Uchaguzi wa Bawacha moto mkali, fomu zaanza kuchukuliwa kwa kasi kubwa, wazito waanza kujitokeza kwa kishindo

Waliojitokeza mapema kabisa kutia nia ni pamoja na Kamanda Elizabeth Mwakipesile ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bawacha wa Mkoa wa Mbeya , Huyu yeye ametia nia kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara .

View attachment 1715034

Nako kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Bawacha Taifa amejitokeza mzito mwingine anayeitwa Aisha Luja , Huyu kamanda mpaka tunaingia mitamboni yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati

View attachment 1715053

Taarifa zilizotufikia zinadokeza kwamba kuna Majina mazito zaidi na ya kushangaza sana yasiyotarajiwa kabisa ambayo yako mbioni kujitokeza kutia nia ya kuchukua uongozi wa Bawacha , endeleeni kutega sikio

Ikumbukwe kwamba mpaka hivi sasa Bawacha ndio Taasisi ya akina mama inayotajwa kuheshimika na kuwa bora zaidi barani Afrika .

Tutaendelea kuwaletea majina mengine ya watia nia wengine kwa kadri yanavyotufikia , endelea kubaki hapa hapa JF kwa taarifa za Uhakika
Kama hutojali mkuu unaweza kutuwekea na CV zao?
 
Hawa ndio mwisho wa siku wanatusaliti kama mdee na wenzake

Safari hii chujio liwe makini kuchungulia walioletwa na CCM na kuwajua ni kuangalia nani anamwaga mipesa hovyo, pili historia ya nyuma nje ya chama na ndani ya chama izingatiwe kwa kila mgombea na mwisho elimu ya mgombea iwe angalau form four kwenda mbele pamoja na kuolewa iwe ni sifa mojawapo ili kuzuia new strains covid 19x
 
Kama hutojali mkuu unaweza kutuwekea na CV zao?
Una hoja nzuri , lakini tunatarajia watia nia zaidi ya elfu 2 , sasa kuweka wasifu wa kila mtu si rahisi , tutakachofanya ni kuweka CV ya watakaopitishwa kugombea , vuta subira kidogo
 
Wale COvido walijiona wao ndiyo chama - ha ha ha kwishney - CDM bana mnatupa rahaa nyieee - hamjui tu!!
 
Safari hii chujio liwe makini kuchungulia walioletwa na CCM na kuwajua ni kuangalia nani anamwaga mipesa hovyo, pili historia ya nyuma nje ya chama na ndani ya chama izingatiwe kwa kila mgombea na mwisho elimu ya mgombea iwe angalau form four kwenda mbele pamoja na kuolewa iwe ni sifa mojawapo ili kuzuia new strains covid 19x
hicho kigezo cha elimu ondoa kabisa kimekujaje wakati hata mwenyekiti wetu alipata dv0 utatusamehe pia cha kuolewa mwenye hii saccos yake alimwacha mkewe na kujitwalia mbunge wa viti maalum hicho kigezo hakitufai
 
Hizo ni fursa za kupata visibility ya kuja kuhamia CCM.
ni kweli kabisa anachukua fomu asipoteuliwa anajiengua na kuja CCM kwa kigezo cha kusema wana kikundi kutoka kaskazini hawana demokrasia kumbe ilikuwa tiketi ya kuondoka
 
Muhimu : Wote wanaofika kwenye ofisi za Chadema kuchukua fomu za kuomba uongozi WAZINGATIE MWONGOZO WA WHO KATIKA KUDHIBITI CORONA
 
Labda kwa faida yako na wengine ni kwamba rufaa ya wahusika inahusu kuvuliwa uanachama, si kuvuliwa uongozi, Kamati kuu kabla ya kuwavua uanachama kwanza iliwavua uongozi, halafu baadaye ikawavua uanachama.

Kwahiyo wao wamekata rufaa ya kupigania uanachama wao ili waendelee kuwa wabunge, hii ni kwa sababu wanaupenda ubunge kuliko uongozi wa Chadema maana katiba hii hii ya Tanzania inayolalamikiwa inamtaka mtu ili awe mbunge ni lazima adhaminiwe na chama cha siasa kwa maana ya kuwa mwanachama na kwa viti maalum ni lazima wapitishwe na chama chao kwanza, kumbuka hawa walijiteuwa wenyewe kwa msaada wa CCM, kuanzia aliyekuwa jela na waliokuwa uraiani.

Kuhusu kujadiliwa rufaa yao hili litafanyika bila shaka bali litafanyika baada ya kuitishwa kikao cha Baraza kuu na kwa mujibu wa Katiba ya Chadema Kikao hiki kwa mwaka kinaitishwa mara 1 tu, huwa kinapangwa na kinakuwa na ajenda nyingi, hiki si kikao cha dharula, muda ukifika kitaitishwa tu.

Nadhani kwa haya machache angalau umeelewa na hatutarajii urudie tena swali hili.
Acheni kudanganya umaa. Hakuna alievuliwa uanachama , ila nijanja yenu kupeleka wabunge bungeni ilikuweka wafuasi kwenye msitari kwamba mlipinga matokeo. Hivyo tumeshawagundua kabisaa
 
Most likely scenario: Mara tu baada ya BAWACHA kumaliza mchakato wa kupata viongozi kuziba pengo la wale walioondolewa na kufukuzwa, Baraza Kuu litakutana na kuamua kuwasamehe wale akina mama ili wawe wanachama wa kawaida tu na wasaidie kujenga chama
Asante kwa taarifa
 
Labda kwa faida yako na wengine ni kwamba rufaa ya wahusika inahusu kuvuliwa uanachama, si kuvuliwa uongozi, Kamati kuu kabla ya kuwavua uanachama kwanza iliwavua uongozi, halafu baadaye ikawavua uanachama.

Kwahiyo wao wamekata rufaa ya kupigania uanachama wao ili waendelee kuwa wabunge, hii ni kwa sababu wanaupenda ubunge kuliko uongozi wa Chadema maana katiba hii hii ya Tanzania inayolalamikiwa inamtaka mtu ili awe mbunge ni lazima adhaminiwe na chama cha siasa kwa maana ya kuwa mwanachama na kwa viti maalum ni lazima wapitishwe na chama chao kwanza, kumbuka hawa walijiteuwa wenyewe kwa msaada wa CCM, kuanzia aliyekuwa jela na waliokuwa uraiani.

Kuhusu kujadiliwa rufaa yao hili litafanyika bila shaka bali litafanyika baada ya kuitishwa kikao cha Baraza kuu na kwa mujibu wa Katiba ya Chadema Kikao hiki kwa mwaka kinaitishwa mara 1 tu, huwa kinapangwa na kinakuwa na ajenda nyingi, hiki si kikao cha dharula, muda ukifika kitaitishwa tu.

Nadhani kwa haya machache angalau umeelewa na hatutarajii urudie tena swali hili.
Kisheria, unapo kata rufaa ya kupinga hukumu na adhabu, hakuna kinacho tekelezwa mpaka kusilizwa kwa rufaa yako. Na rufaa inaweza
1) kudhibitisha hukumu na adhabu
2) au kutupilia mbali hukumu ikiwa na maana na adhabu pia.
3) kuthibitisha hukumu na au kuongeza au kupunguza adhabu.
Vile wasikiliza hukumu wataona inafaa.
 
Umenukuu katiba ya Chadema ?
 
Bawacha bila Mdee na Bulaya ni sawa na Malaya asiye na tacall. Bawacha inakosa mvuto.
 
Back
Top Bottom