Uchaguzi Mkuu kusimamishwa?

Yaleyale kama Zanzibar. Kuna kuchaguana basi nchi hii? Mgombea binafsi wa nini wakati huu? Hata kutafuta mchumba tu hauwi mgombea binafsi! Mnataka akina RA, EL, Mzee Mengi, Manji, Mtume na Nabii Mwigira, Kakobe, Sheikh Ponda, Prof Majimarefu, Dr Remmy Ongara, .....wagombee Urais?
Wacha wagombee si ni watanzania na wana haki ya kugombea kama watanzania wengine bora watimize vigezo vinavyotakiwa, acha kuwabania.
 
Ndugu WC
nafikiri hapa suala si kubadili katiba hukumu iliyoko ni utata wa katiba yenyewe sehemu moja inaruhusu nyingine hairuhusu Mtikila anachosema ni katiba iheshimiwe kwa hiyo kama atashinda kesi katiba haitabadilishwa kwa sababu imeshasema wazi kila mtu ana haki ya kupiga na kupigiwa kura kinachotakiwa kubadilika ni sheria tu za uchaguzi na si katiba.

Serikali ya CCM inadharau Mahakama..iwapo suala ni kubadili Katibu au Sheria za uchaguzi...Waziri Marmo alitakiwa aliambie Bunge, nini Serikali imefanya kutekeleza agizo la Mahakama tangu mwaka jana...na sio kusema suala linahitaji muda..

Muda My Behind...hukumu imetolewa MAY 5, 2006 tena na Majaji 3 wa Mahakama Kuu...tangu 2006 mpaka leo bado wanahitaji muda?!!!
 
Bila mgombea binafsi uchaguzi batili-Mbatia

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesema chaguzi zijazo ni batili kama serikali itakiuka amri ya Mahakama Kuu ya kutokuwepo kwa mgombea binafsi.

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia alisema serikali iliyopo imewekwa kikatiba, hivyo inamsikitisha kuona watendaji wake wanakiuka sheria zilizowaweka madarakani.

Kauli hiyo aliitoa kufuatia kauli ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Bw. Philip Marmo kwamba Uchaguzi Mkuu ujao hautakuwa na mgombea binafsi kama ilivyoamriwa na Mahakama Kuu kwa maelezo kuwa yanahitajika maandalizi ya muda mrefu.

Kauli hiyo ya Bw. Mbatia inaungana na iliyotolewa juzi na Mchungaji Christopher Mtikila kuwa matamshi ya Bw. Marmo ni kuangushwa kwa utawala wa sheria.

Bw. Mbatia alisema anashangazwa na kuwepo kwa kutoheshimiwa kwa mhimili wa mahakama, hasa pale serikali inapouingilia.

Kwa mujibu wa Bw. Mbatia, sheria nyingi hasa za uchaguzi zimetawaliwa na migogoro kutokana na waliozitunga na kuzipitisha kutokuwa makini.

Alisema vyama vya upinzani vimekuwa mstari wa mbele katika kukemea sheria hizo ikiwa ni pamoja na kwenda mahakamani kuzipinga ambako Mahakama Kuu ilikubaliana na hoja zao na kuamuru kufutwa kwa baadhi ya sheria hizo.

“Unajua bwana, mfumo wa siasa Tanzania ni wa kifisadi fisadi tu…anatokea mtu anaamua kuvunja tu sheria kwa manufaa yake binafsi bila kuangalia athari zake.

“…(Marmo) ametoa tamko linalopingana na amri halali ya Mahakama Kuu kwa kutoweka mgombea binafsi, kwa mazingira haya ya kukiuka katiba ya nchi, uchaguzi wa serikali za mitaa haukuwa wa haki na hata huu Uchaguzi Mkuu unaosubiriwa nao hautakuwa wa huru na haki kama serikali itasimama kwenye msimamo wake wa kutokuwepo kwa mgombea binafsi,” alisema Mbatia.

Mwenyekiti huyo alisema sheria nyingi za uchaguzi zimekuwa na ‘viraka viraka’ kutokana na kufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara, na hivyo kuwashauri wanaozitunga na kuzipitisha kuwa makini.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Mwenyekiti wa chama cha Democratic (DP) Mchungaji Christopher Mtikila, aliwataka wananchi kupuuza matamshi hayo ya Bw. Marmo.

Alisema kauli ya Bw. Marmo ni dhahiri imelenga kupingana na amri ya mahakama iliyoamuru kuwepo kwa mgombea binafsi katika chaguzi na kwamba kinyume chake ni kwamba chaguzi hizo ni batili.

Aliishauri serikali kama inaheshimu amri za mahakama ni vema kama maandalizi ya kuwepo kwa mgombe binafsi bado ni vema Uchaguzi Mkuu ukaahirishwa.

Hata hivyo, Bw. Marmo alisema suala hilo linahitaji mchakato wa muda mrefu unaoambatana na gharama kubwa, hali ambayo itasababisha mwaka huu ishindikane utekelezaji wake.
 
Kama ulimsikiliza vizuri alikuwa anaongelea muda. Ni swala ambalo litahitaji kubadili KATIBA. Linahitaji mchakato mrefu kidogo. Hukumu ya mahakama haibadili katiba automatically.

lets wait then,how do you say
 
LHRC imesema itasimamisha uchaguzi iwapo serikali haitalipatia ufumbuzi suala la mgombea binafsi
 
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kinatarajia kwenda mahakamani kusimamisha Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba, 2010 ikiwa serikali itakaidi kubadilisha vipengele vya sheria na kuweka mazingira mazuri ya kuruhusu mgombea binafsi.

Kadhalika, kituo hicho kimekerwa na kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, kwa kutangaza kuwa serikali haitambui kuwepo mgombea binafsi.

Msimamo huo wa LHRC ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wake mkuu, Francis Kiwanga, alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema Mahakama Kuu ilishatoa hukumu mwaka 2006 na kutamka kuwa mgombea binafsi anaruhusiwa na kwamba kitendo cha serikali kudharau amri hiyo ni kosa kisheria.

Alisema ndani ya miezi minne lazima serikali ihakikishe inarekebisha vipengele vya sheria vinginevyo watakimbilia mahakamani ili kupinga uchaguzi usifanyike bila mgombea binafsi kushiriki.

Alisema kuna sheria nyingi zilizowahi kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge katika kipindi kifupi hivyo hatua ya kuruhusu mgombea binafsi inawezekana.

Alitolea mfano wa sheria ya uchaguzi ambayo ilijadiliwa na wabunge na kupitishwa ndani ya siku mbili.

Alisema hukumu ya Mahakama Kuu haijatenguliwa na Mahakama ya Rufaa kama alivyosema Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani hivi karibuni.

Kiwanga alisema serikali inakataa kwa makusudi amri halali ya Mahakama na kwamba ubabe wake huo unakinzana na kifungu cha 14(3) cha Sheria ya utekelezaji wa haki za msingi za binadamu.
 
HOJA YA MGOMBEA BINAFSI :Bomani aishangaa serikali

MWANASHERIA Mkuu wa Kwanza mzalendo nchini, Jaji Mark Bomani amesema serikali inakwamisha bila sababu suala la mgombea binafsi katika uchaguzi,mbali na kuitaka serikali kuacha kigugumizi katika kuruhusu utekelezaji wa suala hilo; alikosoa mfumo wa sasa wa uchaguzi na uteuzi wa mawaziri na kupendekeza kwamba, siyo lazima waziri awe mbunge.

Jaji Bomani ambaye alishawahi kushiriki katika kamati mbalimbali za kutafiti mfumo sahihi wa uchaguzi unaofaa Tanzania, alitoa changamoto kwa Rais Jakaya Kikwete kuwa ndiye anayepaswa kusimamia suala hilo.

Alisema Rais Kikwete ana nguvu na nafasi ya kihistoria kutekeleza uamuzi huo wa mahakama kwa kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu ujao.

Jaji Bomani alisema hatua nzuri na muhimu ya kuanzia katika utekelezaji wa suala la mgombea binafsi na kuboresha mfumo wa uchaguzi Tanzania, ni kupitia upya ripoti ya Jaji Kisanga, jambo alilosema kuwa serikali haijachelewa.

"Ripoti ya Tume ya Jaji Francis Nyalali ni moja kati ya kamati kubwa zilizoundwa na kulifanyia kazi suala hilo na kupendekeza kuwepo mgombea binafsi na kazi hiyo ilifanyika 1991.

Tume ya Jaji Kisanga nayo ikafuata nyayo, pia ripoti ya tume ya Elkit, Bomani na Maina wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa nguvu zote ilipendekeza kuruhusiwa mgombea binafsi," alikumbusha Jaji Bomani katika taarifa hiyo na kuongeza:

"Hata marehemu baba wa taifa, mwalimu Nyerere kwa nguvu zote naye alisimamia hoja hiyo katika hotuba yake kwenye sherehe za sikukuu ya wafanyakazi zilizofanyika mkoani Mbeya 1995 na mahakama za sheria mara kwa mara zimekuwa zikiamua kwa uwazi kuhusu hoja hiyo na zinasisitiza kwamba ni kinyume na katiba ya nchi kuizika hoja ya mgombea binafsi".

"Hakuna ushahidi wowote wenye nguvu wa kuonyesha kwamba, kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi kunaweza kuleta vurugu katika uchaguzi," alisema Jaji Bomani.
 
