Uchaguzi ni wa nini basi?

Unafahamu jumla ya wapiga walioiandikisha 2015!!?? .... Ni 23.78M.. Leo uje useme upande wa ccm tu na mazombi yetu tufike 20M !!?? Fuvu lako litakuwa na matege linapitisha upepo.
 
Uwanyime au uwape uwepo wako, wao hawajali, .........kama hata damu ya asiye mwana CCM haitakiwi kule blood bank, kura ilopigwa kwa mpinzani itahesabiwa kweli?????.. kumbuka pia kumchagua mpinzani ni kum-expose kwenye mauti.
 
Ni muhimu kukusanya taarifa sahihi na za uhakika
Ndugu yangu, kama kutangaza tu matokeo sahihi wahusika wanapigwa mkwara, je huo umuhimu wa kukusanya taarifa sahihi na za uhakika utawezekanaje? Ili iweje? Ngoja nikukumbushe kidogo...katika uchaguzi wa mwaka 2015, idadi ya waliodaiwa kujiandikisha kupiga kura walikuwa ni watu 23,254,485. Hata hivyo idadi ya kura alizodaiwa kupata jiwe na kutangazwa mshindi ilikuwa ni 8,882,935 sawa na asilimia 38% ya waliojiandikisha. Hiyo ndio Tanzania...karibu sana nyumbani.
...na hivyo kuwa na data za nini kinaendelea.
Mmm, mzee mwenzangu, kweli unaishi dunia hii! Eti tuwe na data za nini kinaendelea...hapa naomba nikumbushie alichosema Nguruvi3, utawala huu wa kidikteta hauhitaji kura yako kwa sababu ya kufanya maboresho, wanahitaji uwepo wako ili kuhalalisha mchakato wa uchaguzi, oops, mchakato wa uchafuzi!
 

Kwenye hili la mwisho ni hoja inayohitaji kuangaliwa kwa ukaribu zaidi ukizingatia hili swali la mada hii. "Uchaguzi ni wanini basi"? Naona unapendekeza jibu ambalo linafikirisha. Inawezekana uchaguzi kutumika kama namna ya "kuhalalisha" madaraka? Kwamba, lengo la uchaguzi siyo haya mawili niliyoyataja hapo juu bali kuhalalisha uwepo wa watu madarakani?
 
Nikweli

Ni makosa kudhania tu kuwa watu hawajiandikishi kwa kiwango kikubwa kwa sababu moja au nyingine. Ni muhimu kukusanya taarifa sahihi na za uhakika na hivyo kuwa na data za nini kinaendelea.
Kiuhalisia hiki ndicho kinapaswa kufanyika, kutafuta 'data'

Katika mazingira yaliyopo hilo nalo ni gumu, litapotosha zaidi kuliko kutoa jibu sahihi.
Kuna sheria ya takwimu iliyoundwa makusudi kabisa kudhibiti upatikanaji wa takwimu kutoka taasisi nyingine huru nje ya zile za serikali.

Tamisemi watatoa takwimu halisi ? Yaani wajikaange na mafuta yao!

Tukirudi kwa tume (NEC) nadhani wanadhamana ya ''takwimu'' kiaina
Nao hunyooshewa kidole kila uchao

Wameshindwa kukemea ma-DC kuhusu kutangaza wagombe ikiwa na mamlaka ya kisheria.

NEC imeshindwa kueleza lini kampeni zinazuiliwa lini zinapaswa kuanza.

NEC imeshindwa kueleza sanduku linatokaje kituoni na kurejeshwa nje ya utaratibu.

NEC imeshindwa kueleza kwanini wasimamizi wanakimbia vituo kuchukua fomu wasizopendezwa nazo.

Leo tutegemee takwimu za NEC kuwa tofauti na NEC ilivyo. Real!
NEC kama taasisi nao pia walisikia tangazo la ole wako, sidhani kama wangependa iwe ''ole wao''

Hapa ndipo tunarudi nyumbani Bondei kucheza mdumange!
 
naona akili zinaanza kukurudi. waambie mimi na familia yangu sitanyanyua mguu kuenda kupiga kura uchaguzi wa serikali za mtaa wala ule mkuu wa mwakani.
kwa nn mkuu?kwan mtoa siredi n ccm kindakindaki?
 
Sisi wananchi tupo pembeni tunaangalia kama watapika data au watajitangaza wameshinda Kwa kishindo.
Maana mwitikio wa wananchi kujiandikisha tunaujua na lolote litakalofanyika hasa Kwenye kuiba Kura na kuongeza idadi ya wapigakura hapo ndipo watazidi kutukoroga.

Tunamsihi raisi asithubutu kuwatumbua wakuu wa mikoa na wilaya eti kwasabb kuna idadi ndogo ya wapigakura Kwenye maeneo yao....

Itakuwa aibu kwake na kujishusha hadhi na hata ule uaminifu Kwa wananchi utapungua zaidi,miaka yote hakujawahi kusikia lawama kama hizi zinaenda Kwa wakuu wa wilaya na mikoa huyu raisi ajipime matendo yake kwetu kama anatosha kutuongoza!!!!! Dalili hizi za watu kuchoshwa na udikteta zitazidi zaidi hapo mwakani
 
Kwetu inashangaza sana..
Watu wamegomea kimtindo maana kila kitu kinaenda sawa kabisa, mamiradi mikubwa inafanywa na mapesa ya ndani.....
 
Wasilielie mazingira ya kuendelea kutawala wameyaweka wao na wataendelea shida ni nn. Sisi tunachapa kazi na watawale hadi milele ya duniani. Sio ile ya Muumba
 
Wasilielie mazingira ya kuendelea kutawala wameyaweka wao na wataendelea shida ni nn. Sisi tunachapa kazi na watawale hadi milele ya duniani. Sio ile ya Muumba
Shida ni pale wanapotumia hata hela zako za NSSF kujipa mikopo na kutengeneza miradi hewa........Milele ya duniani kama ulivosema... no longer at ease....
 

Mimi nawashauri wapinzani na nimeshatia ushauri hata kwa baadhi ya viongozi wa upinzani humu kwenye mitandao ya kijamii, badala ya kuhamasisha watu kwenda kupiga kura ni bora wakatumia mwitikio huu wa umma kudai tume huru ya uchaguzi. Nimemshauri kuanzia mwaka kesho mwezi wa tatu au wanne kutangaza maandamano ya amani mara moja kila jumamosi ya mwanzo au ya mwisho wa mwezi kudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya juu.

Madai hayo yatakuwa na uhalali wa umma kwani mpaka sasa umma umedhibitisha kwamba hakuna uchaguzi bali uhuni wa kiwango cha juu. Nina hakika umma uko tayari kwa hilo, Hapa inabidi hata JWTZ washawishiwe kwenye hili kama kuna uwezekano.
 
Hivi yule Naibu Waziri aliyewaombea msamaha kwa Rais wananchi wa jimbo fulani kwa kumchagua mmbunge wa upinzani alijibiwa nini na yule aliyeombwa msamaha?
 
Ni asilimia 0.00000000000000001 ya watanzania ndio wamo humu JF...JF had never been a true reflection of the situation at ground...wananchi wenye nia ya kujiandikisha wanaendelea kujiandikisha kwa wingi
 
Leo umeongea ukweli una siku nyingi Sana husemi Maneno mazito Kama Haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…