Uchambuzi wa nyota kila siku

Uchambuzi wa nyota kila siku

NYOTA YAKO LEO ALHAMIS JULAI 24/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Leo kuwa karibu na jamaa zako wape mawazo yako na waombe wakupe ushauri kutokana na changamoto zinazokukabili watakusaidia.

•Mahusiano yako yapo vizuri ila mtu mpya uliyenae kwa sasa yupo kwako kwa maana ya kimaslahi hana madhara ya nuksi kwako au matatizo dhidi yako ila usimuamini sana unaweza kulia msimu ambae yeye ndio anakucheka.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Leo Hutaweza kuyatatua matatizo yako peke yako unahitaji msaada wa watu wengine bila msaada hakuna mafanikio.

•Safari zako ni nzuri na zina kheri nyingi kwako moyo ukikataa kutoka ghairi panga siku nyingine na lolote unalolitilia shaka ni kweli lizingatie lina umuhimu kwako hata ukijikwaa usichukulie rahisi ipo maana yake.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Leo yafanyie kazi mambo ambayo watu wanayasema jambo la muhimu kwako ni kuwa muangalifu Kuna bahati kubwa mbele yako inakuja.

•Kazi zako ni nzuri na zipo katika hali nzuri licha ya maneno maneno lakini hakuna madhara yoyote dhidi yako kwa sasa kutokana nguvu kubwa inayokulinda kutokana na kikubwa ulichokitoa miezi kadhaa iliyopita unasimamiwa mengi na vingi hivyo jivunie kuwa salama.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Leo itajikuta unakumbana na usumbufu wa hapa na pale katika utekelezaji wa majukumu yako hali hiyo isikutishe mwisho utafanikiwa.

•Kazi zako ni nzuri na zipo katika hali nzuri licha ya maneno maneno lakini hakuna madhara yoyote dhidi yako kwa sasa kutokana nguvu kubwa inayokulinda kutokana na kikubwa ulichokitoa miezi kadhaa iliyopita unasimamiwa mengi na vingi hivyo jivunie kuwa salama.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Leo kuna mvurugano na kutokuelewana kutakaozuka kati ya wewe na wenzako au washirika wako dhamira yao ni kukudhulumu haki yako au kukutapeli lakini hawatofanikiwa.

•Mahusiano yako yatakuwa na utulivu na leo utasikilizwa zaidi na mwenzako jitahidi kutumia zaidi busara kuliko nguvu inaweza kukujengea kinyongo kibaya kwa mwenzako na ukashindwa kufanya mengine ya kimaendeleo kutokana na kinyongo chake.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Leo utajikuta umo katika hali nzuri na ya kufurahisha muda wa jioni baada ya kupata habari nzuri zitakazokufurahisha ungana na watu wako kufurahia habari hizo.

•Mahusiano yako yataingia vurugu na uadui mkubwa ndani yake lakini yote yanapita utulivu utarejea baada ya mmoja wenu kujishusha au kubadilika.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Leo utapata Baraka nyingi na furaha tele jaribu kufanya mambo yako kwa ukamilifu wala usiwe na papara mambo yaende kwa mpangilio maalum.

•Mahusiano yako yataingia vurugu na uadui mkubwa ndani yake lakini yote yanapita utulivu utarejea baada ya mmoja wenu kujishusha au kubadilika.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Leo tengeneza maisha yako yaweke pembeni mambo ambayo unayaona hayana maana Maisha yako ni muhimu sana kwako kuliko jambo lolote.

•Mahusiano yako hayapo sawa ila kwa sasa usiyape kipaumbele kwakuwa sio muda wake sahihi kuyahimili kwakuwa hayawezi kutengemaa kwa sasa hivyo angalia mambo yako ya kiuchumi kwa sasa hayo tatengemaa yenyewe.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Leo zungumza kwa kina mambo yaliyo moyoni kwako kwa watu unaowaamini ili upate suluhu hali hiyo itakuwa majawabu kwa matatizo yanayokukabili Kuwa muwazi na utafanikiwa.

•Kazi zako zinaonekana kuwa na mashaka mengi na kelele za hapa na pale lakini yote yanaonekana yataenda vizuri baada ya muda.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Leo ni siku nzuri na yenye baraka sana kwako tumia siku ya leo kufanya mambo yako mwenyewe yale yote ambayo unayaona ni ya muhimu.

•Utapata habari njema leo na mambo ya kukufurahisha haja zako zitatimia kwa namna usiyoitarajia na wepesi mkubwa utaupata kwenye mambo yako.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Leo jizuie kushiriki katika ubishani wowote ni afadhali uonekane mjinga kuliko kushinda ukiwa hasira Kumbuka Hasira hasara.

•Kazi zako zitaenda vizuri na kwa wepesi mkubwa zaidi pia utanufaika kwenye biashara zako au utaona faida leo na biashara itakuwa nzuri.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Alhamisi ya leo Shirikiana na mtu yoyote unayemtaka unaweza kupata maarifa ya kufanikisha shughuli zako muhimu ulizonazo kwa sasa hata hivyo kuwa makini.

•Utapata vimaudhi vya hapa na pale asubuhi ya leo na siku itakuwa chachu upande wako tamu si tamu chungu si chungu.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim,niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250629-WA0012(26).jpg
 
IJUE NYOTA YAKO (LEO ♌)
sehemu ya tano

(DOGOLI KINYAMKELA (Dr)


MAELEZO YA NYOTA YA SIMBA (LEO ♌)

Hii ni nyota ya Tano katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Julai hadi 22 Agosti

Asili yao ni Moto .
Sayari yao ni Sun (Jua).
Siku yake nzuri ya bahati ni siku ya Jumapili ,
Namba ya bahati ni 1 na 4 .

Malaika wake anaitwa Michael au Raukayaeel na Jini anayetawala Jumapili anaitwa,
Abdulahi Saeed al Madhhab

Rangi zao ni rangi ya Dhahabu (Gold) Nyekundu (Red) na rangi ya Machungwa (Orange) Watu wote wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi zilizochangamka na zenye kuonyesha utajiri kama Dhahabu na Njano nzito au iliyoiva.

Rangi zinazowapa uwezo wa Mapenzi, Mahaba na Furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Nyeusi, Bluu iliyoiva (Indigo) na Bluu ya Samawi (Ultramarine).

Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni, Njano (Yellow) na Njano-Machungwa.

Kito (Jiwe) ni Amber, Chrysolite, Yellow Diamond, Petrified Wood Garnet, Diamond, Jasper, Quartz na Onyx.

Madini yao ni Gold (Dhahabu). Manukato yao ni Maski (Musk) na Uvumba.

MAMBO MUHIMU:-

Sifa ya Nyota hii ni Uimara na Kutokubadilika.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni Unyenyekevu.

Maadili yao ni Uwezo wa Uongozi, Kujiamini, Ukarimu, Ubunifu na Kupenda raha.

Matakwa yao ni Starehe, Haja ya Kung’ara mbele za watu na Kujikweza.

Tabia za kujiepusha nazo ni Kujisifu, Kiburi na Kuamrisha.

USHIRIKIANE NA NANI?

⭐Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Punda na Mshale.

⭐Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Nge na Ndoo.

⭐Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Ng’ombe.

⭐Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Nge.

⭐Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mashuke.

⭐Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mshale.

⭐Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Ndoo.

⭐Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mshale.

⭐Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Punda na Kaa.

KIPAJI CHA SIMBA:

Simba wana kipaji cha ufunuo wa kiungu , wana uwezo wa kuvumbua mambo ambayo yanaweza kuwaletea fedha pamoja na kwamba hazikai.Wanauwezo vilevile wa kuponya kwa kutumia mikono yao kuponya watu na wanakipaji cha asili cha uongozi. (inspired):

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:

Simba ni watu wanaopenda ufahari mkubwa na kutukuzwa. Wanapenda kutumia na wanataka waonekane kwamba wana hali nzuri, wanapenda sana kuheshimiwa.

Jambo kubwa walilonalo ni uwezo wa kuvumbua mambo ambayo watu wengine hawajui.

Ni watu wakarimu lakini wajeuri na wanapenda sana kuonea watu. Wana hisia kali, ni wakali na wanakiburi.Tabia yao ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanaowapenda.

Furaha haina mpaka katika mapenzi ya Simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza dhahiri wanapompenda mtu. Baada ya hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza.

Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika inakua vigumu sana kuyatengeneza.

Tatizo lao kubwa ni kujisahau Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.

KAZI NA BIASHARA ZA SIMBA:

Wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi zifuatazo; kazi za usimamizi, kama katika kampuni yake binafsi au katika mashirika au biashara, kazi za michezo au uongozi wa michezo.Wanatakiwa wafanye kazi za usonara au kazi za kuuza au kutengeneza mavazi ya mitindo.Vilevile wanatakiwa wafanye kazi za uigizaji au uendeshaji sinema au kazi zozote zinazohusika na masuala ya vijana.Kazi yao nyingine ni ya ualimu katika taasisi, shule au vyuo vya ualimu.

MAVAZI NA MITINDO:

Simba mitindo yao iwe ya kifalme, Kitajiri na inayoashiria nguvu na mamlaka, Kitambaa kiwe cha hariri inayongaa au velvet au kilicho tariziwa, Rangi iwe ya Dhahabu. Mavazi yaambatane na Vito vya dhahabu, Wanawake wapendelee kuvaa magauni ya kutokea usiku yawe ya dhahabu au rangi ya machungwa.

MAGONJWA YA SIMBA:

Nyota hii inatawala moyo, sehemu ya juu ya mgongo na bandama.Vilevile inatawala uti wa mgongo na mshipa mkubwa wa damu Matatizo yao makubwa kiafya yanahusiana na maradhi ya kuumwa sehemu ya juu ya mgongo Maradhi yanayotokana na damu kama shinikizo la damu la juu na chini na maradhi ya moyo.Vilevile wanaugua maradhi ya homa ya uti wa mgongo.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA SIMBA:

Wenye nyota hii wanatakiwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, machungwa, maboga, vitu vichachu kama ndimu au malimao na wapende sana kula nyama za ng'ombe, mbuzi na kondoo. Simba wanatakiwa wakaishi au watembelee nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao. Nchi hizo ni Italia na Morocco na miji ni Bombay (India) na Roma (Italia).

MADINI, VITO NA MAFUSHO:

Madini ya Simba ni Dhahabu. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni kama vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.

Mafusho ya Simba ni Sandarusi unachoma siku ya Jumapili kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

DOGOLI KINYAMKELA (Phd) , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
 
NYOTA YAKO LEO IJUMAA JULAI 25/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Leo hata kama ukikubaliana na mtu yoyote jambo lolote ujue atakwambai usubiri kwanza au atakucheleweshea mahitaji yako kuwa na subira na tumia hekima utafanikiwa.

•Kazi zako zitaenda hovyo leo na unaweza kujiharibia au kuharibikiwa kazi yako leo hivyo kuwa makini kwa kila kitu na usilazimishe mambo leo utapata fedheha.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Pamoja na kwamba leo itakuwa siku nzuri kwa kila jambo lako utakalolifanya unashauriwa kuwa usianzishe mambo mapya endeleza yale ya zamani na utafanikiwa tu.

•Utapata maudhi zaidi leo kwanzia mwili wako na watu wako na mambo yako leo yanaonekana kuwa mazito mazito leo.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Leo kuna uwezekano wa urafiki wako kuvurugika unashauriwa kuwa makini katika kuchagua marafiki wengine watakutaka wewe ili kupata kitu na sio marafiki wa kweli.

•Kazi zako zitaenda vizuri na utapata wateja wapya au boss mpya kwenye biashara yako hiyo.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Leo jaribu sana kuwa karibu na watu wa dini ili uweze kubarikiwa mambo yako Fanya ibada kwa mujibu wa imani yako na toa sadaka kwa watoto yatima maskini na wajane na utafanikiwa.

•Pia utapata marafiki wapya au mpenzi mpya safari zako ni nzuri.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Leo usipokuwa makini unaweza kupoteza vitu vya thamani kubwa kuwa makini katika mambo yako hasa nyie ambao mnaotumia usafiri wa umma katika kufanya safari zenu za hapa na pale.

•Utapata furaha leo na habari njema sana itakufikia leo.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Leo jihadhari sana kujumuika na vikundi visivyofaa hasa nyakati za jioni kama una matatizo yanayokusumbua jaribu sana kuwasiliana na wataalamu ili wakusaidie kuondokana na matatizo hayo hata kupata ushauri.

•Mahusiano yako hayana tatizo kwa sasa haya yaliyopo ni ya kupita tu ugomvi au kelele baina yenu zitaisha.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Leo inaonekanakana kuwa mambo yako yapo hatarini kuharibiwa na watu wengine hasa wale ambao wako katika serikali au katika dini. Unatakiwa kuwa mpole kuwa muda huu ili kupisha dhahama hiyo iondoke.

•Safari zako sio nzuri leo kuna dalili za kupatwa na tatizo njiani litakalokuharibia siku yako leo na kazi zako pamoja na muda wako unaonekana utaharibikia njiani.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Leo jaribu kuwa muangalifu na mtu yoyote ambaye utashirikiana nae katika jambo lolote wengine watataka kukuingiza katika mambo ambayo yatakuletea balaa kubwa na hasara kuwa makini sana.

•Mahusiano yako ni mazuri na utulivu utakuwepo kuhusu mgogoro au ugomvi wa nyuma utaisha na mtaelewana kama awali.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Tumia muda huu kukamilisha mambo yako uliyokuwa umepanga kuyafanya Fanya safari kutana na wadau wa biashara zako na tekeleza wajibu wako kazini Mambo mazuri yanakuja.

•Mahusiano yako hayana tatizo lolote kwa sasa ila kuwa nayo makini na usizuie ugomvi pia usitie masikhara katika maongezi ya mwenzako kwakuwa unaweza kuzua mfaraka kwa maneno yako tu ukasababisha kuharibika kwa mahusiano yako hayo.

★NG'OMBE– GEMINI ♊ (Aprili 21– May 20)

Leo ni siku mbaya kwako kuna uwezekano wa wewe kupata balaa katika mambo yako jaribu sana kuwa muangalifu katika kila jambo ambalo umepanaga kulifanya au la si hivyo unaweza kuharibikiwa pakubwa.

•Mahusiano yako ya kindoa au kimapenzi yatastawi na kupendeza zaidi leo kama una jambo lako kwa mtu wako wa karibu muambie atakusikiliza.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Leo Jitahidi kukutana na wakubwa zako wakusaidie kukupa ushauri bila hivyo itakuwa vigumu kwako kutatua matatizo yako yanayokukabili hasa yale yanayohusiana na mapenzi na ndoa.

•Safari zako ni nzuri hazina shaka yoyote nenda.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Ili kukamilisha mipango yako ni lazima ukutane na mtu mmoja mkubwa akiwa yupo hapa au yupo mbali akusaidie kuondokana na yanayokusibu vinginevyo hakuna mafanikio katika jambo lolote.

•Kazi zako zitaenda kwa uzito uzito na makelele lakini mwisho itakuwa vizuri na manufaa yataonekana.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim,niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250629-WA0012(27).jpg
 
NYOTA YAKO LEO JUMAMOS JULAI 26/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILREKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Leo matatizo mengi ambayo utayaona yakikuandama yatakuwa yanatokana na nuksi au husda kwa upande wako tafuta njia ya kuondoa husda hiyo au nuksi hizo kabla hazijaenea sehemu kubwa Weka mambo yako katika mizania sahihi ili maamuzi yako yawe sahihi na kwa faida yako.

•Mahusiano yako ya kindoa au kimapenzi yatastawi na kupendeza zaidi leo kama una jambo lako kwa mtu wako wa karibu muambie atakusikiliza.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Leo inaonekana Nyota yako itakuletea mabadiliko makubwa na mengi sana katika maisha yako yakitokea hayo yakubali tu aidha yakiwa ni mazuri au mabaya hatimaye utamakinika na utaona fanda ya mabadiliko hayo Ondoa khofu.

•Mahusiano yako ni mazuri na utulivu utakuwepo kuhusu mgogoro au ugomvi wa nyuma utaisha na mtaelewana kama awali.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Umekuwa ukizungukwa na matatizo sasa kwa muda mrefu na leo au jumamos hii ndio wakati hasa wa kuyashughulikia hayo matatizo yako na kuyamaliza Kama ulikuwa una safari nenda itakuwa nzuri au kama una kazi iliyokwama ifanye utafanikiwa kwa sababu bahati iko upande wako.

•Mahusiano yako hayana tatizo lolote kwa sasa ila kuwa nayo makini na usizuie ugomvi pia usitie masikhara katika maongezi ya mwenzako kwakuwa unaweza kuzua mfaraka kwa maneno yako tu ukasababisha kuharibika kwa mahusiano yako hayo.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Inaonekana imekuwa vigumu kwako kuamua mambo Fulani na ukajikuta uko katika njia panda itakayokutenganisha na utajiri na umasikini Hii ni juu yako amua kitu gani cha kufanya katika kufikia malengo yako unayoyataka.

•Utapata maudhi zaidi leo kwanzia mwili wako na watu wako na mambo yako leo yanaonekana kuwa mazito mazito leo.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Leo inaonekana utahitaji ushauri wa dharura na wa kitaalamu ili kuweka mambo yako sawa Kutimia kwa mipango yako uliyonayo wakati huu kunategeme wewe utajihusisha na watu wa aina gani kwa sabau wewe mwenyewe hujiwezi kujisaidia Jitenge na watu wenye mawazo finyu.

•Mahusiano yako yana nafasi kubwa zaidi leo hivyo usipuuze hisia zako lwo zitumie vyema kuimarisha furaha na afya yako.

Safari zako ni nzuri sana leo.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Inaonekana umesitasita kwa muda mrefu sasa katika kufanya maamuzi lakini leo ndio siku hasa ya kufanya maamuzi na kutimiza mambo yako hasa yale yanayohusiana na maisha au mapenzi Usiogope fedheha piga moyo konde iwapo unataka kufaulu katika hayo.

•Kazi zako zitaenda vizuri na utakuwa mwenye bahati zaidi kazini kwako na haja zako kwa upana zitafanikiwa jitahidi kuwaza mambo makubwa zaidi ili kusonga mbele na kuyafikia yale matakwa yako halisi.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Leo kuna bahati kubwa sana itakujia upande wako na utapata mshangao kwa sababu watu wengi watakuchangamkia na watakuwa radhi kukufaa na kukusaidia kuyashughulikia matatizo yako yanayokukabili Fungua Milango na kubali ushauri kwa sababu huwezi kujua bahati hii ya sasa itadumu kwa muda gani.

•Kazi zako zitakuwa na kustawi zaidi kwa ujumla shughuli zako zitakuwa na matokeo chanya nzuri kwako na bahati zako zitaongezeka kwa namna usiyoitarajia.

Safari zako ni nzuri.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Leo kuwa na moyo mkunjufu kwa sababu hali hiyo itakufaa zaidi Utakutana na mtu mgeni na atakutaka muwe marafiki mkubalie kwa sababu utapata faida kubwa kwa hilo Jitahidi kujielekeza kwa mambo mema na usijaribu kusema uongo leo unaweza kuumbuka.

•Utapata sifa au pongezi kwa wema wako kwa watu pia hadhi yako itasikika mahala ambapo hujategemea jina lako litatajwa.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Leo ni siku nzuri sana kwako kutafakari kuhusiana na maisha yako ya baadae yaweke pembeni mambo ambayo unayaona hayana maana kwa sababu maisha yako ni muhimu sana kwako kuliko jambo lolote jingine linalokukabili.

•Utapata maudhi asubuhi ya leo na maudhi ya hapa na pale katika siku ya leo.

★NG’OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Leo jitahidi kujiepusha na marafiki wasio na maana au kujiweka katika sehemu ambazo zina makelele mengi kwa sababu unahitaji utulivu wa hali ya juu katika kutekeleza majumu yako yanayokukabili.

•Ikiwezekana Barizi na umpendae unaweza ukapa ufumbuzi au utatuzi wa shida zako zinazokukabili.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Inaonekana umekuwa ukitumia vibaya fedha zako katika siku za hivi karibuni mpaka umeshindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yako ambayo umejipangia wewe mwenyewe Jaribu sana kujiweka mbali na marafiki wabadhirifu iwapo utataka kufaulu katika maisha yako.

•Kazi zako au shughuli utakazoagiza ufanyiwe leo watafanya kinyume na utaudhiwa sana dhidi ya uwaagizao au unaowaagiza.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Umeonyesha roho ya huruma na kuwa na hisani kwa kila mtu kutokana na tabia yako hiyo watu watakuja mara kwa mara ili uwape msaada kama unavyotoa kwa wengine na wakija wasaidie wala usichoke Kama ikiwa utabadili msimamo basi wajulishe wala usione haya.

•Safari zako leo ni nzito nzito lakini utafika salama.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim,niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250629-WA0012(28).jpg
 
UTAWALA WA SAYARI NA NYOTA YAKO.

( DOGOLI (Dr )


Kila sayari ina nyota yake na namba yake, hivyo mtu anaweza akajikuta anapenda kufanya mambo ya sayari fulani kwa sababu ana namba ya sayari hiyo katika tarehe yake ya kuzaliwa.

Mfano mtu ambae amezaliwa tarehe 9, 18, au 27 ya mwezi wowote anabeba sifa za sayari ya mars, hivyo anajikuta ana haraka kwenye mambo yake, ana hasira za karibu, mpambanaji, lakini pia anapenda sex.

Hapa chini nimeainisha kila sayari na namba yake.

a) Mwezi nyota yake ni nyota ya kaa, namba yake ni 2

b) Sayari ya mercury nyota yake ni nyota ya mashuke na mapacha, namba yake ni 5

c) Sayari ya venus nyota yake ni nyota ya mizani na ng'ombe, namba yake ni 6

d) Sayari ya mars nyota yake ni nyota ya punda, namba yake ni 9.

e) Sayari ya jupita nyota yake ni nyota ya mshale, namba yake ni 3

f) Sayari ya satani nyota yake ni nyota ya mbuzi, namba yake ni 8

g) Sayari ya uranus nyota yake ni nyota ya ndoo, namba yake ni 4

h) Sayari ya neptune nyota yake ni nyota ya samaki, namba yake ni 7

i) Sayari ya pluto nyota yake ni nyota ya ng'e, namba yake ni 9

j) Jua nyota yake ni nyota ya simba, namba yake ni 1.

Kila namba ina sifa za sayari fulani, mfano mtu ambae amezaliwa tarehe 6 au 15 ya mwezi wa tano anakuwa na sifa zote za sayari ya Venus, kwa sababu namba 6 ina sifa zinazofanana na sayari ya venus lakini pia nyota yake ni nyota ya ng'ombe ambayo sayari yake ni venus pia.

Mtu ambae amezaliwa tarehe 7 au 16 ya mwezi wa tano, hapa anakuwa na sifa za neptune pamoja na venus. hivyo ni rahisi kuchanganya mambo ya kiroho kwenye utafutaji wake wa pesa na mali,, kwa sababu namba 7 ni namba inayohusu mambo ya imani,,, wakati nyota ya ng'ombe ni nyota inayohusu pesa, mali na vitu vya thamani, hivyo anajikuta anachanganya hizi sifa mbili kwa wakati mmoja katika maisha yake.

Nawatakia siku njema wapendwa.

Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

DOGOLI (Phd) , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
 
JE , NI KIDOLE GANI UNATAKIWA KUVAA PETE YAKO YENYE KITO CHAKO CHA BAHATI?

```(DOGOLI (Dr



Kama nilivyokwisha kueleza kwenye masomo yaliyotangulia kuwa kila mtu, kwa mujibu wa Nyota yake, ana Kito cha bahati kinachoendana na Nyota yake, hapa chini nimekueleza ni kidole gani kinafaa kuvaliwa pete yako.
Usivae pete kwenye kidole chochote au mkono wowote mpaka ujue nishati ya hicho kidole kama inaendana na nishati ya Kito na madini ya pete unayotaka kuvaa.
Hapo ndipo utakapopata matokeo mazuri yatokanayo na vito.

1. KUVAA PETE KWENYE KIDOLE GUMBA

Unapovaa pete kwenye hicho kidole ujue unaashiria AFYA NJEMA na UTAJIRI.

Ndio maana zile healing rings (Pete za uponyaji) huvaliwa kwenye hiki kidole.

Lakini pia matajiri huvaa pete kwenye hiki kidole ili kulinda mali zao zisiondoke.

Kwa hiyo ukishamiliki pete yako, lazima ujue which purposes it serves!

For healing purposes vaa healing ring yako kwenye dole gumba au kama una mali na utajiri wa maana vaa pete yenye Kito chako cha bahati kwenye dole gumba kulinda utajiri wako.
Mara nyingi pete ya dhahabu yenye Kito cha Pyrite au Citrine huvaliwa kwenye dole gumba.

2. KUVAA PETE KWENYE KIDOLE CHA SHAHADA (INDEX FINGER)

Unapovaa Pete kwenye kidole hiki unakuwa unaashiria UTAWALA, NGUVU au MAMLAKA fulani kwenye jamii.

Viongozi hutakiwa kuvaa pete zenye vito vyao kwenye hiki kidole ili kuongeza nguvu zao na utiisho wao kwenye mamlaka waliyo nayo.

Pete husika kwenye hiki kidole hiki pia inamlinda mtu asipinduliwe kwenye uongozi au madaraka aliyo nayo.

Wale wenye nyota za Uongozi kama Capricorn, Leo na Aries au wale wenye majukumu kwenye milango ya uongozi (hususani mlango wa 10 wa kinyota) wanatakiwa kuvaa pete zao kwenye hicho kidole ili kushawishi ama kuvutia nafasi za kiuongozi na madaraka.

3. KUVAA PETE KWENYE KIDOLE KATI (MIDDLE FINGER)

Ukivaa Pete yako kwenye hiko kidole unakuwa unaashiria UJASIRI, UTHUBUTU!

Watu ambao wanakabiliwa na uoga, kutochukua hatua wanaweza kuvaa pete yao kwenye hiki kidole.

Pia kwa wale ambao hawajaoa/ olewa wanaweza kuvaa pete zao kwenye hiki kidole ili kuiambia Universe kwamba wanahitaji wenza wao.
Pete yako ya bahati kwenye hiki kidole hukuunganisha au kukukutanisha na soulmate wako katika mazingira hata ambayo hukutarajia.
Humvuta mtu wako kwako kwa namna ya ajabu sana.
Pia kama mchumba wako aliondoka bila makubaliano nawe unaweza kuvaa pete yako kwenye hicho kidole na kuanza kumuita kila siku usiku wa manane naye atarejea kwako.

4. KUVAA PETE KWENYE KIDOLE CHA PETE!

Hiki huitwa kidole cha pete kwa sababu ndicho kimezoeleka kuvaliwa Pete.
Utamaduni wa kuvaa pete kwenye hiki kidole ni wa wazungu na huvaa kwenye hicho kidole kwa sababu ni kidole laini kuliko vyote, kwa sababu mishipa yake ni michache kulinganisha na vidole vingine na hivyo kukifanya kuwa dhaifu.
Pia, tofauti na vidole vingine, kidole hiki kipo mahali ambapo kinajikuta hakifanyi kazi kama vidole vingine hususani thumb and index fingers, hivyo kuonekana kinafaa kuvaliwa Pete!

Lakini, kinyota hiki kidole huashiria upendo kwa sbb kina mshipa mkubwa wa damu unaoenda mpaka kwenye moyo na hivyo kuwa kidole kinachoashiria Upendo (yaani love)

Kwa hiyo, kinafaa sana kuvaliwa Pete za ndoa na ziwe zinaendana na wanandoa na nyota zao husika ili kuwafanya kuwa waaminifu kwenye ndoa yao, wenye shauku ya kuwa pamoja muda wote, wabunifu na wachangamfu.

Watu wa Nyota ya Simba ambao Nyota yao hutawala kwenye moyo hutakiwa kuvaa vito vyao kwenye hichi kidole.

5. KUVAA PETE KWENYE KIDOLE KIDOGO CHA MWISHO.

Pete ikivaliwa kwenye hicho kidole huashiria kuwa mvaaji anahitaji kujiungamanisha na ulimwengu wake wa kiroho na kitaaluma pia.
Pete kwenye hiki kidole humsadia mtu kuwa na utulivu wa hali ya juu na hivyo kufanya mambo yake kwa makini na kwa uaminifu mkubwa.

Jipatie Kito chako tukutengenezee Pete ya Gold , Silver au Shaba , uvae kwenye kidole chochote utakachoona kinafaa kutokana na nia yako na mambo yako yatakunyookea.


Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ (Phd) , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
 
Soma hapa ili uone sifa za nyota yako
👇👇👇👇👇



IJUE NYOTA YAKO (Gemini ♊)
Sehemu ya tatu

+DOGOLI (Dr)


MAELEZO KAMILI YA NYOTA YA MAPACHA (GEMINI ♊)

Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Mei na 20 Juni

Asili yao ni Upepo .
Sayari yao ni Mercury (Attwarid).
Siku yao ya bahati ni Jumatano
Namba yao ya bahati ni 6

Malaika wake anaitwa Raphael au Mikyaail na Jini anayetawala siku ya Jumatano anaitwa, Barkaan au Ophiel,

Rangi zao ni Bluu, Njano, Njano ya Chungwa Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za njano au bluu isiyoiva ambayo inapendeza ndani ya nyumba.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi ya Samawati (Sky Blue)

Rangi inayowapa uwezo wa kifedha ni rangi ya Kijivu na rangi ya Fedha

Kito (Jiwe) ni Agate na Aquamarine Celestite Howlite Chrysocolla,Quartz, Emarald na Diamond
Madini yao ni Fedha

Manukato yao ni Marashi ya Mrujuani (Lavender), Lilaki maua ya rangi ya zambarau isiyoiva (Lilac), Yungiyungi (Lily of the valley).

MAMBO MUHIMU:-

Sifa zao ni kubadilika badilika katika mambo au maamuzi yao.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni Kuwa na Fikra za ndani kuliko za juu juu.

Maadili yao ni Ujasiri katika mawasiliano, Uwezo wa kufikiria haraka haraka na uwezo wa kujua na kufahamu vitu haraka.

Tabia za kujiepusha nazo ni Kusengenya, Kuumiza wengine kwa maneno makali, Mambo ya juu juu na kutumia maneno ili kuwapotosha watu (Propaganda).

USHIRIKIANE NA NANI?

*Nyota za watu ambao anaoelewana nao ni nyota za Mizani na Ndoo.

*Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mashuke, Mshale na Samaki.

*Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Samaki

*Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Kaa

*Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mizani

*Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mizani

*Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni Nyota za Ng’ombe na Ndoo.

KIPAJI CHA MAPACHA:
Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa cha kuwasiliana na watu ambao wako mbali kwa kutumia akili zao au hisia walizokuwa nazo. Telepathic:

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Mapacha ni watu wenye hisia kali sana ambao wanakasirika upesi, ni watu wasiotulia na wenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kuzungumza.

Wanaweza sana kushawishi watu. wanapenda sana mabadiliko na tofauti na kujua mambo, wanapenda watu na wanapenda kujumuika na watu lakini wakati mwingine hawaeleweki.

Wanapenda sana kusafiri na wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika. Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana, ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.

Katika Mapenzi wanahakikisha kwamba hawawachoshi wapenzi wao. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.

Katika mapenzi, wao wanapenda vitu au mambo tofauti tofauti, wakihisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.

Uaminifu ni kitu kigumu kwa Mapacha.

Mara zote wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje, hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.

KAZI NA BIASHARA ZA MAPACHA:
Kwa vile wenye nyota hii asili yao ni upepo na wao ni wenye kuzaliwa kwenye mawasiliano na uhusiano, wanapenda sana uhuru na uwazi katika kazi zao.

Kazi zao hasa ni zile zinazohusiana na mambo ya utangazaji wa Radio na Televisheni.
Kazi ambazo zinahusika na mambo ya vitabu au uchapishaji vitabu. Kazi za kufundisha na kazi za ushauri nasaha.Vilevile wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi za ukalimani au kazi za biashara lakini zinazohusiana na safari za nje.

MAVAZI NA MITINDO :
Mapacha wanatakiwa kuvaa Nguo zenye Mitindo ya kisanii, nguo ziwe Nyepesi na zilizonyooka Ziwe za Rangi ya Njano na Nyeupe. Kitambaa kiwe kama hariri, chepesi na chenye kumeremeta. Wake kwa waume wapendelee kuvaa Suti na ikiwezekana wasikose kuvaa Gloves.

MAGONJWA YA MAPACHA:
Nyota hii inatawala mabega, mikono, viganja na sehemu ya juu ya mbavu.Tatizo la kutopumzika kwa sababu ya kutafuta mambo mapya ndio yanayosababisha maradhi kwa wenye nyota hii.Wanasahau miili yao na mara nyingi wanapata matatizo ya neva kutokana na uchovu kwa mishughuliko mingi.Magonjwa yao makubwa ni kukosa pumzi (bronchitis), pumu (asthma), matatizo ya kifua, mafua, flu, ajali za mara kwa mara kwenye mikono na mabega.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MAPACHA :
Mapacha wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndio vinavyotawaliwa na nyota yao, kuku, rasiberi, karoti na uduvi.

Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika nchi au miji ifuatayo inayotawaliwa na nyota yao. Nchi hizo ni Ubelgiji na Wales, na baadhi ya miji ni London (Uingereza) na San Fransisco (Marekani).

MADINI, VITO NA MAFUSHO:

Madini ya Mapacha ni Fedha. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni kama vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.
Mafusho ya Mapacha yanaitwa Kashuu Muhlib (kachiri). Mafusho haya yako kama mauwa yaliyo kauka, rangi yake ni kahawia. Kwa kuleta bahati choma siku ya Jumatano kati ya saa 12-1 asubuhi au kati ya saa7-8 mchana.


Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ (Phd) , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
 
NYOTA YAKO LEO JUMAPILI JULAI 27/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

imekuwa vigumu kwako kufanya maamuzi kuhusiana na mambo Fulani na ukajikuta uko njia panda itakayokutenganisha na mambo mengi Leo amua cha kufanya katika kufikia malengo yako unayoyataka.

•Safari zako leo ni nzito nzito lakini utafika salama.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Leo utahitaji ushauri wa dharura na wa kitaalamu ili kuweka mambo yako sawa Kutimia kwa mipango yako uliyonayo wakati huu kunategeme wewe utajihusisha na watu wa aina gani.

•Kazi zako zitaenda hovyo leo na unaweza kujiharibia au kuharibikiwa kazi yako leo hivyo kuwa makini kwa kila kitu na usilazimishe mambo leo utapata fedheha.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Leo ni Jumapili nzuri sana kwako hasa katika kutafakari kuhusiana na maisha yako ya baadae yaweke pembeni mambo ambayo unayaona hayana maana kwa sababu maisha yako.

•Safari zako sio nzuri leo kuna dalili za kupatwa na tatizo njiani litakalokuharibia siku yako leo na kazi zako pamoja na muda wako unaonekana utaharibikia njiani.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Leo matatizo mengi ambayo yatakuandama yatakuwa yanatokana na nuksi au husda kwa upande wako Tafuta njia ya kuondoa husda hiyo au nuksi hizo kabla hazijaenea sehemu kubwa.

•Mahusiano yako yatakuwa sawa zaidi na mwenzako atajutia makosa yake kwako na atajirekebisha
Safari zako ni nzuri.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Leo Ondoa khofu Nyota yako itakuletea mabadiliko makubwa na mengi sana katika maisha yako Yakitokea hayo yakubali tu aidha yakiwa ni mazuri au mabaya hatimaye utamakinika na utaona fanda ya mabadiliko hayo.

•Mahusiano yako yataingia kiza na vurugu zitajaa ndani kwako au kutokuelewana na mwenzako.

★MBUZI– December 22– January 20)

Onyesha roho ya huruma na uwe na hisani kwa kila mtu tabia hiyo watu itawafanya watu mara kwa mara ili uwape msaada kama unavyotoa kwa wengine na wakija wasaidie wala usichoke.

•Mahusiano yako yapo vizuri na hakuna tatizo kubwa kila kitu kitakuwa sawa pia safari zako ni nzuri na zina kheri kwako.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Jaribu sana kujiweka mbali na marafiki wabadhirifu iwapo utataka kufaulu katika maisha yako umekuwa ukitumia vibaya fedha zako katika siku za hivi karibuni kiasi cha kumeshindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yako ambayo umejipangia wewe mwenyewe.

•Mahusiano yako yatakuwa vizuri na watakosa nguvu wafitini wako pia safari zako sio nzuri leo tulia nyumbani kuna misukosuko katika safari zako.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Leo jitahidi kujiepusha na marafiki wasio na tija kwako Unahitaji utulivu wa hali ya juu katika kutekeleza majumu yako yanayokukabili Barizi na umpendae unaweza ukapa ufumbuzi au utatuzi wa shida zako zinazokukabili.

•Utapata habari nzuri sana leo na haja zako zitatimia bila shaka yoyote.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Umekuwa ukisumbuliwa na mikosi na matatizo sasa kwa muda mrefu na leo ndio wakati hasa wa kuyashughulikia hayo matatizo yako na kuyamaliza.

•Kazi zako au shughuli utakazoagiza ufanyiwe leo watafanya kinyume na utaudhiwa sana dhidi ya uwaagizao au unaowaagiza.

★NG’OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Leo kuwa na moyo mkunjufu Jitahidi kujielekeza kwa mambo mema na usijaribu kusema uongo unaweza kuumbuka Utakutana na mgeni na atakutaka muwe marafiki mkubalie kwa sababu utapata faida kubwa kwa hilo.

•Utapata maudhi asubuhi ya leo na maudhi ya hapa na pale katika siku ya leo.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Leo kuna bahati kubwa sana itakujia upande wako watu wengi watakuchangamkia na watakuwa tayari kukusaidia kuyashughulikia matatizo yako yanayokukabili.

•Kazi zako zitaenda vizuri na utapata wateja wapya au boss mpya kwenye biashara yako hiyo.

★KAA– CANCER 🦀(Juni 21– Julai 22)

Umesitasita kwa muda mrefu sasa katika kufanya maamuzi lakini leo ndio siku ya kufanya maamuzi Usiogope fedheha piga moyo konde iwapo unataka kufaulu.

•Utapata furaha leo na habari njema sana itakufikia leo Pia utapata marafiki wapya au mpenzi mpya.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim,niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250629-WA0012(29).jpg
 
Soma hapa👇👇👇



IJUE NYOTA YAKO ♋
Sehemu ya nne

(DOGOLI (Dr)


MAELEZO YA NYOTA YA KAA (CANCER ♋)

Hii ni nyota ya nne katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Juni hadi 22 Julai

Asili yao ni Maji ,
Sayari yao ni Moon Mwezi ,
Siku yake nzuri katika wiki ni siku ya Jumatatu .
Namba yao ya bahati ni 2 na 7 .

Malaika wake anaitwa Gabriel au Jibril, na Jini anayetawala Jumatatu anaitwa Murratul Abyadh au jina la utani anaitwa Abú nuuril abyadh au Phul


Rangi zao ni Nyeupe, Bluu, Hudhurungi (Puce) na rangi ya Fedha (Silver), Wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi zozote ambazo siyo nzito au zenye uwiano na rangi nyeupe.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Nyeusi(Black) na Bluu iliyoiva (Indigo).

Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni rangi ya Machungwa na rangi ya Dhahabu .

Kito (Jiwe) ni Moonstone, Lulu (Pearl). Quartz, Diamond, Moonstone, Peacock Ore
Madini yao ni Fedha (Silver) Manukato yao ni Yasimini (Jasmine) na Msandali (Sandalwood).

MAMBO MUHIMU :-

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo yao ni kujirekebisha na tabia yao ya kusikitika sikitika na kunung’unika.

Ubora wa Nyota hii ni Uongozi.

Maadili yao ni Kung’ang’ania, kuwa na uwezo mkubwa wa kihisia na kupenda malezi.

Matakwa yao ni Maisha ya Kifamilia pamoja na Nyumba yenye amani na maelewano.

USHIRIKIANE NA NANI?

Tabia za kujiepusha nazo ni kupunguza kuwa na hisia kali na kunung’unika nung’unika na kusikitika pasipokuwa na haja ya kunung’unika.

⭐Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Nge na Samaki

⭐Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Punda, Mizani na Mbuzi.

⭐Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Punda.

⭐Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Mizani.

⭐Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Simba.

⭐Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Nge.

⭐Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Mbuzi

⭐Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Nge

⭐Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Mapacha na Samaki.

KIPAJI CHA KAA:

Kaa wana kipaji cha hisia ya kugundua mambo yanayotendeka ikiwa ni pamoja na kubashiri mambo, kumwelewa mtu kwa undani na kujua jambo ambalo mtu anataka kulifanya au jambo litakalotendeka hasa kwenye watu wengi. (Sensitive):

*TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
*
Kaa ni watu wenye tabia ya hisia nzito, wapole na wenye huruma. Ni wenye dhamira ya ulezi na kuwaangalia au kuwahurumia watu wengine, hiyo inaonekana waziwazi katika nyumba zao na familia zao.

Upande mwingine ni watu ambao wana “Gubu,” wakali, wenye kupenda kujishughulisha na wanajiamini sana. Ni watu ambao wanaweza kubadilika lakini wenye msimamo na itikadi, wanaweza kuwa ni wenye wivu mkali na wenye kupenda kudhibiti wapenzi wao.

Hisia ni kitu muhimu sana katika mapenzi kwa Kaa, pamoja na kwamba kimaumbile ni watu wanaopenda kujilinda na wanaogopa sana kuumizwa kimapenzi na wapenzi wao.

Wanapenda sana kuwa karibu na wanayempenda na kuwaonyesha huba na upendo mkubwa. Kwao hakuna mapenzi ya nusu nusu, wanapenda sana kuwa na mtu ambaye atadumu nae milele.

Kaa bila ya kuwa na mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao katika maisha, hivyo basi huwa hawana raha. Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.Ni wagumu sana kuachana na wapenzi na inapotokea huwa hawaagi, wako radhi wao waumie kuliko kuachana na anayempenda.

KAZI NA BIASHARA ZA KAA:

Kaa,Wanatakiwa wafanye kazi za Utabibu kama vile Madaktari au Wauguzi, kazi za baharini kama vile mabaharia, kazi za huduma ya chakula kama hoteli, migahawa, kazi za kuhudumia watoto kama katika shule za chekechea, kazi za benki au kazi za maneja utumishi au kazi za kuandika.

MAVAZI NA MITINDO:

Mavazi yao yawe ya kupwaya pwaya kama ni Magauni yawe ya kuninginia, nguo ziwe zinazo badilika badilika. Mavazi yawe ya rangi ya Fedha na rangi ya Bahari. Vitambaa vyao viwe laini na vyenye kutiririka. Nguo za kike ziwe zenye marinda na Blauzi ziwe laini.

MAGONJWA YA KAA :

Nyota hii inatawala njia kuu ya chakula kuelekea tumboni, mbavu, mfupa wa kidari, tumbo la uzazi, utumbo mdogo na utumbo au sehemu zote za kusagia chakula.Vile vile inatawala bandana na matiti.

Maradhi yao makubwa yanakuwa maradhi yanayosababishwa na gesi, vidonda vya tumbo au kiungulia au maradhi yanayotokana na mwili kuwa mnene au umbo kubwa.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA KAA:

Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula na matunda yafuatayo ambavyo ndivyo vinavyotawaliwa na nyota yao, Mapeas, Kaa au vyakula vya baharini, na mboga kama kabichi na saladi (lettuce).

Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika miji au nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao.Miji hiyo ni New York (Marekani) na Venice (Ugiriki) au nchi za New Zealand na Scotland.

MADINI, VITO NA MAFUSHO:

Madini ya Kaa ni Fedha. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni kama vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.

Mafusho ya Kaa ni Ubani wa aina yeyote wa kawaida au ubani maka unachoma siku ya Jumatatu kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana

Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ (Phd) , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
 
KUTEMBELEA NYOTA YA MTU MWINGINE !

Sehemu ya pili

( DOGOLI (Dr)


Ukweli ni kwamba Nyota haiibiwi, nyota inadhibitiwa/inachafuliwa/inafunikwa au inamalizwa nguvu na wewe mwenyewe binafsi kulingana na matendo yako, mazingira au watu unaohusiana nao hasa uhusiano wanakuathiri Kwa namna Moja ama ingine.

Huwezi kudhibiti wala kuchafua nyota ambayo tayari mwenye nyota ameijua na anaitumia ipasavyo kwa maana tayari inang'aa hiyo ni sawa na kuizuia SGR kwa kukaa mbele ikiwa kwenye mwendo.

Pia mtu ambaye nyota yake tayari imeng'aa na yupo juu kwa kuwa na utajiri, ushawishi, mamlaka na nguvu kubwa mheshimu kwa sababu kuna kazi kubwa ya ziada kaifanya ili kuhakikisha anabaki juu na anakuwa bora kuliko wengine.hayuko pale Kwa bahati, kwanza hakuna bahati Bali ni malipo ya kile kizuri ulichokifanya AWALI

Kwenye topic ya incarnation & Re-incarnation(kufa na kuzaliwa Tena) nilifundisha kwamba hakuna bahati, ni Neno tu la kufarijiana usijione wewe una nuksi ,jambo la kweli na muhimu Kulifahamu ni Kwamba, wale wote(watoto) wanaozaliwa ndani ya FAMILIYA tajiri ndani Yao zipo nafsi ambazo zilishafanya mambo mengi mazuri ndani ya jamii ENZI za nyuma Kabla hazijavua miili Yani kufa Kisha kurudi,hivyo Karma inakurejesha ndani ya koo au FAMILIYA iliyojaliwa ili upate kiinua mgongo chako,hivyoivyo wewe uliyezaliwa kwenye umaskini WA kutupwa USIMLAUMU baba/mama Yako ,jilaumu mwenyewe kwani ijapokuwa hunakumbukumbu ila ulifanya makosa makubwa maisha ya nyuma pengine ulikuwa tajiri ila ulinyanyasa Watu ,pengine ni Laana ya kifamiliya ama ukoo(curse),

Sasa tuendelee

Kwa ufupi ni kwamba nyota sio kipawa wala talanta kama wengine wanavyodai, nyota ni mwongozo wa maisha tangu kuzaliwa mpaka mauti kwa viumbe wote sio mwanadamu tu na ndiyo maana baadhi ya nyota zinanasibishwa na wanyama na wadudu pia asili yake ikinasibishwa na mazingira yaani maji, upepo, udongo na moto.

👉Nyota ni ushirikina kwa watu wasio na maarifa haya,hata mimi zamani niliamini hivyo na hakuna kitu nilikuwa nakichukia kama utabiri wa nyota ila nilivyojikita kwenye kuuelewa ULIMWENGU ndipo nilipoelewa kwa nini elimu hii inapigwa vita na kunasibishwa na uchawi/ushirikina.

Elimu ya nyota ni zaidi ya uchawi
Elimu ya nyota ni zaidi ya ushirikina

Huwezi kuwa na elimu ya nyota halafu wachawi wakakusumbua au waganga wakakuibia/wakakutapeli.

👉Je, umewahi kusikia watu fulani fulani huko wakisema "fulani anatembelea nyota ya fulani?"

Na je, nini ulikuwa mtazamo wako kuhusiana na kauli hiyo au kauli kama hiyo?

Tumefundisha kwa miaka mingi kuhusiana na elimu ya Nyota na angalau watu wengi sana waliotupinga kwa nguvu zote miaka hiyo, hususani miaka ya 2019 kuja 2020 na 21, wengi wao ni wadau wakuu wa elimu hii siku hizi. Huo ni ushindi kwa waalimu wote wa ELIMU YA NYOTA kwa Afrika Mashariki na Kati; kwa hiyo hapa sitaanza kwa kuelezea maana ya nyota, acha niende moja kwa moja kwenye hoja.

Unaposikia watu wanasema kwamba mtu fulani anatumia nyota ya mtu mwingine au nyota za watu wengine, ni ukweli usiopingika kabisa.
Kuna uwezekano mkubwa endapo mtu akiamua kutumia nyota yako au ya mtu mwingine, kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa sababu kila mtu ana aina ya nyota inayosapoti mambo fulani tofauti na wenzake.
Aidha, kuna Nyota ambazo zenyewe kwa asili yake zinasapoti nyota zingine hususani Nyota ya Simba na Nyota ya Ng'ombe.

Mtu akianza kutumia nyota yako kwa maslahi yake, ni wazi kwamba wewe unakuwa unamfanyia kazi yeye kwa kujua au bila kujua, unakuwa unamnufaisha yeye.

Kuna njia nyingi za kutumia nyota ya mtu kufanikisha mambo yako, nitataja njia kadhaa:

1. Tendo la ndoa
Hili tendo ambalo wazungu huliita SEX ni tendo ambalo mtu mke na mtu mme wakikutana kimwili, wanabadilishana nishati zao; huyu anabeba za huyu na yule anabeba za mwenzake. Ndio maana ya neno S.E.X ambalo kirefu chake ni Sacred Energy Xchange!
Kila unapokutana kimwili (kingono) na mtu awaye yote, awe mkeo/ mumeo au la, mnachofanya kiroho mnabadilishana nguvu, unampa zako anakupa zake.
Sasa watu wengi wana nguvu au nishati (au roho) chafu ambazo zinaharibu mambo, sasa wakilala na wewe, wanakuachia zao chafu wanabeba za kwako safi, mkitoka hapo wewe unaharibikiwa wao wanasonga mbele (wametumia nyota yako kujisafishia au kuoshea nyota yako)

2. Huduma za jamii
Kama nyota yako ni safi na inang'aa alafu mtu 'akaiona' na akaitaka, anaweza kuanza kujitolea kukusaidia au kukuhudumia mahitaji yako yote bila kuhitaji chochote kutoka kwako.
Kikawaida utamuona ana roho nzuri (ni sawa), lakini kiuhalisia (kiroho) unakuwa unampa uhuru wa kuitumia nyota yako kufanikisha mambo yake.

3. Kugawa fedha na zawadi kama nguo, viatu, saa nk.
Kama mtu 'akiona' nyota yako inang'aa sana, lakini hujitambui, basi anaweza kuichukua 'kwa kuinunua'
Atafanya hivyo kwa kuchukua pesa na kuinuizia manuizo (spells) fulani fulani, kisha atakupatia kwa mkono wa kushoto na atajitahidi kuhakikisha na wewe unapokea kwa mkono huo. Tendo hilo linakuwa ni alama au Ishara ya mauziano, anakuwa amenunua nyota yako.
Asipotumia fedha anaweza kutumia nguo, saa, viatu, soksi au chochote kinachotoka kwenye mwili wake.

Hii ndio Siri ya Mwiko kutumia Mkono wa kushoto kutoa ama kupokea kitu ,sio Kwa sababu ya sijui mkono kutumiwa maliwatonini(msalani) lahasha Bali ni Njia ya kukwepa mchezo mchafu,ndiomaana hata mwanangu anayetumia mkono WA kushoto nimemfundisha kufanya yote Kwa mkono wake huo kwani ubongo wake WA kulia unanguvu zaidi,ila namfunza kutumia MKONO WA kulia Kwa kupokea,kutoa,kulia na kusalimia mtu.

-usimzuie mtoto kutumia mashoto kama amezaliwa hivyo kwani ubongo wake WA kulia unanguvu kuliko ubongo WA kushoto unaoratibu mguu na mkono WA kulia, wazazi wengi huwacharaza watoto ilihali ni maumbile yake,Kwa kufanya hivyo mtoto anakosa ufanisi kwenye tasnia za sanaa,vipawa vya uongozi,uandishi,ualimu,siasa na michezo kwani Hilo ndio eneo lao la kujidai ,kuliko watumiaji WA mkono na MGUU WA kulia ambao ubongo wao wenye nguvu ni WA kushoto wenye kuratibu mambo mengi kwenye TAALUMA,TAKWIMU,tafiti,hisabati,kukariri na HASA mambo ya kufundishwa ili apokee

‼️NAWAIBIA SIRI HII.
matumizi ya mikono na miguu Binadamu hapo awali/zamani alitumia yote Kwa usawa,Bibi na babu zetu walizaliwa hivyo Lakini baada ya ujio WA DNA MPYA Yani kuingiliwa Kwa DNA kupitia Blood Group/makundi damu Saba/7 Mapya(zingatia ni makundi 7mapya) ambayo ni (+A,-A,+B,-B,+AB,-AB,+O ) yatokanayo na DNA za Mbwa,Nyani aina ya Rhoses(Rh+) na Neadtheral, kulipelekea Vipawa,vipaji vingi kufa Kwa Watu weusi hivyo kusababisha matumizi ya mkono WA kulia na MGUU WA kulia kuwa Kwa 97% huku mashoto wakiwa ni 2% na 1% ikiwa ni wale watumiaji WA vyote ambao group damu zao ni -0( lilifanywa makusudi na whites ili kutokomeza vipaji,vipawa Kwa mtu Mweusi)

Asili ya mtu mweusi ni blood Group -0
Ambaye ni chanzo Cha Ngozi nyeupe Duniani, kundi damu -0 lisipo ingiliwa na UHARIBIFU wowote ule ,mtu ataishi hadi miaka 1200 kama zamani.

📌DNA zinaingiliwaje kupitia mifumo ya damu? Ni rahisi tu,kinachofanyika ni zile chanjo anazopewa mama MJAMZITO hadi mtoto anapozaliwa kuna ajenda za Siri mno kuhusu Kubadili blood group pamoja na kuzorotesha tezi penuel(jicho la tatu) ili tusiinuke Kiroho (hili ni somo Pana napaacha Kwa Leo)

👉Ok iyo ilikuwa ni FAIDA Kwa yule asiyejua mambo hayo,nimalizie MADA yetu nzuri kwamba
ZIPO MBINU AU NJIA NYINGI ZA KUPEANA NYOTA, ACHA NITAJE HIZO TATU TU.

Watu walio kwenye hatari kubwa ya 'kuibiwa' Nyota zao wengi ni wale wa Nyota za Simba na Ng'ombe, wachukue taadhari.

Nyota hizi zinasafisha nyota zote hivyo wenye nyota hizi ni kama dhahabu Kwa Wengine hata km hawajijui.

Kuna namna nyingi za kufanya ili kuilinda nyota yako isichezewe nilishafindisha hapo awali

Nyota yako ikiwa chafu au imechezewa, fanya ufanyavyo, huwezi kutoboa!

SWALI JE UNATAKA KUSAFISHA NYOTA❓


Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ (Phd) , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
 
NYOTA YAKO LEO JUMATATU JULAI 28/2025:
IMG-20250629-WA0012(31).jpg


UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.


★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Kuna mtu uliahidi nae leo mtakutana ni siku nzuri kwa maelewano na kupatana na mtu Masuala ya uchumba posa na ndoa yanahitaji kupangwa upya Mapenzi yataimarika na utapata penzi jipya.

•Utapata matumaini mazuri kwenye mambo yako na utulivu mkubwa utajidhihirisha katika maswala yako pia kazi zako zitaenda vizuri na biashara zako zitastawi zaidi.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Utakuwa na hofu na wasiwasi kutokana na taarifa utakazopokea Siri itavuja na hukumu ya kifungo kutolewa Kuna habari za maziko ya mtu mkubwa yatakuhusu.

•Hayo yanatokana na uadui wa watu kupitia maneno yao yachunguze na usiwaamini watu
Safari zako sio nzuri utapata balaa au bahati mbaya.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Utapokea taarifa au mgeni kutoka kwa mtu aliye mbali Kuna maelewano mazuri na makubaliano utakayo yafikia kwa leo Ule mpango wa uchumba na ndoa iko vizuri Kuna safari ya kumtembelea mwenza wako uñashauriwa uifanyie muda mwingine.

•Utapata maudhi makubwa leo na kuna hasara utaipata katika kazi zako au mambo yako Kuwa makini sana Siku ya leo.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Utapata ushindi katika jambo linalo kusumbua kwa muda mrefu Biashara zitakua nzuri utapata mafanikio na kupata nafasi ya kuongoza kitengo.

•Mahusiano yako hayana tatizo kubwa ila epuka mzaha usio wa lazima kwani unaweza kusababisha mfarakano.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Utajikuta umefufua matumaini kwa mpenzi wako ambaye amekuwa anakusumbua kwa muda mrefu mkutano utakao hudhuria itakuwa ni wa manufaa makubwa kwako.

•Kazi zako zitaenda vizuri na utakuwa na bahati kazini Waza makubwa zaidi.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Utajikuta kwenye upinzani na shida zisizoisha utapata safari ya ghafla Usijihusishe na ubishi utakuletea matatizo kuna kupotelewa na kitu na utapata kesi Hukumu itakayotolewa itakuelemea.

•Mahusiano yako leo yana nafasi kubwa tumia hisia zako kuimarisha mapenzi
Safari zako ni nzuri sana.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Utapokea taarifa mpya shughuli unayotaka kuianza inahitaji kuitangaza kwanza Ila kupata mafanikio unahitajika kuanza upya katika kila jambo unalolitaka kulifanya Hata kama bado hujaamua nyota zinashauri uanze tena.

•Mahusiano yako hayako sawa kwa sasa lakini hali hii ni ya muda tu Safari zako si nzuri utapata maudhi makubwa safarini.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (March 20– March 20)

Jumatatu leo hali yako ya ki uchumi itaimarika shughuli zitakwenda vizuri tarajia kupokea pesa au mali itayo kuongezea kipato Utapata na kuwa na kitu.

•Utapata msaada mkubwa na faraja kutoka kwa watu wa karibu Bahati nzuri itakufuata kazi zako zitaenda vizuri na utapata faida kubwa.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Utafanya safari fupi fupi za hapa na pale siku nzuri kwa masuala ya mapenzi unatakiwa kuwa karibu na na wanachama wenzio Leo mambo yako yanahitaji kuwahusisha watu wenye uzoefu.

•Utapata msaada mkubwa na faraja kutoka kwa watu wa karibu Bahati nzuri itakufuata kazi zako zitaenda vizuri na utapata faida kubwa.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Leo masuala yako ya pesa na kazi uñashauriwa ushirikiane na mwanamke mwenye umri mkubwa mzee au kiongozi na kama suala la maombi ya kitu au jambo fanya kwa maandishi.

•Mahusiano yako yatakuwa na utulivu na amani zaidi
Safari zako ni nzuri.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Fuatilia suala la mkopo masaada utapewa leo utajikuta unafurahia jambo Masuala ya masomo yanahitaji kupewa uzito utapokea barua au pesa jipongeze baada ya kufanikiwa.

•Leo utapoteza kitu muhimu na maadui wako wana nguvu zaidi Jiandae kisaikolojia kwa mapambano kazini.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Bado suala la ugonjwa linakusumbua itapokea taarifa za wizi utakaotokea nyumbani Kutakuwa na kelele na ubishi itakumbana na shutuma au kesi omba msaada.

•Habari njema zitakufikia na utajikuta unatamani ukaribu wa mtu fulani aliyekuvutia Utafanikiwa kumuona na kupata furaha.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim,niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom