Uchaguzi Zanzibar itakuwaje 2010?

Kibunango
Unayajua jaya ama unabisha kwa kuandika kwa kuwa una access na muda wa kuandika ?

KB unaonaje tukianza kuwa na kautaratibu ka kununu credits za kuandika humu? Ka programu kaitwe AKU yaani Andika Kadri Ununuavyo . Hii itawafanya watu watumie maneno yao kwa uangalifu zaidi kama vile salio la simu.🙂
 
Nakandamiza,
Wanasema eti Amani ni mtoto wa mama, si Karume damu. Ndivyo Ali anavyodai kijiweni. Lakini hii ya kuanza kukampeni miaka miwili kabla ni sign of desperation. Hivi Zanzibar hakuna wengine wanaofaa kuongoza mbali ya akina Karume na Mwinyi?
 

Kamanda punguza jazba, maneno mengine unayoandika yanakumaanisha na wewe vilevile...

Naona umeshikia bendera hili, aidha kwa taarifa tu, Amani alianza kuonjesha nia ya kugombea urais wa zenj tokea mwaka 1995, miaka kumi baadae yaani 2005 ndio akaibuka Ali, tena akitaka kugombea uprezi wa Muungano huko kwa wenye vichwa...Sasa kauli za kukebehi na kama kitu hujui ni kujitusi mwenyewe.


KB unaonaje tukianza kuwa na kautaratibu ka kununu credits za kuandika humu? Ka programu kaitwe AKU yaani Andika Kadri Ununuavyo . Hii itawafanya watu watumie maneno yao kwa uangalifu zaidi kama vile salio la simu.🙂
Hapa umekusudia nini Kamanda? mapendekezo mengine ni sawa na kujitia kitanzi wewe mwenyewe... Manake zile kopi na kupataste sijui utalipia kwa kiasi gani...
 
Kibunango kwa akili yako ilivyo maana waijua mwenyewe . Karume anaweza kuwa Rais wa watu kama sisi ? Hebu jiulize yaani Ali au Aman awe Rais wa watu kama mimi si itakuwa balaa . Nakataa . Oh kumbe ni mtoto wa Mama nje ya ndoa ? Siri hii najua anayo Mama na ndiyo Ali kila leo ni mavurugu na ni debe tupu . Kusoma digirr 3 ni kimoja na kuchukua cheti ukaacha akili kwa waalimu Chuoni ni jambo jingine .So alichukua makaratasi akili akamwachia mwalimu wake . Ali hafai hata huko Zanzibar kuwa rais hata mjumbe wa nyumba kumi . Kwanza msikilize then njoo tuseme.
 
Watangaze Karume Kingdom kabisa ili fedha za walipa kodi zisipotee bure kwa uchaguzi hewa,zinazpotea kwa ufisadi zinatosha.
 
Nasikia Ghalib Bilal aliahidiwa amwachie Karume urais 2005 yeye atapewa nafasi 2010 kwa hiyo yupo mkao wa kula anajiandaa kuchukua urais Zanzibar,kama iliyvyokuwa kwa Jakaya 2005
 

JAKAYA Kikwete maarufu kama JK, alichaguliwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Mei 4, mwaka huu mjini Dodoma.

Kikwete ambaye kitaaluma ni Mchumi na Ofisa wa Jeshi Mwandamizi mstaafu aliyefikia cheo cha Luteni Kanali, aliibuka mshindi kwa kuvuka vizingiti vitatu vya kumpata mgombea ndani ya CCM.

Aliibuka kuwa mmoja wa wanachama watano wa CCM waliovuka kihunzi cha mchujo wa Kamati Kuu ya CCM.....

Awali, katika kinyang'anyiro hicho pia walikuwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, John Malecela, Balozi Ali Karume, Balozi Patrick Chokala, John Shibuda na Iddi Simba, ambaye ni Mbunge wa Ilala anayemaliza muda wake.

zaidi hapa
 
Kwa jinsi JK anavyopenda serikali yenye wizara nyingi kwanini asituweke wizara maalumu kwa ajili ya vichekesho na Ali Karume awe waziri.

Digrii ya Kusonga Ugali
 
Kwa jinsi JK anavyopenda serikali yenye wizara nyingi kwanini asituweke wizara maalumu kwa ajili ya vichekesho na Ali Karume awe waziri.

Digrii ya Kusonga Ugali

Hiyo wizara ya vichekesho na porojo si ndo anaongoza Khatib? Kumbuka MKKJ alimwita "Comical Khatib"
 
Kama yeye na kaka yake hawatatumia dola ili kumsaidia ashinde, why not? Tusimhukumu kwa sababu Kaka yake ni rais au kwa sababu Baba yake alikuwa Rais, hapo tutakuwa hatumtendei haki mtanzania mwenzetu. Tutachotakiwa kujua anataka urais ili kiwe nini? Kuendeleza Zanzibar? Au kuweka tu historia?
Labda swali la kujiuliza ni kwanini ameamua kuweka historia ya kutangaza mapema namna hii? Kuna nini?
 
mwaka juzi kuna wakati balozi karume kipindi chake cha ubalozi kiliisha akarudi nyumbani...alikuwa akijinadi kwa uhakika kuwa lazima apewe kazi anayoitaka ..kama rais akimpangia kazi asiyoitaka ..ataikataa..
 
Hii thread ni fitina na majungu tu!
Mnataka Ali aondolewe ili wewe upewe ubalozi?

Hampewi ng'o!
 
Hii thread ni fitina na majungu tu!
Mnataka Ali aondolewe ili wewe upewe ubalozi?

Hampewi ng'o!

watu kama hawa wameshazoea UTWANA ..basi tena kila mara wataona halali hata bwana akiteleza...hakuna anayetaka cheo cha ubalozi hapa...watu wanakata ishu..na ishu si ubalozi wa kudumu wa ali karume...bali tunamjadili baada ya kutamka kuwa anautaka urais wa zanzibar...

,,ukitaka kuujua upande wa pili wa familia ya kifalme ya KARUME..tafuta mandishi ya ALI NABWA al marhoom!!!!
 
Balozi Ali Karume atangaza kugombea urais wa Zanzibar




Kigeugeu Re:

Hii thread ni fitina na majungu tu!
Mnataka Ali aondolewe ili wewe upewe ubalozi?

Hampewi ng'o!


Ndio maana huwa tunasema kuwa viongozi wetu ni reflection yetu sisi wananchi, maana kiongozi kasema kwanza halafu mwananchi anyetaka kutawaliwa naye kajibu hapo chini, kweli JF tuna kazi kubwa sana ya kuelimisha wananchi.

Mungu Aibariki tu Tanzania Yetu, na vilema wetu wa akili awabariki pia!
 
Ndio maana huwa tunasema kuwa viongozi wetu ni reflection yetu sisi wananchi, maana kiongozi kasema kwanza halafu mwananchi anyetaka kutawaliwa naye kajibu hapo chini, kweli JF tuna kazi kubwa sana ya kuelimisha wananchi.

ES,

Ama kweli Tz we have a very long way to go! Kwani Karume alizaliwa awe balozi?
 
I Like Dat Es,,kibunango.....

""walizaliwa Wawe Mafisadi"'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…