Uchawi nadhani ni neno la kiswahili linalojirudia sana mpaka linakera
Ila yawezekana ni kwa ufinyu wa lugha kugusa maana halisi
Binasfi nikisikia neno uchawi akilini inakuwa mbali na mazoea ya kusikia neno lenyewe tena na tena mpaka linachosha.!
Mf kwetu afrika kulingana na masimulizi yenye kujirudia imefikia mtu akisikia neno uchawi mara nyingi anawaza hirizi na wanga matako wazi.!
Ila kama kweli unalengo la kulielewa neno uchawi vizuri lazima ujiweke mbali na attachment za kiswahili
Vile mtu hujiwazii kuwa chochote duniani zaidi ya vile wewe ulivyo
Mfano ni muhimu kujiweka kwa unganishi wa maisha na kujiona huna tofauti na wengine.. Ila ajabu maisha hayakubali kivitendo jambo hili zaidi ya nadharia tu
Namaanisha kujua neno uchawi asili yake kulianza kwa sababu ya watu kujiwekea madaraja na hadhi
Mpaka watu wakatafuta maana ya mtu kukosa na kudhalilika mpaka kufa huku wengine bila jitihada wakihodhi mpaka kufa kwao na vizazi vyao
Ni rahisi kujibu ni hila za mifumo ya kiutawala ila undani wake ni zaidi ya uhalisia
Itoshe kusema Kuna nguvu nje ya ufahamu wa kawaida inahusika kusukuma gurudumu la maisha