Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Chonde Zitto kama unaanza matusi basi ujue wengine nao wanaweza kukutusi kama unavyowatusi hawa wazee...regardless of their flaws huwezi kupanda jukwaani kumtukana mzee kama yule bila sababu ya msingi

JARIBU UONE::::::::
 
Kampeni inapopamba moto!

Zitto matatani Busanda

Imeandikwa na David Azaria, Geita; Tarehe: 11th May 2009

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma ameziingiza kampeni za Uchaguzi Mdogo zinazoendelea katika Jimbo la Busanda wilayani Geita mkoani Mwanza, dosari, baada ya kuongoza kuteketeza kwa moto bendera ya CCM iliyokuwa imezingwa katika jeneza. Zitto ndiye aliyewasha kiberiti. Tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni katika Mji mdogo wa Katoro yalipo makao makuu ya jimbo hilo.

Viongozi kadhaa wa chama hicho pamoja na wafuasi wao walimpokea Zitto aliyewasili juzi wilayani Geita kwa ajili ya kampeni hizo, na kisha kuanza maandamano kwenda katika eneo la mkutano lililoandaliwa na chama hicho huku wakiwa wamebeba jeneza hilo lililofunikwa kwa bendera ya CCM.

Baada ya kufika katika eneo hilo, viongozi hao waliliweka jeneza hilo chini na kisha kuliteketeza kwa moto, kazi iliyoongozwa na Zitto aliyewasha kiberiti, huku wafuasi wa Chadema wakishangilia kwa vigelegele na miluzi, hali ambayo nusura isababishe vurugu baada ya wafuasi wa CCM kuingilia kati.

Baadhi ya wana-CCM waliokuwapo katika eneo hilo, walilaani kitendo hicho na kueleza kwamba ni jambo ambalo kama lisipodhibitiwa, linaweza kusababisha umwagaji wa damu katika kampeni hizo kwa vile wafuasi wa CCM hawataendelea kuvumilia wakiona hali hiyo waliyoiita ni kashfa kwa chama chao.

Akizungumzia hali hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Geita, Dani Mollel alikiri kupata taarifa za kuwapo kwa tukio hilo kutoka kwa Mkuu wa Polisi kwa mdomo, na kueleza kuwa ni vyema suala hilo likapelekwa katika ofisi yake kwa maandishi ili iwe rahisi kuchukua hatua.

Source: HabariLeo
 
The sideshows are going to distract the much eeded dialogue, and if CHADEMA is not focused, it runs the risk of confusing voters.
 
Huyu Mzee wenzake wanamwita TINGATINGA sasa vijana kama wanamwona kama 'ki-bajaji' tahadharini, kumbuka ule msemo wa kumwona simba kanyeshewa mvua ukafikiria nyani.
 
Hakuna matatizo yeyote hapo,hizo ni siasa za CCM ambazo CUF wameshazizoea kule Zenji.

Kwa maana Wafuasi wa Sultani CCM huwa na kazi ya kuvunja milingoti na kuziporomosha bendera za CUF ,lakini naona huko sasa mkuki umewageukia ,hongera Zitto na hata kadi wakirudisha zichome moto hapo hapo uwanjani ,na vile vile wafuasi wa Chadema wawe tayari kwa lolote dhidi ya hawa vikaragosi wa Sultani CCM wanaodai wanaona uchungu na kama damu itamwagika tutahesabu ni matokeo ya mapambano katika kumuondosha Sultani CCM na vinyago vyake ,hakuna kurudi nyuma mambo ni mbele kwa mbele mpaka CCM wafahamu kwanini maji mto yanaelekea baharini na hata yakiingia kwenye ziwa bado yatatafuta njia ya kuelekea baharini.
 
si hivyo tuuu mbona mama yake ZITTO ambaye ni mlemavu aliiiba pesa za walemavu na kukimbilia Mwanza hakuna anayemtukana au basi tuu anataka umaarufu kupitia mgongo wa mzee malecela?

au pesa za MENGI zinamlewesha?

Kuna ulazima gani wa kumuingiza MAZA hapa mkuu? Not cool, at all.
 
Na karibu kuna mbunge mwengine wa CCM atafariki ,tegeni sikio tu

Na hili inatokana na kuendelea kukataliwa CCM mbele ya macho ya wananchi ni vifo na vilio kwa wafuasi wa Sultani CCM.
 
Nilishuhudia uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, nikiwa Moshi, Dar, Morogoro na Arusha. Makundi niliyoona yakiwa kwenye mikutano ya Augustino Lyatonga Mrema yalikuwa yanafanya kila mtu aamini kwamba Mrema angeongoza angalau kwenye hiyo mikoa.

Kilichotoka kwenye majumuisho ya kura huko kulikoitwa ndio ngome ya NCCR-Mageuzi kwa wakati huo ndio CCM na NCCR-Mageuzi waligawana kura. Lakini CCM iliendelea kuwa ndiyo yenye kura nyingi.

Sasa mimi picha huwa kawaida zinaniambia tu kwamba huenda Busanda kuna ushindani lakini haziniiambii kwamba ushindi utakuwa kwa CHADEMA moja kwa moja... mijitu ya CCM haipigi makelele bwana lakini wanajua kupiga kura...

Mnapiga mkutano wenu, makofi mengi etc. kesho yake balozi wa nyumba kumi kumi arudi anasawazisha mambo. kwa kuwa vyama vya upinzani havina viongozi huko kwenye kaya.

Yetu macho, najua kuna watu watasema mbona Tarime iliwezekana... lakini Tarime iliwezekana kwa sababu Tarime ilikuwa ngome ya CHADEMA hata kabla ya kifo cha Mh. Chache Wangwe.

Nawatakia ushabiki mwema.
 
Jamani mbona hao madiwani unasema walikuwa wananunua shahada Wamechoka kiasi hiki!!!!! Hivi wanaelewa kwanza nini wanafanya au ni umasikini ndiyo unawaponza!!!! Au elimu duni inawaponza , maana kama umasikini halafu wangekuwa na elimu kidogo wangegundua kuwa They NEED CHANGES kujaribu na upande wa pili wa shilingi ili waone kama kweli wataendelea kuwa masikini kiasi hicho. Maana inaonesha hata chakula mchana hawajapata si kwa kutaka bali hali ngumu.

Busanda Show the Tanzania that : - Ili kukomesha IFISADI you need CHANGES, na ni sasa.

Lazima atakuwa amekosea hasa huyo wa pili hawezi kuwa diwani labda mjumbe wa shina.
 
Nilishuhudia uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, nikiwa Moshi, Dar, Morogoro na Arusha. Makundi niliyoona yakiwa kwenye mikutano ya Augustino Lyatonga Mrema yalikuwa yanafanya kila mtu aamini kwamba Mrema angeongoza angalau kwenye hiyo mikoa.

Kilichotoka kwenye majumuisho ya kura huko kulikoitwa ndio ngome ya NCCR-Mageuzi kwa wakati huo ndio CCM na NCCR-Mageuzi waligawana kura. Lakini CCM iliendelea kuwa ndiyo yenye kura nyingi.

Sasa mimi picha huwa kawaida zinaniambia tu kwamba huenda Busanda kuna ushindani lakini haziniiambii kwamba ushindi utakuwa kwa CHADEMA moja kwa moja... mijitu ya CCM haipigi makelele bwana lakini wanajua kupiga kura...

Mnapiga mkutano wenu, makofi mengi etc. kesho yake balozi wa nyumba kumi kumi arudi anasawazisha mambo. kwa kuwa vyama vya upinzani havina viongozi huko kwenye kaya.

Yetu macho, najua kuna watu watasema mbona Tarime iliwezekana... lakini Tarime iliwezekana kwa sababu Tarime ilikuwa ngome ya CHADEMA hata kabla ya kifo cha Mh. Chache Wangwe.

Nawatakia ushabiki mwema.

