Uchaguzi Mkuu Kenya: Ghasia zaanza Kisumu

Uchaguzi Mkuu Kenya: Ghasia zaanza Kisumu


AFRIKA MASHARIKI



kenya_ghasia.jpg
​

Na Mwandishi Wetu, Mashirika

Posted Jumatatu,Marchi11 2013 saa 9:21 AM

KWA UFUPI

Mahakama Kuu ya Kenya (Supreme Court) ndicho chombo chenye uwezo wa kutengua matokeo ya urais yaliyotangazwa na Bodi ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC).

Jopo la majaji watano ndilo litakalosikiliza rufaa ya mgombea wa Cord, Raila Odinga nao ni Jaji Mkuu, Dk Willy Mutunga ambaye ni Rais wa Mahakama hiyo wengine ni Majaji Dk Smokin Wanjala, Njoki Ndung'u, Philip Tunoi, Jackton Boma Ojwang na Mohamed Ibrahim.


​
Nairobi: Polisi wa kutuliza ghasia juzi walilazimika kutumia mabomu ya machozi Mjini Kisumu kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakipinga kutangazwa kwa matokeo ya urais ambayo mgombea wao, Raila Odinga alianguka.

Vurugu hizo ziliibuka, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta.

Maelfu ya vijana wamekuwa wakirandaranda kwenye maeneo kadhaa ya Kisumu wakichoma majengo na kufunga barabara, huku wakiimba: "Bila Raila, hakuna amani."

Vurugu hizo zilizoanza juzi jioni zimesababisha maduka kufungwa huku makundi ya vijana wenye hasira wakiendelea kurandaranda mitaani wakipambana na polisi ambao walifanya jitihada za kuwatuliza na kurejesha amani.

Ilielezwa kwamba, muda mfupi tu baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kumtangaza Kenyatta kuwa mshindi, zaidi ya vijana 100 waliibuka na kuanza kuwarushia mawe polisi na muda mfupi baadaye idadi ya vijana hao iliongezeka na kusambaa katika maeneo karibu yote ya Kisumu.

Odinga ambaye alikuwa mgombea wa Muungano wa Cord, amewataka wafuasi wake kuwa watulivu kwa kuwa anahitaji kufuata mkondo wa sheria kupinga matokeo hayo.
Matokeo hayo yaliyotangazwa juzi, yalimpa ushindi Kenyatta aliyesimama kwa tiketi ya Muungano wa Jubilee, wa asilimia 50.07 dhidi ya asilimia 43 alizopata Raila.


Raila atinga mahakamani
Muungano wa Cord, leo utawasilisha vielelezo mahakamani kupinga ushindi wa Kenyatta.

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Kenya, Amos Wako ametajwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa jopo la wanasheria watakaopinga ushindi wa Kenyatta.


Jopo hilo la wanasheria linaongozwa na mwanasheria mkongwe, George Oraro na baadhi ya mawaziri wakiwamo; Mutula Kilonzo, James Orengo na Ababu Namwamba ambao ni washauri wakuu wa jopo.

Oraro alimtetea aliyekuwa Waziri wa Viwanda, Henry Kosgei wakati alipokabiliwa na kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya ICC, The Hague.

Wengine wanaounda timu hiyo ni Gitobu Imanyara, Pheroze Nowrojee, Chacha Odera, Ambrose Rachier na Paul Mwangi.


Cord imepanga kufungua kesi ikitaka Mahakama itengue hatua ya kutangazwa kwa Kenyatta kuwa Rais wa Kenya kwa kuwa taratibu za ukusanyaji matokeo zilikiukwa.
Tangu juzi, jopo hilo la wanasheria lilikuwa na vikao mfululizo kuandaa ushahidi wa kesi hiyo ikiwamo kukusanya vielelezo watakavyosimamia katika kesi hiyo kwa mujibu wa Kifungu namba 163 cha Katiba ya Kenya.


Mfuasi wa Uhuru afariki
Shamrashamra za kushangilia ushindi wa Kenyatta ziliingia doa kwenye Mji wa Nyeri baada ya lori lililobeba mashabiki wa mgombea huyo kutumbukia kwenye korongo na kuua mtu mmoja. Katika ajali hiyo watu 30 walijeruhiwa lakini wakiwa katika hali mbaya.


Mwili wa mtu aliyefariki ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Nyeri wakati wengine waliojeruhiwa wamelazwa kwenye hospitali hiyo.

Lori hilo lilikuwa likienda maeneo ya Giakanja kwa ajili ya kukusanya mashabiki wengine na kuanza safari ya kuzunguka mitaa ya mji huo kushangilia ushindi.

Kamanda wa Polisi Nyeri, Kirunya Limbitu alithibitisha ajali hiyo na kusema lori hilo lilikuwa kwenye mwendokasi na kupoteza mwelekeo kabla ya kutumbukia kwenye korongo na kupinduka.


 
Taaratibu Uchaguzi Huo Unanyofoka... Kweli Ulikuwa wa HAKI? Rais wa CCM ameupongeza
 
Kwa ukabila wa Kenya ulivyo Huwezi kumshinda Mkikuyu bila msaada wa Mkalenjing RAO alifanya kosa kubwa sana kumuachia Ruto sasa anataabika. Hata wakienda round two ataanguka tena! akubali yaishe kwa amani bila kumwaga damu za wakenya.
 
Kwa ukabila wa Kenya ulivyo Huwezi kumshinda Mkikuyu bila msaada wa Mkalenjing RAO alifanya kosa kubwa sana kumuachia Ruto sasa anataabika. Hata wakienda round two ataanguka tena! akubali yaishe kwa amani bila kumwaga damu za wakenya.
exactly!
 
Kama anaoushahidi wamechakachua kura zake,ruksa kwenda mahamani lakini si fujo
 
pole sana wakenya


Nimeangalia Citizen Tv na walionesha tukio hilo vizuri sana na kuwahoji watu wa kutosha. Kwa maoni yangu, halikufikia kiwango cha kuandikwa kwenye gazeti na kupewa uzito kama walivyofanya mwananchi. Ni tukio dogo sana, ni wahuni wachache sana. Hata idadi ni ndogo sana. Bado Mpaka jana jioni kenye ilikuwa shwari kwa ujumla, based on their Citizen TV NA NTV
 
nasikia uhuru anahaha kumbembeleza raila aache kwenda mahakamani. Ingekuwa Raila ni mgombea uchwara kama vile wengi wa huku angeshawishiwa kwa pesa.

Kuna ushahidi mzito -- mitandao iliiingiliwa na kuharibiwa ili mtindo wa manual utumike kama vile zamani ili walioandaliwa wapate kuiba kura!

jaji Mkuu Mutungi atakayeongoza jopo la kusikiliza kesi amesema itakuwa open case na hivyo kuonyeshwa ktk TV live kabisa. Kundi la raila likiweza tu kuonyesha mitandao ya kielectronic ilikuwa disabled kimakusudi, na siyo bahati mbaya, basi Kenyatta atatema ushindi aliopewa na IEBC na uchaguzi kurudiwa baina ya wawili hao.
 
nasikia uhuru anahaha kumbembeleza raila aache kwenda mahakamani. Ingekuwa Raila ni mgombea uchwara kama vile wengi wa huku angeshawishiwa kwa pesa.

Kuna ushahidi mzito -- mitandao iliiingiliwa na kuharibiwa ili mtindo wa manual utumike kama vile zamani ili walioandaliwa wapate kuiba kura!

jaji Mkuu Mutungi atakayeongoza jopo la kusikiliza kesi amesema itakuwa open case na hivyo kuonyeshwa ktk TV live kabisa. Kundi la raila likiweza tu kuonyesha mitandao ya kielectronic ilikuwa disabled kimakusudi, na siyo bahati mbaya, basi Kenyatta atatema ushindi aliopewa na IEBC na uchaguzi kurudiwa baina ya wawili hao.
Uchaguzi umeisha na tayari rais ametangazwa,hizo stori za kwamba mgombea wako anabembelezwa hazina mashiko. Kwa busara ya kawaida kwa kuangalia matukio ya 2008, Mahakama haiwezi jiingiza ktk maamuzi ambayo yataitumbukiza Kenya ktk ghasia na machafuko. Uhuru ndiye rais mpya wa Kenya,hata kama ni ukweli mchungu kwako!
 
Haya mambo ya vurugu, wanaoumia ni watoto na vikongwe. I hope JK na kundi lake wataingilia kabla damu zaidi hazijamwagika
 
Amegombea uraisi mara ngapi vile?

Uhuru amegombea Mara mbili...na raia Mara mbili pia.........mwaka 2002 Raila alimuunga mkono Kibaki....Mwaka 2007 uhuru akamuunga mkono Kibaki dhidi ya Uhuru...

Just Angelia wakikuyu walivyo waajanja...walimtumia Raila 2002....aliposhtuka 2007 ..wakaungana dhidi yake....mwaka huu wakawatumia Kalenjin....hawa wataendelea kutawala Kenya sana tu
 
Mwaka 2002 uhuru aligombea akiungwa mkono na Moi na Kalenjin .......na Kibaki akiungwa mkono na Raila na Jaluos.....( Kumbe Kibaki na uhuru walikuwa wanajuana..Matokeo yalipotoka...a uhuru akiwa kiongozi wa upinzani...Kibaki...Rais ....lol waliposhtuka too late)
2007 ....Raila na makabila mengine wakaungana....Kibaki akiungwa mkono Na Uhuru...
 
Back
Top Bottom