Uchaguzi 2020 Wasanii waliochukua fomu za kugombea ubunge kupitia vyama mbalimbali Uchaguzi Mkuu 2020

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Wakati joto la Uchaguzi Mkuu linazidi kupamba moto wasanii nao hawakubaki nyuma kuignia kwenye kinyang'anyiro cha kutaka kuwawakilisha wananchi kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Miongoni mwa waliojitokeza ni pamoja na:

1. Webiro Wassira maarufu kama Wakazi

Huyu ni mwimbaji wa Hip Hop amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama cha ACT Wazalendo ya kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika Uchaguzi Mkuu ujao Oktoba 2020.

>>Uchaguzi 2020 - Wakazi achukua fomu kugombea Ubunge Ukonga kupitia ACT Wazalendo

2. Rashid Mwinshehe (Kingwendu)
Huyu ni msanii wa vichekesho amechukua fomu kuomba ridhaa ya chama cha Mapinduzi kugombea ubunge jimbo la Ilala katika uchaguzi mkuu wa Octoba 2020.

>> Uchaguzi 2020 - Rashid Mwinshehe (Kingwendu) achukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Ilala

3. Steve Nyerere

Huyu ni msanii wa vichekesho amechukua fomu kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kugombea ubunge jimbo la Iringa Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa Octoba 2020.

>> Uchaguzi 2020 - Steve Nyerere achukua fomu ya Ubunge Iringa Mjini - CCM

4. Muhsein Awadhi Said (Dkt. Cheni)
Huyu ni msanii Muigizaji Mkongwe na Mshereheshaji maarufu amechukua fomu kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kugombea ubunge jimbo la Ilala katika chaguzi mkuu wa Octoba 2020.

>> Uchaguzi 2020 - Muhsein Awadhi Said (Dkt. Cheni) achukua fomu ya kuwania Ubunge Ilala kupitia CCM

5. Emmanuel Mathias (MC PiliPili)
Huyu ni msanii wa vichekesho amejitokeza kuchukua fomu ya kugombea Ubunge BAHI kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu 2020

>> Uchaguzi 2020 - MC PiliPili ajitokeza kuchukua fomu ya kugombea Ubunge Bahi kupitia CCM

5. Asha Baraka
Huyu ni Mwenyekiti wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta)hivyo anagusa kundi la sanaa amejitokeza kuchukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu 2020.
>> Uchaguzi 2020 - Asha Baraka achukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kinondoni

6. Dkt. Godfrey Nyahongo 'Bonta Maarifa'
Huyu ni Msanii wa Hip Hop amechukua fomu kuomba ridhaa kugombea Ubunge Kahama Mjini kupitia CCM

>>Uchaguzi 2020 - Msanii wa Hip Hop Dkt. Godfrey Nyahongo 'Bonta Maarifa', achukua fomu kuomba ridhaa kugombea Ubunge Kahama Mjini kupitia CCM


7. Sylvester Mujuni 'Mpoki'
Huyu ni msanii wa vichekesho Tanzania amechukua fomu kuomba ridhaa ya CCM kugombea Ubunge Jimbo la Kigamboni.

>> Uchaguzi 2020 - Sylvester Mujuni 'Mpoki' achukua fomu kuomba ridhaa ya CCM kugombea Ubunge Jimbo la Kigamboni


8. Joachim Marunda Kimaryo (Master Jay)
Huyu ni Producer mkongwe amechukua fomu ya kugombea Ubunge Rombo kwa tiketi ya CCM.

>> Uchaguzi 2020 - Producer mkongwe Master Jay achukua fomu ya kutia nia Ubunge Rombo kwa tiketi ya CCM

9. Jacob W. Mkweche 'Ringo'
Huyu ni Msanii wa vichekesho amechukua fomu kugombea Ubunge Jimbo la Songea Vijijini.

>>Uchaguzi 2020 - Msanii wa vichekesho Jacob W. Mkweche 'Ringo', achukua fomu kugombea Ubunge Jimbo la Songea Vijijini
 
Karibu Jimboni Mheshimiwa
 

Attachments

  • salim.binti_20200720_083817_1.jpg
    salim.binti_20200720_083817_1.jpg
    105.4 KB · Views: 2
Kwangu Mimi ninaowaona kuwa kweli wana nia njema na wakichaguliwa wataleta Tija kutokana na Umakini na Utendaji Wao ni hawa #5 na #8 tu.
 
Nachoshindwa kuamini mpaka sasa ni Haji Manara kutokutia nia jimbo lolote.yule bwana kiherehere nini kimemsahaulisha.
 
Huyu kila kipindi anagombeaga ila hapatagi hata kura 5. Yani ni mchovu fulani hivi asiyejua afanye nini.


Ha ha ha kumbe ni mchovu eee anasindikiza wenzake tuu................ so hata sasa hivi watamtupilia mbali sio?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom