Uchakachuaji wa Rasimu ya Katiba huu hapa

Uchakachuaji wa Rasimu ya Katiba huu hapa

kwa sasa ccm wamelewa katiba yao kwa hiyo hawasikii kitu chochote
 
"It is enough that the people know there was an election. The people who cast the votes decide nothing. The people who count the votes decide everything" - Joseph Stalin
Nimeipenda naomba niicopy kwa ruksa yako na It is enough that the people know there was an election. The people who cast the votes... - Joseph Stalin at BrainyQuote

Watu tunadhani tunatenda miujiza na uchakachuaji wa kura kumbe wenzetu waliliona hili kabla ya mwaka 1953 Joseph Stalin | Biographies | The Cold War | National Cold War Exhibition

Inauma lakini ndiyo hali ya dunia
 
kama swala ni la wazi namna hii kwanini mnaoweza msiende mahakamani?
 
**PRECAUTION: Kama hujui Hesabu usisome.!!
--------------------------

Wazungu husema ukiwa muongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri. Ukisema leo kuwa hujaoa halafu baada ya mwezi ukanikopa hela ili umtumie mkeo ni wazi kuwa utaumbuka.. Ukiamua kudanganya jitahidi kuwa na kumbukumbu sana (Liars must have a good memory).

Katibu wa Bunge Maalum leo katangaza kuwa jumla ya kura zote za Zanzibar ni 219. Japo Samuel Sitta alisema juzi kuwa wajumbe wa Zbar ni 210 but ngoja tukubaliane tu na Katibu kuwa ni 219 (hata km wamechakachua).

Kwa maana hiyo, theluthi mbili ya 219 ni 146. Na Theluthi moja ni 73.

Hivyo basi ili Rasimu ikwame kwa upande wa Zbar ilihitaji kura 74 au zaidi za kuikataa. Yani idadi yoyote ambayo itazidi 73 (theluthi moja) ingekwamisha Rasimu.

Wajumbe wa UKAWA kutoka Zbar ni 67, japokua wao wamesema ni 65 wakimaanisha wawili walipiga kura ya NDIYO. Tukubaliane nao kama tulivyokubaliana nao kwenye idadi ya wajumbe wa Zbar kuwa 219 badala ya 210.

Sasa twende kwenye Hesabu (Maths). Tuseme UKAWA walioikataa Rasimu ni 65 kama walivyosema. Ongeza 8 waliopiga HAPANA (wajumbe 7 plus Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar aliyeikataa jana). Hadi hapo utapata kura 73.

Ongeza Abdallah Abbas ambaye aliondoka Bunge la Katiba na hakupiga kura. Jumla ni 74.

Hadi hapo tayari kura hizo zimeshazidi theluthi moja, ambayo ni 73. Lakini cha ajabu tunaambiwa Rasimu imepita. Imepitaje??

Kama waliokataa wamezidi theluthi moja, inakuaje tena waliokubali nao wazidi theluthi mbili? Hii hesabu mbona haipo? CCM wamechakachua wakashindwa kuweka hesabu vzr.!

Jamani chakachua kote lakini linapokuja swala la hesabu utaumbuka tu. Always number never lie.!

Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Malisa GJ || Your Partner in Critical Thinking.!
Mkuu siku zote mahala popote inaposema idadi ya Kura za Ndiyo lazima ifike theruthi mbili haitazami theruthi moja kwanza bali 2/3 kama imetimia. Kama wajumbe walikuwa 219 na wakati wa upigaji kura - Ndiyo wakafika 146, basi mchezo kwisha haitazamwi 1/3 kuwa ilitakiwa kuwa chini ya 73.

Nimeyasoma matokeo ya Kura yameonyesha 2/3 ya Zanzibar walisema ndiyo ni 147 na 2/3 ya 219 ni 146, unless mnazo namba tofauti na hizo zilizowekwa. na upande wa bara wajumbe 411 theruthi 2 ni 274 kura za ndiyo zimezidi hata kama wabunge wa UKAWA wangekuwepo bado ushindi ni wao. Swala hapa labda ni kujiuliza Je, kweli kura za ndiyo zilifika 147?.

