Uchaguzi CUF: Prof. Lipumba ambwaga Prof. Safari

Anatafuta gear ya kurudi CCM.
Si avumilie tu...je akina mzee Julius wange aamua kukata tamaa enzi hizo CCM isingekuwepo.Walivumilia mpaka sasa watu wanakula matunda.
 
Tangu mwanzo nilisema ni uchaguzi zuga na wagombea boya. Niliamini Prof. Safari alilijua hilo. Sasa tuisubiri hiyo press conference yake ya kutangaza kujitoa CUF.

Pia nilisema Prof. Safari ana high convincing power na ana ulimi wa upanga wa makali kuwili mwenye kuweza kutema sio cheche tuu, bali moto utakao ilipua CUF.

Kwa CCM huu ni mtaji muhimu katika kukabiliana na CUF kama alivyofanya Tambwe Hiza. Tusubiri na tuone.
 
Ndio. Ana akili inayojitegemea kidogo. Huwezi kumlinganisha na Lipumba na usomi wake!

Haya mkuu ndio Tanzania yetu hii. Lipumba hana akili, Tambwe ana akili. Instersting observation. Lakini mimi naona tofauti kidogo, ni much better mtu anayepigania kuwepo opposition Tanzania ambayo inaweza kuleta manufaa kwa nchi. Kuliko mtu anayekubali kununuliwa. siasa mchezo mzuri kweli.

Prof Safari anatakiwa kuwa makini sana na anayoongea kama kweli yuko serious na siasa. Siasa zake za uislamu kama zimekataliwa CUF sioni kama ztakubaliwa na CCM, unless kama anataka kutumiwa tu kuivuruga CUF na upinzani na kutupwa. Angekuwa mjanja angetumia kushindwa kwake kujijenga kwa ajili ya baadae, angekubali kushindwa na kuwashukuru waliompa kura 6 na kuwapongeza walioshinda. Na kujiandaa kwa ajili ya miaka mitano ijayo. U profesa wake utaonekana kwenye hiyo press conference. Na sijui mwandishi gani ataenda.
 
Prof.Safari ni mamluki tu kwani kura kapata ya familia yake tu,sasa utasema kaonewa,CUF muwe makini na mamluki katika wanachama wenu,pia mkubaliane na vyama vingine vya upinzani vilivyo makini namna ya kuungana katika uchaguzi wa 2010 kinyume na hapo mtaifaidisha CCM.
 
Huyo profesore akacheze pachanga tu ,alizani jamaa hawajamsitukia ,hivi ukose uongozi halafu siku ya pili uzindue kitabu,haoni kama uwazi wa kuwa yeye ni pandikizi ulikwisha julikana zamani na sera zake za kukivuruga chama zilikwisha gundulika, CCM wamekwenda mchomo vibaya sana na ndio hivyo wanaume wa vita wameingia na slogan kali sana ya kuwambia sasa ni mapambano kwenye uwanja wa kura hakuna kuibiwa mtu ,mambo ya mafisadi kujisimika kwa kura za wizi yameisha na yamepitwa na wakati. Unajua suali moja ambalo ni hatari kumuuliza mgombea ni kama kumuulizia nani katibu wako wa tawi au mwisho wa ukurasa wa Katiba ya chama chako kumeandikwa nini na hayo jamaa ameshindwa kuyajibu ,sasa huoni kama ni pandikizi halafu mgombea wa nafasi nyeti kama hizi inakuwa vizuri ikiwa anatoka katika moja ya nafasi za juu ya chama.

Kwa kweli wito uliotolewa na Viongozi wa CUF unahitaji kupokelewa na vyama vingine vya upinzani...."Tukatae CCM kuchukua kura zetu kwa nguvu kwa kuwa wao hawana haki ya kutawala."
Kama ni ubabe basi na CUF wanauweza..hayo ni maneno murua kabisa ambayo ndiyo yanayohitajiwa kutumiwa katika kupambana na mafisadi ,asie na mwana abebe jiwe CUF-Zanzibar watawaonyesha Watanganyika namna ya kukabiliana na wezi wa kura na nakuhakikishieni kama mapambano kuanza dhidi ya serikali yataanzia hapo na hayatasimama mpaka kieleweke ,jamaa wameshaamua kuikataa CCM kinguvu na mnachotakiwa huko Tanganyika ni kufuata nyayo za waZanzibari ili kuing'oa CCM madarakani ,mafisadi wanapakushika kwa kuwa CCM ipo madarakani lakini leo hii CCM ikiangushwa kutakuwa hakuna wakili wala jaji fedha waliyokwiba wairudishe au watanyea debe ,ndivyo wanavyotaka kufanyiwa lakini hili la kubembelezana mara katoroka mara kaonekana yote kwa sababu serikali iliyopo madarakani wamekwiba pamoja. Raisi mwizi ,jaji mwizi wakili mwizi hivi nani atamfunga mwenziwe ,tusafishe njia kwa kuing'oa CCM.
 
