Bila shaka sisi wapenda siasa tunajua kuwa kuna kijana mwenye umri wa miaka 44 ambaye anaweza kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais huko Senegali.
Mitandaoni watu wanajadili kuhusu umri na uongozi wa nchi. Kutokana na assessment yangu ya haraka huko mitandaoni, nimeona kuwa vijana hawako tayari kuongozwa na vijana. Sababu kubwa zikiwa ni 1) hofu ya viongozi vijana kuweza kubadili katiba ili waendelee kukaa madarakani, 2) kutokuwaamini vijana kwa sababu hawana uzoefu, 3) wasiwasi kuwa vijana wanaweza kulewa madaraka.
Sababu hizo ni za msingi ila nasikitika kuona kuwa zinatolewa na vijana wenyewe. Hapo ndiyo naelewa kwa nini vijana wengi hawajitosi kwenye siasa na wachache waliopo wanaishia kuwa chawa na wachumia tumbo.
Ikiwa vijana wenyewe hawajiamin, hata wazee hawawezi kutuamini. Nadhani hii ndiyo sababu hata mzee akistaafu anapewa tena extension ya mkataba coz hakuna vijana wanaojiamini.
Katika kampeni zake FAYE alisema wao wanahitaji mageuzi makubwa na kuwa wazee waliopo wameshindwa kwa kiasi kikubwa.
Ikumbukwe kuwa vijana wawili walijitokeza kuwania nafasi ya juu zaidi katika nchi yao (Senegal).
1. BASSIROU D. Faye (Jinsia: Me Umri: 44)
2. ANTA B. Ngomu (Jinsia Ke, Umri: 39).