Serikali inapaswa kuendelea kufanya maboresho katika uchaguzi wa shule za kata

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wakuu habari za uzima?

Leo nimeona nigusie kidogo kuhusu shule za serikali zinapofanya uchaguzi kwa wanafunzi waliofaulu kuendelea na masomo ya sekondari kutokea msingi.

Kama sitakuwa na nimekosea mchakato wa kumuhamisha mwanafunzi kutoka shule aliyopangiwa kwenda shule nyingine huwa ni shuguli kubwa na wazazi wengi hawana uelewa waanzie wapi.

Kuhamisha wanafunzi mara nyingi hutokana na sababu ya umbali, nafikiri serikali inapaswa kutazama upya katika uchaguzi kipindi wanapopangia wanafunzi.

Kwanini wanafunzi wasiwe wanachaguliwa katika maeneo yao ya karibu ili kupunguza gharama kwa wazazi na tatizo la usafiri lililokithiri hapa dar_es_salaam?

Wanafunzi wengi utawakuta mpaka saa mbili wapo vituo vya daladala, kila gari linalokuja linakimbizana na muda kukusanya hesabu ya boss huku wanafunzi Hawa wakiendelea kuwepo tu katika vituo hivyo.
Wakati wakirudi kutoka shule stori inakuwa ni ile ile mpaka saa mbili usiku wanafunzi bado wapo wanalanda landa barabarani.

Mtoto anafika nyumbani amechoka hoi! Hivi mtoto huyu anasoma sangapi??

Pili, serikali ijaribu kuangalia namna ya kuzifanyia marekebisho mchakato mzima wa kuhama ili kuwe na wepesi wa kuhamisha mtoto.

Sisemi kama mchakato huu ni mbovu ila tujaribu ku urahisisha.
Tazama mfano.

1.unaandika barua ya kuomba nafasi kwenye shule mwanafunzi anayotaka kuhamia, kama nafasi ipo ikipitishwa......
2. Barua utapeleka kwenye shule anayotaka mwanafunzi ili ipitishwe na mkuu wa shule na ikipitishwa....
3. Unapeleka kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri anakotoka mwanafunzi ili naye aipitishe...
4. Maombi hayo utayapeleka kwa katibu tawala mkoa kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uhamisho.

Wazazi wengi hawajui hata waanzie wapi na waishie wapi, na wanafunzi nao pia baadhi hawafahamu.

Mtoto amesoma ukonga mpaka anamaliza akifaulu anaenda kutupwa chanika zingiziwa sehemu ambayo itamfanya arudi pale pale kwenye hadha ya usafiri.
mtoto amekulia na kusomea g/mboto kwanini asipelekwe juhudi hapo na anaenda kutupwa ubungo au Temeke?

Kwanini watoto Hawa msiwachague maeneo ya karibu na sehemu wanazotoka ili kuepusha hadha nzima wanayokumbana nayo katika usafiri hapa Dar_es_salaam?

Faida zitakazopatikana ni pamoja;
•mtoto atafika shule kwa wakati huku akili ikiwa haijachoka.
•ni rahisi mzazi kufika shule kujua maendeleo ya mtoto na kuhudhuria vikao.
•mtoto atajipatia muda wa kujisomea.

Kama serikali itaboresha shule hizi za kata kwa kuongeza walimu, na vifaa vya kufundishia nafikiri hili litasaidia kupunguza watoto kuishia kwenye mabanda ya mihogo, mimba na athari zingine wanazokumbana nazo.

Nitoe rai kwa wazazi kufatilia kwa juhudi maendeleo ya watoto wao.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom