Uchaguzi US: 2020

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,407
31,392
UCHAGUZI US

Ni miezi miwili imebaki kwa Taifa kubwa la Marekani kufanya uchaguzi.
Wiki mbili zilizopoita Democrats na Republican vilifanya mikutano ya kuwathibitisha wagombea.

Mwaka huu kutokana na gonjwa la Corona, vyama vimefanya isivyozoeleka ''unconventional convention
Rais Trump akiwa 'incumbent' akipingwa na mgombea wa Dems VP Joe Biden wakati wa utawala wa Obama.
VP Pence ataendelea ikiwa Trump atashinda, na Senata Kamala Harris atakuwa VP ikiwa Biden atashinda.

Kuna mengi yanaendelea kuhusiana na uchaguzi wa Marekani. Gonjwa la Corona limebadili mambo yanavyofanyika kuanzia (convention) hadi mikutano ya kampeni.
Lakini pia Rais Trump amebadili mwenendo wa mambo mengi akitafuta namna ya ushindi

Gonjwa la Corona lililochukua roho za Wamarekani 180,000 halitoi nafasi nzuri kwa Rais Trump kwa kile kinachosemwa kushindwa kuongoza dunia au Taifa lake katika mapambano ya Corona.

Matukio ya weusi kuuawa na Polisi na hivyo kulipa nguvu kundi la Black Lives matter nguvu nalo limegeuza mwenendo wa uchaguzi kwa namna tofauti, nzuri kwa Joe Biden mbaya kwa Trump.

Kadri muda unavyosonga matukio hayo yanageuza mwenendo na kuwa mzuri wa Trump na mbaya kwa Joe Biden. Kuna sababu!

Katika mabandiko ya uzi wa uchaguzi wa Marekani, niliwahi kueleza kutoafikiana na kundi la Black Lives Matter(BLM) kutokana na kuongozwa na ima watu wasio na uwezo au ufahamu wa mambo.
Ni kundi linaloungwa mkono na wengi kutokana na matukio na si kutokana na ujenzi wa hoja.

Haiwezakani weusi waue weusi wenzao na BLM wawe kimya. BLM wadhani kuna uonevu wa Polisi ikiwa miji mingi wanayoishi kama Chicago ni mauaji ya weusi kwa weusi kwa wingi kuliko yale a Polisi.

Hivyo, reactions ya BLM mara nyingi inaongozwa na hisia na si ukweli kwa kuzingati historia.
Kwa mantiki hiyo, niliweka wazi kuwa kundi hili litakuwa tatizo kwa Joe Biden

BLM wanataka Police defund bila kueleza watapata nini kutokana na defund. Haiwezekani kufeli kwa maelezi ya familia kuwe tatizo linalohitaji pesa. Kwamba, defund itasaidia commnity programs. Hii ni stupid excuse!
Matatizo katika black communities ni kutoka na 'failure katika family level'' na hasa elimu

Rais anatumia vurugu kuwatisha weupe kwamba, weusi wanakuja juu na huenda ukawa mwanzo wa mwisho . Lakini pia katika vurugu hizi, kuna cultural war ambayo nchi za nje kama Urusi zinatumia kuwagawa Wamarekani. Mgawanyiko wa Wamarekani unampa fursa nzuri sana Rais Trump.

Marekani ina weupe wengi kuliko weusi na hali yoyote itakayochagiza weupe kupiga kura kwa mgombea itatoa ushindi. Rais Trump amekomalia sana vurugu zinazoendelea kwa kile wanachosema ' stoke fear'

Kabla ya vurugu, Trump alikuwa na hali ngumu. Hoja ya uchumi ilikuwa mfu kutokana na wengi kupoteza kazi. Hoja ya corona ilikuwa inamtafuna, na sasa amefanikiwa kuziua hoja zote mbili , yaani uchumi na corona kutokana na vurugu za BLM.

Lakini si hilo, katika mzunguko wa habari za siku nyingi ni vurugu na hilo linampa Trump nafasi ya kufanya vitu vyake katika kuhakikisha anahujumu uchaguzi au anabadili mwenendo.

Mfano, suala la kura kwa njia ya Posta na jinsi alivyohamisha na anavyozorotesha shughuli za Posta makusudi.
Pili, leo kuna taarifa wa national intelligence hatawajibika kwa kundi la Bunge linalojulikana kama Gang of 8

Gang of 8 linapokea taarifa zote za usalama na nyeti. Wiki chache zilizopita Intel iliripoti kuwa Russia wameendelea na juhudi za kumsaidia Trump. Hivyo, Trump na Director wake wanataka kuficha uchafu

Hayo yote yanafanyika kwasababu ya focus kuhamia kwenye vurugu zaidi katika news circle.

Haina maana maandamano ni mabaya, kwa nchi zenye uhuru wa maoni hiyo ni haki. Tatizo ni pale makundi ya watu weye vurugu kama waporaji wanapokuwa sehemu ya maandamano.
Hii maana yake ni kuwa BLM wana responsibility ya kuhakikisha usalama, wameshindwa na sasa wanaiumiza Democrats kuliko kuisaidia .

Tutaendelea kujadili kadri tunavyosonga mbele
 
Binafsi naona Biden anapwaya sana; nimeanza kuamini kuwa Trump anaweza kupita kwa urahisi sana, kwa hiyo mambo haya ya kitoto ya kutamba, kutukana, kulalamika na kusema maneno bila kuchambua athari zake tutaendelea kuwa nayo hadi 2024; na jamaa alivyo na akili mbovu anaweza kukataa kuondoka White House baada ya hapo. White house haitakuwa ile iliyokuwa inaheshimiwa sana; ile Rose Garden sasa inaonekana kama makaburini, na nasikia hata Airfoce One itakuwa inaonekana kama British Airways au the defunct Trump Airline. Tabu kweli
 
Binafsi naona Biden anapwaya sana; nimeanza kuamini kuwa Trump anaweza kupita kwa urahisi sana, kwa hiyo mambo haya ya kitoto ya kutamba, kutukana, kulalamika na kusema maneno bila kuchambua athari zake tutaendelea kuwa nayo hadi 2024; na jamaa alivyo na akili mbovu anaweza kukataa kuondoka White House baada ya hapo. White house haitakuwa ile iliyokuwa inaheshimiwa sana; ile Rose Garden sasa inaonekana kama makaburini, na nasikia hata Airfoce One itakuwa inaonekana kama British Airways au the defunct Trump Airline. Tabu kweli
Defeating a sitting President is a heck of a job. Pamoja na kwamba ilishatokea huko nyuma kwa akina Carter na Bush senior, Ila huyu jamaa anajua kuwatisha watu wa mlengo wake kuhusu vurugu zinazoendelea sasa hivi. Suala la kukataa kuondoka White House kama atashindwa hilo halitawezekana. It's not up to him. Because at noon on January 20th If a new president is elected... the police force, the secret service, the military, all the executive branch officers, will respond to the command and the direction of the new president.
 
KWANINI TRUMP BADO ANA 'UPPER HAND'?
Pamoja na kura za maoni kuonyesha Trump akiwa nyuma, bado Rais huyo ana nafasi katika uchaguzi ujao.
Kuna sababu kadhaa ikiwemo 'advantage' ya Rais mgombea pamoja na uzembe wa Mgombea wa Democrats

Moja ya sifa za Trump ni kuwa offensive tena akitumia uongo kwa kujua ni wachache wanaoutafuta ukweli.

Trump hategemei ukweli, anachotaka ni fursa tu ya kukutana na wapiga kura wake na kuwajaza uongo.
Ndivyo ilivyotokea katika convention iliyomalizika. Kwamba, Trump campaign ilitengeneza uongo bila woga

Faida y pili ni Rais kuwa na 'kipaza sauti'. Trump hutumia kauli zinazoondoa watu kwenye mada halisi na kumjadili yeye au kauli yake huku akifanya mambo mengine.

Mwaka 2016 Trump alisisitiza sana Dems na Obama wanataka kuiba uchaguzi 'rig'.
Alifanikiwa kuzuia vyombo vya usalama kuchukua hatua zitakazoonekana kama kuthibitisha kauli zake.

Wakati hayo yakiendelea, nyuma ya pazia Trump alikuwa anafanya kazi na Russia na kufanikiwa kuwavunja moyo blacks na kumpaka Hillary Picha mbaya ikiwemo emails n.k.
Kamati ya senate ya bipartisan imethibitisha pasi shaka kwamba Russia ilifanya hivyo kumsaidia Trump

Ndivyo anavyofanya sasa, kwamba, anataka kuendeleza mada ya vurugu , black lives matter n.k.

Hayo yakiendelea, Trump anaficha madhaifu ya vifo 180,000 kutokana na kushindwa kwake katika Corona.
Anaficha watu milioni 29 waliopoteza ajira . Anaficha unemployment ambayo ipo katika 10% n.k
Anaficha rekodi yake na Russia ambayo ni mbaya hasa akimuogopa Putin kwa kiwango cha juu kabisa.
Orodha ni ndefu.

Wakati akielekeza umma katika vurugu zinazoendelea, Trump anafanya vitu vyake kuhujumu idara ya Posta.
Trump anaendelea kuficha taarifa za intel community kuhusu Russia na jinsi inavyomsaidia hata leo hii.
Trump anaendelea kuwagawa Wamarekani katika makundi na hivyo kumsaidia katika asilimia za wapiga kura.

Haya yote yanawezekana kwasababu Dems na Joe Biden wameshindwa kutumia fursa ya udhaifu wa Trump kumsomea hukumu ya makosa yake mbele ya Umma.

Siku zote uchaguzi huwa ni hukumu kwa incumbent, lakini Dems hawanaonekani kutumia fursa hiyo. Joe Biden amekuwa ana 'play safe' badala ya kuwa offensive.

Trump amefanikiwa kumhamisha Joe Biden kutoka katika hoja za msingi zinazogusa wananchi na kujikuta anaongelea vurugu. Laiti Biden angejitokeza mapema na kukemea vurugu asingekuwa hapo alipo, hakufanya.

Wakati Trump akiendelea na Blacl lives matter watu wake wapo bize wakifanya yao, Russia wakitumbukiza mfarakano huku taasisi za umma zikifanyiwa figisu.

Yapo yanayoendelea nyuma ya pazia, anayosema Trump ni kukuonyesha 'mng'aro wa kitu' ambacho sicho wenyewe wakisema ''shiny object''

Kura za maoni zitabadilika kuelekea siku chache zilizobaki na hapo Biden kampeni wata panic.

Tusemezane
 
Binafsi naona Biden anapwaya sana; nimeanza kuamini kuwa Trump anaweza kupita kwa urahisi sana, kwa hiyo mambo haya ya kitoto ya kutamba, kutukana, kulalamika na kusema maneno bila kuchambua athari zake tutaendelea kuwa nayo hadi 2024; na jamaa alivyo na akili mbovu anaweza kukataa kuondoka White House baada ya hapo. White house haitakuwa ile iliyokuwa inaheshimiwa sana; ile Rose Garden sasa inaonekana kama makaburini, na nasikia hata Airfoce One itakuwa inaonekana kama British Airways au the defunct Trump Airline. Tabu kweli
Kheee! Jirani mara hii umebadili gia?

Mbona bado mapema sana 🤣.
 
'LOSERS AND SUCKERS'
Habari inayozizima viungani DC ni ile ya gazeti la Atlantic inayomkariri Rais Trump akiwaita askari losers and suckers. Habari imentikisa Trump kwasababu moja, imegusa veterans , kundi tiifu kwake lakini pia imegusa familia za askari kwa maelefu.

Taarifa ya Atlantic imethbitishwa na media nyingine kwa namna moja au nyingine.
Rais Trump amejitahidi sana kuikanusha, lakini historia yake ya nyuma inamhukumu moja kwa moja

1. Ni muongo ambaye uongo wake umethbitishwa katika maelfu na hivyo haaminiki tena mbele ya jamii
2. Aliwapenda majenerali wakati wa kampeni na wote amewatimua kwa aibu na fedheha
3. Hana mahusiano mazuri na familia za askari waliofariki ikiwemo ya McCain aliyemwita loser
4. Hakuna anaemtetea zaidi ya watiifu ambao mbele ya jamii nao huonekana ''wakujikomba''
5. Trump mwenyewe anajichanganya. Anaposema kauli imetolewa na aliowafukuza ina maana ni ya ukweli!

Hakuna shaka kauli ya losers and suckers imetikisa sana kampeni yake kwa mtazamo wowote.

Kosa kubwa ni kuamini hilo litamuathiri katika uchaguzi! Trump ana asilimia 36-45 ya wapiga kura wake watiifu sana ambao hata kama ni kufa wapo tayari kusimama naye. Hivyo, katika kundi hilo hatapoteza kitu

Trump huenda akapoteza wapiga kura katika wale waliotoka Dems na kumuunga mkono pamoja na independents.
Jambo la kuzingatia hapa si kupoteza wapiga kura, Trump hahitaji makundi hayo kumpigia kura.

Trump anahitaji ile asilimia 36 ya wafuasi wake, halafu ahakikishe makundi mengine hayapigi kura 'voter suppression'. Mwaka 2016 weusi hawakupiga kura. Trump alishinda state 3 muhimu kwa kura si zaidi ya 70,000

Hapa ndipo suala la kura za 'posta'' linapoingia. Trump hataki kura kwa njia ya Posta ingawa wapiga kura wengi kwa upande wake wanatumia njia hiyo. Kwanini basi akatae njia inayoweza kumsaidia?

Hoja hapa ni kutaka makundi kama ya Weusi wasipige kura. Hili linawezekana kwa kuweka vituo mbali, au kuviweka katika njia hatarishi zitakazokatisha tamaa wapiga kura(voter suppression')

Trump hahitaji kura mpya, anazo za uhakika kutoka makundi ya Weupe na ndio maana anawatisha kuhusu weusi. Taarifa ya Atlantic ni sawa na ile ya 'access Hollywood' haitamuondolea watu wake.
Anachohitaji ni 'voter suppression''

Katika kundi linalomsaidia Trump ni black lives matter(BLM).
Kundi hili linalo organize maandamano na mengine kuwa na vurugu linasaidia sana upande wa Trump.
Huu ndio msingi wa Trump kukomalia law and order.

Kura za maoni zinaonyesha Wamarekani mwezi Juni waliunga mkono BLM kwa takribani 62% .
Mwezi wa nane ni asilimia 53 tu. Hii maana yake ni kuwa vurugu zinazoendelea zimepunguza uungwaji mkono.

Athari za jambo hili ni moja, kwamba, wasiomtaka Trump hawatataka kupiga kura . Tayari BLM itakuwa imemsaidia Trump katika 'voter suppression''. Hicho ndicho anachohitaji wala si kura yoyote, ana uhakika wa 36%

Tusemezane
 
KUELEKEA UCHAGUZI

November 3 ni siku itakayoamua ikiwa Rais Trump ataendelea au VP Biden atakuwa Rais mpya.
Kwa miezi kadhaa mengi yamepita lakini kubwa ni kubadili kwa mwelekeo wa uchaguzi kutokana na Corona. Gonjwa limesababisha kuyumba kwa uchumi na ndiyo kubwa lililojiri.

Gonjwa la Corona si kwamba limeua watu wengi Marekani, lakini pia limebadili mwelekeo wa mambo mengi sana.

Mwezi January Rais Trump alijipigia chapuo la uchumi ambao aliukuta umetengenezwa.
Hii ilikuwa karata kubwa na ilielekea hakuna ambaye angeweza kuikabili.

Corona ilipoingia uchumi ukayumba na hapo Obamacare ikaiubuka, hisia kali dhidi ya ubaguzi zikashamiri.
Corona imelezimu upigaji wa kura kwa njia ya Posta na hilo lingeathiri sana Gerrymandering na voter suppression.

Matatizo yakawa mbele ya resolute desk ndani ya Oval office. Kwa bahati mbaya Rais Trump hakuona kina chake na wapi yanaelekea. Leo akitazama nyuma pengine anajuta kwanini hakutenda hivi au vile.

Hofu ya Republican imetanda ikihofu meli ya Trump inaweza zama na mzigo na hivyo seneti kuangukia ubawa wa kushoto.

Hofu ya Rais Trump dhidi ya Joe Biden ilikuwa sahihi na sasa inaonekana bila darubini.

Sakata la Ukraine lililopelekea mashtaka dhidi ya Trump lililenga kumjengea zengwe Biden.
Hii ilikuwa ni mapema sana wakati wa primary ya Dems. Washauri walimuona Biden kama Tishio kwa Trump kuliko wagombea wegine.

Haikuwa rahisi kuona kwanini Trump alimhofia sana Biden, mtu ambaye kujieleza kwakwe ni hafifu kuliko hata waombea kama Bernie Sanders, Butegig , Kamala Harris au Amy C.

Biden alianza kampeni kwa kusuasua mwishoni alimaliza kwa ushindi dhidi ya Sanders hata kule ambako aliweka jina bila kufika au kutangaza kama Texas, Boston n.k. Jambo hili lilionyesha kitu kimoja kwamba Biden alipendwa tu. Kwa mantiki hiyo Biden hakuwa na gundu la Hillary ambalo hakuna anayelieleza ni kwanini!

Hofu ya Rais Trump dhidi ya Biden ilikuwa ni ya kweli. Trump amejaribu kumpa majina na kumtafutia makosa au kashfa lakini hazishiki kama ilivyokuwa kwa Hillary Clinton. Kwasasa Trump anatafuta sababu zote zaile

Kura za maoni zinaonyesha hali ya kuelemewa. Kura za maoni haziwezi kutabiri Urais kama ilivyokuwa mwaka 2016. Hata hivyo kuna tofauti ya nyakati na mazingira ingawa ukweli unabaki pale pale, kura za maoni si kipimo.

Somo la mwaka 2016 lilikuwa kubwa na kila tahadhari kuhusu utabiri ni muhimu.

Jambo moja linaloonekana wazi ni jinsi kampeni zilivyo. Haitarajiwi Rais Trump aende Georgia, Texas, Arizona
Hizo ni ngome za Republican, kukampeni eneo hilo kunaonyesha dalili za hali tete maeneo hayo

Mtazamo huo una upande mwingine. Rais Trump ni mzuri sana na asiye na haya.
Katika mazingira yaliyopo bado anakusanya watu na bila aibu anaeleza hata uongo unaojulikana dhahiri shahiri. Trump si mjinga ! ana asilimia 36-40 ya wafuasi waliotayari kwa lolote lile katika kumpigani.

Wafuasi hao wataamini atakachosema hata kama si kweli. Mathalan, leo kuna watu wamehojiwa na kusifia ''Healthcare plan' ya Trump kutoka mdahalo wa jana. Ukweli ni kuwa Trump hajawahi kuwa na page 1 ya healthplan. Mfano wa pili, wapo wanaoamini laptop na email ya Rudy Giuliani iliyoandikwa na Urusi ni kweli.
Intel community ya Marekani imeeleza Giuliani kutapeliwa katika hilo, lakini leo wapo wanaoamini.

Trump ana uwezo wa kufanikiwa sana katika mazingira ya ghasia. Hisia za ubaguzi zinamsaidia sana ndiyo maana Trump anasiamama na KKK au Proud Boys. Hata kama ni makundi yasiyokubalika Trump anaelewa nini anafanya.
Makundi hayo apo vijijini hasa kwa watu wasio na elimu na huko ndipo Trump alipowekeza na kujikita.

Wingi wa watu wanaopigia kura za awali haimaanisha ni Democrats. Kuna hisia kubwa za ''urangi'' hivyo kuleta ushindani mkubwa sana kati ya weupe na watu wa Rangi. Hili ni advantage sana kwa Rais Trump.

Tofauti ya 2016 na 2020 ni moja, kwamba, Trump ni incumbent na anahukumiwa kwa miaka 4 aliyokaa madarakani
2016 hakuwa na historia yoyote kisiasa na alionekana kama mfanyabishara aliyefanikiwa sana.
Miaka 4 imepunguza wigo wa zile asilimia 36-40 kwa kiasi fulani.

Kashfa dhidi ya Veteran, ugomvi na wanasiasa hata wa chama chake, hukumu ya Covid na yanayotokana , yote yapo katika sanduku la kura. Hali hiyo ndiyo inayoweza kuleta utofauti wa Biden na Hillary.
Lakini pia persona ya Biden ni tofauti na ya Hillary.

Bado mkanganyiko unaendelea hasa katika mazingira ya kura ambako Posta inatumika kuhujumu, na kila mbinu zinafanyika kuzotesha zoezi la kura. Hayo yanafanywa kwa ufundi mkubwa, tutajadili !

Tusemezane
 
Kwa kweli sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana tena sana. Natabiri wengi hamtaamini kitakachotokea Marekani hapo kesho. Sote tuna mengi ya kujifunza katika uchaguzi wa Marekani ukilinganishwa na kilichotokea hapa kwetu nyumbani. Nunueni pop-corn, na tafuteni nafasi nzuri mkae mtulie mshuhudie maajabu ya kesho. Kuna mengi ya kujifunza.
 
Kama Biden atashinda itakuwa ni sababu ya kura za vijana; kwa majukumu yangu ya kila siku huwa ninainteract na vijana wengi na wako fired sana kumwondoa Trump Madarakani. Wengi wa waliopiga kura mapema ni vijana wa miaka 18 mpaka 28.

Trump akishinda, itakuwa ni watu weupe ambao hawana elimu kubwa; ndio wako fired sana kuhakikisha kuwa mtu wao anabaki pale. Kwa bahati mbaya hata sehemu kubwa ya wakulima wa vijijini ambayo huwa ni ngome kubwa ya republican sasa hivi wamegawanyika. Katika majirani zangu wawili ambao ni wakulima wote wanamchukia sana Trump kwa sababu walipata hasara sana kwenye kilimo chao miaka miwili iliyopita kwa kukosa soko la China, wakati handouts za serikali hazilingani na gharama zao za kilimo. Mbaya zaidi watu hao wanapenda sana ile faraja ya kujipatia kipato chao badala ya kupewa handouts na serikali.

Wanawake nadhani bado wamegawanyika equally kwa Trump na kwa Biden, halafu hispanics wengi wanamtaka Trump kwa sababu ya kuongozwa na viongozi wao wa dini, hasa wakatoliki wanaichukia sana demokrat hata kama mgombea Biden ni mkatoliki mwenzao.
 
Kama Biden atashinda itakuwa ni sababu ya kura za vijana; kwa majukumu yangu ya kila siku huwa ninainteract na vijana wengi na wako fired sana kumwondoa Trump Madarakani. Wengi wa walipiga kura mapema ni vijana wa miaka 18 mpaka 28.

Trump akishinda, itakuwa ni watu weyupe ambao hawana elimu kubwa; ndio wako fired sana kuhakikisha kuwa mtu wao anabaki pale. Kwa bahati mbaya hata sehemu kubwa ya wakulima wa vijijini ambayo huwa ni ngome kubwa ya republican sasa hivi wamegawanyika. Katika majirani zangu wawili ambao ni wakulima wote wanamchukia sana Trump kwa sababu walipata hasara sana kwenye kilimo chao miaka miwili iliyopita kwa kukosa soko la China, wakati handouts za serikali hazilingani na gharama zao za kilimo. Mbaya zaidi watu hao wanapenda sane ile faraja ya kujipatia kipato chao badala ya kupewa handouts na serikali.

Wanawake nadhani bado wamegawanyika equally kwa Trump na kwa Biden, halafu hispanics wengi wanamtaka Trump kwa sababu ya kuongozwa na viongozi wao wa dini, hasa wakatoliki wanaichukia sana demokrat hata kama mgombea Biden ni mkatoliki mwenzao.
Like us, in 2016 the US made a mistake the first time but I definitely doubt if they will repeat that same mistake the second time and one can take that to the bank ndugu yangu. Blowout? Why not, just may be!

In Tanzania we made a mistake in 2015 lakini badala ya kujisahihisha we have decided to make even a bigger one and for that we should suffer and yes, we deserve whatever we get...we just never learn!

Kosa si kosa bali kurudia kosa!
 
North Eastern states nyingi ambazo pia ni populous sana ziko kwenye himaya ya Bidem kwa hiyo wakishaaza kutoa data, hakutakuwa na surprise yoyote labda Senator Susan Collins tu. Ngaja tusubiri wakishaleta Virginia, North Calorina, South Calrolina, Georgia na Florida ndipo tutaanza kujua mweleko wa uchaguzi huu.
 
Likely Trump atashinda Florida
North Carolina bado ni competetive
Suprise ni Ohio
 
Likely Trump atashinda Florida
North Carolina bado ni competetive
Suprise ni Ohio
Duh, kwa mambo yanavyokwenda, karibu nitainua mkono kwamba nilikosea. Trump anashinda sehemu ambazo sikumpa nafasi hata kidogo. Haya ni maajabu! Kweli umdhaniye ndiye, siye. Sasa ni kusubiri tu miujiza.
 
Duh, kwa mambo yanavyokwenda, karibu nitainua mkono kwamba nilikosea. Trump anashinda sehemu ambazo sikumpa nafasi hata kidogo. Haya ni maajabu! Kweli umdhaniye ndiye, siye. Sasa ni kusubiri tu miujiza.
Michigan, Wisconsin na Penn state zitaamua nani mshindi

So far hakuna surprise katika electoral map. Georgia sikuwahi kufikiri GOP wata lose hata siku moja.
 
''Vote by mail'' italeta mtafaruku. Trump alikuwa mjanja aliposema mataokeo yatangazwe usiku
 
''Vote by mail'' italeta mtafaruku. Trump alikuwa mjanja aliposema mataokeo yatangazwe usiku
No clear winner mpaka sasa ila naona kama Biden anapewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda Wisconsin, Michigan, Nevada na Arizona. Akishinda hizi Biden atafikisha 270 na Rais mpya kapatikana ingawa Trump anategemewa kuweka pingamizi.

Ikitokea hivyo hata Trump akishinda Pennsylvania hawezi kushinda.
 
Defeating a sitting President is a heck of a job. Pamoja na kwamba ilishatokea huko nyuma kwa akina Carter na Bush senior, Ila huyu jamaa anajua kuwatisha watu wa mlengo wake kuhusu vurugu zinazoendelea sasa hivi. Suala la kukataa kuondoka White House kama atashindwa hilo halitawezekana. It's not up to him. Because at noon on January 20th If a new president is elected... the police force, the secret service, the military, all the executive branch officers, will respond to the command and the direction of the new president.
trump out.jpg
Siku itakapofika hakutakuwa na namna...
Wamarekani hawarudii kosa!
 
Back
Top Bottom