Uchaguzi DMV USA: Udini na status quo vyatawala

environmental

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,054
137
UCHAGUZI DMV USA: UDINI NA STATUS QUO VYATAWALA


Ndugu zangu wana DMV wote salaam; sote tunajua kwamba tupo kwenye heka heka za kampeni ya uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya yetu ya DMV. Napenda nizungumzie mambo ambayo yanatia dosari na tusipokuwa makini na kuchelewa kuyafumbua basi itakuwa majuto ni mjukuu.

Swala la udini ni tishio ambapo bwana Iddi Sandaly na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakilitumia kama karata ya kushinda uchaguzi wa Jumuiya. Katika jumuiya yetu tuna makundi ya aina mbili

· a) Watu ambao wanajua kinachoendelea, na
· b) Watu ambao hawajui chochote na hawajijui kwamba hawajui na pia hawa ndo wengi sana hapa na wako "vulnerable". Watu wa namna hii ndo Iddi Sandaly na wafuasi wake wanawa "brainwash" kwa kutumia "gear" ya dini ili wampigie kura.

Kuna ndugu zetu Waislam kutoka kwenye group (a) wamemkataa Iddi Sandaly na propaganda zake za udini na wanam support Liberatus Mwang'ombe. Kipindi cha kama mwezi na nusu uliopita Iddi Sandaly alihudhuria family day (cookout) ya TAMCO na akasikika kulalamika kwa waumini wenzake wa Kiislam kwamba CHADEMA (akimaanisha Liberatus Mwang'ombe) wanampokonya kiti chake cha jumuiya.

Baada ya siku chache na katika kuendeleza udini wake bwana iddi sandaly aliongea na mchungaji wa kanisa moja hapa DMV na kumwambia kwamba bwana Liberatus Mwang'ombe hafai kuwa kiongozi wa Jumuiya kwa sababu haamini mungu, na wakati huo huo bwana Liberatus Mwang'ombe alifanya mkutano wa kampeni kwenye park na kabla ya kuanza mkutano, bwana Liberatus Mwang'ombe alimuomba mchungaji mmoja afungue mkutano kwa maombi na yule mchungaji alifanya hivyo; lakini cha kushangaza Iddi Sandaly na watu wake wakalalamika kwamba kwa nini Liberatus Mwang'ombe hakuleta na muislam asali kabla ya mkutano?


Uchaguzi wa Jumuiya yetu ulikuwa umepagwa kufanyika July 20th 2014 na bila sababu yoyote kutolewa ukabadilishwa kwenda August 9th 2014 na kabla ya hapo ulikuwa ufanyike tokea mwezi February 2014 kama katiba inavyosema kwamba uchaguzi uitishwe miezi miwili kabla ya muda wa uongozi uliopo madarakani kuisha, lakini cha kushangaza tarehe ya uchaguzi imebadirishwa na tume ya uchaguzi zaidi ya mara nne. 
Lengo kuu la ubadilishaji wa tarehe ya uchaguzi tukaambiwa ni kuupisha mwezi mtukufu wa Ramadhani uishe, lakini ukweli ni kwamba baada ya Iddi Sandaly kuona watu wengi hawamtaki ikabidi mwenyekiti wa DMV Board of Trustee na mjumbe wa tume ya uchaguzi ambao wamekuwa wakimsaidia Iddi Sandaly wazi wazi waje na mkakati na mbinu za kumsaidia Iddi Sandaly aweze kutumia huo mwanya wa kufuturu pamoja na Waislam wenzake kila weekend ili kuwaomba wampigie kura kwa sababu ni mwenzao na alishawahi kuwa mwenyekiti wa TAMCO ( Tanzania Muslim Community in Washington DC).
Lakini jambo la kujiuliza hapa; Je, kwani Waislam wakifunga kazini hawaendi? Na je kama Ramadhani ndiyo sababu kwani huu uchaguzi ni wa kidini ama wa watu wote? Na je wale wanajumuiya wasabato wanaosali jumamosi ambayo ni siku ya uchaguzi watakuwa wametendewa haki?

Majibu ya hayo maswali yote hapo juu yanajieleza; na kuna ushahidi mzito kwamba katika kipindi hiki cha mfungo Iddi Sandaly na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakipigia simu Waislam wanaom support Liberatus Mwang'ombe na kuwaambia kitendo Chao cha kutom support Iddi Sandaly ambaye ni Muislam mwenzao ni dhambi kwa mungu na kuwazuia kumchagua kafir (Liberatus mwangombe); na pia Iddi Sandaly na baadhi ya Waislam wenzake wamepanga kwamba kila muislam awapigie kura watu wafuatao:-


· Rais, Idd Sandaly – TAMCO
· Makamu, Salma Moshi - TAMCO
· Katibu, Said Mwamende- TAMCO
· Treasury, Jasmine Rubama - TAMCO


Wagombea wenye imani tofauti na Iddi Sandaly na ambao hawatakiwi kuwaongoza Waislam ni kama ifuatavyo :-

· Liberatus Mwang'ombe - Raisi wa Jumuiya
· Harriett Shangarai - Makamu wa raisi
· Solomon Cris, - Makamu wa Katibu
· Bernadeta Kaiza- Makamu wa katibu

Huyo Bernadeta Kaiza yeye aliongezwa jina lake juzi lakini hakuwepo tokea mwanzo. Mantiki ya kumuongeza Bernadeta ni baada ya madhambi yao ya udini kugundulika. Bernadeta anatumika bila kujitambua! Zaidi, fomu ya Bernadeta ya kurudisha kwenye Tume ya Uchaguzi imesainiwa na Idd Sandaly na Asha Nyang'anyi (katibu wa Tume ya Uchaguzi); hii inakiuka miiko na maadili ya Tume ya Uchaguzi. 
Katika hii kampeni ya uchaguzi wa Jumuiya yetu ya DMV kuna watu ambao wamekuwa kero na wamesahau majukumu yao katika huu mchakato wa uchaguzi na kuonyesha upendeleo wa wazi wazi kwa Iddi Sandaly kwa maslahi yao binafsi na leo nitawataja kwa majina:-

Asha Nyang'anyi (katibu wa Tume ya Uchaguzi) huyo dada amekuwa na ubaguzi wa kutisha kwa Liberatus Mwang'ombe na wakristo wanaogombea uongozi na nitatoa mfano. Katika mkutano wa kampeni za Liberatus Mwang'ombe June 28th 2014 kule Meadowbrook Park, ChevyChase, Maryland; darasa la Kiswahili ni moja ya mambo ambayo Liberatus Mwang'ombe alisema kama akichaguliwa na wana DMV ataliboresha na akalalamikia uongozi wa Iddi Sandaly kwa kushindwa kuliendeleza darasa, maana uongozi wa Iddi Sandaly haukuwa na plan "B", na kwamba madai ya Iddi Sandaly kwamba darasa la Kiswahili lilikufa baada ya kanisa lilitumika kama venue kufungwa hazikuwa na msingi kwa sababu darasa la Kiswahili lilikufa tokea February 2014 wakati kanisa lilifungwa May 2014.


Hiki ndicho alicho kisema ndg. Liberatus Mwangombe juu ya darasa la Kiswahili
<font size="4">


Kitu cha kushangaza Asha Nyang'anyi baada ya kuona video clip ya hotuba ya Liberatus Mwang'ombe (hapo juu) akaamua kumwandikia email akilalamika kwamba Liberatus anadanganya kuhusu darasa la Kiswahili. Kitu cha kusikitisha ni hivi, Asha Nyang'anyi kama mjumbe wa tume ya uchaguzi kwa nini amjibie tuhuma Iddi Sandaly wakati yeye anatakiwa kuwa neutral? Na malalamiko ya kuwa na mgongano wa maslahi yalifikishwa kwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kwamba Asha Nyang'anyi hatuna imani naye lakini hamna jibu lililotolewa mpaka leo hii.



Hapa Liberatus akijaribu ku sisitiza alicho kisema juu ya dara la Kiswahili
<font size="4">



Moja ya mashariti ya kugombea uongozi ni lazima uwe na makaratasi, kuna dada anaitwa Linah Mwabuka aliomba kugombea nafasi ya mweka hazina msaidizi, kwa shinikizo la Asha Nyang'anyi jina lake likatupwa kwa kigezo cha hana makaratasi ili hali mgombea wa makamu wa raisi Salma Moshi (Muislamu) na yeye hana makaratasi lakini kwa sababu za dini yaani TAMCO mwenzao akabakishwa. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba nani ni bora? mTanzania kama Asha Nyang'anyi na Iddi Sandaly ambao wameukana uraia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa raia wa Marekani au mTanzania ambaye hakupenda kuwa na hali hiyo ya kutokuwa na makaratasi? Kwa nini mTanzania kwa mTanzania tunabaguana? Jibu la swali hilo alikuwa nalo mgombea wa ukatibu msaidizi bwana Solomon Cris alipotamka wazi kwamba kama wana DMV watampa ridhaa ya kuongoza japo yeye ana makaratasi basi atahakikisha hicho kipengele kina ondolewa chenye sura ya ubaguzi.

Kilichomtokea bwana Solomon Cris ni hiki hapa alichoandika iddi sandaly:-&#8232;&#8232;&#8232;&#8232;&#8232;&#8232;&#8232;&#8232;&#8232;&#8232;

Kwa kuwa Iddi Sandaly na Asha Nyang'anyi wako pamoja (accomplices) kwenye kufanya hujuma kwenye uchaguzi wa jumuiya yetu basi baada ya muda kuna tangazo likatolewa kupitia blog ya vijimambo na mtu aliyeandika hajulikani (alikuja anonymous) na katiba iko wazi kwamba usipokuwa "active member" huwezi kushiriki hata kuuliza swali mpaka uwe mwanachama. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba waliju aje kwamba yule aliyeomba kujazwa kwa nafasi za kugombea zilizokuwa wazi kama alikuwa mwanachama hai wa Jumuiya? Na je kwanini huyo mtu atumie vijimambo blog badala ya website ya jumuiya ama email? Na pia ushahidi wa kumkomoa Solomon Cris upo hapo chini; pia cha kushangaza mpaka sasa hivi katika nafasi nne zilizokuwa wazi ni nafasi moja tu ambayo Solomon Cris anagombea ndo imejazwa na huyo Bernadeta Kaiza. Na kweli tangazo likatoka na kurushwa hewani kuongeza mgombea mpya.



Hiki ndicho alicho kiandika Idd Sandaly kwenye group la WhatsApp la watu wa DMV. Amri hii ilifutwa na Solomon akawekewa mpinzani huku akiwa katikati ya kampeni na muda wa kurudisha fomu ukiwa umeisha zaidi ya mwezi


Idd order to Tume.jpg



Asha Nyang'anyi akiwa kama katibu wa Tume ya Uchaguzi amekuwa na maamuzi binafsi bila kuwashirikisha wajumbe wengine mfano niliandika email ya kulalamikia kwamba mbona uchaguzi unabadilishwa tarehe kila mara bila sababu za msingi? Akanijibu kama Asha Nyang'anyi kwa email binafsi badala ya kutumia email ya Tume ya Uchaguzi.

Katika moja ya sababu za Asha Nyang'anyi kumpinga Liberatus Mwang'ombe ni deal ambazo kama Liberatus Mwang'ombe akipata Uraisi wa Jumuiya atazigawa bila upendeleo. Mfano kila wanapokuja wageni ubalozini kutoka Tanzania kuna tender huwa zinatolewa kama vile chakula n.k, kitu kinachofanyika watu wa ubalozini wanamtafuta Raisi wa Jumuiya ambaye ni Iddi Sandaly na yeye (Iddi) anamfuata Asha nyang'anyi na Asha Nyang'anyi anachukua pesa anapiga panga na kumtafuta mtu wake atakaye mlipa leftover, ndo maana huyu dada kila wageni wakitoka Tanzania huwa hakosi ubalozini na ndo maana anaogopa Liberatus Mwang'ombe akichukua uongozi atakua amekwisha.

Dj Luke wa Vijimambo blog; huyu bwana japo kuwa DMV imem support muda wote lakini cha kusikitisha ni jinsi anavyotumia blog yake kumsaidia Iddi Sandaly kwa kuachia comments chafu za kumchafua Liberatus Mwang'ombe na wafuasi wake lakini cha kushangaza ni kwamba huyu DJ Luka anatembea na "deportation letter" mfukoni na maisha ya hapa yamemshinda anaondoka anytime kurudi bongo lakini swali la kujiuliza hapa ni kwamba kwa sababu yeye kapigwa P.I ndo anataka jumuiya ya DMV iishi kwa chuki? Hizo comments za watu wa Iddi Sandaly anaziachia na za Liberatus Mwang'ombe anazitosa na juzi tu ndo kaacha mambo ya comments lakini "is too late" japo yeye anaondoka zake lakini majeraha anayoyaacha nyuma yake kamwe hayatapotea. Zaidi, Liberatus Mwangombe alikuwa ni mmoja ya watu wanao changia kwenye blog ya Vijimambo (yaani alikuwa nasaidia kutoa post Vijimambo); cha kushangaza ame mtoa Liberatus Mwangombe kwenye admin ya Vijimambo kipindi hiki cha uchaguzi bila sababu. Hii yote ni kumpa ukumbi Idd Sandaly kwaajili ya ma deal na ubalozi akishinda. By the way; Idd Sandaly ni admin Vijimambo pia ambaye ameacha blog ya Jumuia ikiwa na post ya mwisho toka November 13, 2013 lakini ana post vijimambo. Ushahidi huu hapa TANZANIA COMMUNITY IN WASHINGTON DC AREA

Dj Luke kwa nini anampinga Liberatus Mwang'ombe na kutumia blog yake kummaliza Liberatus? Huyu kamanda yuko desperate anatafuta hela ya mwisho mwisho ya kwenda bongo kuanzia maisha na Asha Nyang'anyi na Iddi Sandaly ni moja ya wajumbe wake kwenye kamati ya sherehe ya vijimambo na hata kwenye Facebook na email lazima Iddi Sandaly am Cc ama tag DJ Luka. Dj Luke yeye na Iddi Sandaly kila sherehe ya Vijimambo hutumia jumuiya yetu kama inaalika viongozi kutoka Tanzania kwa kupitia ubalozini wakati wakifika hapa hiyo inakuwa siyo sherehe ya jumuiya bali ya Vijimambo na wanatoza watu pesa mlangoni kwa hiyo jamaa anaogopa Liberatus akimshinda Iddi Sandaly mambo yake yataharibika. Mfano, Idd Sandaly alitumia power ya Jumuiya kumualika Mh. January Makamba kwenye uhuru day December 2013. Wana DMV walichajiwa $60.00 kwenda kumuona January Makamba. Sherehe hii ilitangazwa kuwa itakuwa classic; cha ajabu walitupeleka kwenye GODAUNI ambalo lina vumbi, viti vivhache, chakula cha baridi, vyoo mtu akiwa njee anamuona wa ndani, pombe zilikuwa served under miners na kulikuwa hakuna security. Ushahidi jinsi Vijimambo ikishirikiana na Idd Sandaly kuwa rip off waTanzania huu hapa VIJIMAMBO: TANZANIA UHURU NIGHT WASHINGTON, DC, MHE. JANUARY MAKAMBA KUWA MGENI RASMI . Malalamiko yalikuwa mengi, lakini sita yaandika leo; cha muhimu ni kujua kuwa January Makamba amesafiri na pesa za walipa kodi huku Iddy Sandaly na Vijimambo wakishirikiana kuwa rip off waTanzania wenyewe

Huu hapa chini ni ushahidi wa DJ Lu kumpinga Liberatus mwangombe toka siku za awali alipo tangaza nia

Lucas Libe1.jpg Lucas Libe.jpg Bila kupoteza muda, Liberatus Mwangombe alithibitisha jinsi DJ LU anavyo ongea mambo ya uongo kwa manufaa binafsi. Liberatus alitoa ushahidi wa kuwa mwanachama hai right away WhatsAPP. ushahidi huu hapa chini

Receip Libe ATC.jpg

Mwamoyo Hamza; huyu mzee ni mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya DMV na ni kazi aliyoomba mwenyewe lakini cha kusikitisha amekuwa akiendesha shughuli za hiyo nafasi kama ni mali yake binafsi, wagombea ambao si Waislam wamemwandikia email za malalamiko juu ya Asha Nyang'anyi lakini hakuna email anayoijibu na kwa sababu yeye ndo alimteua Asha Nyang'anyi basi wote pamoja na Iddi Sandaly wanahakikisha Iddi Sandaly anachukua uraisi. Kuna taarifa kutoka kwenye source zangu kwamba mzee Mwamoyo Hamza anamwita Liberatus Mwang'ombe ni kijana mhuni bila ushahidi na kama hana ushahidi basi ni ubaguzi wa dini "at its best" na si shangai hata "official picture" ya Liberatus Mwang'ombe imewekwa akiwa na ki t-shirt ili kumfanya awe wanavyotaka wao na hii siyo haki kwenye jumuiya yetu iliyoko America nchi ya dunia ya kwanza. Wito wangu kwa wana DMV amkeni na muende kujiandikisha na mkampigie kura mpinga matabaka ya aina zote na huyu si mwingine bali ni Liberatus Mwang'ombe mwisho wa kujiandikisha ni August 7th 2014. Tembelea blog ya uchaguzi ya kijana huyu mwenye msimamo na asiye yumbishwa kwa kufuata link hii http://libe4dmvpresident2014.blogspot.com/



Hili ni tangazo la kiofisi ambapo wamemuweka Liberatus na ka T-Shirt ili wathibitishe tuhuma wanazo mpa kuwa ni muhuni


Wgombea.jpg

HIli ni Tangazo la kwanza lililo tolewa na tume; hapa Liberatus amevaa suti. Baada ya kuona Liberatus anazidi kukonga nyoyo za wana DMV; Tume ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Hamza Mwamoyo wakatoa picha hapo juu Liberatus akiwa amevaa ka T-shirt ili watimize azma yao kuwa kijana huu ni muhuni

Screen Shot 2014-06-26 at 11.17.25 PM.png

Rai yangu kwa Asha Nyang'anyi na Idd Sandaly; tunaomba mtendeeni haki huyu kijana Liberatus Mwangombe na muache udini.

Asanteni sana.

- MWISHO -
 
Last edited by a moderator:
Kuna ndugu zetu Waislam kutoka kwenye group (a) wamemkataa Iddi Sandaly na propaganda zake za udini na wanam support Liberatus Mwang'ombe. Kipindi cha kama mwezi na nusu uliopita Iddi Sandaly alihudhuria family day (cookout) ya TAMCO na akasikika kulalamika kwa waumini wenzake wa Kiislam kwamba CHADEMA (akimaanisha Liberatus Mwang'ombe) wanampokonya kiti chake cha jumuiya.

Baada ya siku chache na katika kuendeleza udini wake bwana iddi sandaly aliongea na mchungaji wa kanisa moja hapa DMV na kumwambia kwamba bwana Liberatus Mwang'ombe hafai kuwa kiongozi wa Jumuiya kwa sababu haamini mungu, na wakati huo huo bwana Liberatus Mwang'ombe alifanya mkutano wa kampeni kwenye park na kabla ya kuanza mkutano, bwana Liberatus Mwang'ombe alimuomba mchungaji mmoja afungue mkutano kwa maombi na yule mchungaji alifanya hivyo; lakini cha kushangaza Iddi Sandaly na watu wake wakalalamika kwamba kwa nini Liberatus Mwang'ombe hakuleta na muislam asali kabla ya mkutano?&#8232;
Watu wengine bana yaani fikra za Udini mnazo nyie lakini cha kwanza ni kulaumu watu wengine. Sasa kama nimekuelewa huyu Iddi aliposema Chadema wanampokonya kiti chake ina maana hiyo Chadema ni dini gani? nashindwa kuunganisha...

Na kama huyu mtu ni Muislaam na kaenda kuongea na Mchungaji wa Kikristu kuhusu huyu Mwang'ombe kuwa hafai kuongoza! hapa sielewi vile vile inahusu nini tatizo yeye kwenda kumuona Mchungaji au? na hiyo list ya wagombea mbona ni mchanganyiko tu au kuna wengine wamepigwa panga kwa sababu ya dini zao!

Swala la mkutano. Je, sio utamaduni wetu tunapofungua mikutano kufanya maombi kama anavyodai huyu Idd au? maana tumlaumu mtu kwa makosa ya kweli. Udini haufai lakini kwa jinsi ulivyoeleza hapo juu inaonyesha wewe mwenyewe ndio una matatizo na huyu Idd na pengine kutokana na dini yake na sasa unajenga hofu ya udini kwa wale wasojua na hawajui!..
 
ok, kumbe watanzania hadi marekani wanagombania fursa za kutafuna pesa za Watanzania wenzao kwa gia ya jumuiya?

Waislamu asilimia 99 kwenye chaguzi udini ni moja ya silaha yao, usiombe hiyo sehenu pawe na misikiti mingi.

Hata Mrema kwenye uchaguzi mdogo wa Temeke asingemtumia mzawa Sheikh Kasim Mtopea, kwakweli asingeshinda uchaguzi ule.

Ila Kwakuwa JK Huwa anakwenda sana marekani na wanakutana na huyu mwislamu mwenzake Idd Sandaly basi yawezekana ndiye aliyemshauri hivyo maana hata yeye alitumia udini kurudi ikulu kinguvu hata lipumba alishiriki uhaini huu.
 
Watu wengine bana yaani fikra za Udini mnazo nyie lakini cha kwanza ni kulaumu watu wengine. Sasa kama nimekuelewa huyu Iddi aliposema Chadema wanampokonya kiti chake ina maana hiyo Chadema ni dini gani? nashindwa kuunganisha...

Na kama huyu mtu ni Muislaam na kaenda kuongea na Mchungaji wa Kikristu kuhusu huyu Mwang'ombe kuwa hafai kuongoza! hapa sielewi vile vile inahusu nini tatizo yeye kwenda kumuona Mchungaji au?

Swala la mkutano. Je, sio utamaduni wetu tunapofungua mikutano kufanya maombi kama anavyodai huyu Idd au? maana tumlaumu mtu kwa makosa ya kweli. Udini haufai lakini kwa jinsi ulivyoeleza hapo juu inaonyesha wewe mwenyewe ndio una matatizo na huyu Idd na pengine kutokana na dini yake na sasa unajenga hofu ya udini kwa wale wasojua na hawajui!..

Mkuu za masiku mengi na pole na Swaum, wewe ni mkongwe hapa JF utaumbuka Idd ni mtu hatari sana mimi sipo marekani ila kuna ushaidi usiyo na shaka idd kusambaza msg kwa waislam na wapo waislam wanaojitambuwa wamekatb imani yao kuhusishwa na uchaguzi.

kura zikipigwa kidini hakuna hata muislamu mmoja atakayepata ungozi DMV.
 
Hivi kuna nini kwenye jumuiya?

Mbona wanatumia nguvu nyingi sana kugombea hizo nafasi za uongozi...?

Kuna fursa za ulaji?

Kuna pesa ya uhakika na kupiga picha na Rais akiwa Washngton Dc.

Idd Sandaly amesharamba utamu0wake anashangb mnataka kumuondo, yaani ameshazoea kukaa high table na Kikwete akija DC sasa wapiga box wanataka kumuamishia back bench.

Hivi kwani Rais wa wabeba mabox NN teritory zake zinaishia Atlanta tu?
 
kwa jinsi nilivyosoma post number one nimejikuta naishiwa kabisa na moyo na matumaini ya watanzania walio kwenye DMV community kupata kiongozi wa maana....


Ningesema mengi sana, lakini kwa heshima tu ya mleta post na wagombea wenzake, naomba niwe kimya

IT IS A SHAME REALLY

MAYBE HATA HIYO JUMUIYA SIO YA LAZIMA KAMA HIKI NDICHO TUNACHOONA KUTOKA KWA WAGOMBEA
 
Mkuu za masiku mengi na pole na Swaum, wewe ni mkongwe hapa JF utaumbuka Idd ni mtu hatari sana mimi sipo marekani ila kuna ushaidi usiyo na shaka idd kusambaza msg kwa waislam na wapo waislam wanaojitambuwa wamekatb imani yao kuhusishwa na uchaguzi.

kura zikipigwa kidini hakuna hata muislamu mmoja atakayepata ungozi DMV.
Mkuu kama ni kweli uyasemayo na una hakika kura zikipigwa kidini hakuna muislaam atakaye pata uongozi! Sasa hofu yenu haswa nini maana kajitia chongo mwenyewe au sivyo? Na huyu Idd atakuwa mjinga kiasi gani atumie dini wakati anajua hana support ya kutosha akifanya hivyo! yaani sielewi kabisa kinachowakwaza. I mean tupeni sababu haswa na motive inayoweza kumsaidia huyu Idd apate ushindi lakini sio kutumia dini maana tukubali ukweli kwamba siku hizi community zetu zimegeuka, vijiwe vyetu ni ktk mabaa ya ulevi au misikitini/makanisani kwa wale wanaojiita walokole sio tena ktk migahawa/cafe kama walivyokuwa wazee wetu kujia umri wa kina sisi.

Hivyo utakuta wanaokutana bar au pub wana ushikaji na wale wanaokutana misikitini na makanisani pia wana ushikaji wao hivyo sio swala la nani kafanya nini ila sisi wenyewe tumechukua njia hizi wenyewe kujenga marafiki na maswahiba. Leo hii naweza kabisa kuku challenge unionyeshe marafiki zako basi bila shaka watakuwa wale mnaokutana Bar/Pub au kanisani/msikitini maana hatuna vijiwe nje ya hapo. Hizi Jumuiya zetu zenyewe ni Unafiki mtupu, haya uyasemayo ni pamoja na mengi niliwahi kuyaona na kuyasikia. Itazame hiyo list ya wagombea mbona wameisha sema wote ni waislaam ilihali tunaonyeshwa wagombea tofauti? hii sio kampeni yenu nyie against Idd/waislaam? Je, kuwa mwanachama wa TAMCO ni kosa?

Udini upo tena sana tu, na umetokana na maamuzi yetu wenyewe kutoshirikiana kama Watanzania bali kupitia imani zetu za dini na makabila. Msiba wa Muislaam hutawakuta wakristu makabirini wala msiba wa Mkristu hutawakuta Waislaam na kama wapo basi ni wale wanatoka sehemu moja ama mtu wa kijiwe chao. Hii ndio jamii tulochagua sisi wenyewe kutenganishwa kwa imani zetu za dini nje ya hapo sioni kabisa ushahidi hapo juu kuhusu huyu Idd na Udini zaidi ya kwamba tunapewa story ya upande mmoja hatukuonyeshwa ya Mwang'ombe.
 
Kuna pesa ya uhakika na kupiga picha na Rais akiwa Washngton Dc.

Idd Sandaly amesharamba utamu0wake anashangb mnataka kumuondo, yaani ameshazoea kukaa high table na Kikwete akija DC sasa wapiga box wanataka kumuamishia back bench.

Hivi kwani Rais wa wabeba mabox NN teritory zake zinaishia Atlanta tu?

Tentacles za prezdaa zinaanzia ATL na ku-extend mpaka Vienna, Ikungulayabashashi, Ouagadougou, Tirana, Kathmandu, mpaka pande za Nagorno-Karabakh huko.
 
Mkuu kama ni kweli uyasemayo na una hakika kura zikipigwa kidini hakuna muislaam atakaye pata uongozi! Sasa hofu yenu haswa nini maana kajitia chongo mwenyewe au sivyo? Na huyu Idd atakuwa mjinga kiasi gani atumie dini wakati anajua hana support ya kutosha akifanya hivyo! yaani sielewi kabisa kinachowakwaza. I mean tupeni sababu haswa na motive inayoweza kumsaidia huyu Idd apate ushindi lakini sio kutumia dini maana tukubali ukweli kwamba siku hizi community zetu zimegeuka, vijiwe vyetu ni ktk mabaa ya ulevi au misikitini/makanisani kwa wale wanaojiita walokole sio tena ktk migahawa/cafe kama walivyokuwa wazee wetu kujia umri wa kina sisi.

Hivyo utakuta wanaokutana bar au pub wana ushikaji na wale wanaokutana misikitini na makanisani pia wana ushikaji wao hivyo sio swala la nani kafanya nini ila sisi wenyewe tumechukua njia hizi wenyewe kujenga marafiki na maswahiba. Leo hii naweza kabisa kuku challenge unionyeshe marafiki zako basi bila shaka watakuwa wale mnaokutana Bar/Pub au kanisani/msikitini maana hatuna vijiwe nje ya hapo. Hizi Jumuiya zetu zenyewe ni Unafiki mtupu, haya uyasemayo ni pamoja na mengi niliwahi kuyaona na kuyasikia. Itazame hiyo list ya wagombea mbona wameisha sema wote ni waislaam ilihali tunaonyeshwa wagombea tofauti? hii sio kampeni yenu nyie against Idd/waislaam? Je, kuwa mwanachama wa TAMCO ni kosa?

Udini upo tena sana tu, na umetokana na maamuzi yetu wenyewe kutoshirikiana kama Watanzania bali kupitia imani zetu za dini. Msiba wa Muislaam hutawakuta wakristu makabiurini wala msiba wa Mkristu hutawakuta Waislaam na kama wapo basi ni wale wanatoka sehemu moja ama mtu wa kijiwe chao. Hii ndio jamii tulochagua sisi wenyewe kutenganishwa kwa imani zetu za dini nje ya hapo sioni kabisa ushahidi hapo juu kuhusu huyu Idd na Udini zaidi ya kwamba tunapewa story ya upande mmoja hatukuonyeshwa ya Mwang'ombe.

Umejaza maandishi mengi ya bure ni nonsense, hakuna sehemu yoyote kwenye mafundisho ya ukristo tunapofundishwa mkristo ndugu yake ni mkristo mwenzanke, jamii ya wakristo ukiwaingia kwa gia ya uchaguliwe kwa ukristo wako ujuwe imekula kwako.

mimi kwenye parish yetu tuna Vatcan sports club ambapo wanachama na viongozi ni ruksa dini zote kuna jamaa anaitwa omari tumemchaguwa kwa kishindo mara mbili mfululizo kuwa mwenyekiti wa club yetu na mkristo mwenzetu tumemtosa na club ni mali ya kanisa. na pia tuna healh center na martenity hizi ni huduma sawa kwa wote
 
Poleni sana wandugu. Watoto wa mafisadi na washika pembe wao wanawatayarisha na maisha ya bongo. DJ Luke akirudi hapa haitakuwa tabu ku connect na akina Kibonde.
 
Back
Top Bottom