1: Ujuaji na kujifanya unajua elimu ya fedha. Kama zilivyotaaluma nyingine elimu ya fedha huwezi kuijua automatikali. Unatakiwa ujifunze in/out.
2: Akili kutawaliwa na Mitazamo ya kijadi. Nenda shule/Chuo uajiliwe. Ukikosa ajira unakaa hadi ije. Ndani ya miaka miwili ya kusubiri akili inakuwa imejaa mabuibui, ukungu na magugu ya ujinga.
3: Akili zimazofikilia kutumia muda wote badala ya kuzalisha. Tulikuwa na wachimbaji wadogo mahala flani wote ukiwauliza ikitokea wamepata dhahabu wanasema wanaenda brekibya kwanza Dubai kutumia.
4: Kutegemea Siasa au mabadiliko ya Chama tawala ndio yalete mafanikio yao binafsi. kuna matajiri wengi licha ya hali ya kisiasa kuwa mbaya hadi jana US imeiweka kwenye list ya nchi hatari duniani raia wake kuishi. Unaweza kutajirika ukiwa hata Afganstan hata Somalia. Sio lazima CCM itoke madarakani ndio utoboe. Hizo ni njozi za wapinzani sio raia anayejitafuta.
5: Kuoa mwanamke mgomvi. Maandiko yanasema ni afadhali kukaa mwenyewe jangwani kuliko kukaa na mwanamke mgomvi. Kwenye magomvi kumejaa mapepo ya umasikini na utapanyi. Akili mbili zilizopatana zikiamua lao na kiwa siriasi hakuna cha kuwashinda.
6: Kuwa na imani kubwa na Allah na Mungu wa kikristo na kushindwa kuihamishia imani hiyo kwenye utafutaji. Huwezi kumuamini Mungu anayejinasibu ni Tajiri na anayemiliki mali zote alafu ukabaki masikini. Wengi wamejagua imani iwafanye kuwa watu wema masikini, wafikirie mbinguni/peponi na kwenda kusali na kushindwa kucapitalize imani hiyo kwenye utafutaji.
7: Hofu ya kufa. Maombi ya ulinzi mtu anaposafiri bongo ni mengi kuliko ulaya ambako uwezekano wa mtu kufa kwenye bodaboda au gari ni mdogo. Hii imepelekea kuwa na vikundi vingi vya kufa na kuzikana badala ya vikundi vya kupeana mitaji na madili ya maana. Pia mtu akijua anaweza kufa muda wowote anakoswa morali ya kusaka mali.
8: Uoga wa kwenda sehemu mpya. Kama miaka ya 50 mtu alitoka Canada hadi Mabuki misungwi kutafuta Almasi [ Williamson ]. Wewe Kutoka Mwanza tu kwenda Misungwi porini au Kwenye mgodi mkubwa kuliko zote Afrika Sengerema Nyanzaga angalau uangalie Fursa unataka hadi uwe unamjua mtu huko au upewe kibali na ukoo. Mara unaogopa kuumwa na nyoka, mara kurogwa. Vasco Da Gama angekuwa na hizo akili asingesafiri siku 317 kwenda India kununua viungo, piripiri na urojo akiwa hamjui mtu huko.
9: Kuamini Uchawi na Ushirikina kuliko Mungu. Yaani hadi watu wa dini wanaamini Mungu yupo lakini ikija suala la kurogwa kwenye utafutaji Mungu wao hana kazi wala msaada. Uzembe, kutokujua mbinu, ukosefu wa uvumilivu na uvivu binafsi vyote excuse unapewa uchawi. Wachina wanaenda hadi Congo hawalogwi. Kama unaamini uchawi sana basi utumie huohuo uchawi ukusaidie kuliko kubaki unaupromote. Hata Mungu anasema ni afadhali uwe baridi au moto. Mchawi au mwanamaombi.
10: Story nyingi za uongo kuwa kuna mtu flani alikuwa wa kawaida ghafla akapata dili kubwa akawa tajiri. Utajiri ni bahati, utajiri ni nyota. Wengi wanafanya mambo kinyonge wakidhani ipo siku itatokea zali la mentali watoboe ghafla. Ndio maana kundi kubwa la vijana linaimani ya kutoboa kwa kubet kuliko michakato.
Naomba kuwasilisha.
Mjumbe hauwawi, haya nimeyapata katika kutafakari mstakabali wa umasikini wangu binafsi.