Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,938
- 6,846
Kithuku,
Wote tuna ugonjwa wa kupenda. wewe kama mwalimu unavutia kwa walimu wenzako. Utamkataaje mwanafunzi kwa dhana kuwa ati akichaguliwa atafanya fujo? Kwa nini asichaguliwe kwanza na akifanya fujo baadaye sheria ifutae mkondo? haya ni yale yale ya wakina Bush kudai demokrasia Palestina na kukataa uamuzi wa wapalestina kuchagua Hamas! Ukikubali demokrasia hauwezi kuingilia unapoona inaelekea usikokutaka.
Migomo, maandamano yote ni ishara ya kukata tamaa na mfumo uliopo. Kama mfumo huo unaoutetea ungekuwa unafanya kazi haya yote yasinge tokea. Na vyombo kama hivi vikitumiwa vizuri vinasaidia sana kuepusha haya matatizo kwa sababu wanakuwa wa kwanza kuufahamisha uongozi yanayowakera wanafunzi na vile vile kuuelezea msimamo wa viongozi kwa wanafunzi. habari mbaya ikiletwa na mtu waliye na imani nae mara nyingi wanachelea kufanya fujo. Ni pale uongozi unapotaka kuwaburuza, kukataa kuwaambia ukweli n.k. ndipo hali inapochafuka. Ufaransa Vyuo Vikuu viliingia mitaani mwaka 1968 kudai heshima uhuru zaidi katika vyuo vyao. Wanafunzi hawa huwa hawasiti kuingia mitaani kwenye suala ambalo wao wanaona linawagusa, kuanzia ada hadi vita vya vietnam!
Mfano wa Kihiyo haukuwa sahihi. Yule aliumbuliwa na wenzake aliodai alisoma nao na baada ya kupitia kumbukumbu ndipo ikaonekana kuwa kweli alifoji. Hapa utawala ulioisha mkubali huyu mwanafunzi wanatoa shutuma baada ya kuona kuwa anaweza kushinda uchaguzi! Hakuna mahali walipoleta mashahidi au ushahidi wa hizo shutuma zao. Kwa nini utawala huo huo usiulizie huko Uganda wenyewe ili kupata uhakika wa shutuma zao kabla ya kuzitoa hadharani. Itakuwaje leo ndio wadai vyeti lukuki ambavyo pengine vimeishapotea. Wanashindwa nini wao kuwasiliana na wizara ya elimu, vyuo, shule za sekondari, msingi hadi chekechea kabla ya kufanya uamuzi huo? Mpaka sasa sijaona mahali walipotoa uthibitisho kuwa huyu bwana amefoji nje ya hizo tuhuma. Wangekuwa na uthibitisho wala wasingempa huo muda wa kwenda kuleta vyeti vingine. Ni summary dismissal. Ni mchezo wa kitoto wanaotaka kufanya walimu wenzako.
Amandla!