anaweza kuwanga la hasha Wanga wana Sheria

zao za kiuchawi ukitaka kuwa Mwanga lazima uzifuate hizo sheria ya kwanza uweze kumtowa Mwanao au ndugu yako au

mzazi wako unayempenda kikowa ili Wanachama Wenzako wamle nyama ndipo unapopata wewe cheo kuwa na wewe una

sauti kwenye hicho chama cha uwanga kazi kweli ipo kwa hawa ndugu zetu Wanga King'asti
 
Last edited by a moderator:
mimi mwenyewe nilikuepo kwenye tukio hili kwa taarifa tu huyu mdada hakuwa mchawi bali ni mgonjwa wa akili aliondoka kwao usiku wa manane na kukutwa kwenye nyumba ya mtu ambayo ipo karibu na soko linaitwa mwambene kata ya Ilomba mbeya wakazi wa eneo hilo walijua mchawi bali alikuwa mgonjwa baada ya majirani na ndugu zake kuthibitisha hilo na ameitimu TEFILO KISANJI UNIVERSITY 2008/2011 Kilichopo mkoani mbeya.
Mkuu Luiz Kama ni kweli ni mgonjwa wa akili huyu bibie kwanini hawampeleki hospiatli kumtibia huo ugonjwa wa kail?
 
Last edited by a moderator:
Teofilo Kisanji University is owned by the Moravian Church in Tanzania . Its origin is a Theological College which was established in the early 1960s. In 2004 the Moravian leaders decided to transform the Theological College into a University. The University was granted a certificate of Provisional Registration in April, 2006 and a Certificate of Full Registration in September 2007. In 2010, the University received a signed charter and rules from the President of the United Republic of Tanzania.

Kwa kuwa katokea kanisani lazima waje wapindishe kuwa siyo mchawi.
 
Usipogusia udini huwa hufurahi!Kazi unayo mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom