NYOTA YAKO LEO JUMATANO JULAI 23/2025:
UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.
MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.
★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)
Jamaa zako wako kàtika hali ya uhitaji kuwa karibu na wape misaada Leo utapokea maombi mengi ya watu kutaka kusaidiwa au kukopeshwa Shughulika suala la elimu na mahitaji ya mtoto Kuna jamaa yako wa karibu atakupa msaàda kama ukiuhitaji.
•Safari zako sio nzuri ingawa utaenda na kufika salama ila njiani maudhi mengi.
★MASHUKE– VIRGO ♍(Agosti 23– September 23)
Shughulika masuala ya nyumbani leo hakuko vizuri Kuna taarifa za magonjwa na kutokuelewana na wazee au viongozi Lipo jambo hujalifanyia kazi kama ulivyotakiwa litakuletea shida ikiwa utaendelea kudharau.
•Utapoteza kitu muhimu Leo na itakufikia habari mbaya ya huzuni au utashuhudia tukio la kukuhuzunisha leo Mungu akusimamie kwa yote.
★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)
Utapokea msaada mkubwa kutoka kwa mwenzio mahusiano mapya yatakuletea neema Leo uko kwenye nafasi nzuri ya kupokea mkopo uliouomba fuatilia utapata Utaingia makubaliano ya kupewa unachotaka siku nzuri kwa kujistarehesha na mwenzio Timiza ahadi ulizojiwekea zitakunufaisha siku zijazo.
•Kazi yako haitapokelewa vizuri na utalaumiwa au kupuuziwa na ikiwa unatafuta kazi kwa leo haijakaa vizuri upande wako ngoja upite muda kidogo au siku ya Leo ipite.
★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)
Acha tabia yako yako ya kulazimisha mambo leo kuwa mpole siku haijakaa sawa kwako Utajikutà unagombana na kuzozana na kila mtu chunga majibu yako yatakufikisha pabaya Usifanye mambo kwa haraka haraka au papara utapata tatizo ambalo litahitaji msaada Omba na utasaidiwa japo kwa uchache.
•Maswala yako ya kikazi yapo vizuri na utapata faida na wateja wapya kwenye biashara yako na kazini mwako wataongezeka marafiki wapya.
★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)
Utapokea mgeni ambaye ni rafiki yako mkubwa kuna taarifa za mbali kutoka kwa mtu uliye anzisha nae mahusiano hivi karibuni Mipango yako inahitaji makubaliano ya maandishi siku nzuri kwa maelewano kwa waliohitilafiana Habari za ndoa na posa zitasogezwa mbele.
•Safari zako ni nzuri hazina shaka yoyote.
★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)
Vizingiti vimekuwa vingi na leo usifanye jambo ambalo unategemea litakuletea faida Mafanikio yako yataanza kudidimia chukua hatua mapema leo utajikuta unagombana na mtu na utapata lawama na taarifa za ugonjwa.
•Utapata habari nzuri Leo na kuna mtu atakupa kitu kizuri kwa namna usiyoitarajia.
★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)
Tarajia kufifia au kuzorota mfumo wako wa biashara au kazi hii inatokana siku ya jana jumanne haukuifunga vizur watu walikuwekea husuda majira ya jion leo utapokea ujumbe utakao kupa matumaini na utaiona nuru kidogo.
•Kazi zako Leo zitakuwa nzito nzito na lawama nyingi juu yako ikiwa ni kazi mpya basi subiri siku ipite ndio uendelee na mipango hiyo na ikiwa ya zamani vumilia ni mapito tu.
★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)
Mpangilio mpya katika shughuli zako utakuletea mafamikio una nafasi kubwa ya kufanya vizuri Biashara na kazi zitakuinua na kukujengea heshima katika jamii Leo utapata jukumu la kusimamia jambo na kupewa kitengo ukiongoze.
•Kazi zako zitaenda vizuri na mipango yako itaenda vizuri haswa ile mikubwa na yenye faida kwako.
★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)
Siku ambayo utakuwa na pilika pilika za kushughulikia msuala ya kikundi au wanachama weka mkazo katika jambo hili Una nafasi kubwa ya kufanya vizuri utafanikiwa kupata marafiki wapya Ambao watakunyanyua usikose kuhudhuria mkutano utakao itishwa hivi karibuni.
•Siku yako leo itakuwa ya utulivu furaha na faraja zaidi haswa kwenye mahusiano yako ndoa yako au mapenzi yako mtu wako wa karibu atakufurahisha zaidi na anaweza kukupa moja ya vitu vizuri kwa namna usiyoitarajia au akakupa maneno ya faraja kwako.
★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)
Ule mtiririko wa mambo kwenda vizuri hauko kama inavyokuwa Kutakuwa na vikwàzo na kukwama tafuta msaada kwa wanaojua Kuna uadui unafanywa kukuvugia kazi na biashara zako hali ya ya kipato itaporomoka.
•Utapokea taarifa nzuri sana leo na mambo mazuri yatakutokea haja zako nyingi zitatimia na utafanikiwa.
★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)
Rudisha mahusiamo mazuri kwa jamaa zako leo panga safari ya kukutana nao
Mpango wa kuanzisha shughuli yoyote ile kwa sasa hautakwenda vizuri iwapo hutamshirikisha ndugu au jamaa yako Leo utapata au kupokea kitu kipya ambacho kitakufurahisha kutoka kwa mtu wako wa karibu.
•Safari zako ni nzuri ila usiwahi utapata maudhi maudhi lakini utafika salama.
★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)
Utapata utakacho na utapokea pesa na taarifa za kupatikana kwa kazi uliyouwa unaitafuta Hali ya kipato itakuwa imenyooka fuatilia madai na stahiki zako.
•Leo uko kwenye nafasi nzuri ya kufanikisha malengo yako jihadhali na matumizi yâsiyo ya lazima Mpamgilio wa nyumbani uko vizuri kaa wazee kwa ushauri mzuri.
★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim,niwatakie siku njema na mafanikio mema
MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.