Hawa wasomi siasa haiwafai.......
...Wasomi siasa haiwafai...ila Vilaza akina Mbowe ndo inawafaa!!!! kweli HII ndio Tanzania tuitakayo!!!!
Hawa wasomi siasa haiwafai.......
..tatizo CUF huku Tanzania Bara ni chama cha KIDINI.
Bulesi tusaidie CUF walisimamisha Mgombea gani kule Tarime...?au waliside na Chama gani...?Vp Kiteto nako walishirikiana na nani?Safari na Lipumba wote ni wasomi wazuri ila sasa Lipumba sidhani kama ana jipya linaloweza kukisaidia chama chake; nilitegemea wakati wa uchaguzi wa Tarime angeonesha leadership qualities kwa kushauri chama chake kutosimamisha mgombea na kuunga mkona Chadema hakufanya hivyo!! Safari on the other hand anaweza kufanikiwa kupata wafuasi wengi wa dini ya kiislam kwasababu ya itikadi yake; he is a hardliner oppositionist kwahiyo anaweza kukaa na Chadema wakaweka mikakati imara!!
Siku kama 2 zilizopita nilimsikia Profesa huyu akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC.Katika mahojiano hayo Profesa SAFARI alitangaza nia yake ya kutaka kugombea Uenyekiti wa Taifa Chama cha Wananchi(CUF)..Katika maelezo yake alisema kwamba lengo hasa la kugombe ni kutaka kurudisha uhai wa CUF ambacho(kwa mujibu wa maelezo yake) ni kama kimepoteza umaarufu na kwamba kinahitaji mabadiliko ya uongozi ngazi ya Taifa kwani uongozi wa sasa umekaa muda mrefu na haujaleta mabadiliko yoyote(alizungumzia suala la CUF kutokuwa na mbunge hata mmoja wa kuchaguliwa kutoka Tanzania bara),pia alizungumzia suala la mikutano ya CUF kutokuwa na mahudhurio ya kuridhisha kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo alisema kwamba sasa hivi mpaka wanachama waambiwe kuwa kutakuwa na Pilau ndio mahudhurio kidogo yanakuwa ya kuridhisha...Binafsi namfahamu Profesa SAFARI kama Mwanasheria maarufu na mtaalamu mahiri wa Lugha yetu adhimu ya Kiswahili...Swali,,Je kwa wanaomfahamu Profesa huyu,ana uzoefu gani katika mambo ya kisiasa???,anaweza kuvaa viatu vya Profesa Lipumba???,hivi uchaguzi mkuu wa CUF unafanyika lini???....Mkuu Mzee Mwanakijiji ninaomba kama inawezekana ufanye mahojiano na Profesa huyu na kuyaweka hapa maana kwa jinsi nilivyomsikia ana uchungu sana na jinsi CUF ilivyopoteza umaarufu(kwa mtizamo wake)..Naomba kuwasilisha wakuu...Mbarikiwe sana
Hivi kilichomtimua kazi kule Chuo cha Diplomasia ni nini? Si kwa sababu alipeleka gari lenye namba za kidiplomasia kwenye mkutano wa wa CUF?
Mkuu Balantanda niwie radhi kwa kuongeza maswali badala ya majibu
Mtarajiwa,
Yaani Lipumba ashindwe CUF, ajiunge na CHADEMA ndipo upinzani unoge? Akishindwa huko CUF, CHADEMA ndiko ataweza? Kama matarajio yetu ni kunogesha upinzani kwa njia hiyo tumepotea. Nadhani CUF kuna tatizo la kimfumo ambapo mwenyekiti anakuwa na cheo kama ceremonial wakati the real power ni katibu mkuu. If this is not changed watamaliza maprofesa wote with minimal gains hasa bara.
CUF njia panda uchaguzi Tarime
2008-09-26 09:14:05
Na Muhibu Said
Hatua ya vyama vya Chadema na NCCR-Mageuzi kusimamisha wagombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime, mkoani Mara, imekiweka Chama cha Wananchi (CUF) njiapanda, baada ya makao makuu ya chama hicho hadi sasa kushindwa kuamua mgombea wa chama kipi kati ya vyama hivyo `wampigie debe`.
Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na TLP, ni vyama vilivyoamua kuunda ushirikiano wa kisiasa katika kambi ya upinzani na miongoni mwa makubaliano waliyofikia katika ushirikiano huo, ni pamoja na kushirikiana katika chaguzi kwa lengo la kukishinda katika uchaguzi na kuking`oa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Wilfred Lwakatare aliliambia Nipashe ofisini kwake jijini Dar es Salaam juzi kuwa, hadi sasa makao makuu ya chama hicho, hawajafikia uamuzi wa mgombea wa chama kipi wamuunge mkono katika uchaguzi kwa madai kwamba suala hilo linahitaji busara kabla ya kuamua.
``Sisi baada ya kuona uwezo wetu ni mdogo wa kushinda jimboni humo, tuliamua kumwondoa mgombea wetu. Wenzetu NCCR na Chadema wamesimamisha wagombea. Mgombea wa chama kipi kati ya hivyo tuelekeze nguvu zetu, suala hilo linahitaji busara ya hali juu kuamua,`` alisema Lwakatare.
Hata hivyo, alisema watafikia uamuzi wa mgombea wa chama kipi wampigie debe, mara tu watakapopata taarifa kutoka kwa uongozi wa CUF Tarime kutokana na upepo wa kisiasa katika kinyang`anyiro cha uchaguzi huo utakavyokuwa ukienda.
``Tutakapopata taarifa kutoka uongozi wa CUF Wilaya ya Tarime, ndipo tutaamua namna ya kushiriki uchaguzi huo,`` alisema Lwakatare.
Hata hivyo, Lwakatare alisema kwa sasa wamempeleka Tarime, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya CUF, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la chama hicho, Mustapha Wandwi, kushiriki uchaguzi wa marudio wa udiwani.
Uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Tarime , ambao unafuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wake, Chacha Wangwe aliyefariki dunia kwa ajali ya gari katika eneo la Pandambili, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, Julai 28, unatarajia kufanyika Oktoba 12, mwaka huu.
Katika uchaguzi huo, Chadema imemsimamisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Charles Mwera wakati NCCR-Mageuzi, imemsimamisha Enock Haruni, maarufu kama `Machomanne`, ambao watapambana na mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemsimamisha Christopher Ryoba Kangoye kuwania kiti hicho.
SOURCE: NIPASHE
Tarime ni soo!
2008-09-26 16:35:51
Na Mwandishi Wetu, Tarime
Wakati siku za kuelekea uchaguzi mdogo wa kumsaka mbunge wa Jimbo la Tarime zikizidi kukaribia, hali ya kisiasa mjini hapa imeanza kuwa tete baada ya wafuasi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kuendelea kufanyiana visa mfululizo, vikiwemo vile vya kumwagiana pilipili na kuwatwangana mawe mikutanoni.
Uchaguzi huo mdogo, unatarajiwa kufanyika Oktoba 12, ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Marehemu Chacha Wangwe, aliyefariki mjini Dodoma Julai 28 mwaka huu baada ya kupata ajali ya gari.
Jana, muendelezo wa visa vya baadhi ya wafuasi wa vyama hivyo vya CCM, CHADEMA, NCCR-Mageuzi na DP ulifikia pabaya baada ya Mwenyekiti wa UDP, mchungaji Christopher Mtikila kupigwa jiwe la kichwa wakati akiwa kwenye mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya Sabasaba.
Mtikila alijeruhiwa vibaya na kukukimbiziwa hospitali mjini hapa ambako inadaiwa alishonwa nyuzi saba.
Kutokana na vibweka vinavyoendelea katika kampeni za kuelekea siku ya uchaguzi huo, , viongozi mbalimbali wa vyama vilivyosimamisha wagombea wamekuwa wakitoa kauli tofauti kuhusiana na yanayojiri.
Dk. Sengondo Mvungi (NCCR-Mageuzi)
Yeye aliripotiwa kuwa kiongozi wa kwanza kufanyiwa vurugu wakati wa kampeni jimboni humo.
Mvungi alikumbana na kadhia ya kutimuliwa kwa mawe wakati akimnadi mgombea wa chama chake cha NCCR.
Baada ya hapo, Dk. Mvungi ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alilaani tukio hilo na kueleza kuwa ni la hatari, kwani hakuna chama chenye hakimiliki ya jimbo hilo.
Pius Msekwa (CCM)
Makamu huyu Mwenyekiti wa CCM, naye alionja ya joto ya jiwe ya kufanyiwa vituko vya kampeni hizo wakati alipokuwa akimnadi mgombea wa chama chake, Bw. Ryoba Kangoba.
Msekwa alifanyiwa fujo na kuzomewa na watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa vyama pinzani.
Aidha, wafuasi wawili wa chama chake wameripotiwa kuumizwa baada ya mmoja kupigwa jiwe na mwingine kumwagiwa pilipili.
Kutokana na hali hiyo, bosi huyo namba mbili wa CCM akailalamikia hali hiyo na kuripotiwa akitishia kulifikisha suala hilo kwa Rais Jakaya Kikwete ili hatimaye zifanyike taratibu za kudhibiti hali ya namna hiyo ambayo ni ya hatari.
Christopher Mtikila (DP)
Baada ya kasheshe la jana la kupigwa mawe kwenye uwanja wa Sabasaba, amekaririwa akilalamikia hali hiyo aliyodai kuwa imetokana na njama za wapinzani wake.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mtikila amekaririwa leo asubuhi akisema: ``Nilitoa taarifa mapema kwa Msimamizi wa Uchaguzi na OCD.. niliwaeleza juu ya agizo la mimi kupigwa mawe...``
Freeman Mbowe (CHADEMA):Mbowe na chama chake cha CHADEMA wamekuwa nao wakilalama kuonewa na askari polisi walio katika operesheni kali ya kulinda amani katika jimbo hili.
Aidha, kwa nyakati tofauti, yeye, Katibu Mkuu wake Dk. Wilbroad Slaa na Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho, Halima Mdee, wamekuwa wakitoa madai ya kuonewa kwa kunyimwa viwanja vya kufanyia kampeni za mgombea ubunge wa chama chao, Bw. Charles Mwera.
Prof. Ibrahim Lipumba (CUF)
Baada ya kutosimamisha mgombea jimboni humo ili kuwapa fursa wenzao wa upinzani jimboni humo, Prof. Lipumba na chama chake wamekuwa katika wakati mgumu wa kuamua wamuunge mkono mgombea yupi baada ya wenzao kuwasaliti kwa kusimamisha mgombea zaidi ya mmoja, kinyume cha makubaliano.
Mkanganyiko huo unadaiwa kutokea baada ya vyama vinavyoungana nacho katika umoja wao wa vyama vikiwemo vya CHADEMA, TLP na NCCR-Mageuzi kushindwa kumsimamaisha mgombea mmoja, hasa baada ya NCCR na CHADEMA kusimamisha wagombea wawili tofauti.
Hata hivyo, ingawa CUF Tarime wameamua kumuunga mkono Bw. Charles Mwera wa CHADEMA, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Wilfred Lwakatare, amekaririwa asubuhi ya leo akisema kuwa wamemtuma jimboni humo kiongozi wao Mustafa Wandwi ili kuangalia ni mgombea yupi anayeelekea kukubalika zaidi ili hatimaye wamuunge mkono.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi jimboni humo limesema liko makini katika kudhibiti vitendo vyote vinavyoashiria kuvunja amani.
Akizungumza na Alasiri juzi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Liberatus Barlow, amesema FFU na polisi wengine kibao waliomwagwa jimboni humo wamejipanga vilivyo katika kuhakikisha kuwa uvunjifu wa amani unadhibitiwa ipasavyo.
