Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
CUF ni chama muflis. Huu uchaguzi wa leo, si lolote, si chochote ni zuga tuu ili kutimiza matakwa ya katiba yao. Wameweka wapinzani zuga ili umma uone CUF kuna demokrasia, hakuna demokrasia yoyote ndani ya cuf ni udikteta, umujahidina na usultani wa kisiri siri.
Seif Sharif Hamad anasemekana ni mwana haram wa Sultan Jamsid. Hii ni siri kubwa ya ndani. Akishika uongozi Zanzibar, anayakana Mapinduzi Matukufu ya Januari 64. Analivunja Baraza la Mapinduzi na kuutambua rasmi uhuru wa Zanzibar wa Desemba 63. Anatoa msamaha kwa kwa ukoo wa Kisultani na kurudisha Usultani Zanzibar maana yeye mwenywe ni Sultan kisiri siri. Usultan utakaorejeshwa sio wa utawala tena bali ceremonial tuu. Nasaba ya mwisho ya Sultan wa Persia ni Mfalme wa Brunei. Ukoo wa Ottoman Empire katika kujitanua, wanamfalme walisambaa maeneo mbalimbali, wale waliokuwa watiifu kwa Mfalme Baba yao, waliposhika visiwa walijitangaza ma Sultan chini ya Falme ya Persia na ndivyo alivyofanya Seyyid Said Bin Barghash alipoitwaa pwani ya Afrika Mashariki toka Sofala mpaka Lamu, na visiwa vyote na eneo lakilomita kumi/20 la bara toka usawa wa bahari. Nduguye alitwaa visiwa vya Brunei baada ya kukuta utajiri mkubwa wa mafuta, akauvua Usultani na kujitangazia ufalme.
Ni nasaba hii ya Kisultani ndio inamfanya mfalme huyo kuwa mfadhili mkubwa wa CUF kupitia kwa Seif Sharrif Hamad. Viongozi wa CUF Zanzibar wanalielewa hili ndio maana hawathubut kumpinga Seif hata chembe.
Sio siri CUF ina viongozi wazuri, waadilifu, wenye uwezo wa uongozi na upeo wa kuona mbali ka Juma Duni na Hamad Rashid, wana CUF wanajua Seif 'kwishney' hana uwezo wowote kwa sasa zaidi ya fedha za Mfalme lakini hakuna wa kukohoa kwa sababu ni Sultan.
Seif ana siasa za jazba, chuki, hasira na dalili za kulipiza kisasi ndio maana anautaka urais wa ZnZ kwa udi na uvumba, na siku zote huwa anashinda, lakini kamwe hapewi nchi, wenye nchi wayajua hayo yalijificha moyoni mwake.
Hata uchaguzi Zanzibar ukiitishwa kesho, Seif anashinda sio kwa sababu ni mahiri, bali anapendwa na wote waliolizwa na Mapinduzi. Hata asipopiga kampeni yoyote, bado atashinda kwa sababu Wapemba hawakushiriki Mapinduzi na Washirazi na masalia ya Sultan ndio watakao mchagua.
Kama CUF wangekubali kumsimamisha Juma Duni ama Hamad Rashid urais wa Zanzibar, nawahakikishia mpaka wana CCM wataichagua CUF na wenye nchi wataikabidhi nchi.
Lipumba nae hana jipya, ni nyimbo zile zile. Huyo mgombea Mkristu ameweka hapo boya tuu ili kufuta hisia za udini huku bara na watampa vijikura vya kuzugia ili demokrasia ionekane kumbe ni kiini macho.
Prof. Safari ndio hafai, hafai kabisa, kama Lipumba asipochaguliwa na akachaguliwa Safari, basi hiyo itakuwa ni kazi ya Seif kamtosa Lipumba.
Prof. Safari alinifundisha sheria pale Mlimani, hakuna ubishi ana uwezo mkubwa kiakili, ni mwanasheria mahiri na high convincing power. Tatizo jamaa ana ulimi wa upanga, Jamaa ni Mujahidina na Muslim Fundamentalist ambaye akiishika CUF, wakipokwa ushindi, jamaa atawaconvince wale Blue Guard wajitoe muhanga.
Kama Seif ni moto na Safari ni moto, kitakachofuatia ni mlipuko tuu. Wote wana jazba, seif ana kauli za ukali, Safari ana mdomo mchafu na anachukia ukiristo akiwaita Makafir.
Mikutano ya CUF itakuwa nu upanga wa makali kuwili.
Naona nisiseme sana hebu tusubiri matokeo.
Wewe mdomo wako ni mchafu na hujui ulisemalo wana huna uhakika nalo,unaposema Seif ni mtoto wa haramu fahamu kuwa umekwenda mbali sana maana mama yako hadi hii leo hajakuhakikishia nani baba yako.si uongo ni kweli au vipi ?
Chama cha CUF kuwa ni cha kisultani,kiarabu,kifalme kidini basi kwa yote hayo hakijaishinda CCM na bado CCM ipo mbali sana maana ni mafia ,na hao masultani huwachiwa milango wazi wakawinda mpaka wakachoka na wanyama wengine kuondoka nao,hao watawala wako hakuna anaesema kwin'yoo,watawala wako wameuza rasilimali ya nchi hii kama mali yao binafsi.
Baraza la Mapinduzi litaondolewa na Serikali ya Mapinduzi itaondolewa maana dunia ya leo hakuna serikali ya Mapinduzi kuna serikali zinazochaguliwa na wananchi upo ? Hivyo hilo si la CUF ni la kila anependa demokrasia ,natumai unaelewa isemwapo serikali ya Mapinduzi !
Inaonyesha Usultani unakupa shida na pengine hujui wapi katika dunia ya leo wapo hawa au kwa lugha nyengine wanaitwa King na Queen,tawala au nchi zenye kutumia vyeo hivyo zipo nyingi tu labda jamaa watakuelimisha ,ila kwa Zanzibar hilo halipo wala halitorudi maana watu wanahitaji maendeleo si sultani au malkia ,huyu sultani aliekuwepo ,Sultani CCM ameshawatosha ,ikiwa unaelewa maana ya sulutani.
Zaidi unaonyesha mawazo duni uliyokuwa nayo ,Seif au CUF imeshasema wazi matu yeyote ataruhusiwa kushitaki hata kama tatizo lilitokea zamani sana ,uhuru huo utakuwa wazi lakini sio kwa serikali kulipiza kisasi au kumkamata mtu hizo ni siasa za CCM na utawala wake.
Kama unakumbukumbu ulizia ni msichana gani aliekamatwa kwa nguvu na hawa akina Karume na kushindiliwa Chupa kwenye sehemu za siri na baadae kupoteza maisha ,gazeti la dira liliwahi kuandika hayo ,hivyo wazee wa mtoto na ndugu wapo na mashahidi wapo siku yeyote wanaweza kupeleka mashitaka ,siku utakapopatikana utawala wenye kujali sheria na haki za Binadamu ,memngine na kama hayo hayatafanywa na CUF kama Chama bali ni mambo binafsi ambayo yatasikilizwa kwenye vyombo vya sheria vitakavyowajibika kutekeleza haki.Seif hatafuti madaraka maana alisshafika mpaka Uwaziri kiongozi anachokitafuta Seif ni kikubwa zaidi ya hayo madaraka ,kiongozi kama Seif si rahisi kupatikana ,hilo ulielewe maana ni mtu asiekuwa na muhali,hakuonei wala hakudhulumu anakupasulia wazi na kukupa uhuru wa kujitetea wala hana urafiki wa huyu ni mwenzetu au mwenzangu ,haogopi kukueleza ukweli na ameonekana kwenye viriri na majukwaa mbalimbali hana utani kwenye kuitetea haki ,mmeona alivyomripua Kikwete ambae mpaka leo hajakaa sawa ,maana anamjua vilivyo Seif Sharif ni mtu wa aina gani katika mambu ya siasa,siasa inasomwa na kufanyiwa kazi ,katika mapambano ya siasa hakuna kuzubaa au kulaza damu ,wanasema unajibu mapigo na ndio hivyo mapigo ya Raisi wenu yamejibiwa kwa vile ilivyopigwa.
Jamaa ndie huyo ameshitangazia kuwa hana mpinzani naona mmeanza kutetemeka.