Uchaguzi US: 2020

Wacha1

Sina uhakika kama tupo katika 'same page'' kuhusu hoja ya Mag3

Tunaongelea uchaguzi wa Marekani na jinsi ambavyo taasisi za nchi hiyo zilivyosimama imara katika kulinda masilahi mapana ya Demokrasia ya nchi yao.

Mfano, Trump kwa kutumia mamlaka yake alimteua mtu alichangisha pesa zake kuua shirika la Posta.
Kila state ina utaratibu wake wa uchaguzi na hivyo taratibu nyingine mbadala zilifuatwa.

Pamoja na hayo Mahakama kama Taasisi nyeti ililazimisha shirika la Post lihakikishe masanduku yanafika kwa wakati
Wakati huo huo postmaster general aliitwa na kamati ya Bunge chini ya kiapo na kuahidi kufanikisha uchaguzi

Rais Trump alitaka uchaguzi wa 'vote by mail'' ufutwe kabisa. Taasisi zikamwambia hiyo si kazi ya Rais
Juzi Jumatano , Rais Trump alikuwa na maongezi na Gavana wa Arizona na Georgia kuwashawishi. Walikataa

Hiyo ni mifano tu lakini uharibifu ni mkubwa sana hasa katika taasisi kama DOJ. Hata hvyo uimara wa Taasisi hizo bado upo licha ya uharibifu. Majuzi wakati Trump anashangilia Bus la Biden kuzingirwa na wahuni wake, FBI wamefungua uchunguzi bila kujali ukubwa wa Rais.

Miaka 4 iliyopita kulikuwa na maandamano ya kumpinga Trump.
Wote walioandamana waliambiwa hawana haki ya kumuondoa Trump, wasubiri miaka 4.
Miaka 4 baadaye wale wale walionyimwa haki sasa wanapewa haki ndiyo shamra shamra tunazoziona

Rais Trump alisema kulikuwa na 'fraud' katika kura za 2016 ndiyo maana Hillary alishinda kwa popular vote
Trump aliunda tume ambayo baada ya kuchunguza ilibaini hakuna tatizo na hivyo alishindwa kufanya lolote

Marekani kuna kamisheni ya uchaguzi, hata hivyo shughuli za uchaguzi zinaratibiwa katika ngazi za vitongoji ,miji, majiji n.k. kwa kufuata sheria za state husika.

Mfano, kuna state zina vote kwa mail tu hakuna kituo cha uchaguzi.

Kuna state zinaanza kuhesabu kura za posta kwanza, halafu za watu waliopiga na zingine ni kinyume

Ukifuatilia kwa ukaribu uchaguzi wa Marekani una matokeo makubwa matatu
Urais ni Biden
Senate itabaki kwa GOP
House itabaki kwa Dems

Chaguzi zote zimefanyika na kura kuhesabiwa kwa haki na uwazi ndiyo maana kuna tofauti hiyo.

Haya yanawezekana kwasababu uchaguzi wa Marekani si mali ya mtu au watu au kundi la watu.
Si mali ya GOP au Dems, ni mali ya wananchi. Hakuna mamlaka juu ya kura za watu.
Hatukuona mabomu, virungu au FBI wakibeba maboksi.

Hatukuona wagombea wakitiwa ndani ili kupisha hujuma zinazoratibiwa na vyombo vile vile vinavyopaswa kutoa haki na kusimamia haki.

Hoja hapa si personality, ni mifumo na kwamba wenzetu mifumo yao inaruhusu kujitawala kwa maana kwamba wananchi ndio wenye mamlaka.

Hii ni tofauti na nchi zinazoendelea ambako uchaguzi ni njia ya kujenga uhalali si mchakato wa kupata uhalali.

Hapa ni kuwa kwa nchi za kiafrika '' the end justifies the means''.
Kwa tulichokiona Marekani ni ''legitimacy derived from institutional procedure''

Ni kwa msingi huo Mag3 anasema kuna uchaguzi kama tulioona , halafu kuna vitu vingine vinavyofanana na uchaguzi yeye akiita uchafuzi
Chadema wanasema uchaguzi wa Tanzania ni uchafuzi lakini hawana evidence ya kile wanachosema. Walishika kura na Zito Kabwe (kibaraka) akawa anatembea nazo mitaani na kuonyesha kila alikokuwa anakwenda lakini hana ushahidi wowote ule usiotia shaka wapi alizipata. Ukishika mali ya wizi unamkamata mwizi kama unaweza na kumpeleka polisi. Siku hizi unaweza kuchukua video kutoka simu yako ya mkononi na ku-present as evidence, ameshindwa kufanya hivyo. Then unaambiwa Halima Mndee wameshika kura kwenye bag na kuamua kuzichoma. Kwanini wasimshike mwenye bag na kumpeleka polisi?

Ujinga mtupu wa kulalamika na kula pesa za walipa kodi bila kunawa mikono.

BTW demokrasia ya USA ni more than 300 years huwezi ukalinganisha na Tanzania ya miaka 60 then kuna vibaraka ambao wanataka kujitajirisha kwa njia chafu.

Vyama vya upinzani Tanzania vina safari ndefu kwa sababu ya tamaa ya madaraka.
 
Chadema wanasema uchaguzi wa Tanzania ni uchafuzi lakini hawana evidence ya kile wanachosema. Walishika kura na Zito Kabwe (kibaraka) akawa anatembea nazo mitaani na kuonyesha kila alikokuwa anakwenda lakini hana ushahidi wowote ule usiotia shaka wapi alizipata. Ukishika mali ya wizi unamkamata mwizi kama unaweza na kumpeleka polisi.
Na kiongozi akitoa tuhuma nzito kama wizi wa kura anahatarisha amani.
Ni wajibu wa Polisi kumfungulia mashtaka.

Kila mahali palipokuwa na mabegi ya kura feki hakuna aliyechukuliwa hatua na Polisi.

Lakini pia utampeleka 'mwizi' Polisi ili iweje? Polisi aliyetangaza matokeo kabla ya , OCD Hai unamplekea kesi ya wizi wa kura unategemea nini?

Kura feki zenye mhuri wa NEC zilipatikanaje na kama NEC hawahusiki walipaswa kuchukua hatua dhidi ya waliotoa tuhuma. Yule mwenye karatasi feki ndiye mwenye ushahidi si yule aliye kimya

Siku hizi unaweza kuchukua video kutoka simu yako ya mkononi na ku-present as evidence, ameshindwa kufanya hivyo. Then unaambiwa Halima Mndee wameshika kura kwenye bag na kuamua kuzichoma. Kwanini wasimshike mwenye bag na kumpeleka polisi?
Kama video ya simu ni ushahidi jeshi la Polisi lingeshamuondoa OCD wa Hai
IGP kasema wanachunguza video wewe unasema video inaweza kuwa ushahidi.!!!!
Ujinga mtupu wa kulalamika na kula pesa za walipa kodi bila kunawa mikono.
Yeah! pesa za walipa kodi zinaliwa na wengi tu! hili nalo ni la kuzungumzia? Twende zetu kwenye V8 ya viyoyozi
BTW demokrasia ya USA ni more than 300 years huwezi ukalinganisha na Tanzania ya miaka 60 then kuna vibaraka ambao wanataka kujitajirisha kwa njia chafu.

Vyama vya upinzani Tanzania vina safari ndefu kwa sababu ya tamaa ya madaraka.
Tuna miaka 60 ya Uhuru, muda kama Marekani lilikuwa limeshapiga hatua kubwa sana.
Hatukupaswa kuwa hapa, tunafanya kazi kwa template ya wajanja.
Hakuna tunachovumbua hata kimoja, halafu eti tusubiri 300 yrs.

Tuna miaka 30 ya vyama vingi, kila mwaka tumepiga hatua, mwaka huu tumeanza upya.
Vyama vya upinzani havina tatizo, tuna tatizo na mfumo ndiyo maana CCM hawakubali yawepo mabadiliko.

Walikataa katiba yaWarioba kwasababu ingetupa tupa tume huru ya uchaguzi.
Mwenyekiti wa tume mstaafu mh Lubuva alisema tunahitaji tume huru.

Lubuva aliyesema hayo siku anastaafu kwasababu alimalizika muda wake.
Tume ya uchaguzi ambayo mwenyekiti wake Marehemu aligombea CCM!

Hatuhitaji miaka 300 kufikia Marekani.Ghana na Botwasana wanafanya chaguzi zao hadi unapata raha na ni template ya Afrika.Habari zao ni za kujivunia

Kwa hili la miaka 300 ni ujinga tu, tuna template kutoka kwingine ikiwemo Ghana.
Tatizo la nchi masikini na hasa Afrika, viongozi hawazijengi nchi zao kimifumo, wanajenga himaya zao.

Viongozi wa Afrika hawajali Taifa likauwaje kesho wanajali wanatawala vipi leo.
South Korea tulikuwa kundi moja, nchi masikini mwaka 1960, Korea ni first world. Hawakusubiri miaka 300

Mkutano wa nchi za kundi la 77 uliwahi kufanya Tanzania - Arusha.
China ilikuwepo leo ni second economy hawakusubiri upuuzi wa miaka 300

Wakati unataka tusubiri miaka 300 kuwa kama Marekani halafu tunaambiwa baada ya miaka 5 nchi itakuwa kama Ulaya. Hivi tunahitaji miaka 300 ya kusimamia uchaguzi !?

Mimi nakushauri tuangalie uchaguzi wa Marekani! huko ndiko kwenye uchaguzi
 
Na kiongozi akitoa tuhuma nzito kama wizi wa kura anahatarisha amani.
Ni wajibu wa Polisi kumfungulia mashtaka.

Kila mahali palipokuwa na mabegi ya kura feki hakuna aliyechukuliwa hatua na Polisi.

Lakini pia utampeleka 'mwizi' Polisi ili iweje? Polisi aliyetangaza matokeo kabla ya , OCD Hai unamplekea kesi ya wizi wa kura unategemea nini?

Kura feki zenye mhuri wa NEC zilipatikanaje na kama NEC hawahusiki walipaswa kuchukua hatua dhidi ya waliotoa tuhuma. Yule mwenye karatasi feki ndiye mwenye ushahidi si yule aliye kimya

Kama video ya simu ni ushahidi jeshi la Polisi lingeshamuondoa OCD wa Hai
IGP kasema wanachunguza video wewe unasema video inaweza kuwa ushahidi.!!!!

Yeah! pesa za walipa kodi zinaliwa na wengi tu! hili nalo ni la kuzungumzia? Twende zetu kwenye V8 ya viyoyozi

Tuna miaka 60 ya Uhuru, muda kama Marekani lilikuwa limeshapiga hatua kubwa sana.
Hatukupaswa kuwa hapa, tunafanya kazi kwa template ya wajanja.
Hakuna tunachovumbua hata kimoja, halafu eti tusubiri 300 yrs.

Tuna miaka 30 ya vyama vingi, kila mwaka tumepiga hatua, mwaka huu tumeanza upya.
Vyama vya upinzani havina tatizo, tuna tatizo na mfumo ndiyo maana CCM hawakubali yawepo mabadiliko.

Walikataa katiba yaWarioba kwasababu ingetupa tupa tume huru ya uchaguzi.
Mwenyekiti wa tume mstaafu mh Lubuva alisema tunahitaji tume huru.

Lubuva aliyesema hayo siku anastaafu kwasababu alimalizika muda wake.
Tume ya uchaguzi ambayo mwenyekiti wake Marehemu aligombea CCM!

Hatuhitaji miaka 300 kufikia Marekani.Ghana na Botwasana wanafanya chaguzi zao hadi unapata raha na ni template ya Afrika.Habari zao ni za kujivunia

Kwa hili la miaka 300 ni ujinga tu, tuna template kutoka kwingine ikiwemo Ghana.
Tatizo la nchi masikini na hasa Afrika, viongozi hawazijengi nchi zao kimifumo, wanajenga himaya zao.

Viongozi wa Afrika hawajali Taifa likauwaje kesho wanajali wanatawala vipi leo.
South Korea tulikuwa kundi moja, nchi masikini mwaka 1960, Korea ni first world. Hawakusubiri miaka 300

Mkutano wa nchi za kundi la 77 uliwahi kufanya Tanzania - Arusha.
China ilikuwepo leo ni second economy hawakusubiri upuuzi wa miaka 300

Wakati unataka tusubiri miaka 300 kuwa kama Marekani halafu tunaambiwa baada ya miaka 5 nchi itakuwa kama Ulaya. Hivi tunahitaji miaka 300 ya kusimamia uchaguzi !?

Mimi nakushauri tuangalie uchaguzi wa Marekani! huko ndiko kwenye uchaguzi
Tuchunguze tuhuma anazotoa Kibaraka Zito Kabwe, labda wewe humfahamu Zito, kwa sisi ambao tunamfahamu wala hatubabaishi. Ni tapeli wa kutupwa awaambie sasa wajinga wenzake daily maverick et al wamsaidie msaliti mkubwa. Ndiye huyu huyu alisema JPM yuko Germany hoi na amekufa. Kama unamwamini sana Mwajiri akufanyie kazi Watanzania wamesema No! Ni huyu huyu Zito ambaye alilia sana na tukamchangai alipokuwa Kenya na kulialia kwamba kuna watu wanataka kumuua wakati anajiunga JF. Kibaraka mkubwa!

Kwa hiyo siku zote ni Chadema pekee ambao wanaibiwa kura? Wacheni kuchekesha watu JPM kapiga kazi hadi mabeberu wanaweweseka. Wale ambao walifikiri Tanzania ni shamba la bibi no more.

Mbowe aka Mlevi wa konyagi kawa mbunge kwa miaka mingapi Hai? Je, amefanya nini kwenye jimbo lake ambalo hata kidogo tu anaweza kujivunia? Zero sasa hapo unataka wamchague tena? watanzania sio wajinga! JPM alifanya kampeni na kuweka wazi kwamba kama wanahitaji maendeleo lazima wachague wawakilishi wa CCM na wananchi wameona kwa vitendo kazi iliyofanyika kwa miaka 5 sasa hapo unataka ushahidi gani?

BTW hamia USA kama unawapenda sana maana sisi na Tanzania yetu damu damu. Its a free world out there to be explored.

BTW unaongelea Botswana na nchi gani vile West Africa. I am sorry usilinganishe Tanzania na nchi zingine, Botswana kwa Tanzania ni kama mkoa moja tu. Kuna miji 2 au mitatu tu. Francis Town, Gaberone na mji moja mpakani na South Africa.

USA maendeleo yao ni kwa sababu ya kuwa na cheap labour mwanzoni (Kutegemea watumwa) na kuzikamua nchi masikini kwenye exchange rate mechanism. Hilo jambo hadi leo wanaliendeleza ndio sababu Wazungu wanaichukia sana Tanzania kwa sababu wanafahamu muziki wetu. Hizi hatua ambazo JPM anafanya hadi sasa zinawashitua na Watanzania kuwa watumwa kwenye nchi yao itakuwa mwisho na mwiko.

Unapoongelea China watu kama Zito, Tundu Lisu wangenyongwa hiyo ni fact sasa hapa kwetu si wanapeta. Kama unaona China wamefanya hivyo na wako hatua kubwa kwa nini JPM akifanya hivyo unalalamika? Maendeleo hayaji kwa kubembelezana, chunguza hao wezi ambao unawatetea utagundua ufedhuli wao.

Sijasema usubiri miaka mia tatu nimesema Demokrasia iliyopo USA ni takriban 300 years ya kuwanyonya watu masikini na kuendeleza biashara ya utumwa. Sipo impressed na utajiri ambao umepatikana kwa dhuluma ya utumwa, na kunyonya nchi masikini za Afrika then kujisifia ati mmeendela ni ujuha na upumbavu wa kiwango cha lami. Hatua ambayo Tanzania inapiga ni kutokana na juhudi za wananchi wenyewe bila kunyonya na kufyonza kama mrija.
 
Wacha1

Sina uhakika kama tupo katika 'same page'' kuhusu hoja ya Mag3

Tunaongelea uchaguzi wa Marekani na jinsi ambavyo taasisi za nchi hiyo zilivyosimama imara katika kulinda masilahi mapana ya Demokrasia ya nchi yao.

Mfano, Trump kwa kutumia mamlaka yake alimteua mtu alichangisha pesa zake kuua shirika la Posta.
Kila state ina utaratibu wake wa uchaguzi na hivyo taratibu nyingine mbadala zilifuatwa.

Pamoja na hayo Mahakama kama Taasisi nyeti ililazimisha shirika la Post lihakikishe masanduku yanafika kwa wakati
Wakati huo huo postmaster general aliitwa na kamati ya Bunge chini ya kiapo na kuahidi kufanikisha uchaguzi

Rais Trump alitaka uchaguzi wa 'vote by mail'' ufutwe kabisa. Taasisi zikamwambia hiyo si kazi ya Rais
Juzi Jumatano , Rais Trump alikuwa na maongezi na Gavana wa Arizona na Georgia kuwashawishi. Walikataa

Hiyo ni mifano tu lakini uharibifu ni mkubwa sana hasa katika taasisi kama DOJ. Hata hvyo uimara wa Taasisi hizo bado upo licha ya uharibifu. Majuzi wakati Trump anashangilia Bus la Biden kuzingirwa na wahuni wake, FBI wamefungua uchunguzi bila kujali ukubwa wa Rais.

Miaka 4 iliyopita kulikuwa na maandamano ya kumpinga Trump.
Wote walioandamana waliambiwa hawana haki ya kumuondoa Trump, wasubiri miaka 4.
Miaka 4 baadaye wale wale walionyimwa haki sasa wanapewa haki ndiyo shamra shamra tunazoziona

Rais Trump alisema kulikuwa na 'fraud' katika kura za 2016 ndiyo maana Hillary alishinda kwa popular vote
Trump aliunda tume ambayo baada ya kuchunguza ilibaini hakuna tatizo na hivyo alishindwa kufanya lolote

Marekani kuna kamisheni ya uchaguzi, hata hivyo shughuli za uchaguzi zinaratibiwa katika ngazi za vitongoji ,miji, majiji n.k. kwa kufuata sheria za state husika.

Mfano, kuna state zina vote kwa mail tu hakuna kituo cha uchaguzi.

Kuna state zinaanza kuhesabu kura za posta kwanza, halafu za watu waliopiga na zingine ni kinyume

Ukifuatilia kwa ukaribu uchaguzi wa Marekani una matokeo makubwa matatu
Urais ni Biden
Senate itabaki kwa GOP
House itabaki kwa Dems

Chaguzi zote zimefanyika na kura kuhesabiwa kwa haki na uwazi ndiyo maana kuna tofauti hiyo.

Haya yanawezekana kwasababu uchaguzi wa Marekani si mali ya mtu au watu au kundi la watu.
Si mali ya GOP au Dems, ni mali ya wananchi. Hakuna mamlaka juu ya kura za watu.
Hatukuona mabomu, virungu au FBI wakibeba maboksi.

Hatukuona wagombea wakitiwa ndani ili kupisha hujuma zinazoratibiwa na vyombo vile vile vinavyopaswa kutoa haki na kusimamia haki.

Hoja hapa si personality, ni mifumo na kwamba wenzetu mifumo yao inaruhusu kujitawala kwa maana kwamba wananchi ndio wenye mamlaka.

Hii ni tofauti na nchi zinazoendelea ambako uchaguzi ni njia ya kujenga uhalali si mchakato wa kupata uhalali.

Hapa ni kuwa kwa nchi za kiafrika '' the end justifies the means''.
Kwa tulichokiona Marekani ni ''legitimacy derived from institutional procedure''

Ni kwa msingi huo Mag3 anasema kuna uchaguzi kama tulioona , halafu kuna vitu vingine vinavyofanana na uchaguzi yeye akiita uchafuzi
Umewahi kuwa msimamizi wa uchaguzi wa Tanzania au USA? Je, unaweza kutoa mapungufu ya chaguzi za Tanzania na za USA au nchi nyingine yeyote ambayo wewe umeshiriki? Je, umetumia vigezo vipi? kama hujawa Returning officer, poll clerk au Count clerk kwenye chaguzi unawezaje kusema hayo unayosema?

Kwanza kabisa unaona tofauti iliyopo baina ya Tanzania 60yrs old na USA more than 300yrs. Then unaangalia tulipotoka na pale tunapotaka kwenda then unaaangalia taifa kubwa lenye uwezo mkubwa kama USA kulionea wivu taifa kama Tanzania?

I hope we are in the same page hususan ukiangalia mchango wa taifa dogo la miaka 60 jinsi lilivyokomboa Nchi zote za Southern Afrika na USA ambayo ndio inayadhulumu mataifa madogo kwa uonezi. Au tusema USA ni mshiriki mkubwa wa Belgium ambayo ni dhulumaji mkubwa wa utajiri wa Congo na USA ndio wafaidika wakubwa.
 
View attachment Bye bye.mp4

Huyo jiwe wa Marekani anaondoka tu hata afanyeje...bye bye Jiwe wa USA!​

Donald John Trump...Make America Great Again
Benito Andrea Mussolini...Rendi l'Italia di nuovo grande
Maximilien Robespierre...Rendre la France encore plus belle
Adolf Schicklgruber Hitler...Machen Sie Deutschland wieder großartig
 
Tuchunguze tuhuma anazotoa Kibaraka Zito Kabwe, labda wewe humfahamu Zito, kwa sisi ambao tunamfahamu wala hatubabaishi. Ni tapeli wa kutupwa awaambie sasa wajinga wenzake daily maverick et al wamsaidie msaliti mkubwa. Ndiye huyu huyu alisema JPM yuko Germany hoi na amekufa. Kama unamwamini sana Mwajiri akufanyie kazi Watanzania wamesema No! Ni huyu huyu Zito ambaye alilia sana na tukamchangai alipokuwa Kenya na kulialia kwamba kuna watu wanataka kumuua wakati anajiunga JF. Kibaraka mkubwa!

Kwa hiyo siku zote ni Chadema pekee ambao wanaibiwa kura? Wacheni kuchekesha watu JPM kapiga kazi hadi mabeberu wanaweweseka. Wale ambao walifikiri Tanzania ni shamba la bibi no more.

Mbowe aka Mlevi wa konyagi kawa mbunge kwa miaka mingapi Hai? Je, amefanya nini kwenye jimbo lake ambalo hata kidogo tu anaweza kujivunia? Zero sasa hapo unataka wamchague tena? watanzania sio wajinga! JPM alifanya kampeni na kuweka wazi kwamba kama wanahitaji maendeleo lazima wachague wawakilishi wa CCM na wananchi wameona kwa vitendo kazi iliyofanyika kwa miaka 5 sasa hapo unataka ushahidi gani?

BTW hamia USA kama unawapenda sana maana sisi na Tanzania yetu damu damu. Its a free world out there to be explored.

BTW unaongelea Botswana na nchi gani vile West Africa. I am sorry usilinganishe Tanzania na nchi zingine, Botswana kwa Tanzania ni kama mkoa moja tu. Kuna miji 2 au mitatu tu. Francis Town, Gaberone na mji moja mpakani na South Africa.

USA maendeleo yao ni kwa sababu ya kuwa na cheap labour mwanzoni (Kutegemea watumwa) na kuzikamua nchi masikini kwenye exchange rate mechanism. Hilo jambo hadi leo wanaliendeleza ndio sababu Wazungu wanaichukia sana Tanzania kwa sababu wanafahamu muziki wetu. Hizi hatua ambazo JPM anafanya hadi sasa zinawashitua na Watanzania kuwa watumwa kwenye nchi yao itakuwa mwisho na mwiko.

Unapoongelea China watu kama Zito, Tundu Lisu wangenyongwa hiyo ni fact sasa hapa kwetu si wanapeta. Kama unaona China wamefanya hivyo na wako hatua kubwa kwa nini JPM akifanya hivyo unalalamika? Maendeleo hayaji kwa kubembelezana, chunguza hao wezi ambao unawatetea utagundua ufedhuli wao.
Uzi huu ni wa uchaguzi wa Marekani. Hatujataja watu wa Tanzania na si kawaida yetu kujadili personality.
Hapa tunajadili mada objectively. Kama una tatizo na Zitto, Tundu Lissu au Mbowe watafutie mahali panapofaa vent out your frustrations, tag 'em etc. Ukiandika kama ulivyoandika hapo juu hiyo tunaiita 'ranting'.

Muhimu: Hatujadili personality
Sijasema usubiri miaka mia tatu nimesema Demokrasia iliyopo USA ni takriban 300 years ya kuwanyonya watu masikini na kuendeleza biashara ya utumwa. Sipo impressed na utajiri ambao umepatikana kwa dhuluma ya utumwa, na kunyonya nchi masikini za Afrika then kujisifia ati mmeendela ni ujuha na upumbavu wa kiwango cha lami. Hatua ambayo Tanzania inapiga ni kutokana na juhudi za wananchi wenyewe bila kunyonya na kufyonza kama mrija.
Well, Marekani ilikomesha biashara ya utumwa karne nyingi tu. Ni Taifa la kwanza kuwa na Teknolojia za viwanda 'industrial revolution''. Ndio wagunduzi wa mitambo na hata hii JF ni kazi yao kupitia satelite.
Kama walivyogundua vitu vingi duniani , leo tena wana ugunduzi wa chanjo ya COVID-19
US ni next level

Lakini basi tujiulize, kwanini sisi tupo nchi masikini sana duniani miaka 60 baada ya Uhuru na chini ya CCM?

Kwanini si Kenya, majirani zetu? Tujiulize kwanini Korea kusini tuliokuwa nao miaka ya 60 si wenzetu tena?
Kwanini Botswana si katika kundi letu?

Haya ndiyo maswali unayotakiwa uyajue na ujiulize mbele ya keyboard kabla ya' rant'
Hao akina Zitto hawajawahi kutawala leo unawabebeshaje zigo la Umasikini la miaka 60 ya CCM?
 
Umewahi kuwa msimamizi wa uchaguzi wa Tanzania au USA?
Hapana sijawahi hata siku moja.
Je, unaweza kutoa mapungufu ya chaguzi za Tanzania na za USA au nchi nyingine yeyote ambayo wewe umeshiriki?
Ninaweza kutoa mapungufu ya uchaguzi, siwezi kutoa mapungufu ya uchaguzi na kitu kingine
Je, umetumia vigezo vipi?
Kigezo ni kimoja, kuna mahali wanafanya uchaguzi. Kuna sehemu nyingine wana taratibu zinazofanana na uchaguzi.
kama hujawa Returning officer, poll clerk au Count clerk kwenye chaguzi unawezaje kusema hayo unayosema?
Hao ninawaona huko Marekani na UK. Hapa Afrika nimewaona Ghana , Kenya na South Afrika.
Namuomba mungu nisije nikapewa fursa hiyo, kilimo cha magimbi na ngogwe hapa Bondei kinatosha
Kwanza kabisa unaona tofauti iliyopo baina ya Tanzania 60yrs old na USA more than 300yrs.
Vipi tofauti ya Tanzania 60 yrs na Kenya appr. 60yrs
Vipi Tanzania ya 60 yrs na South Korea?
Vipi Tanzania ya 60 na India ya 70?

Uslinganishe Tanzania na Marekani , ni usiku na giza!
Then unaangalia tulipotoka na pale tunapotaka kwenda then unaaangalia taifa kubwa lenye uwezo mkubwa kama USA kulionea wivu taifa kama Tanzania?
Marekani haiwezi kuonea wivu Tanzania. Uchumi wa California ni moja katika ya chumi kubwa duniani.
Meya wa New York anaendesha uchumi mkubwa kuliko wa Tanzania.
Jimbo la Texas linalingana na ukubwa wa Tanzania na kubwa zaidi kiuchumi.
Marekani haina sababu za kuionea Tanzania hata kwa bahati mbaya. Hakuna na hilo sahau kabisa.
I hope we are in the same page hususan ukiangalia mchango wa taifa dogo la miaka 60 jinsi lilivyokomboa Nchi zote za Southern Afrika na USA ambayo ndio inayadhulumu mataifa madogo kwa uonezi. Au tusema USA ni mshiriki mkubwa wa Belgium ambayo ni dhulumaji mkubwa wa utajiri wa Congo na USA ndio wafaidika wakubwa.
Eeeh!
 
Marekani haiwezi kuonea wivu Tanzania. Uchumi wa California ni moja katika ya chumi kubwa duniani.
Meya wa New York anaendesha uchumi mkubwa kuliko wa Tanzania.
Jimbo la Texas linalingana na ukubwa wa Tanzania na kubwa zaidi kiuchumi.
Marekani haina sababu za kuionea Tanzania hata kwa bahati mbaya. Hakuna na hilo sahau kabisa.
Mkuu Nguruvi3, unajadiliana na watu wajinga sijawahi kuona. Eti Tanzania iko kwenye vita ya uchumi...adui wanayepigana naye eti ni Marekani! Huu uchaguzi wa Marekani umeiacha uchi Tanzania kama nchi iliyojaa wanafiki na wajinga wengi labda kuliko taifa lolote lile duniani. Fikiria bado wanaoamini upuuzi wanaousoma mtandaoni kwamba Trump bado ana chake nchini humo...yaani huyo tapeli atikise misingi imara ya miaka zaidi ya mia tatu! Watu walikimbia nchi zao na kuhamia Marekani kuzikataa tawala za kifashisti na kifalme halafu leo atokee mhuni moja aliye-fluke uongozi awarudishe huko...acheni utani jamani!

Poor Donald!.jpg
Masikini Trump, kama angezaliwa Afrika angepata zaidi ya asilimia 80% ya popular vote!​
 
Mkuu Nguruvi3, unajadiliana na watu wajinga sijawahi kuona.
Mkuu kuna kitu unakielewa '' social responsibility '' si kwa mantiki halisi lakini kitu kitu kinachofanana fanana na hicho, unanielewa nadhani
Eti Tanzania iko kwenye vita ya uchumi...adui wanayepigana naye eti ni Marekani!
Yeah! na wanaamini kwa dhati kabisa kuna vita ya uchumi kati ya US na Tanzania!
Kinachonishangaza ni ushujaa wao , kwamba, wanaongea bila kujali nafsi zao zinawaambiaje.
Huu uchaguzi wa Marekani umeiacha uchi Tanzania kama nchi iliyojaa wanafiki na wajinga wengi labda kuliko taifa lolote lile duniani. Fikiria bado wanaoamini upuuzi wanaousoma mtandaoni kwamba Trump bado ana chake nchini humo...yaani huyo tapeli atikise misingi imara ya miaka zaidi ya mia tatu! Watu walikimbia nchi zao na kuhamia Marekani kuzikataa tawala za kifashisti na kifalme halafu leo atokee mhuni moja aliye-fluke uongozi awarudishe huko...acheni utani jamani!
Department of Homeland Security(DHS) wanasema uchaguzi wa 2020 ulikuwa the most secured in American History.

Pili, kazi ya kuhesabu kura imeendelea bila kujali Trump anasema nini au anataka nini.

Leo wanasema wale watu waliochaguliwa na AG Barr kuchunguza madai ya Trump hawajaona fraud

IArizona imebebwa na Biden, ni nyumbani kwa Seneta McCain na bila amemjibu Trump kutoka alikopumzika.

Arizona ni Red state na mara ya mwisho Democrats kushinda ilikuwa mwaka 1992 wakati wa Clinton.
Tena Bill alishinda kwasababu Peros aligawana kura na mgombea wa Republican

Imetangazwa Georgia ambayo ni Red state sasa imeangukia kwa DemS. Georgia ndipo alipozikwa Rep John Lewis.

Siku Biden alipofikisha viti 270, secret service walihamia nyumbani kwake bila kumuomba na msafara wa Biden na Kamala ni ule wa Rais na Makamu mtarajiwa. Haya yanafanyika bila kujali Trump anasema nini.

Pamoja na Trump kutaka kuifanya Marekani ionekane kama third world, bado Wababe hao wa dunia wamethibitisha kuwa taasisi zao zinafanya kazi kikamilifu likiwemo jeshi la nchi hiyo.

Tunaposikia Tanzania kulikuwa na uchaguzi, inaleta tabu kueleweka masikioni hasa kuiona tofauti katika Uchaguzi na maigizo au Uchafuzi ambao kuna nyakati vitu hivyo vinafanana sana na Uchaguzi.

Mkuu Mag3, tunapojadiliana na akina Wacha ni sehemu ya majukumu na wajibu wetu kwa jamii yetu.
Ni ngumu lakini ni ngumu zaidi kuwatelekeza!

Well, Marekani ilikomesha biashara ya utumwa karne nyingi tu. Ni Taifa la kwanza kuwa na Teknolojia za viwanda 'industrial revolution''. Ndio wagunduzi wa mitambo na hata hii JF ni kazi yao kupitia satelite.
Kama walivyogundua vitu vingi duniani , leo tena wana ugunduzi wa chanjo ya COVID-19
US ni next level

Lakini basi tujiulize, kwanini sisi tupo nchi masikini sana duniani miaka 60 baada ya Uhuru na chini ya CCM?

Kwanini si Kenya, majirani zetu? Tujiulize kwanini Korea kusini tuliokuwa nao miaka ya 60 si wenzetu tena?
Kwanini Botswana si katika kundi letu?

Haya ndiyo maswali unayotakiwa uyajue na ujiulize mbele ya keyboard kabla ya' rant'
Hao akina Zitto hawajawahi kutawala leo unawabebeshaje zigo la Umasikini la miaka 60 ya CCM?
Highlighted basic things, utumwa USA haukutokomea karne nyingi kama unavyodai. USA wamekuwa ndio wezi wakubwa wa kisasa kuanzia rasilimali na kuua raia wengi wasio na hatia. Mfano jinsi walivyoshirikiana na Belgium kuitokomeza Congo (Zaire) na rasilimali zake.

Covid-19 ipo USA sio tatizo la Tanzania.

Nchi kubwa ambayo inaeneza magonjwa mbali mbali na baadaye inajisifia kupata chanjo ni ya ajabu na aibu. Kama USA pamoja na washirika wao hawazionei nchi changa kwa nini wanang'ang'ania ''Exchange Rate Mechanism'' (ERM) ambayo inawapendelea?
 
Highlighted basic things, utumwa USA haukutokomea karne nyingi kama unavyodai. USA wamekuwa ndio wezi wakubwa wa kisasa kuanzia rasilimali na kuua raia wengi wasio na hatia. Mfano jinsi walivyoshirikiana na Belgium kuitokomeza Congo (Zaire) na rasilimali zake.
Kama wanafanya hivyo ni kwa msaada wa Waafrika. Mobutu alimuua Lumumba
Hili ndilo tatizo la Waafrika, kwamba, wanauana wenyewe halafu wanasingizia mataifa makubwa
Nyerere aliwahi kusema ' kama unaambiwa jambo la kipuuzi na wewe ukalikubali basi wewe ni mpuuzi zaidi''
Covid-19 ipo USA sio tatizo la Tanzania.
Hatujui kama ni tatizo au la, hatuna takwimu wala hatujui nini kinaendelea. Tuendelee na maisha ya nchi masikini
Nchi kubwa ambayo inaeneza magonjwa mbali mbali na baadaye inajisifia kupata chanjo ni ya ajabu na aibu.
Magonjwa mbali mbali ni yapi? Covid ni Pandemic na wala haukuanzia Magharibi. Yapi mengine unayoongelea?
Kama USA pamoja na washirika wao hawazionei nchi changa kwa nini wanang'ang'ania ''Exchange Rate Mechanism'' (ERM) ambayo inawapendelea?
Exchange rate inawahusu wao na wenye chumi zinazofungamana. Sisi Tanzania uchumi wetu upo tu haufungamani na uchumi wowote kwa maana kwamba uchumi wetu ukianguka huko dunia hawajui kimetokea nini. South Africa wanaweza kunena wakasikilizwa, si Tanzania

Ni kwa mantiki hiyo, exchange rate na nadhani unaongelea aya sarafu. Nakuhakikisha kama ni sarafu Tshs ni ya Tanzania tu, pengine na Kenya, Uganda na Burundi. Huko Duniani haijulikana hivyo kudai ERM ni kichekesho

Narudia tena uchumi wetu haufungamani na chumi nyingine , unadai ERM ya nini?
 
BAADA YA GEORGIA NA ARIZONA NINI KIMBAKI?

Matokeo ya mwisho ya Arizona na Georgia yamekamilika.
Georgia kuna marudio ya kuhesabu kura kwa mkono kutokana na malalamiko ya Rais Trump.

Kuna sababu za kufanya hivyo! Trump ana malalamiko ya kuibwa kura hana ushahidi, sasa hivi anatufuta kitu chochote cha kuthibitisha madai yake. Kwa namba zilivyo hakuna kitakachobadilika

Georgia na Arizona zilikuwa Red state na tegemeo la Trump.
Masanduku ya kura za askari aliyotegemea yamehasabiwa, yamempigia Biden zaidi kuliko Trump.

Katika mazingira ya kawaida Trump alitakiwa kufanya transition na kumwezesha Biden kuanza kuunda serikali.
Trump amegoma na kuzuia hata daily briefing kumfikia Biden.

Amekataa kumtambua hadi sasa akisaidiwa na seneti na Reps wa Republican

Kwa maseneta na Reps wa Republican sababu kubwa ni kumuogopa Trump.

Akiwa na kura milioni 70 na ushawishi kwa GOP, wengi wanahofia siku zijazo ikiwa Trump ataamua kuwaendea kombo. Wameamua kukaa kimya

Katika mambo aliyofanikiwa Rais Trump ni kuwaweka GOP mfukoni na kuwafanya ma'coward'

Madai ya kwamba uchaguzi umeibwa si mageni. Mwaka 2016 alikuwa na madai kama hayo kabla ya uchaguzi.
In fact yalisaidia sana kuzuia habari za Russia kwa hofu kuwa kitu chochote kingethibitisha madai yake

Kama ilivyokuwa 2016, mwaka 2020 amekataa kusema tayakubali matokeo.

Wakati wa kampeni, Trump alisema njia pekee ya yeye kushindwa ni kuibwa kwa kura.

Hiyo ni kabla ya kura na anajua wapo watakao amini au kutilia shaka.
Amerudia sana kiasi cha baadhi kuamini na wakiulizwa ushahidi hawana kama ambavyo yeye hana.

Madai ya Trump yanashadidiwa sana na Televisheni na vyombo vya habari vya Russia.
Ukisoma habari kutoka Russia huchelei kuamini kuwa kweli kuna wizi umefanyika na kwamba amedhulumiwa.

Maswali ya kujiuliza, Rais Trump ndiye mwenye vyombo vya usalama ikiwemo DOJ.
Kwanini basi hachukui hatua dhidi ya taarifa zozote za uhalifu? Hakuna aliykamatwa au kushtakiwa

Pili, ni wapi kumekuwa na fraud kubwa ya kuweza kubadili matokeo ya uchaguzi?
Jumla ya kura zilizomwingiza WH 2016 ni chini ya 80,000. Jumla ya kura alizoshindwa Michigani pekee ni 100K+.

Tatu, Kama kuna fraud kwanini iwe katika urais na si useneta au uwakilishi? Katika senate bado Republican wanaongoza, na katika House Dems wanaongoza ingawa wampoteza viti. Kwanini huko hakuna fraud?

Trump anaipeleka Marekani katika level ya chini sana.
Hii ni kwa mambo mengi tu, kuanzia norms and tradition hadi sheria.

Kwa bahati nzuri sana mambo aliyofanya mabaya ni mengi na yamekuwa normal hata hayasemeki.
Hivyo hili la kukataa kumtambua mshindi ni mlolongo tu wa mambo kinyume na taratibu za Marekani.

Kitu kimoja anachosahau, Marekani ni Taifa kubwa na limejengwa juu ya misuko suko mingi.

Trump ni marudio tu ya wengi waliopita na kuna template ya ku deal nao kama ilivyowahi kutokea.

Ni suala la muda tu Rais Trump anaweza kujikuta na wakati asiotarajia.

Taasisi za Marekani zina kiwango , baada ya hapo hakuna anayeweza kuvuka kiwango husika.

Tusemezane
 
https://www.independent.co.uk/news/...secutor-daniel-r-alonso-lawsuit-b1722783.html

''An ex-Manhattan prosecutor has warned that “subpoenas and seizures” await President Donald Trump following his presidency

Daniel R Alonso, who acted as Manhattan District Attorney Cyrus Vance’s top deputy from 2010 to 2014 and is now in private practice, made the projection toThe New York Times.

“There are subpoenas and seizures and documents all over the place, as well as constant meetings with lawyers,” Mr Alonso said, adding, “It would certainly not be pleasant for him.”

The comment comes as part of a report by The Times considering that Mr Trump is more vulnerable than ever to a pending grand jury investigation by Mr Vance, a Democrat, into his business and his taxes. .... ...
 
Kuna sababu za kufanya hivyo! Trump ana malalamiko ya kuibwa kura hana ushahidi, sasa hivi anatufuta kitu chochote cha kuthibitisha madai yake. Kwa namba zilivyo hakuna kitakachobadilika.

Ngoja leo niwe msanii kwa kuwa Wakili wa Shetani. Nitoe maoni ya upande wa pili. Ushahidi hupatikana kwa kufanya ukaguzi. Kwa hiyo huu ni muda muafaka kupitia upya kura. Na kwa kuwa hakuna kura zilizoibiwa, hata akikagua kwa magnifying glass, hatopata kitu. Kwa hiyo tumwachie aangalie wee mpaka achoke; hapati ushahidi. Isn't it then kinda premature kusema hana ushahidi wakati ndio michakato ya kupitia upya kura inafanyika? Tuache mpaka mwisho tuone kama ushahidi upo au la.

Katika mazingira ya kawaida Trump alitakiwa kufanya transition na kumwezesha Biden kuanza kuunda serikali.

Uchaguzi huu mazingira yake "ya kawaida" ni ya kulinganisha na ya Gore-Bush saga. Gore aliconcede lini? [Disemba 13]; Lini Bush Jr alitambuliwa Rasmi kwamba ni rais mteule?

Madai ya kwamba uchaguzi umeibwa si mageni. Mwaka 2016 alikuwa na madai kama hayo kabla ya uchaguzi.

Waliosema uchaguzi umeibiwa mwaka 2016 walikuwa Democrats, na stori za udukuzi wa Urusi, ambazo uchunguzi rasmi nadhani ulifanyika na kuonekana madai hayakuwa ya kweli.

Kama ilivyokuwa 2016, mwaka 2020 amekataa kusema tayakubali matokeo.
Na ndivyo pia kwa Team Biden: "Whatever happens, do not concede", alisikika Mdemokrati mwandamizi akimwambia Biden.

Maswali ya kujiuliza, Rais Trump ndiye mwenye vyombo vya usalama ikiwemo DOJ.
Kwanini basi hachukui hatua dhidi ya taarifa zozote za uhalifu? Hakuna aliykamatwa au kushtakiwa
...
Pili, ni wapi kumekuwa na fraud kubwa ya kuweza kubadili matokeo ya uchaguzi?
Jumla ya kura zilizomwingiza WH 2016 ni chini ya 80,000. Jumla ya kura alizoshindwa Michigani pekee ni 100K+.

Tatu, Kama kuna fraud kwanini iwe katika urais na si useneta au uwakilishi? Katika senate bado Republican wanaongoza, na katika House Dems wanaongoza ingawa wampoteza viti. Kwanini huko hakuna fraud?

Trump alichukua hatua kwa kuanzisha CISA. Na kuweka executive order ya kuhakikisha chaguzi zijazo (ukiwemo huu) uchunguzwe na vyombo vya usalama ili kuzuia au kubaini kuvurugwa uchaguzi na mataifa ya nje.

Pili, hiyo kauli ya hakuna fraud kubwa kiasi cha kubadili matokeo inasigana na hoja kuu ya kwamba hakuna fraud.

Tatu, mfumo wa shirikisho unatoa mamlaka ngazi za chini ambako kunaleta fursa za wizi kufanyika. Trump alishinda uchaguzi huu kwa kura nyingi, viti vingi vya Seneti na Congress, kwa kiwango ambacho hakikuwahi kuonekana toka 1776. Sema tu, wizi wa kura ulizipunguza sana. Hata hivyo, siku ya uchaguzi bado Trump alikuwa anashinda, ikabidi wasitishe kuhesabu ili waibe kura za Urais tu, tena bila haya wala kujificha kivile (the end justifies the means); panga pangua Trump asipewe awamu ya pili.

Trump anaipeleka Marekani katika level ya chini sana.
Hii ni kwa mambo mengi tu, kuanzia norms and tradition hadi sheria.

Upande wa pili nao unaamini hivyohivyo kwamba Biden na Democrats ni sellout to the globalist cabal na kwamba walichofanya kwenye uchaguzi huu ni putsch/coup against the republic, na kwamba, if they get away with it this time, this is the very end of American Republic.

[/End of Devil Advocate Play]

Kwa sisi wapenzi watazamaji tusio na upande wowote, senema ya uchaguzi huu wa Marekani imefikia patamu: Stelingi wala Kubwa la Maadui hawajulikani nani ni nani.
 
Masikini Mlenge, nilitaka sana kujibu hoja zako lakini nimeshindwa kwani ni hoja za nguvu mno. Kuzijibu kunahitaji ujasiri usio wa kawaida ambao kusema kweli sina.

Ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba tarehe 20/1/2021, Joe Biden anaapishwa kama Rais wa 46 wa Marekani. Hayo ya tuhuma za wizi wa kura ni porojo tu.

Kama Trump angezaliwa Afrika...hapana, naota tu!
 
Back
Top Bottom