Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 876
- 4,101
Zaman tuliaminishwa kwamba Prof ni mtu msomi na mwenye uwezo mkubwa wa kutambua mema na mabaya.
Leo hii profesa akiwa ndani ya taasisi ya dini ambapo tunaamini analelewa kiroho anapotuhumiwa kuwabagua binadamu na kuelekezwa wasipewe huduma hata ya chakula ni fedhea sana kwa kanisa na wasomi.
Unajiuliza profesa anawezaje akajihusisha na masuala ya kuuza chakula na vinywaji? Cafeteria inawezaje KUWA Sehemu ya profesa kusimamia utoaji huduma?
Mambo mengine jaribuni kuyatafakari na kuona namna ambavyo mtayavumilia hata kama msipoyapenda. Nchi si mali ya watu fulani wala familia fulani kama ambavyo sasa familia chache zenye fedha zimeamua kutuamulia namna ya kuishi .
Mtu wa aina hii taasisi za kidini zinamkumbatia wa kazi gani?