Mkuu kama ni kweli uyasemayo na una hakika kura zikipigwa kidini hakuna muislaam atakaye pata uongozi! Sasa hofu yenu haswa nini maana kajitia chongo mwenyewe au sivyo? Na huyu Idd atakuwa mjinga kiasi gani atumie dini wakati anajua hana support ya kutosha akifanya hivyo! yaani sielewi kabisa kinachowakwaza. I mean tupeni sababu haswa na motive inayoweza kumsaidia huyu Idd apate ushindi lakini sio kutumia dini maana tukubali ukweli kwamba siku hizi community zetu zimegeuka, vijiwe vyetu ni ktk mabaa ya ulevi au misikitini/makanisani kwa wale wanaojiita walokole sio tena ktk migahawa/cafe kama walivyokuwa wazee wetu kujia umri wa kina sisi.
Hivyo utakuta wanaokutana bar au pub wana ushikaji na wale wanaokutana misikitini na makanisani pia wana ushikaji wao hivyo sio swala la nani kafanya nini ila sisi wenyewe tumechukua njia hizi wenyewe kujenga marafiki na maswahiba. Leo hii naweza kabisa kuku challenge unionyeshe marafiki zako basi bila shaka watakuwa wale mnaokutana Bar/Pub au kanisani/msikitini maana hatuna vijiwe nje ya hapo. Hizi Jumuiya zetu zenyewe ni Unafiki mtupu, haya uyasemayo ni pamoja na mengi niliwahi kuyaona na kuyasikia. Itazame hiyo list ya wagombea mbona wameisha sema wote ni waislaam ilihali tunaonyeshwa wagombea tofauti? hii sio kampeni yenu nyie against Idd/waislaam? Je, kuwa mwanachama wa TAMCO ni kosa?
Udini upo tena sana tu, na umetokana na maamuzi yetu wenyewe kutoshirikiana kama Watanzania bali kupitia imani zetu za dini na makabila. Msiba wa Muislaam hutawakuta wakristu makabirini wala msiba wa Mkristu hutawakuta Waislaam na kama wapo basi ni wale wanatoka sehemu moja ama mtu wa kijiwe chao. Hii ndio jamii tulochagua sisi wenyewe kutenganishwa kwa imani zetu za dini nje ya hapo sioni kabisa ushahidi hapo juu kuhusu huyu Idd na Udini zaidi ya kwamba tunapewa story ya upande mmoja hatukuonyeshwa ya Mwang'ombe.