Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
- Thread starter
- #41
[FONT=ArialMT, sans-serif]Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amewaandikia barua maprofesa wawili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akiwaomba wawe marafiki wa mahakama katika usikilizwaji wa rufaa ya mgombea binafsi itakayosikilizwa na Mahakama ya Rufaa Aprili 8, mwaka huu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Maprofesa hao, ambao ni wanasheria kitaaluma na wahadhiri waandamizi, ni Jwan Mwaikusa na Palamagamba Kabudi, ambaye ni Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha UDSM.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika barua yake ya Machi 3, mwaka huu, Jaji Mkuu amewaomba maprofesa hao kuwa marafiki wa mahakama na wajielekeze katika hoja zao kama mahakama inaweza kutamka kifungu gani cha katiba kinakwenda kinyume cha Katiba.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, Aprili 8, mwaka huu, Profesa Mwaikusa na Kabudi watachangia hoja kuhusu shauri hilo, litakaposikilizwa na Mahakama ya Rufani, mbele ya jopo la majaji saba linaloongozwa na Jaji Mkuu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mahakama hiyo inatarajia kusikiliza rufaa ya serikali dhidi ya uamuzi uliotolewa na waliokuwa majaji wa Mahakama Kuu; aliyekuwa Jaji Kiongozi, Amir Manento, Salum Massati (sasa Jaji wa Mahakama ya Rufaa) na Thomas Mihayo (Mstaafu).[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Majaji hao katika hukumu yao, walikubaliana na hoja zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Democrat (DP), Mchungaji Christopher Mtikila za kuwapo mgombea binafsi katika uchaguzi wa siasa nchini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Jopo la majaji saba wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Jaji Mkuu, linawajumuisha Jaji Eusebia Munuo, Januari Msofe, Nathalia Kimaro, Mbarouk Salim, Dk. Stephen Bwana na Benard Ruanda, watasikiliza rufaa hiyo.[/FONT]