Kwa hiyo pamoja na kushindwa kaa Ukawa wangekuwepo nina hakika baadhi ya ibara zingepata ushindani mkubwa kwa faida ya wananchi lakini kwa sababu wote walitoka nje na kuacha goli wazi, CCM walipiga magoli kwa kisigino sasa tunacholalamika kipi ikiwa ssi wenyewe tulifanya maamuzi ambayo hayakutazama mbinu za CCM ktk kuipata katiba waitakayo. Kifupi tumerudishiwa katiba ya CCM iloboreshwa na hii ni kutokana na viongozi wachache wanaopenda sana kujijengea nafasi za uongozi kwa kutumia jina la wananchi. Haifai..
 
eti GREAT THINKER!!KHAA! Wenzio wenye akili ndogo wanajipanga jinsi ya kuzuia kile wanachoona ni tatizo, we umekalia kulalamika.

taifa haliendelei kwa kua mpo wengi kama wewe ambao badala mjipange kuchukua hatua pindi rasim hiyo itakapokuja mtaani muikatae kwa kura ya hapana. we unalilia lia kwa kilichokwishatokea.

CHUKUA HATUA DOGO, KULALAMIKA HAKUKUSAIDI KITU. Ingia mtaani hamasisha wenzio mpige kura ya HAPANA kwa wingi maana kule mjengoni wamefanikiwa kutokana na nyinyi UKAWA kukimbia mchakato. naaminu mngekaa mpaka mwisho hali ingekua tofauti na ilivyo sasa.

mnaitisha maandamano kudai haki, mnakimbia na kuwaacha wananchi wajiongoze. sijawahi ona kabisa mahala kokote dunian viongozi wa upinzani wakiwakimbia wananchi wao wakati wa maandamano.

BORA ENZI YA JINO KWA JINO, BEGA KWA BEGA NA MAPANGA SHAA INGERUDI, NINA HAKIKA KUSINGEKUA NA WALALAMISHI WENGI TENA KATIKA SEHEM ZA GREAT THINKERS AMBAPO WANAJAMII WENGI HAWAFIKI HUKU.
Tatizo umekariri nenda kasome wimbo la mageuzi nchi za kiarabu, kenya lilivyokuja.. utajua kinachofanyika..unafikiri kila kitu lazima uingie kichwa kichwa tu..
 
Unajisumbue bure hesabu zenyewe hujui! Nakuonea huruma sana!

Hizi hesabu alianza mahamedi mtoi akaja Tumaini Makene akaja Mungi ukaja wewe na Leo umerudia makosa Yale Yale uliyofanya Jana na walio Fanya wenzio!

Maswala ya mahesabu hebu achaneni nayo na mfanye mkiwa mmetulia sio kwenye pressure namna hii!
Hujui hesabu we endelea kupotosha!
Kawadanganye bavicha wenzio kuwa wewe unajua hesabu!Yani wote mnaandaliwa vya kuandika lakini hamkagui kilicho andikwa mnarudia makosa ya wenzenu.

Ukweli huko hapa

Mwenye nguvu!!...muite power..star tv.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu siku zote mahala popote inaposema idadi ya Kura za Ndiyo lazima ifike theruthi mbili haitazami theruthi moja kwanza bali 2/3 kama imetimia. Kama wajumbe walikuwa 219 na wakati wa upigaji kura - Ndiyo wakafika 146, basi mchezo kwisha haitazamwi 1/3 kuwa ilitakiwa kuwa chini ya 73.

Nimeyasoma matokeo ya Kura yameonyesha 2/3 ya Zanzibar walisema ndiyo ni 147 na 2/3 ya 219 ni 146, unless mnazo namba tofauti na hizo zilizowekwa. na upande wa bara wajumbe 411 theruthi 2 ni 274 kura za ndiyo zimezidi hata kama wabunge wa UKAWA wangekuwepo bado ushindi ni wao. Swala hapa labda ni kujiuliza Je, kweli kura za ndiyo zilifika 147?.

Kwa hiyo pamoja na kushindwa kaa Ukawa wangekuwepo nina hakika baadhi ya ibara zingepata ushindani mkubwa kwa faida ya wananchi lakini kwa sababu wote walitoka nje na kuacha goli wazi, CCM walipiga magoli kwa kisigino sasa tunacholalamika kipi ikiwa ssi wenyewe tulifanya maamuzi ambayo hayakutazama mbinu za CCM ktk kuipata katiba waitakayo. Kifupi tumerudishiwa katiba ya CCM iloboreshwa na hii ni kutokana na viongozi wachache wanaopenda sana kujijengea nafasi za uongozi kwa kutumia jina la wananchi. Haifai..

Faida gani wange sababisha ukawa?we wacha hao wenye nguvu waipitisha hiyo katiba kwa nguvu.
 
Tanzania inawatu wengi kama wewe ndo maana nchi inazidi kudidimia..mnJiona mna akili kumbe hamna kitu..umekomia ubachela kwa hiyo mtu akijiita bachela jf unapigia mstari huyu mtu ni bachela..sijui kwa nini ccm imekusanya nazi nyingi namna hii..

Nazi zipi mkuu fafanua tukupate.
 
zilipotoka za NDIO ndipo zilipotoka za HAPANA. kama unanaona umechakuchuliwa, waambie UKAWA wakuhimize uandamane mtaani na sio jf halafu tutakutana huko nikuoneshe ukilaza wangu.

NAKUSISITIZA KIJANA ULIYEAMUA KUWA BACHELA, TAMBUA NAFASI YAKO WEWE KAMA WEWE USISUBIRI FLANI ATAMBUE NDIPO NAWE UTAMBUE KILICHOTQMBULIWA NA MWENZIO. UNGANA NA MLETA MADA NENDENI SEHEM HUSIKA MKADAI HAKI, JF HAPAWEZI HATA ROBO KUKUPATIA HAKI YAKO.

wacha kutisha watu wewe ndugu,wewe nani hadi uwatishie watanzania wenzako?mambo ya aibu hayo.
 
Faida gani wange sababisha ukawa?we wacha hao wenye nguvu waipitisha hiyo katiba kwa nguvu.
kazi tulowatuma UKAWA ni kuhakikisha haki za waanchi zinapatikana. Hili swala la Uzanzibar na Utanganyika halimnufaishi mwananchi hata mmoja kwa njia yoyote ile zaidi ya kugawana umaskini na kujenga nafasi za kazi kwa viongozi wengi zaidi.

Kama Ukawa wangekuwepo mambo mengi sana yangebadilishwa kwa sababu sio kila kitu kilipita kwa kura mia kwa mia, Hapana. Tulichopewa ni katiba ya CCM iloboreshwa na wala hatukutaka katiba ya Chadema ama CUF bali ya wananchi. haya maswala ya Siasa na uroho wa madaraka ndio umetuponza sisi..Wakati mwingine viongozi wakubali kwamba wao wenyewe wana mapungufu makubwa na hasa kutokuwa na mbinu za kisiasa.
 
Wakuu Mimi naomba kuuliza! Sasa ina maana hii katiba pitishwa ndio katiba mpya au kuna taratibu endelevu? Kwa nini wananchi tusipigie kura rasimu zote mbili tupate muafaka! Wajumbe sio waamuzi wa maisha ya kila Mtanzania.
 
Unajisumbue bure hesabu zenyewe hujui! Nakuonea huruma sana!

Hizi hesabu alianza mahamedi mtoi akaja Tumaini Makene akaja Mungi ukaja wewe na Leo umerudia makosa Yale Yale uliyofanya Jana na walio Fanya wenzio!