Wakati huohuo, katika kuthibitisha kuwa Polisi wako makini, tayari wameshawanasa watu wanne wanaotuhumiwa kumvurumishia mawe Mchungahji Mtikila jana na kuwawezesha kuburuzwa kortini.
Walionaswa na polisi katika tukio hilo la jana na ambao leo wamepandishwa kizimbani ili kujibu mashtaka.
Kamanda Barlow amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mussa Peter, Mwita Chacha, Hafidh Stanslaus na Mwita Kilongo.
Amesema watuhumumiwa hao, mmoja alikamatwa wakati wa tukio la kupigwa kwa Bw. Mtikila na wengine watatu walikamatwa jana katika msako wa Polisi uliofuatia kujiri kwa tukio hilo la kupigwa kwa Mtikila.
SOURCE: ALASIRI
`Ndoa` ya Chadema, TLP, CUF yavunjika
2008-09-13 09:40:54
Na Simon Mhina
Ushirikiano wa kisiasa kati ya vyama vinne vya upinzani, umesambaratika baada ya vyama vitatu kati ya hivyo kuamua kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi mdogo wa Tarime.
Wenyeviti wa vyama hivyo, Augustine Mrema (TLP) Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR- Mageuzi) juzi walifanya kikao cha kujadili uchaguzi huo, na kumtenga mwenzao wa Chadema, Freeman Mbowe.
Japokuwa Profesa Lipumba alisema kwamba taarifa za kumwalika Mbowe zilitumwa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilibrod Slaa, alisema hakuna mwaliko wowote uliotumwa kwa bosi wake na Chama chake hakina mawasiliano yoyote na viongozi wa vyama hivyo vitatu.
Hata hivyo, Profesa Lipumba hakuweza kueleza kwamba walitumia njia gani kumpelekea Mbowe taarifa.
``Unajua hapa katikati kumetokea sintofahamu zilizosababishwa na kifo cha Wangwe (Mbunge wa zamani wa Tarime, Chacha), kuna kamgogoro baridi kanafukuta ndio maana hawakuhudhuria,`` alisema.
Alisema vyama vitatu vimeamua kuweka mgombea mmoja ili kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa Tarime.
Lipumba alisema baada ya kikao cha viongozi wakuu, wamepeleka madaraka yao kwa viongozi wa vyama vyao Jimbo la Tarime.
``Vikao vya wenyeviti wa taifa havitoshi, tunataka wenzetu wa Tarime nao wakutane, wao wanajuana na wanaelewa mazingira yao zaidi. Tunataka nao watuletee mapendekezo yao,`` alisema.
Hata hivyo, kiongozi huyo alisema kwamba ushirikiano wa vyama hivyo, hauondoi haki ya kila chama kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sera na katiba yake.
Awali akitoa taarifa za kikao hicho, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa NCCR, Faustine Sungura, alisema kwa kauli moja, viongozi hao wamependekeza mgombea wa Chama hicho apitishwe.
Alimtaja mgombea aliyependekezwa kuwa Enock Haruna Marwa maarufu kwa jina la Macho Manne.
Sungura alisema kikao hicho kilichofanyika siku nzima, viongozi wa Chadema waliingia mitini.
Alisema haelewi ni kwanini viongozi wa Chadema waliingia mitini bila kutoa taarifa yoyote.
Awali akizungumzia sakata hilo, Dk. Slaa alisema pamoja na kutengwa na wenzao, wataendelea na maandalizi yao ya kuingia vitani.
``Tutaingia vitani kivyetu vyetu, hatuwezi kurudi nyuma. Lazima jimbo la Tarime tutalirudisha mikononi mwetu,`` alisema.
Alisema kutokana Chadema kutengwa ghafla na wapinzani wenzake, kitachukua hatua kadhaa kuhakikisha Jimbo hilo haliendi CCM kama ilivyokusudiwa.
Alisema Tarime kuna rasilimali nyingi ambazo zinaporwa, hivyo waporaji wanaweza kuhakikisha wanasaidia mkakati wowote wenye lengo la kuifanya Tarime iwe ya CCM.
Mbunge huyo alisema Chadema kina mtaji mkubwa wa kisiasa Tarime, hivyo hakitishwi wala kubabaishwa na uamuzi wa kutengwa.
Vyama vya Chadema, TLP na CUF vilianza ushirikiano rasmi bungeni na kuunda kambi rasmi ya upinzani ambayo inatambulika rasmi bungeni.
Tangu kifo cha Wangwe kilichotokea kwa ajali ya gari Julai 28, 2008 iliyotokea kijiji cha Pandambili, Kongwa mkoani Dodoma akiwa safarini kwenda Dar es Salaam, kumekuwa na mvutano wa wazi baina ya viongozi wa kambi hiyo.
Tukio la kipekee lililotokea ni pale mazishi ya Wangwe yalipoahirishwa Julai 31, 2008 kutokana na familia kutaka uchunguzi wa kujitegemea juu ya chanzo cha kifo cha mbunge huyo, hali iliyowagawa viongozi hao kwenye makundi mawili.
Chadema wamekuwa wakilaumu wenzao kwamba walitaka kutumia msiba huo kupata faida ya kisiasa Tarime na kukiangamiza chama hao. Lawama ambazo pia zimeelekezwa kwa CCM.
SOURCE: NIPASHE
hakuna demokrasia yoyote ndani ya cuf ni udikteta, umujahidina na usultani wa kisiri siri.
Seif Sharif Hamad anasemekana ni mwana haram wa Sultan Jamsid. Hii ni siri kubwa ya ndani. Akishika uongozi Zanzibar, anayakana Mapinduzi Matukufu ya Januari 64. Analivunja Baraza la Mapinduzi na kuutambua rasmi uhuru wa Zanzibar wa Desemba 63. Anatoa msamaha kwa kwa ukoo wa Kisultani na kurudisha Usultani Zanzibar maana yeye mwenywe ni Sultan kisiri siri.
Sio siri CUF ina viongozi wazuri, waadilifu, wenye uwezo wa uongozi na upeo wa kuona mbali ka Juma Duni na Hamad Rashid, wana CUF wanajua Seif 'kwishney' hana uwezo wowote kwa sasa zaidi ya fedha za Mfalme lakini hakuna wa kukohoa kwa sababu ni Sultan.
Seif ana siasa za jazba, chuki, hasira na dalili za kulipiza kisasi ndio maana anautaka urais wa ZnZ kwa udi na uvumba, na siku zote huwa anashinda, lakini kamwe hapewi nchi, wenye nchi wayajua hayo yalijificha moyoni mwake.
Lipumba nae hana jipya, ni nyimbo zile zile. Huyo mgombea Mkristu ameweka hapo boya tuu ili kufuta hisia za udini huku bara na watampa vijikura vya kuzugia ili demokrasia ionekane kumbe ni kiini macho.
Prof. Safari ndio hafai, hafai kabisa, kama Lipumba asipochaguliwa na akachaguliwa Safari, basi hiyo itakuwa ni kazi ya Seif kamtosa Lipumba.
Prof. Safari alinifundisha sheria pale Mlimani, hakuna ubishi ana uwezo mkubwa kiakili, ni mwanasheria mahiri na high convincing power. Tatizo jamaa ana ulimi wa upanga, Jamaa ni Mujahidina na Muslim Fundamentalist ambaye akiishika CUF, wakipokwa ushindi, jamaa atawaconvince wale Blue Guard wajitoe muhanga.
Nimekusoma Mwalimu,kimsingi hata mimi simjfahamu sana Profesa Safari(zaidi ya kufahamu kwamba ni mwanasheria na pia mchangiaji wa vipindi vya redio na luninga vinavyohusiana na Lugha yetu adhimu ya Kiswahili),ndo maana nikawaomba wanajamii humu ndani kama wanamfahamu watujuze Profesa huyu ni mtu wa aina gani hasa...Ubarikiwe sana Mwalimu Zawadi
CUF ni chama muflis. Huu uchaguzi wa leo, si lolote, si chochote ni zuga tuu ili kutimiza matakwa ya katiba yao. Wameweka wapinzani zuga ili umma uone CUF kuna demokrasia, hakuna demokrasia yoyote ndani ya cuf ni udikteta, umujahidina na usultani wa kisiri siri.
Seif Sharif Hamad anasemekana ni mwana haram wa Sultan Jamsid. Hii ni siri kubwa ya ndani. Akishika uongozi Zanzibar, anayakana Mapinduzi Matukufu ya Januari 64. Analivunja Baraza la Mapinduzi na kuutambua rasmi uhuru wa Zanzibar wa Desemba 63. Anatoa msamaha kwa kwa ukoo wa Kisultani na kurudisha Usultani Zanzibar maana yeye mwenywe ni Sultan kisiri siri. Usultan utakaorejeshwa sio wa utawala tena bali ceremonial tuu. Nasaba ya mwisho ya Sultan wa Persia ni Mfalme wa Brunei. Ukoo wa Ottoman Empire katika kujitanua, wanamfalme walisambaa maeneo mbalimbali, wale waliokuwa watiifu kwa Mfalme Baba yao, waliposhika visiwa walijitangaza ma Sultan chini ya Falme ya Persia na ndivyo alivyofanya Seyyid Said Bin Barghash alipoitwaa pwani ya Afrika Mashariki toka Sofala mpaka Lamu, na visiwa vyote na eneo lakilomita kumi/20 la bara toka usawa wa bahari. Nduguye alitwaa visiwa vya Brunei baada ya kukuta utajiri mkubwa wa mafuta, akauvua Usultani na kujitangazia ufalme.
Ni nasaba hii ya Kisultani ndio inamfanya mfalme huyo kuwa mfadhili mkubwa wa CUF kupitia kwa Seif Sharrif Hamad. Viongozi wa CUF Zanzibar wanalielewa hili ndio maana hawathubut kumpinga Seif hata chembe.
Sio siri CUF ina viongozi wazuri, waadilifu, wenye uwezo wa uongozi na upeo wa kuona mbali ka Juma Duni na Hamad Rashid, wana CUF wanajua Seif 'kwishney' hana uwezo wowote kwa sasa zaidi ya fedha za Mfalme lakini hakuna wa kukohoa kwa sababu ni Sultan.
Seif ana siasa za jazba, chuki, hasira na dalili za kulipiza kisasi ndio maana anautaka urais wa ZnZ kwa udi na uvumba, na siku zote huwa anashinda, lakini kamwe hapewi nchi, wenye nchi wayajua hayo yalijificha moyoni mwake.
Hata uchaguzi Zanzibar ukiitishwa kesho, Seif anashinda sio kwa sababu ni mahiri, bali anapendwa na wote waliolizwa na Mapinduzi. Hata asipopiga kampeni yoyote, bado atashinda kwa sababu Wapemba hawakushiriki Mapinduzi na Washirazi na masalia ya Sultan ndio watakao mchagua.
Kama CUF wangekubali kumsimamisha Juma Duni ama Hamad Rashid urais wa Zanzibar, nawahakikishia mpaka wana CCM wataichagua CUF na wenye nchi wataikabidhi nchi.
Lipumba nae hana jipya, ni nyimbo zile zile. Huyo mgombea Mkristu ameweka hapo boya tuu ili kufuta hisia za udini huku bara na watampa vijikura vya kuzugia ili demokrasia ionekane kumbe ni kiini macho.
Prof. Safari ndio hafai, hafai kabisa, kama Lipumba asipochaguliwa na akachaguliwa Safari, basi hiyo itakuwa ni kazi ya Seif kamtosa Lipumba.
Prof. Safari alinifundisha sheria pale Mlimani, hakuna ubishi ana uwezo mkubwa kiakili, ni mwanasheria mahiri na high convincing power. Tatizo jamaa ana ulimi wa upanga, Jamaa ni Mujahidina na Muslim Fundamentalist ambaye akiishika CUF, wakipokwa ushindi, jamaa atawaconvince wale Blue Guard wajitoe muhanga.
Kama Seif ni moto na Safari ni moto, kitakachofuatia ni mlipuko tuu. Wote wana jazba, seif ana kauli za ukali, Safari ana mdomo mchafu na anachukia ukiristo akiwaita Makafir.
Mikutano ya CUF itakuwa nu upanga wa makali kuwili.
Naona nisiseme sana hebu tusubiri matokeo.
Lipumba
Siku kama 2 zilizopita nilimsikia Profesa huyu akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC.Katika mahojiano hayo Profesa SAFARI alitangaza nia yake ya kutaka kugombea Uenyekiti wa Taifa Chama cha Wananchi(CUF)..Katika maelezo yake alisema kwamba lengo hasa la kugombe ni kutaka kurudisha uhai wa CUF ambacho(kwa mujibu wa maelezo yake) ni kama kimepoteza umaarufu na kwamba kinahitaji mabadiliko ya uongozi ngazi ya Taifa kwani uongozi wa sasa umekaa muda mrefu na haujaleta mabadiliko yoyote(alizungumzia suala la CUF kutokuwa na mbunge hata mmoja wa kuchaguliwa kutoka Tanzania bara),pia alizungumzia suala la mikutano ya CUF kutokuwa na mahudhurio ya kuridhisha kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo alisema kwamba sasa hivi mpaka wanachama waambiwe kuwa kutakuwa na Pilau ndio mahudhurio kidogo yanakuwa ya kuridhisha...Binafsi namfahamu Profesa SAFARI kama Mwanasheria maarufu na mtaalamu mahiri wa Lugha yetu adhimu ya Kiswahili...Swali,,Je kwa wanaomfahamu Profesa huyu,ana uzoefu gani katika mambo ya kisiasa???,anaweza kuvaa viatu vya Profesa Lipumba???,hivi uchaguzi mkuu wa CUF unafanyika lini???....Mkuu Mzee Mwanakijiji ninaomba kama inawezekana ufanye mahojiano na Profesa huyu na kuyaweka hapa maana kwa jinsi nilivyomsikia ana uchungu sana na jinsi CUF ilivyopoteza umaarufu(kwa mtizamo wake)..Naomba kuwasilisha wakuu...Mbarikiwe sana
Chuki tupu. Lengo la chama chochote ni kutekeleza matakwa ya katiba yao kama ilivyoelekezwa na msajili wa vyama. Ni lazima katiba ifuatwe sasa wewe Pasco sijui unataka nini. Mi naona poa tu kama wanatekeleza katika na hiyo ndiyo democrasy. Mengine huko chini sikusoma maana nimeona waste of time baada ya kuona mwanzo statement yako. Unajua kila siku introduction ni muhimu sana kuvutia interest za wasomaji.
CUF huku bara ni very artificial, support base yake hasa ni ya waswahili, iliterates na baadhi ya vijana wenye jazba kutokana na kutambua kuwa uduni wao unatokana na sera mbaya za chama tawala. Bahati mbaya wameweza kupenetrate kwenye sehemu ndogo sana bara, lakini ZNZ ni hadithi nyingine. CUF ZNZ iko very organised, inaweza kuchukua na kutawala dola effectiveky hata in half hour notice. Kitu ambacho huku bara bado hakipo.
Profesa Lipumba nni mtu mwenye personality inayostahili kwa chama kikubwa kama CUF. Lakini sio profesa Safari, Profesa Safari anatakiwa aanzishe chama cha shari na atangaze itikadi zake zote for sure atapata wafuasi, lakini kama CUF wakitaka wabomoe mafanikio kidogo waliyoyapata bara basi wamchague Safari kuwa mwenyekiti.