William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Nimesona Thread nzima, Sijaona hao waheshimiwa wenye link nzuri na NEC na CC, walivyoweza kutupatia kwa uhakika list ya waliopitishwa na waliotemwa!
Habari naziona za vipande vipande na Zingine zinatofautiana na za magazeti ya hapa nchini, kwa mfano issue ya Dada Salome Mbatia...
"CCM yatema mawaziri wanane kuwania NEC
2007-08-02 10:27:47
Na Mary Edward, PST Dodoma
Wakati Chama cha Mapinduzi kimeshikwana kigugumizi kuwataja wagombea waliotemwa na waliopitishwa kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, imebainika kuwa, Mawaziri na Naibu Mawaziri wanane, wametupwa nje ya kinyang`anyiro hicho.
Mawaziri hao, wametemwa kwenye kikao cha mchujo cha siku mbili cha NEC kilichokutana mjini hapa juzi na jana.
Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu mbalimbali vimewataja baadhi ya vigogo walioenguliwa kuwania nafasi hiyo nyeti ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Salome Mbatia na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Rita Mlaki.
Hali kadhalika, vyanzo hivyo vya habari, vimewataja Bw. Kisyeri Chambiri na Chacha Mwita Gachuma kuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri ndani ya chama hicho ambao safari hii wametupwa nje kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara.
Vigogo wengine wa CCM ambao wametemwa kwenye mchujo huo ni pamoja na Bw. Didas Masaburi na Chacha Nyamoyo Wambura? aliyekuwa akigombea ujumbe wa NEC kupitia Umoja wa Wazazi Tanzania.
Taarifa zaidi zilidai kuwa, mwenyekiti wa sasa wa Mkoa wa Mtwara aliyekuwa akigombea ujumbe wa NEC, alianguka na kupoteza fahamu kikaoni baada ya jina lake kuondolewa katika mchujo huo."
Mzee Dar na Killtime, mnasema hii habari ina ukweli zaidi ya habari zilizoko kwenye thread yetu? Kubainika ni ukweli as a fact?
Hali kadhalika, vyanzo hivyo vya habari, vimewataja Bw. Kisyeri Chambiri na Chacha Mwita Gachuma kuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri ndani ya chama hicho ambao safari hii wametupwa nje kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara.
Vigogo wengine wa CCM ambao wametemwa kwenye mchujo huo ni pamoja na Bw. Didas Masaburi na Chacha Nyamoyo Wambura? aliyekuwa akigombea ujumbe wa NEC kupitia Umoja wa Wazazi Tanzania.
Maulid Ahmed, Dodoma
HabariLeo; Friday,August 03, 2007 @00:03
http://www.dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=3289
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), jana kilitangaza wagombea mbalimbali waliopitishwa kuwania nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.
Wagombea hao ni wale wanaowania uenyekiti wa chama hicho kwa ngazi ya Wilaya na Mikoa na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia katika makundi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Uenezi na Itikadi, waliopitishwa kwa Kundi la Tanzania Bara kuwania viti 20 vya NEC ni pamoja na Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba.
Wengine ni Abdulrahman Kinana, Novatus Makunga, Tarimba Abbas, Filbert Bayi, Shyrose Bhanji, Juma Kapuya, Hamida Kilua, Lucas Kisasa, John Komba, Dk. Makongoro Mahanga, Mohammed Mamoon, Wilson Masilingi, Bernard Membe, William Ngeleja, Kingunge Ngombale-Mwiru, Salim Hamis Salim Chicago, Frederick Sumaye, William Lukuvi, Siwajibu Clavery, Jaka Mwambi, Job Ndugai, John Simbachawene, Abdul Adam Sapi, Frank Uhahula, Dk. Diosdorus Kamala, Said Kilahama, Nicolas Zakaria, Dk. David Mathayo, Aggrey Mwanri, David Holela, Isdore Shirima, Stephen Wassira, Christopher Gachuma, Enock Chambiri, Maurus Mhimbila, Profesa David Mwakyusa, Emmanuel Mwambulukutu, Amos Makala, Baanda Ayoub Salum na, Jackson Msome.
Wengine ni Aborgast Godogodo, Dk. Alex Msekela, Constantine Kanyasu, Amos Siyantemi, Mohammed Mkumba, Profesa Idris Mtulia, Profesa Samwel Wangwe, Andrew Chenge, Jared Kaduga, John Chiligati, Pascal Mabiti, Said Fundikira, Abeid Mwinyimsa, Charles Kagonji, Ibrahim Msengi, Hassan Ngwilizi na Hashim Chakiondo.
Kwa kundi la Vijana ambao wana nafasi 15, waliopitishwa ni Mwamini Lusingu, Abdallah Mayomba, Omar Kiliati, Zainabu Kawawa, Sixtus Mapunda, Vanessa Mugeta, Nape Nnauye, Jerry Slaa, Ashura Selemani, Neema Mwakabonga, Deogratius Ndejembi, Edwin Sanda, Melkiador Januari, Penias Kaindoa, Rajabu Katunda, Benno Malisa na Paul Kirigini.
Wengine ni Lutengano Mwalywiba, Sara Ally, Adela Ngasigwa, Rose Juma, Magembe Magembe, Pili Jadir, Jenista Mboneko, Violet Mzikandaya, Raymond Mwangwala, Lucy Mayenga, Francis Mtinga, Suleiman Nchambi, Hussein Basheikh na Rodgers Shemwelekwa.
Kwa nafasi 15 za Wazazi Bara, wagombea ni Fortunata Kabeja, Enock Kalumuna, Selina Mkonji, Mohammed Nondo, Salum Tambarizeni, Tambwe Hizza, Mustapha Yakub, Mussa Azzan Zungu, Ruth Msafiri, Thomas Ngawaiya, Henry Shekifu, Richard Nyaulawa, Innocent Kalogeris, Margaret Makanga, Aziz Jawad Aziz, Dickens Shindika, Dk Zainab Gama, Adam Malima, Stella Manyanya, Athuman Mfutakamba na Mgosi Bakari.
Nafasi 20 za Umoja wa Wanawake (UWT), waliopitishwa ni Halima Mamuya, Sifa Swai, Asha Baraka, Khadija Kopa, Jackline Liana, Anne Makinda, Jane Mihanji, Fatuma Mkwawa, Rita Mlaki, Regina Chonjo, Sophia Simba, Margaret Sitta, Kate Kamba, Shamsa Mwangunga, Pindi Chana, Amina Mrisho Saidi, Janath Kayanda, Sakina Kabeza, Anne Malecela, Salome Mbatia na Zakia Meghji.
Wengine ni Jackline Noni, Anna Magowa, Dk. Rehema Nchimbi, Chiku Galawa, Halima Kihemba, Fatma Kimario, Elizabeth Mwaipwani, Gulazar Sabil, Margaret Mkanga, Lydia Boma, Zuhura Mikidadi, Hellen Bogohe, Esther Nyawazwa, Mwanaidi Kiongoli, Zainab Vullu, Esha Stima, Diana Chilolo, Tatu Ntimizi, Dk. Aisha Kigoda, Mwantumu Mahiza na Beatrice Shelukindo.
Hata mimi nimeshangaa, habari nyingi tulizokuwa tunaletewa hapa ni uongo mtupu. Ni tofauti na wakati ule wa uchaguzi wa rais ambapo mambo mengi yalikuwa sahihi.
Huyo mama Rita mmemsema bure kumbe yumo bado kwenye kapu la wanawake. Hivi hizi habari mlizitoa wapi? Hivyo hivyo kwa huyo mtoto wa JK.
In future kama huna uhakika na habari, usiilete hapa. Kwa kuandika majungu tutapoteza heshima ya JF
Kilitime,
Nakubaliana na wewe. Hata baadhi ya magazeti mambo mengine wanachukua hapa. Sasa kama tunaandika majina ya watu ka makosa kiasi hivyo ni vibaya sana kwa reputation ya JF.
Mimi ningetaka wale wote walioandika habari za uongo hapa angalau waombe msamaha kama ambavyo IPPMEDIA wameomba msamaha.
Tukionekana mara mbili au tatu, tunasema mambo ambayo baadaye yanakuja kujulikana ni uwongo, huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa JF.
hii ni dunia kijana na kuna mengi mnoooooooooo kuchoka nayo, otherwise u just gonna have to give up on life kama umechoka the so called UDAKU ! kwani wee hujui watu walipolelewa, tz !