Uchaguzi Mkuu Kenya: Ghasia zaanza Kisumu

Uchaguzi Mkuu Kenya: Ghasia zaanza Kisumu

Wakenya watulie wasikubali kurudi kwenye machafuko kama ya 2007/2008.wanasiasa wa afrika ni kichefuchefu.
 
Bora Uhuru kuliko Raila, hii ni personal assessment yangu.
Wakenya tulieni na jengeni taifa lenu, ninyi mtakaopogana kumbukeni hamtoonja hata chembe ya senti ya utamu wa urais kwa mnayempigania, bali mtapata madhila na hata ulemavu kwa kuhamasishwa juu ya vurugu/maandamano.
Kuweni makini majirani zetu, MSITUMIWE.
ndio maana ccm inaamini itatawala milele, kulingana na misimamo ya aina hii.
 
.....................
Jopo la majaji watano ndilo litakalosikiliza rufaa ya mgombea wa Cord, Raila Odinga; nao ni Jaji Mkuu, Dk. Willy Mutunga ambaye ni Rais wa Mahakama hiyo, wengine ni Majaji Dk. Smokin Wanjala, Njoki Ndung'u, Philip Tunoi, Jackton Boma Ojwang na Mohamed Ibrahim.

Source: Mwananchi, Jumatatu, Marchi 11, 2013
Ila kwa politiks za kikabila huko Kenya sijui hapa hawa majaji wataamuaje, kwa uwiano wao wa kikabila haonekani kuwa sawa! Halafu Majaji hao ni sita, siyo watano unless Rais wa mahakama hiyo asihesabiwe!
 
Waluo wamechoka kutawaliwa na kunyanyaswa na wakikuyu.....kwani ni wakikuyu 2 iliandikwa watawale...? huu si ungoz wa kiflme
 
Odinga si atulie tu!Maisha ya Kenya si lazima awe Odinga tu!apumzike aombe Uhuru ampe hata uwaziri amalizie miaka yake akiwa waziri ingawa ni tajiri anaweza kufanya biashara zake!sio lazima awe kiongozi!kura hazikutosha

Hapana; swala siyo umri au utajiri wa mtu, bali ni kujenga utaratibu unaowapa watu wote haki saw katika kugombe nafasi za uongozi wa nchi katika ngazi mbalimbali. Swala kubwa hapa ni utaratibu wa kumpata kiongozi wa nchi.
 
Wakenya watulie wasikubali kurudi kwenye machafuko kama ya 2007/2008.wanasiasa wa afrika ni kichefuchefu.
Nakubaliana nawe 100. Vurugu hazisaidii sana iwapo bado kuna njia ya kisheria. Katiba ya Kenya ni nzuri kuliko yetu kwa vile eti sisi baada ya kiapo cha Rais basi mambo ndiyo mwisho. Kenya wenzetu hawana upuuzi wa aina hiyo; haki ya kura iko pale pale na itashindwaniwa mahakamani kama kawaida.
 
Nitasikitika ssana nikiona tena Kenya inaingia matatani shauri ya wanasiasa, Sijui tutatumia utaratibu gani wa kupata vuingozi bila siasa, Nimeichukua siasa sana shauri ya WANASIASA
 
Wapasuane tu. Neema kwetu
Arusha mpaka sasa bado ni high season, wageni wa kumwaga tunakula bata.
 
... Kweli kuna tishio la maana hapo?

Ghasia kubwa huanzishwa na ghasia ndogo ndogo kama hizo.
Watu hufanya makosa kama hayo hapo kwenye blue, na ndio ghasia kubwa hutokea.
Ghasia za nchini Tunisia zilianza kwa mtu mmoja kujichoma moto, baadaye serikali ikapinduliwa.
Mdharau mwiba, mguu huota tende.
 
Mimi nafikiri wakenya wameshaamua. Hata kama kura zilipigwa kwa kufuata ukabila ni muhimu maamuzi ya watu yakaheshimiwa. Nilikuwa namsupport Odinga lakini ni vizuri nikiri kuwa kwa namba za wapiga kura zilivyo nchini Kenya nahisi Uhuru kashinda kihalali. Wajaluo walimpigia Odinga na Wakikuyu ambao ni wengi walimpigia Uhuru.
 
Yaani waafrica ni wagumu kukubali matokeo! Odinga utashindwa tu! Tafuta cha kufanya

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hata wao 2015, watamuomba mzee atulie tu, na hata wale wafuasi wake wataombwa kutulia tu.
 
Polisi wa kutuliza ghasia, wamelazimika kutumia mabomu ya machozi nchini Kenya, mji wa Kisumu kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakipinga matokeo ya urais ambayo mgombea wao, Raila Odinga alishindwa katika uchaguzi uliofanyika nchini humo.


Vurugu hizo ziliibuka, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta.


DOKEZO
Mahakama Kuu ya Kenya ndicho chombo pekee chenye uwezo wa kutengua matokeo ya urais yaliyotangazwa IEBC.

Jopo la majaji watano ndilo litakalosikiliza rufaa ya mgombea wa Cord, Raila Odinga; nao ni Jaji Mkuu, Dk. Willy Mutunga ambaye ni Rais wa Mahakama hiyo, wengine ni Majaji Dk. Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Philip Tunoi, Jackton Boma Ojwang na Mohamed Ibrahim.

Source: Mwananchi, Jumatatu, Marchi 11, 2013

Hii ndio Afrika yetu ngoja na tuone mwisho wa yote...
 
hivi una ushaidi gani wewe wa kusema kura zimeibiwa?
pale mashine zilipogoma ni ushahidi wa mwanzo kabisa maana yalitoka matokeo kwenye majimbo ambayo uhuru aliongoza mpaka kufikia kura milioni mbili pointi tano na hapo ndipo mashine zikaanza kukorofisha na hata matokeo yalipoendelea kutoka kukawa na tofauti ya kura zisizopungua laki tano kwa kipindi kirefu sana mpaka mwisho mwishoni ndipo odinga akasogea kwa nguvu wakati alishachelewa tayari.kuleta mitambo mibovu kwa nchi yenye siasa ngumu kama za kenya ni hatari sana.huu ni mtizamo na hisia tu
 
Ghasia kubwa huanzishwa na ghasia ndogo ndogo kama hizo.
Watu hufanya makosa kama hayo hapo kwenye blue, na ndio ghasia kubwa hutokea.
Ghasia za nchini Tunisia zilianza kwa mtu mmoja kujichoma moto, baadaye serikali ikapinduliwa.
Mdharau mwiba, mguu huota tende.
afadhali umuongezee maarifa
 
Back
Top Bottom