Kama Lipumba na seif sharif ni wanasiasa wa kweli basi na wao wangeachia ngazi, yani miaka nenda rudi wao wapo tu,hawana tofauti na haya majambazi ya CCM.Wote hawataki kuachia madaraka kwa vijana. Kama wanataka mabadiliko basi waanze wao kuachia ngazi.
 
Safari Ni Mtaalam na asiekubali kuyumbishwa. Akina hamad rashid na wengine hawakumfanyia Uadilifu Prof Safari. Moja ya Sababu ya Prof. Safari kutolewa Chuo cha Diplomasia ni kuwa alikwenda kumhoji prof. Lipumba akiwa Jela. Wakuu wa nchi wakajua jamaa ni CUF, wakamtoa DIPLOMASIA.

Suala la kuandika kitabu ni fani yake, acha aweke wazi Uozo uliopo CUF may be wanaweza kubadilika, msimamo wake wa kimsingi kuwa tofauti yake na akina Seif na Lipumba ni juu ya kusisitiza kuwepo kwa katiba Huru na hilo ndio msimamo wa wadau wengi ambao wanapenda kuona nchi inabadilika. Uelewa wa wajumbe nalo ni Muhimu sana.

Moja ya tatizo la Upinzani ni kukosa wasomi wengi, na wasomi wetu wengi wamekuwa waoga na wengi wao wanaona bora kubakia CCM kulinda maslahi yao. Kuliko Ku-risk maisha yao.

Nimjuavyo hawezi ingia CCM...!!!
 
Safari Ni Mtaalam na asiekubali kuyumbishwa. Akina hamad rashid na wengine hawakumfanyia Uadilifu Prof Safari. Moja ya Sababu ya Prof. Safari kutolewa Chuo cha Diplomasia ni kuwa alikwenda kumhoji prof. Lipumba akiwa Jela. Wakuu wa nchi wakajua jamaa ni CUF, wakamtoa DIPLOMASIA.

Suala la kuandika kitabu ni fani yake, acha aweke wazi Uozo uliopo CUF may be wanaweza kubadilika, msimamo wake wa kimsingi kuwa tofauti yake na akina Seif na Lipumba ni juu ya kusisitiza kuwepo kwa katiba Huru na hilo ndio msimamo wa wadau wengi ambao wanapenda kuona nchi inabadilika. Uelewa wa wajumbe nalo ni Muhimu sana.

Moja ya tatizo la Upinzani ni kukosa wasomi wengi, na wasomi wetu wengi wamekuwa waoga na wengi wao wanaona bora kubakia CCM kulinda maslahi yao. Kuliko Ku-risk maisha yao.

Nimjuavyo hawezi ingia CCM...!!!

Profesa Safari kutunga kitabu cha uozo CUF baada ya kupata kura sita
Na Elias Msuya

Siku chache baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kufanya uchaguzi mkuu na kuwarudisha madarakani viongozi waliokuwepo awali, mmoja wa wagombea walioshindwa, Profesa Abdallah Safari amesema anatunga kitabu kueleza hatma ya uanachama wake kwa chama hicho.


Katika uchaguzi huo, Profesa Safari aligombea nafasi ya mwenyekiti na kuambulia kura sita, akiwa nyuma ya mgombea mwingine Koplo John Masanja aliyepata kura 10, huku Profesa Ibrahim Lipumba akirejea madarakani kwa kupata kura 646.


“Sikufurahishwa na uchaguzi ule kwa ujumla. Wamenidhalilisha sana kwa kuniuliza maswali ya kipuuzi na kusahau mchango wangu katika chama.


“Mimi nilijitolea kama wakili kukitetea chama mpaka nikafukuzwa kazi katika chuo cha Diplomasia. Sikujali nikaendelea kukitetea chama changu. Ilifika mahali nikampoteza baba yangu mzazi nikiwa nakihangaikia chama, Halafu leo nakuja kuulizwa maswali ya kipuuzi vile?” alihoji na kuongeza:


”Siku ile nilikuwa na familia yangu, mke na watoto wangu, nao walihuzunika kuliko hata mimi.


”Kwa hiyo sasa natunga kitabu changu ambacho kitaitwa ‘Haja ya kuwa na Tume huru ya Uchaguzi’. Humo nitaeleza kila kitu ikiwamo hatima ya uanachama wangu ndani ya CUF,” alisema Profesa Safari.


Akielezea kwanini alishindwa kujibu swali lililomtaka amtaje jina la katibu wake wa tawi wakati wa kuomba kura, Profesa Safari alisema hilo nalo lilikuwa swali la kipuuzi kwakuwa yeye anachojua katibu wa tawi lake ni Mwanamke, hiyo inatosha.


“Mimi ni mwanasheria, naelewa ninachokifanya, niliwaeleza kuwa katibu wangu ni Mwanamke hiyo inatosha. Sasa ya nini nimtaje jina? Hayo yalikuwa ni maswali ya kipuuuzi tu,” alisema na kuendelea kutamba… “Mimi nimetunga vitabu vingi vinavyotumiwa vyuo vikuu na sekondari, Muulize Lipumba ametunga kitabu gani,”


Profesa Safari alisema kwamba kulikuwa na njama za muda mrefu ndani ya CUF za kummaliza kisiasa na ndiyo maana hata kauli za viongozi zilikuwa zikiashiria hivyo.


“Viongozi walishasema kuwa hawawezi kumwachia nguruwe shamba la mihogo, hivyo ndiyo maana walifanya kila mbinu kuhakikisha kuwa sipati kura katika uchaguzi ule. Siyo kwamba sikuwa na Timu ya kampeni, nilikuwa na timu yangu na meneja wa kampeni alikuwepo lakini hujuma,” alisema.


Akieleza tofauti iliyopo kati yake na viongozi wa juu wa chama cha CUF, Profesa Safari alisema kuwa ipo haja ya kuwa na tume huru ya uchaguzi ndani ya CUF.


Akieleza hatima ya uanachama wake wa CUF na kama yuko tayari kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) endapo atajitoa CUF, Profesa Safari alisema alisema kamwe hawezi kufanya hivyo.


Alidai kuwa mwaka 1995 nilipotoka Uingereza, CCM walimtaka ajiunge nao na wakamuahidi nafasi kubwa kama vile ukatibu mkuu katika Wizara ya Katiba na Sheria, jaji lakini alikataa.


Pamoja na kuonyesha wazi kuitupia virago CUF, alisema yuko njia panda kwa sababu hajaona chama chochote chenye mwelekeo mzuri kisiasa.


Alisema kuwa Tanzania bado hakuna vyama thabiti vinavyoendesha siasa za ukweli.


”Ninatafakari mwelekeo wangu. Ni mapema mno kusema nitafanya nini baada ya hapo.....give me time (Nipe muda) nitaeleza nitakapozindua kitabu changu,” alisema.


Kwa sasa naishi kwa kutegemea vitabu vyangu. Ndiyo mimi ni wakili lakini hasa nategemea vitabu vyangu” alisema Profesa Safari.


Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Wilfred Lwakatare alikanusha madai ya Profesa Safari kudhalilishwa kwenye uchaguzi huo.


“Chama chetu kinafuata taratibu na kanuni, na kwakweli, aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi ule alizingatia hilo. Maswali yote yaliyoulizwa yalikuwa sahihi kabisa na hakukuwa na swali la kumdhalilisha mtu,” alisema Lwakatare.


Alifafanua: “Tusema kwamfano mtu anaulizwa, Unamfahamu katibu wako wa tawi nay eye akashindwa kujibu, hilo ni swali la kumdhalilisha?” alihoji Lwakatare


Alisema kuwa kama Profesa Safari anaona amedhalilishwa, ni vema angefuata taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwenye vikao halali”


Alikanusha madai kwamba kitendo cha kuwarudisha viongozi wale wale waliokuwepo ni kinyume cha demokrasia.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
Viongozi CUF wajipanga upya

2009-03-02 10:10:00
Na Muhibu Said


Wabunge wanne na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wameangushwa katika uchaguzi wa kuwapata wajumbe wa kuunda Baraza Kuu jipya la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) Taifa.

Katika uchaguzi huo, `vigogo` wanne wa chama hicho wamepoteza nafasi zao walizokuwa wakizishikilia kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Kati ya wabunge walioangushwa, yumo aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mchakato wa mkataba tata ulioipa kampuni hewa ya Richmond zabuni ya kufua umeme wa dharura, Mohamed Habib Mnyaa.

Mbali na Mnyaa, ambaye ni Mbunge wa Mkanyageni, wabunge wengine waliobwagwa katika uchaguzi huo ni Salim Hemed Khamis (Chambani), Meryce Emmanuel (Viti Maalum-Maswa) na Magdalena Sakaya (Viti Maalum-Tabora).

Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi aliyeshindwa kutetea nafasi yake katika Baraza Kuu, baada ya kuangushwa ni Abbas Juma Mhunzi, ambaye ni Waziri Kivuli wa Fedha katika Baraza hilo.

Wengine waliopoteza nafasi zao katika Baraza Kuu kwa kushindwa ni Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Muheza, Jamal Mselem, Clara Mwatuka, Juma Athumani Juma na Sudi Yusufu Mgeni.

`Vigogo` hao wa CUF, ambao ni kati ya wanachama 107 wa chama hicho waliogombea nafasi hizo, waliangushwa katika Mkutano Mkuu, uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam kati ya Februari 23-27, mwaka huu.

Matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya CUF, Jaji Usi Khamis Haji.

Aidha, Baraza Kuu limemthibitisha Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF Taifa, Joran Bashange kuwa Naibu Katibu Mkuu mpya Tanzania Bara, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Mjumbe wa Baraza hilo, Wilfred Lwakatare kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Baraza Kuu pia, limemthibitisha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Juma Duni Haji kuendelea kushikilia wadhifa huo kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom