Uchambuzi: Upande mwingine wa online dating platform

mzee wa nguna

Senior Member
Dec 5, 2012
132
113
Brethren,
NB: Msiniombe reference kwa vile huu ni uchambuzi na maoni binafsi mimi babu yenu kwa kushirikiana na marafiki zangu wa karibu (Hawapo JF), kwa lengo la kupeana tahadhari.

Ni hivi; Utafiti ulioufanywa kwa miaka miwili mfululizo imegundulika huko mtandaoni ni mizaha mingi bila nia halisi za mahusiano. hata kwa wale walioweka picha na maelezo ya kutosha, ni bahati sana kukutana na watu halisia. Watumiaji wengi wanachofanikiwa ni kupata 'hookups' za muda mfupi tu na aghalabu mtu mkweli mwenye nia mtandaoni.

Wapo baadhi wamejisajili kimkakati kuendesha biashara za kupiga pesa ndefu na utapeli wa aina mbalimbali kwa mtaji wa UPWEKE, UGENI na kukosa umakini kwa baadhi ya watumiaji wa hizo website. Mara zingine huko pia ni chaka la walioshindikana katika jamii zinazowazunguka kutokana na tabia mbaya, wanaunda maelezo mazuri ya kuwashawishi 'victims' huku wakijijua wao ni tatizo. Mambo ni mengi, mengine ya kutisha, mf. unaweza kufikiri umepata mchumba kumbe anakuita akuchinje auze viungo vyako....

Tukienda mbele turudi nyuma; Sio rahisi mtu kukuamini sana wewe ambaye umejiweka mtandaoni kama tangazo la biashara. Kwanza umepataje ujasiri wa kuji-display!? lazima atakuwa anakustukia kila mara.

Wadau, hebu tujadili nini kifanyike kwa kuzingatia tamaduni zetu na ukuaji wa sasa wa teknolojia ili kufaidika zaidi na majukwaa hayo.
 
Nimekumbuka ushuhuda WA jamaa mmoja,alipata mchumba kutoka nje,basi wakawa wanawasiliana na mambo yakawa freshi Tu,,,,jamaa alikuwa anafanya kazi tanesco dar,,,so akawa anatumiwa hela za kutosha Tu na huyo banati (banati ni msamiati wa Kiswahili ukimaanisha mwanamke/binti).

Kumbe bwana sio banati ni kidume mwenzie,,,,jamaa alikuwa anatumiwa dolali mpaka anakwambia kazi aliona haina maana tena,,,kumbe katumiwa picha feki za banati lkn mhusika ni mwanaume.

Wakakubaliana aende ulaya,matayarisho fresh mwamba kakwea pipa mara paap ulaya hii hapa! Alivyofika anakutana na jamaa ambaye alimwambia mwenyeji wako amepata Safar ya ghafla so hatokuwa Kwa siku kadhaa,,,,jamaa Akaona kweli,Ila kipindi chote alichokuwa pale alihudumiwa vizur Sana,,,,,mwisho wa siku akachanwa live kuwa hakuna banati wala nini Ila mhusika ni Yule jamaa,,,,,basi ikabidi jamaa aliwe coz hakuwa na namna yupo ugenini na huku dar kazi kaacha Kwa nyodo anavyosema yeye mwenyewe,,,,kwahiyo kuna masahibu mengi Sana ktk hizi plat forms
 
Vipi kuhusu wanaotafuta wachumba humu jf na wao wapo hatarini?
 
Vipi kuhusu wanaotafuta wachumba humu jf na wao wapo hatarini?
Kikubwa wawe Makini,,,wahakikishe siku ya Kwanza kuonana iwe public place,sio hotelini au magetoni,,,,,binadamu siku hizi hawaaminiki kabisa.

Hasa banati wawe Makini Sana maana wao wakitumiwa nauli Tu safari!
 
Kwa kuongezea hawa ambao wanaenda nje ya inchi ndo wawe Makini zaidi,,,,kuna banati mmoja alienda Capetown kukutana na boy wake,,,,,lkn akashangaa badala ya kupokelewa pale, safar ikianza kwenda huko mashambani na tofauti na pale Capetown alipoambiwa mwenyeji wake anakaa!

Wakampeleka maporini huko wakambaka na kumlawiti pia,kumbe Hilo genge ndo ilikuwa mambo Yao hayo,kama haitoshi waka mmwagia vinyesi pia,,,,akaja kuokotwa Hoi,kakaa hospital masiku kadhaa,kupimwa akakutwa na upungufu WA kinga mwilini.

Akarudi dar anajuta,,,,,watu wawe Makini Sana aisee!
 
Back
Top Bottom