Uchaguzi ni wa nini basi?

Swadakta mkuu Uchaguzi huu ni kwa ajili ya kuwaonesha mabeberu kwamba hat sisi bado tuko kwenye domokrasia na watu wana kikubali sana chama kikongwe na wamechoka na fyama pinga maendeleo na wasio wazalendo. Ndio maana mtu kama mimi bora niendelee kuuza zangu dagaa na sangara nipate ugali kuliko kwenda kwenye usanii au unafiki. Rai yangu siku zote turudi kwenye Chama kimoja maana haitakuwa mara ya kwanza na pia ukizingatia Rais wetu anafanana sana na Mwalimu kwa maana naye alipoona fyama pinzani vitarejesha nyuma mpango wa maendeleo miaka ya Sitini alifutilia mbali vyama hivo so naye afutilie mbali. Na pia ni ushauri wangu akina Mbowe na wenzake waondolewe kabisa katika uongozi wao na wahukumiwe kwa kumuua Akwilina.
Tufute vyama vingi tuwe huru. Pia Katiba impe mamlaka Raisi kuwachagua Watawala wengine kuanzia ngazi ya vitongoji na mitaa hadi huko juu

 
Mkuu kwa hayo uliyoyaeleza ni sawa kwa asilimia 100 Sasa na tujiulize kwanini Viongozi wa vyama vya upinzani bado wanataka ligi iendelee pamoja na kwamba wamefungwa mikono na miguu? Kwanini wasije na plan B ?
 
Kwa mawazo haya, uchaguzi ni uchafuzi na matumizi mabaya ya fedha za umma.
 
Ehee, tuambie Mzee Mwanakijiji. Yamekukuta yepi hadi unaandika namna hii? ushaacha miaka mingi ati!!
 

Mzee Mwanakijiji uko sahihi kabisa kwa asilimia mia moja.
 
Ni kituko kwa awamu hii kufanya uchaguzi,siwezi poteza muda ilhali mshindi teyari wameshampanga watawala
Nalog off
 
Kazi ilimalizwa pale ikulu kwenye kikao cha watendaji wa kata.

Maelekezo, nyenzo na bahasha walizopewa tunaona matokeo yake huku mitaani.

Hakuna mpinzani,

kwenye kata yako akishinda mpinzani huna kazi.

Wapinzani nitateua mwenyewe.
 

Ni sahihi kabisa hasa kutokana na yalio kwisha kutokea hapo kabla.
 
Watumishi et wanalazimishwa kujiandikisha. So WHAT?

Hawataenda piga kura
 
Maneno mazima sana haya... je tunahakikishiwaje risasi kutopotea njia kwa mara nyingine kisa uchaguzi?
 
Yako wapi?

Tuliandika wiki moja tu iliyopita kuhusu uchaguzi. Tukasema lengo la kupiga debe watu wajiandikishe ni kutafuta uhalali wa idadi ya waliojiandikisha.

Wangapi watapiga kura hilo si tatizo. Je, kura zitahesabiwa hilo si tatizo!

Lengo ni ushindi kwa asilimia 100.
Mbinu ya kubadilisha masanduku haifanyi kazi siku hizi. Mbinu mpya ni kuwaondoa wagombea.

Ikiwa nia ilikuwa nzuri ya watu kushirikia uchaguzi, nia hiyo isingekuwa tofauti na kuwa na wagombea pia. Kilichotokea ni kutafuta idadi halafu kuondoa wagombea!

Wapinzani ni watu wa ajabu sana. Hivi haya hawakuyaona?
Hadi yanaandikwa hawakuweza kusoma na kufikiri japo kidogo?

Leo Chadema wanasema hawatashiriki! inashangaza maana maandiko yalikuwa ubaoni.
Kwa Zitto na ACT, nanyi mtatumika kama hamtakuwa makini

Kuweni makini na mtego uliowekwa! usijekuwachonganisha na wenzenu mkiwa wakiwa wote

Kinachotakiwa ni vitongoji 2 ACT, 2 CUF-Lipumba, 2 TLP Mrema.
Tayari uchaguzi utakuwa wa vyama vingi, huru na haki

Kwa asilimia hiyo itakuwa kama 0.2 na Chama chetu cha CCM kitashinda kwa asilimia 99.8!!
 
Hakika huwezi ukakiita hiki kinachoendekea, kitachohitimisha tarehe 24 mwezi huu kama UCHAGUZI bali inastahili kwa asilimia 100 kuita ni UCHAFUZI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…