Uchaguzi ni wa nini basi?

Naona dalili zoote za mtanzania kuanza kujitambua ingawa mchakato unaenda taratibu sana. Ila kuna tatizo ninaloliona hapa kama ifuatavyo
1; Hivi kuna mtumishi wa umma hata mmoja atakwenda kujiandikisha kupiga kura au kwenda kupiga kura yenyewe? kama hivyo ndivyo basi kuanzia sasa waache malalamiko yao ya kila siku maana wanao uwezo mkubwa sana wa kuutingisha utawala huu lakini wao ndio wa wa kwanza kuuwezesha
2; Watumishi wa umma kote nchini wanashindwa kuwashawishi wake zao/ waume zao na familia zao kususia uchaguzi huu ili kumuonyesha tu mwamba mkuu kuwa na yeye ni mtumishi tu wa umma
3; Kwenye sakata la vyeti fake kuna watu wanajulikana wameonewa tu na wengine walikosea padogo tu hawa nao hawaoni umuhimu wa kuungana na kushawishi wanafamilia zao kumtingisha mwamba hadi aite jeshi?
4; Kuna wafanyabiashara walioahidiwa kuishi kama mashetani wapo tu nao kazi kujipendekeza tu
 
Uchaguzi ni wa nini Basi?
As usual, always helping our country to do the best and to be more pure than pure. Tatizo ni vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa vya ukoo zaidi au vimekuwa binafsi zaidi. Wengine vyama vyao vimekuwa vya mfukoni zaidi. Zito Kabwe amejitajirisha kutokana na position aliyokuwanayo i.e kufahamu the working of Government system na kuchuma pesa yeye mwenyewe binafsi, Mbowe kujitajirisha yeye mwenyewe binafsi nk. sasa katika hali kama hiyo utaona kabisa Watanzania walio wengi hawawezi kuwapa kura. Hata pale wakati Dr. Slaa alipokuwa Chadema alipigwa vita, its all about money and not democracy.

Watu wanashabikia democracy iliyopo UK, USA nk lakini angalia hizo democracy ni za miaka mingapi? UK more than 500 yrs Vile vile hakuna democracy ki-vile ambavyo wengi Africa wanaaminishwa, there is a lot of money behind the scenes supported by the media and financial services, campaign rules etc. the white man w ill always undermine the black man because they are afraid one of these days Africa will have more JPM 's and they will have more trouble. Its a pity that many Tanzanians and especially those who migrated to USA and other countries have joined the band wagon of opposition parties who are there for themselves (money). Their main agenda is to discredit the current government effort to improve the lives of Tanzanians. People should look at the big picture and challenge the government on basic issues which affect the majority of Tanzanians. JPM has transformed this country in barely 4yrs, improvements of many sectors etc.

Swala la kutojiandikisha sina facts hivi sasa kufahamu ni wangapi hawajajiandikisha lakini mara nyingi wengi huenda karibu na siku za mwisho etc.

Kuhusu swala la kupiga kura hilo lazima litokee hata kama atakayepiga kura ni moja kwa sababu hiyo ndio mandate tuliyojiwekea kikatiba. Nafahamu wengi hawatakwenda kupiga kura lakini hilo ni shauri lao watakapokwama ndio watafahamu umuhimu wa kupiga kura.
 
JF ingekuwa sehemu ya kutafuta njia za ufumbuzi wa matatizo kama hivi, nina hakika isingekuwepo.
Sasa hivi imevumiliwa kuwepo kwa sababu imeonekana ni mahali pa kubadilishana mipasho tu basi.

Heshima Mkuu 'Tindo.' Sijui kama mapendekezo yako haya yatasikilizwa na kufanyiwa kazi.
 
Duh nimekuelewa mwamba
 
Ni bora wajitangazie wao maana hukua sehemu ya dhuluma. Kwavyovyote itakavyokua lazima watashinda tu.
 
Heshima mkuu Nguruvi. Uliyoandika hapa ni ukweli mtupu katika muonekano wa nadharia za 'kisomi' (academic theories).
Ukitazama hali ya kidunia, mambo haya ya 'uhalali' (legitimacy) iwe kisheria au kisiasa, ni mambo yanayotengenezewa nafasi yawepo baada ya unajisi wake.
Tawala za akina Idd Amin Dada na wengine, sijui kama tunaweza kusema kwamba walikosa 'legitimacy' ya aina yoyote baada ya uwepo wao, hata kupitia njia zisizo sahihi.

Hali sasa hivi imezidi kuwa mbaya kwa sababu mifumo ya kimataifa iliyokuwa inapingana haipo tena. Kwa hiyo tunaona ilivyo rahisi sasa kwa viongozi kukandamiza na hata kuua wananchi bila ya uoga wa makaripio toka nje. Hali imekuwa ngumu sana sasa. Hata mahakama, kama ICC, kumshitaki kiongozi aliyepo kwenye madaraka inakuwa ngumu sana, kama ilivyoonekana na Bashir kule Sudan.

Hali hii imewapa viongozi wenye tabia za ukandamizaji kuwa na ujasiri wa kufanya wanavyopenda nchini mwao.
Suluhisho lipo kwa wananchi pekee, wanapoamua kukataa kukandamizwa.
 

Kwa maoni yangu hali iko hivi:

1. zuio la Raisi dhidi ya wapinzani limesababisha siasa zetu kukosa msisimko ambao ungepelekea watu kujiandikisha.

2. wananchi na wapiga kura hawauchukulii kwa uzito uchaguzi wa serikali za mitaa. Wapiga kura hawaoni umuhimu wa nafasi zinazogombewa ktk uchaguzi huu.

3. CCM au chama tawala hawaoni kama kuna tishio kwa chama chao hivyo hawaoni ulazima wa kujiandikisha kupiga kura na kukihami chama chao.

4. Wapinzani hawaoni kama uchaguzi wa serikali za mitaa au ushindi ktk uchaguzi huu utabadili mazingira mabaya ya kisiasa yaliyoko nchini.

5. Vyama vyote vya siasa vimejikita zaidi ktk harakati za udiwani, ubunge, na Uraisi. Wananchi wamejengwa kiimani kuwa uchaguzi muhimu ni ule wa madiwani, wabunge, na Raisi.
 
Ni asilimia 0.00000000000000001 ya watanzania ndio wamo humu JF...JF had never been a true reflection of the situation at ground...wananchi wenye nia ya kujiandikisha wanaendelea kujiandikisha kwa wingi
Ok hizo data zako nadhani haziko sahihi.Taarifa inayotokea kwenye mtandao wa JF kwa mtu mmoja tu,baada ya dakika tano tu, imeshasambaa kijiji kizima.Nikupe mfano kidogo tu.Walipochomoa waya kule Morogoro dakika taarifa ilienea nchi nzima na sisi huku kijijini tulizipata.

Kwa hiyo kutudanganya kwamba eti hawapati taarifa unajindanganya mwenyewe.Na kama wanajiandikisha kwa wingi iweje ma dc na ma rc kupewa tahadhari ya kibarua chao, endapo watu hawatajiandikisha.Hii ni hali halisi kuwa zoezi ni teeeteee sio nzuri.

Muda wa kujiandikisha kwa miaka ya nyuma,ulikuwa unaongezwa kutokana na wingi wa watu waliojitokeza,lakini sasa hivi muda unaongezwa kwa watu kutokujitokeza.

Hata mimi binafsi sijashawishiwa na yeyote kutokujiandikisha au kujiandikisha ila sitapoteza hata nusu dakika kwenda kujiandikisha kwa sababu kama viongozi wote wameshateuliwa,kuna haja gani ya kujiandikisha.Yaani wanatufanya Watanzania wote kuwa rubber stamp.Tumewaona na tumewasoma kwa maneno ya vinywa vyao.

Mtoa post nakuambia hivi juzi hapa kwetu walikuja maafisa kutaka kuhamasisha watu wakajiandikishe,kilichowapata tutawaomba watujulishe humu,ili ujue mambo sio kama unavyotaka kutudanganya.

Ieo hii Jumapili maafisa watendaji wamepita kwetu kijijini kwa zoezi hilohilo wakanikuta, wakaniomba niende kujiandikisha.Jibu nililowapa niliwaambia sitajiandikisha na muda huo sina.Waliponiuliza ni kwa nini,niliwaambia warudi baadae niwape jibu nikiwa na nafasi nzuri.

Viongozi wetu wasitufunike kwa neti ya mbu wakiamini kuwa hatuoni.Nawaambia hivi hiyo neti waliyotufunika nayo ina matundu tena mengi tu, tunaona.

"Haki huinua taifa,bali dhambi ni aibu kwa kila mtu"
 
usipojiandikisha ni wewe mwenyewe umepoteza haki yako na baada ya uchaguzi ukiinua sauti kulaumu utakuwa ni mnafiki kwani kura hukupiga kwa hiyo kaa kimya tu
 
usipojiandikisha ni wewe mwenyewe umepoteza haki yako na baada ya uchaguzi ukiinua sauti kulaumu utakuwa ni mnafiki kwani kura hukupiga kwa hiyo kaa kimya tu
....amepoteza haki ya kufanya nini?
Kwa nini ni mazuzu kiasi hiki? Mnawachukuliaje hasa Watanzania, kwamba ni watu wasio na uelewa, who need decisions to be made for them??
 
M Mazuzu nchi hii hamuwezi kuisha hivi na Elim yako unataka utuaminishe kwamba hapo alipo Mbowe yupo kwaajili ya kuutafuta utajili? Huna aibu LA sivyo wewe ni wale wale lumumba buku 7
 
Kama ataendelea kuminya demokrasia akifikiria watanzania hawana akili ,uchaguzi mķuu ujao hali itakua mbaya zaid. Uwezo wa viongoz kutafakari impact ya maamuz yao ni mdogo sana. Mh bado hajajua ukubwa wa nafasi yake kuwa kila jambo analolisema huchukuliwa kama sheria yeye analipuka tu.
 
Kwa Tanzania uchaguzi wa haki bado sana. Kiukweli sioni haja ya kujiandikisha zaidi ya kupata kitambulisho kwa ajili ya shughuli zenye kuhitaji uwepo wa kitambulisho, ila si kwa kupiga kura.
wameanza lini kutoa hivyo vitambulisho?
 
siasa zetu bongo zimekua mbovu sana, natambua umuhimu wa kura yangu kwa kiongozi nimpendae lakini mfumo wetu haunishawishi kwenda kupanga foleni na kupiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…