Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
KUTOKUWEPO kwa jina la mgombea urais wa serikali ya wanafunzi (DARUSO) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Odong Odwar raia wa Uganda aliyekuwa akikubalika na wanachuo walio wengi, baada ya jina lake kuondolewa katika kinyanganyiro hicho kwa madai kuwa hakuwa na sifa ya kuwa chuoni hapo kimesababisha wanafunzi wengi kususia uchaguzi huo.
Pamoja na wanafunzi wengi kususia uchaguzi ila wachache waliojitokeza kupiga kura waliongozwa na wasichana, huku wavulana wengi wakionekana kuvinjari sehemu mbalimbali katika vituo vya kupigia kura chuoni hapo bila kupiga kura.Hata hivyo ilielezwa kuwa sababu kubwa iliyofanya wavinjari katika vituo hivyo ni kuwabainisha wenzao ambao walidhaniwa kuwa wangekaidi na kusaliti msimamo wao.
Mwitikio wa uchaguzi haukuwa mkubwa baada ya wapiga kura wengi kukataa kupiga kura kwa kile walichodai kuwa mgombea waliyekuwa wanamtaka hakuwepo hivyo hawakuwa na sababu ya kupiga kura kumchagua mtu asiye chaguo lao.Hata hivyo kulikuwa na kampeni ya chinichini chuoni hapo iliyolenga kuzua wanafunzi kutopiga kura ingawa baadhi yao walionekana wakivinjari katika vituo vya kupigia kura bila kupiga kura.Habarii hii na Jackson Odoyo na Christopher Maregesi
Akitoa maoni yake kuhusu uchaguzi huo, Mwendamseke alisema kwa hali iliyojitokeza, Rais mpya wa Daruso atakuwa na kazi ngumu katika uongozi wake, kwa sababu idadi kubwa ya wabunge ni wale waliokuwa wanamuunga mkono Odwar.
Alisema anatakiwa kuchanga karata zake vizuri, kwani chuo hicho kina wanafunzi zaidi ya 15,000, lakini waliopiga kura ni 730 tu na rais kushinda kwa kura 395..
HII NI AIBU KWA TAIFA, UCHAGUZI GANI WALIOMCHAGUA RAIS NI ASILIMIA 2 na nukta kadhaa tu ya WAPIGA KURA? HAINA TOFAUTI NA ZILE KURA ZA MARUHANI KULE PEMBA. HIZI NI PROTEST VOTES BY ABSCONDENCE. ILA IPENDEZA ZAIDI KAMA WOTE ELFU 15 WANGEKWENDA NA KUPIGA KURA ZA HAPANA! HATA HIVYO UJUMBE UMEFIKA KWA WATAWALA, HAO WAGOMBEA HAWATAKIWI. NA KWANINI HILO BUNGE LISIPIGE TU KURA YA KUTOKUWA NA IMANI YA HUYO RAIS MPYA UCHAGUZI UKARUDIWA TENA? AU KWANINI YASIFANYIKE MAPINDUZI TU?
Asha
Akitoa maoni yake kuhusu uchaguzi huo, Mwendamseke alisema kwa hali iliyojitokeza, Rais mpya wa Daruso atakuwa na kazi ngumu katika uongozi wake, kwa sababu idadi kubwa ya wabunge ni wale waliokuwa wanamuunga mkono Odwar.
Alisema anatakiwa kuchanga karata zake vizuri, kwani chuo hicho kina wanafunzi zaidi ya 15,000, lakini waliopiga kura ni 730 tu na rais kushinda kwa kura 395..
HII NI AIBU KWA TAIFA, UCHAGUZI GANI WALIOMCHAGUA RAIS NI ASILIMIA 2 na nukta kadhaa tu ya WAPIGA KURA? HAINA TOFAUTI NA ZILE KURA ZA MARUHANI KULE PEMBA. HIZI NI PROTEST VOTES BY ABSCONDENCE. ILA IPENDEZA ZAIDI KAMA WOTE ELFU 15 WANGEKWENDA NA KUPIGA KURA ZA HAPANA! HATA HIVYO UJUMBE UMEFIKA KWA WATAWALA, HAO WAGOMBEA HAWATAKIWI. NA KWANINI HILO BUNGE LISIPIGE TU KURA YA KUTOKUWA NA IMANI YA HUYO RAIS MPYA UCHAGUZI UKARUDIWA TENA? AU KWANINI YASIFANYIKE MAPINDUZI TU?
Asha
Jamani jamani! Kwa nini mnapenyeza hizi siasa zenu tenganishi na gombanishi kwenye masuala ya wanafunzi? Waacheni wanafunzi waendeshe mambo yao huko shuleni, sasa ninyi wanasiasa kwa nini mnawavuruga? Mnazungumzia bunge sijui kitu gani, bunge la shuleni ni bunge? Hebu acheni utani! Haya mambo ya viranja wa shule mnayaingilia ya nini kama si tu kupenda fujo? Huko hakuna wabunge wala chochote, kuna viranja na wasaidizi wao, basi! Na sifa ya kwanza ya kuwa kiranja shuleni ni lazima kwanza uwe mwanafunzi, ukifeli shule au ukifukuzwa kwa utovu wa nidhamu na ukiranja wako utaisha (hata kama umejibandika fancy titles kama "rais", "waziri", "mbunge" etc, vyote hivi ni delusional).
Binafsi nimeshachoshwa kabisa na hii mijadala ya viranja wa shule hapa JF. Na tena kuna elements za grandiosity zinazoambatana na hii kitu, maana sioni viranja wa vyuo vikuu vingine wakijadiliwa hapa, bado kuna watu wanadhani Tanzania kuna chuo kikuu kimoja tu! Wanafunzi wa chuo kikuu Mlimani mtabakia kujadili mambo ya viranja wenu kutwa kucha hapa, wakati wenzenu wa Tumaini, St Augustine, Dodoma, Morogoro Muslim nk wanapiga kitabu kisawasawa, mwishowe wao watafaulu na kutoka na degree nzuri na kuchukua nafasi muhimu za ajira, ninyi mtabaki na ujinga wa kugombea uchaguzi wa viranja! Upuuzi tu! Na nimefurahi sana kuona taasisi mbalimbali zikiwaajiri bila uaguzi wahitimu wa vyuo vyetu vikuu vingine zaidi ya Mlimani, nimeona mawakili, tutorial assistants (hata Mlimani wapo wa kutoka Tumaini), waalimu, madaktari na wataalamu wengine.
Kalieni migomo tu, mkisusa wenzenu wanakula!
Hii nayo kali jamani
Katiba ya Daruso inasemaje kuhusu kura za kumchagua rais??
au hata akishinda kwa kwa asilimia 2 ya wanachuo waliotakiwa kupiga kura anachukua urais??
Haya bwana kweli kazi hipo hapo???
Mkuu Kithuku,
demokrasia ya kuchagua viongozi wa chama cha wanafunzi wa vyuo vikuu haifai kuachiwa ikaingiliwa na watu wasioamini uhuru wa boz la kura. Wakiachiwa mlimani watakwenda kwingine na mchezo utakuwa the same.
Bado hakuna report kuwa uongozi wa vyuo vingine ulivyotaja hapa umeingilia chaguzi za wanafunzi. Hiyo ikitokea utasikia the same dozier ikitokea hapa kama kawa.
Kwa nini uongozi wa chuo ambao kwa miaka mingi umekuwa unawapa wanafunzi uhuru wa kuchagua viongozi wao leo all of the sudden baada ya Mukandala kuwa VC umeamua kuingilia power ya box la kura na kutaka kuweka mtu wanayempenda wao?
Uongozi wowote makini wa taasisi ya elimu (shule au chuo) lazima uhakikishe kuwa viranja wanaochaguliwa kuongoza wanafunzi wenzao ni miongoni mwa watu wanaoweza kufanya nao kazi. Kiranja yuko baina ya wanafunzi wenzake na uongozi wa chuo, kwa hiyo viongozi wa chuo ni wadau muhimu, hawawezi kupuuzwa katika suala la upatikanaji wa viranja. Vyuo vyote huwa vinahusisha maofisa wao katika hatua fulanifulani za mchakato wa kupata viranja, na hii pia ni sehemu ya malezi ya hao wanafunzi, hawawezi kuachwa wajipeleke tu wanavyotaka, lazima taratibu na kanuni zizingatiwe, zikiwamo za malezi.
Kama menejimenti ya UDSM walikuwa na sababu za kuamini kuwa mtu fulani miongoni mwa wanafunzi hawawezi kufanya naye kazi kama kiranja, hakuna mtu nje ya chuo mwenye mamlaka ya kuwaingilia katika uendeshaji wa chuo, wanafunzi ndio wanaopaswa kujadili na walimu wao na wafikie muafaka, kwani wao(wanafunzi na walimu) ndio wadau.
Ninavyoelewa mimi na kwa uzoefu wangu kama mwalimu, mwanafunzi asiyekubalika kwa walimu na utawala wa chuo kamwe hafai kuwa kiranja, na iwapo kwa bahati mbaya amepitishwa kitakachofuatia ni fujo tu, maana badala ya kuendesha mambo kwa faida ya wadau wote wa chuo, atakuwa kila siku na ugomvi na utawala na watakaoumia zaidi ni wanafunzi wenzie, na matokeo yake hata viwango vya elimu vitashuka. Na hakuna mwalimu anayependa kuona kiwango cha ufanisi wake kinashuka sababu tu ya kiranja fulani.
Napenda kukutaarifu kuwa vyuo vyote makini hufuatilia uchaguzi wa wanafunzi kuhakikisha wanapatikana wawakilishi wanaoweza kufanya kazi vizuri na wadau wote chuoni, na ndio maana maofisa wa chuo kama Dean of Students huhusika katika mchakato na hutoa taarifa kwa uongozi wa juu. Sasa chuo kikiwa legelege na kumbeleza demokrasia feki (ambayo mimi naona ni mdebwedo tu), matokeo yake ni kuruhusu watu wenye fujo kuingia katika uongozi wa wanafunzi na kuharibu kabisa dhana nzima ya uwakilishi wa wanafunzi katika masuala ya uendeshaji wa chuo.
Uongozi wowote makini wa taasisi ya elimu (shule au chuo) lazima uhakikishe kuwa viranja wanaochaguliwa kuongoza wanafunzi wenzao ni miongoni mwa watu wanaoweza kufanya nao kazi. Kiranja yuko baina ya wanafunzi wenzake na uongozi wa chuo, kwa hiyo viongozi wa chuo ni wadau muhimu, hawawezi kupuuzwa katika suala la upatikanaji wa viranja. Vyuo vyote huwa vinahusisha maofisa wao katika hatua fulanifulani za mchakato wa kupata viranja, na hii pia ni sehemu ya malezi ya hao wanafunzi, hawawezi kuachwa wajipeleke tu wanavyotaka, lazima taratibu na kanuni zizingatiwe, zikiwamo za malezi. Kama menejimenti ya UDSM walikuwa na sababu za kuamini kuwa mtu fulani miongoni mwa wanafunzi hawawezi kufanya naye kazi kama kiranja, hakuna mtu nje ya chuo mwenye mamlaka ya kuwaingilia katika uendeshaji wa chuo, wanafunzi ndio wanaopaswa kujadili na walimu wao na wafikie muafaka, kwani wao(wanafunzi na walimu) ndio wadau. Ninavyoelewa mimi na kwa uzoefu wangu kama mwalimu, mwanafunzi asiyekubalika kwa walimu na utawala wa chuo kamwe hafai kuwa kiranja, na iwapo kwa bahati mbaya amepitishwa kitakachofuatia ni fujo tu, maana badala ya kuendesha mambo kwa faida ya wadau wote wa chuo, atakuwa kila siku na ugomvi na utawala na watakaoumia zaidi ni wanafunzi wenzie, na matokeo yake hata viwango vya elimu vitashuka. Na hakuna mwalimu anayependa kuona kiwango cha ufanisi wake kinashuka sababu tu ya kiranja fulani.
Napenda kukutaarifu kuwa vyuo vyote makini hufuatilia uchaguzi wa wanafunzi kuhakikisha wanapatikana wawakilishi wanaoweza kufanya kazi vizuri na wadau wote chuoni, na ndio maana maofisa wa chuo kama Dean of Students huhusika katika mchakato na hutoa taarifa kwa uongozi wa juu. Sasa chuo kikiwa legelege na kumbeleza demokrasia feki (ambayo mimi naona ni mdebwedo tu), matokeo yake ni kuruhusu watu wenye fujo kuingia katika uongozi wa wanafunzi na kuharibu kabisa dhana nzima ya uwakilishi wa wanafunzi katika masuala ya uendeshaji wa chuo.
HII NI AIBU KWA TAIFA, UCHAGUZI GANI WALIOMCHAGUA RAIS NI ASILIMIA 2 na nukta kadhaa tu ya WAPIGA KURA? HAINA TOFAUTI NA ZILE KURA ZA MARUHANI KULE PEMBA. HIZI NI PROTEST VOTES BY ABSCONDENCE. ILA IPENDEZA ZAIDI KAMA WOTE ELFU 15 WANGEKWENDA NA KUPIGA KURA ZA HAPANA! HATA HIVYO UJUMBE UMEFIKA KWA WATAWALA, HAO WAGOMBEA HAWATAKIWI. NA KWANINI HILO BUNGE LISIPIGE TU KURA YA KUTOKUWA NA IMANI YA HUYO RAIS MPYA UCHAGUZI UKARUDIWA TENA? AU KWANINI YASIFANYIKE MAPINDUZI TU?
Asha
dada Asha.. ni 0.26%
Nasema hivi, na naomba nieleweke vizuri. Anapoteuliwa mtu kuwa mkuu wa taasisi ya kielimu, anakabidhiwa dira, mwelekeo na malengo ya taasisi hiyo na anawajibika kwa aliyemteua kuhusu utekelezaji. Mimi nikipewa nafasi kama hiyo, siwezi kuruhusu kamwe mazingira yoyote yatakayonisababisha nishindwe kutimiza wajibu wangu ipasavyo. Miongoni mwa mazingira kama hayo, ni viongozi wa wanafunzi wenye hulka ya kupenda migogoro, ambayo inaweza kwa hakika kuwaharibia kazi viongozi wa chuo na waalimu. Kwa hiyo uongozi wa chuo una wajibu wa kuwashauri wanafuzi na kuwasaidia kimalezi ili wachague viongozi wanaokubalika na wanaoweza kufanya kazi na utawala wa chuo. Jitihada za kushauri zikishindikana (mfano kutokana na kiburi cha wanaoshauriwa), basi ni wajibu wa uongozi wa chuo kuweka msimamo wazi kuwa mtu fulani hatumtaki, na kama hilo mnaita kuingilia basi sioni ubaya wa kuingilia huko. Siwezi kumkubali mtu wa kuja kuniharibia kazi, eti nabembeleza demokrasia, huo ni upuuzi! Demokrasia ya wanafunzi chuoni ina mipaka, na mipaka yake inaishia kwenye misingi, kanuni, viwango na taratibu ambazo utawala wa chuo ndio unaosimamia. Pale ambapo nina mamlaka (mfano kama ni sehemu ya utawala wa chuo), sitamkaribisha kwenye uongozi mtu wa kuja kuniharibia kazi, huyo hatapata uongozi hata akifanya nini, maana mambo yakiharibika chuoni hawaulizwi viranja wa wanafunzi (hawa ni wa kupita tu, kila mwaka wanachaguliwa wapya), watakaoulizwa ni utawala wa chuo. Kwa hiyo utawala una haki na wajibu wa kulinda viwango vya taaluma, nidhamu, na kusimamia misingi na dira ya chuo. Mwanafunzi asiyefaa uongozi kwa maoni ya utawala wa chuo (ambao wameaminiwa na taifa kama walezi wa wanafunzi hao) kamwe asiruhusiwe kuwa kiongozi chuoni, anaweza kwenda kuwa kiongozi mahali pengine huko atakapoondoka chuoni, anaweza kwenda kuwa diwani huko au chochote atakachoweza huko kwingine ambako uongozi wa chuo hauhusiki, lakini ndani ya chuo ni lazima mamlaka ya chuo iheshimiwe. Huo ndio msimamo wangu.
Kithuku mbona hao akina Mukandala wasikate kwa maelezo ya wazi kama yako kwamba hawawataki wale viongozi wengine bali wanawataka ama wanamtaka huyu aliyechaguliwa basi badala ya kuwapiga na kuanza kuuliza uhalali wao wa kuwepo Chuoni hapo ?Mbinu hizi nawe ungaliweza kuzitumia ili kumridhisha bwana wako ambaye amekupa madaraka usionekane kushindwa ?
Bado, Mkuu, nami haujani'convince' kuwa kwa sababu wao ni wanafunzi wenye grandiose titles basi menejimenti ya chuo ndiyo wenye mamlaka ya kuwachagulia viongozi! Kwa msimamo wako, basi hawa vijana wageuzwe idara ya Chuo ili uongozi waweze kufanya wanachotaka. Hakuna mahali ambapo uongozi unaingilia mambo ya wanafunzi, period, isipokuwa pengine China na Zimbabwe! Ni hiki kiburi kwa wale wanaoongoza cha kutokuwasikiliza wanafunzi ati kwa sababu wao ndio waliopewa dhamana ya kuongoza ndiko kunakopelekea migomo na malumbano yote kuanzia kwenye Vyuo Vikuu (hata hicho cha Tumaini pamewahi kutokea malumbano) hadi shule za msingi. Ni lazima wale wanaopewa dhamana ya kuongoza wajifunze kuwaheshimu wanaowaongoza. Vitisho na ubabe havina nafasi katika jamii ya leo. Kuwaita viranja ni kuwatukana.
Hizo students unions unazozizungumzia ni kwenye mifumo iliyokuwa na vyuo vikuu kwa miaka mingi na zimeweza kufikia mahali pa kuweza kujiendesha bila kutegemea ada kutoka kwa wanafunzi. Student union hizo zinamiliki mabweni, clubs na kadhalika na hauwezi kuzilinganisha hata siku moja na DARUSO.
Unachodai wewe si kuheshimu sheria, bali ni kuwanyenyekea viongozi. Masuala ya uchaguzi, kukosekana kwa maji, n.k. vinaingiaje kwenye huko kutii sheria?