mzee wa nguna
Senior Member
- Dec 5, 2012
- 132
- 113
Brethren,
NB: Msiniombe reference kwa vile huu ni uchambuzi na maoni binafsi mimi babu yenu kwa kushirikiana na marafiki zangu wa karibu (Hawapo JF), kwa lengo la kupeana tahadhari.
Ni hivi; Utafiti ulioufanywa kwa miaka miwili mfululizo imegundulika huko mtandaoni ni mizaha mingi bila nia halisi za mahusiano. hata kwa wale walioweka picha na maelezo ya kutosha, ni bahati sana kukutana na watu halisia. Watumiaji wengi wanachofanikiwa ni kupata 'hookups' za muda mfupi tu na aghalabu mtu mkweli mwenye nia mtandaoni.
Wapo baadhi wamejisajili kimkakati kuendesha biashara za kupiga pesa ndefu na utapeli wa aina mbalimbali kwa mtaji wa UPWEKE, UGENI na kukosa umakini kwa baadhi ya watumiaji wa hizo website. Mara zingine huko pia ni chaka la walioshindikana katika jamii zinazowazunguka kutokana na tabia mbaya, wanaunda maelezo mazuri ya kuwashawishi 'victims' huku wakijijua wao ni tatizo. Mambo ni mengi, mengine ya kutisha, mf. unaweza kufikiri umepata mchumba kumbe anakuita akuchinje auze viungo vyako....
Tukienda mbele turudi nyuma; Sio rahisi mtu kukuamini sana wewe ambaye umejiweka mtandaoni kama tangazo la biashara. Kwanza umepataje ujasiri wa kuji-display!? lazima atakuwa anakustukia kila mara.
Wadau, hebu tujadili nini kifanyike kwa kuzingatia tamaduni zetu na ukuaji wa sasa wa teknolojia ili kufaidika zaidi na majukwaa hayo.