Maswala ya mahesabu hebu achaneni nayo na mfanye mkiwa mmetulia sio kwenye pressure namna hii!
Hujui hesabu we endelea kupotosha!
Kawadanganye bavicha wenzio kuwa wewe unajua hesabu!Yani wote mnaandaliwa vya kuandika lakini hamkagui kilicho andikwa mnarudia makosa ya wenzenu.

Ukweli huko hapa

Ni vizuri na wewe ukafanya analysis kama alivyofanya mwenzio ili sisi tupime...........
 
Wakuu Mimi naomba kuuliza! Sasa ina maana hii katiba pitishwa ndio katiba mpya au kuna taratibu endelevu? Kwa nini wananchi tusipigie kura rasimu zote mbili tupate muafaka! Wajumbe sio waamuzi wa maisha ya kila Mtanzania.
Kama utapewa nafasi ya kupiga kura ni kwa rasimu hii ya 3 kumbuka tu kwamba Ni rasimu ile ile toka ya kwanza isipokuwa imepitia ngazi za marekebisho kama hatua ya uandishi wake.

Kwa hiyo Hata kama wewe utapewa nafasi ya kupiga kura nani atakuwa msimamizi wa kura hizo? bila shaka chombo cha serikali hii hii ilopitisha katiba hii kwa hiyo tumeliwa na inawezekana katiba hii ikaanza kutumika mara moja kwa sababu hata yale waloomba wapinzani walipokwenda kunywa juice Ikulu hawakupewa nafasi ya kuyabadilisha ama kuyajadili.
- Katiba ndio imeshapita. Jadi yetu -Ukigoma kula chakula cha usiku, utalala njaa hakuna wa kukuamsha!
 
kazi tulowatuma UKAWA ni kuhakikisha haki za waanchi zinapatikana. Hili swala la Uzanzibar na Utanganyika halimnufaishi mwananchi hata mmoja kwa njia yoyote ile zaidi ya kugawana umaskini na kujenga nafasi za kazi kwa viongozi wengi zaidi.

Kama Ukawa wangekuwepo mambo mengi sana yangebadilishwa kwa sababu sio kila kitu kilipita kwa kura mia kwa mia, Hapana. Tulichopewa ni katiba ya CCM iloboreshwa na wala hatukutaka katiba ya Chadema ama CUF bali ya wananchi. haya maswala ya Siasa na uroho wa madaraka ndio umetuponza sisi..Wakati mwingine viongozi wakubali kwamba wao wenyewe wana mapungufu makubwa na hasa kutokuwa na mbinu za kisiasa.

Kama unaamini kwamba CCM ilishinda Ununge Shinyanga Mjini, ntakuunga mkono kwamba UKAWA wangalileta impacts...Vifungu vya Rasimu vilikuwa vinapita kwa wengi wape na siyo theluthi za kila upande!
Ripoti za kamati zilionesha kukosekana kwa 2/3 ILA zilipitishwa!Kumbuka hata sura ya 1&6 hazikufikia tamati Bali zilichakachuliwa!
Mawazo kama hayo ni kwa yule asiyewajua CCM walivyo mashetani
 
Unajisumbue bure hesabu zenyewe hujui! Nakuonea huruma sana!

Hizi hesabu alianza mahamedi mtoi akaja Tumaini Makene akaja Mungi ukaja wewe na Leo umerudia makosa Yale Yale uliyofanya Jana na walio Fanya wenzio!

Maswala ya mahesabu hebu achaneni nayo na mfanye mkiwa mmetulia sio kwenye pressure namna hii!
Hujui hesabu we endelea kupotosha!
Kawadanganye bavicha wenzio kuwa wewe unajua hesabu!Yani wote mnaandaliwa vya kuandika lakini hamkagui kilicho andikwa mnarudia makosa ya wenzenu.

Ukweli huko hapa

Ametoa hoja jibu hoja usilete emotions. Mleta hoja kaleta hesabu na wewe toa ya kwako tuone kama inapingana.
 
Back
Top Bottom