Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 58
Kulingana na hii report toka kwa mwanabulogi hakingowi. Uchaguzi wa serikali ya wanafunzi anaotaka Mukandala hatimaye umefanyika bila yule mgombea mwenye umaarufu na ambaye dikiteta mukandala hakutaka kumruhusu agombee na kupelekea machafuko na uonevu wa FFU wiki jana.
Hatimaye Mukandala ameonyesha its true colors kwa kulazimisha kile anachotaka yeye kwenye throats za wanafunzi huku akijinadi kuwa mtetezi na mwendelezaji wa demokrasia Tanzania. No wonder ni mshauri wa Kikwete na serikali ya ccm iliyowapiga wafuasi wa Chadema siku chache kabla ya uchaguzi wa kiteto.
kwa habari zaidi na picha za matukio click hapa au visit blog ya hakingowi

KUTOKUWEPO kwa jina la mgombea urais wa serikali ya wanafunzi (DARUSO) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Odong Odwar raia wa Uganda aliyekuwa akikubalika na wanachuo walio wengi, baada ya jina lake kuondolewa katika kinyanganyiro hicho kwa madai kuwa hakuwa na sifa ya kuwa chuoni hapo kimesababisha wanafunzi wengi kususia uchaguzi huo.
Pamoja na wanafunzi wengi kususia uchaguzi ila wachache waliojitokeza kupiga kura waliongozwa na wasichana, huku wavulana wengi wakionekana kuvinjari sehemu mbalimbali katika vituo vya kupigia kura chuoni hapo bila kupiga kura.Hata hivyo ilielezwa kuwa sababu kubwa iliyofanya wavinjari katika vituo hivyo ni kuwabainisha wenzao ambao walidhaniwa kuwa wangekaidi na kusaliti msimamo wao.
Mwitikio wa uchaguzi haukuwa mkubwa baada ya wapiga kura wengi kukataa kupiga kura kwa kile walichodai kuwa mgombea waliyekuwa wanamtaka hakuwepo hivyo hawakuwa na sababu ya kupiga kura kumchagua mtu asiye chaguo lao.Hata hivyo kulikuwa na kampeni ya chinichini chuoni hapo iliyolenga kuzua wanafunzi kutopiga kura ingawa baadhi yao walionekana wakivinjari katika vituo vya kupigia kura bila kupiga kura.Habarii hii na Jackson Odoyo na Christopher Maregesi
kwa habari zaidi na picha za matukio click hapa au visit blog ya hakingowi