Uchakachuaji wa Rasimu ya Katiba huu hapa

Uchakachuaji wa Rasimu ya Katiba huu hapa

Kulikuwa wanaotaka serikali tatu na serikali mbili.serikali mbili wameshinda
Kumbe!!
Ndio maana baada ya kupitishwa wajumbe wakawa wanaimba "LIWALO NA LIWE, POTELEA MBALI, UBAYA UBAYA TU!!"

Nilidhani tunatengeneza makubaliano kama taifa, kumbe ilikuwa ni mashindano katika namuna ya kukomoana, Mtu anasema eti Ubaya ubaya, yaani maana yake, amelipiza ubaya kwa kupitisha katiba ile, maneno hayo ya kejeli dharau, mipasho na matusi yatabaki kama kumbukumbu ya upumbavu wetu kama taifa.
 
Kwani hii mada yako itasaidia kukwamisha kupatikana kwa katiba mpya?

Pole sana ndugu yangu. kinachofanyika hapa siyo kuzuia utaratibu wa KATIBA MPYA YA CCM. kinachofanyika ni kuweka sawa historia, kitu ambacho watu wenye akili na busara huona ni muhimu kufanya.
 
kazi tulowatuma UKAWA ni kuhakikisha haki za waanchi zinapatikana. Hili swala la Uzanzibar na Utanganyika halimnufaishi mwananchi hata mmoja kwa njia yoyote ile zaidi ya kugawana umaskini na kujenga nafasi za kazi kwa viongozi wengi zaidi.

Kama Ukawa wangekuwepo mambo mengi sana yangebadilishwa kwa sababu sio kila kitu kilipita kwa kura mia kwa mia, Hapana. Tulichopewa ni katiba ya CCM iloboreshwa na wala hatukutaka katiba ya Chadema ama CUF bali ya wananchi. haya maswala ya Siasa na uroho wa madaraka ndio umetuponza sisi..Wakati mwingine viongozi wakubali kwamba wao wenyewe wana mapungufu makubwa na hasa kutokuwa na mbinu za kisiasa.

Tumerogwa na nani sisi Watanzania? Hivi una kumbukumbu wewe? Unakumbuka kama MaCCM yalizikataa Tunu za Taifa za Uwazi, Uadilifu na Uwajibikaji huku wajumbe wa UKAWA wakiwemo humo Bungeni?
Hata kwa kususia kwao Bunge la Katiba bado Ukawa walikuwa wakipigania haki ya Wananchi, wengi wenu mnapotosha kwamba Ukawa walitoka kwa ajili ya Uzanzibar na Utanganyika tu. Hapana.
Ukawa walisusia Bunge la Katiba kwa kutaka rasimu iliyotokana na maoni ya Wananchi (watu wanaiita ya Warioba) ndio ijadiliwe, lakini MaCCM yalikuwa na ajenda ya chama chao, wakaisimamia na kupuuza maoni ya wananchi.
Unadhani Ukawa wangefanya nini wakiwa ndani ya Bunge na uchache wao ili kulishinikiza Bunge kujadili rasimu iliyotokana na maoni ya Wananchi? Ilikuwa ni uamuzi sahihi kutokuwa sehemu ya waliochakachua maoni ya Wananchi.
Kwanini kabla ya kuwalaumu Ukawa kutokuwa Bungeni, kwanini usilaumu MaCCM kwa kuitupa rasimu iliyotokana na maoni ya Wananchi? Kwanini unalikalia kimya hilo? Kwanini husemi kitu kuhusu uhuni huo kwa Taifa letu?
Ukawa walifanya kila njia kutetea rasimu ya maoni ya Wananchi, lakini MaCCM yakatumia hila nyingi na hata kuwanunua baadhi ya wajumbe wa Ukawa na kundi la 201 ili wawaunge mkono. Hilo linajulikana, lakini hamsemi.
Isitoshe ukaja kufanyika uhuni wa Mjumbe kuruhusiwa kupiga kura akiwa nje ya Bunge, achilia mbali akiwa nje ya nchi, bado tuendelee kuwa na imani na Bunge hilo kufanya kazi kwa haki? Inasikitisha.
Kiukweli kabisa huu ni uhuni mkubwa sana kufanywa na watawala wetu katika historia ya Tanzania. Inasikitisha sana, inauma sana. Mkumbuke hii nchi ni yetu sote, hakuna mwenye nayo zaidi ya mwingine. Tutafia na kuzikwa hapa.
Hivyo, unaweza kuwa ni upungufu wa akili kuona kwamba Ukawa ndio walioshindwa baada ya rasimu kupitishwa na Bunge la Katiba,Ukweli ni kwamba walioshindwa ni wananchi kwa rasimu iliyotokana na maoni yao kutupwa.
Kwa kawaida tunapokosa mvua, huwa tunamuomba mwenyezi Mungu ili atujaalie mvua. Na tunapoibiwa kilicho haki yetu, pia huwa tunamuomba mwenyezi Mungu kuirudisha haki yetu. Tuanze kufunga na kuomba.
Mungu awabariki sana wapendwa na wazalendo wa nchi yetu, Mungu aibariki Tanganyika na Zanzibar. Mungu awabariki wote wenye mapenzi mema.
Ova
 
hahahaha! Kumbe unaogopa eeh!! kama kweli we kidume au kujike, ingia mtaani kaandamane uone ntakufanya nini....
 
219X(1/3)=73 naambiwa Rutashobolwa maana yake ni asiyefundishika kwa Kihaya. Je, hili ni ukweli au wananionea kwa vile mie najilia samaki nchanga.

mkuu kwakweli zile ni akili za senene kabisa
 
Ninachojua mwanasheria wa zanzibar alikataa baadhi ya sura si katiba yote. Great thinker mara nyingi huwa hana upande! Kwa kuwa unatamani kuwa great thinker endelea kufanya mazoezi tu ya kutoakuwa na upande utafikia viwango vya great thinkers na ninavyokuona hutachukua muda mrefu miaka 40 tu utafikia viwango hivyo

Hizo Sura na Ibara alizokataa akidi ilitimia?
 
Back
Top Bottom