Yaleyale kama Zanzibar. Kuna kuchaguana basi nchi hii? Mgombea binafsi wa nini wakati huu? Hata kutafuta mchumba tu hauwi mgombea binafsi! Mnataka akina RA, EL, Mzee Mengi, Manji, Mtume na Nabii Mwigira, Kakobe, Sheikh Ponda, Prof Majimarefu, Dr Remmy Ongara, .....wagombee Urais?

Acha uzembe na uvivu wa kufikiri wewe, aliyekwambia hao wote hawawezi ni nani-------huu ndo uvivu ambao hatuitauhtaki katika Tanzania ya leo, kama bado ni immature tafadhali kaa kimya, kila mtu ana haki ya kugombea na kuwa kiongozi haimaanishi ngozi wala jinsia ili mradi awe na maadili ya Uongozi (Leadership integrity) Serikali lazima ikubali, make mahakama hata yenyewe ya Rufaa imeishanza kuwabana, kwa sababu hakuna shida yoyote
 
.......na Sheikh Yahya nae kashatabiri Uchaguzi mwaka huu HAKUNA. tusubiri tuone
 
Yaleyale kama Zanzibar. Kuna kuchaguana basi nchi hii? Mgombea binafsi wa nini wakati huu? Hata kutafuta mchumba tu hauwi mgombea binafsi! Mnataka akina RA, EL, Mzee Mengi, Manji, Mtume na Nabii Mwigira, Kakobe, Sheikh Ponda, Prof Majimarefu, Dr Remmy Ongara, .....wagombee Urais?

Acha uzembe na uvivu wa kufikiri wewe, aliyekwambia hao wote hawawezi ni nani-------huu ndo uvivu ambao hatuitauhtaki katika Tanzania ya leo, kama bado ni immature tafadhali kaa kimya, kila mtu ana haki ya kugombea na kuwa kiongozi haimaanishi ngozi wala jinsia ili mradi awe na maadili ya Uongozi (Leadership integrity) Serikali lazima ikubali, make mahakama hata yenyewe ya Rufaa imeishanza kuwabana, kwa sababu hakuna shida yoyote ya kuzuia mgombea binafsi---halafu mbona CCM wanaombea sana Tanzania kupata vurugu na aliyesema kuwa sisi tunaogopa sana vurugu ni nani---vurugu ni sehemu ya Mapinduzi Fikra (mindset revolution), bila kupitia huko ujue hiyo nchi haiwezi pata maendeleo kamwe----Historia inaonyesha kuwa nchi zote za ulaya magharibi na Marekani zimepita huko na ndo maana unaona kuna heshima na uadilifu kwenye Uongozi. Sasa kama Tanzania bado hilo tukio halijatokea basi there's one day---one day if not today then is gonna be tomorrow, in our coming generation if not this one vurugu na mwamko wa watu kifikra itakuja tokea. Historia lazima itakuja timia , upumbavu wote huu utakwisha and watu watanyooshwa na ndipo maadili ya Uongozi yatakuwepo na heshima ya Mtanzania itarudi.
 
Kwani sheria inasemaje kama uchaguzi hautafanyika nani atashika hatamu?
 
Mh... Dalili zinazidi kuonekana... Wanamtumia jamaa huyu kuandaa mazingira?

Hata Marmo naye jana kasema ikiwa mahakama ikipitisha uwezekano uliopo ni kuahirisha uchaguzi naona sasa hata wao wameanza kuliona hilo
 
CCM watakapoona mahakama imewabana kisawasawa walitalisukuma suala hili kwenye kura ya maoni. Wana mbinu na njia nyingi za kutokea. Kwa kifupi ni kwamba wasichotaka CCM kifanyike nchi hii hakitafanyika.

Kama ccm watalisukumizia hilo suala la mgombea binafsi kwenye kura za maoni hapo ndipo wapinzani wanaweza kuwabana kuwa it does not make sense kuwa na kura za maoni juu ya suala moja katika katiba yetu wakati kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kubadilishwa kwenye katiba; kwahiyo itakuwa jambo la busara kufanya review ya katiba yote ili iendane na mabadiliko ya nchi and then kuitisha kura ya maoni kuona kama wananchi wanakubaliana na mabadiliko yaliyopendekezwa kwenye hiyo draft!! Ninahakika CCM would rather admit independent candidates kuliko review ya constitution yote!!
 
Wagombea binafsi kutaleta watu wa maana bungeni ambao wataweza kuleta challenge za maendeleo kwa taifa letu kuliko wabunge wa sasa ambao wanaangalia zaidi maslahi ya vyama vyao kuliko maslahi ya watanzania
 
Kitu hiki hakiwezekani Tanzania kama tu vyama vya upinzani ni kukataa na kufanya mabadiliko ya katiba na tume huru ndio kitu kikubwa hiki jamani na sio vingine
 
Back
Top Bottom