Unaweza kuwa sahihi hapa lakini mara nyingi sehemu ambazo watu wanasimama imara na kulinda kura zao hali huwa hiiwi hivyo. CCM wanajua sana kuiba kura kwa hiyo huonekana wamepata kura nyingi lakini ni baada yakuiba!!! Kumbuka 1995 Dar ambako Mrema alikuwa anashabikiwa sana waliamua kuvuruga baada ya kugundua kuwa hawajapata kitu na kuiba kusingewasaidia. Hata huko Tarime kama wakina-mura wasingelinda kura zao basi ungeona ccm imeshinda kwa asilimia 0.001
 
Nilishuhudia uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, nikiwa Moshi, Dar, Morogoro na Arusha. Makundi niliyoona yakiwa kwenye mikutano ya Augustino Lyatonga Mrema yalikuwa yanafanya kila mtu aamini kwamba Mrema angeongoza angalau kwenye hiyo mikoa.

Kilichotoka kwenye majumuisho ya kura huko kulikoitwa ndio ngome ya NCCR-Mageuzi kwa wakati huo ndio CCM na NCCR-Mageuzi waligawana kura. Lakini CCM iliendelea kuwa ndiyo yenye kura nyingi.

Sasa mimi picha huwa kawaida zinaniambia tu kwamba huenda Busanda kuna ushindani lakini haziniiambii kwamba ushindi utakuwa kwa CHADEMA moja kwa moja... mijitu ya CCM haipigi makelele bwana lakini wanajua kupiga kura...

Mnapiga mkutano wenu, makofi mengi etc. kesho yake balozi wa nyumba kumi kumi arudi anasawazisha mambo. kwa kuwa vyama vya upinzani havina viongozi huko kwenye kaya.

Yetu macho, najua kuna watu watasema mbona Tarime iliwezekana... lakini Tarime iliwezekana kwa sababu Tarime ilikuwa ngome ya CHADEMA hata kabla ya kifo cha Mh. Chache Wangwe.

Nawatakia ushabiki mwema.
sema CCM wanajua kuiba kura hapo nitakuelewa. ndiyo maana sasa hivi wanajiandaa kufanya huo umafia. Lakini jamaa wamewadhibiti kikamilifu.sasa Busanda lilikuwa jimbo la CCM, lakini naamini watalipoteza kabisa hilo halina ubishi. CCM kwisha habari yao, wajue kwamba watanzania wamechoshwa na serikali ya ubabaishaji iliyojaa uswahiba huku wananchi wanakuwa kama wakimbizi kwenye nchi yao.
 
Kwani sheria zinasemaje kuhusu kuchoma nguo ya kijani au nyekundu au nyeusi? Kwani nguo ngapi zinachomwa zenye rangi ya kijani?? je wanalilia jeneza wanaogopa kufa??? Sultani siku zake zinakaribia kwisha hivyo anatafuta mzimu wa kuzikwa naye.
 
Nilishuhudia uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, nikiwa Moshi, Dar, Morogoro na Arusha. Makundi niliyoona yakiwa kwenye mikutano ya Augustino Lyatonga Mrema yalikuwa yanafanya kila mtu aamini kwamba Mrema angeongoza angalau kwenye hiyo mikoa.

Kilichotoka kwenye majumuisho ya kura huko kulikoitwa ndio ngome ya NCCR-Mageuzi kwa wakati huo ndio CCM na NCCR-Mageuzi waligawana kura. Lakini CCM iliendelea kuwa ndiyo yenye kura nyingi.

Sasa mimi picha huwa kawaida zinaniambia tu kwamba huenda Busanda kuna ushindani lakini haziniiambii kwamba ushindi utakuwa kwa CHADEMA moja kwa moja... mijitu ya CCM haipigi makelele bwana lakini wanajua kupiga kura...

Mnapiga mkutano wenu, makofi mengi etc. kesho yake balozi wa nyumba kumi kumi arudi anasawazisha mambo. kwa kuwa vyama vya upinzani havina viongozi huko kwenye kaya.

Yetu macho, najua kuna watu watasema mbona Tarime iliwezekana... lakini Tarime iliwezekana kwa sababu Tarime ilikuwa ngome ya CHADEMA hata kabla ya kifo cha Mh. Chache Wangwe.

Nawatakia ushabiki mwema.

Kasheshe,
Aliyeshinda kura za uchaguzi wa 1995 alikuwa ni Lyatonga Mrema. UWT ilibidi waingilie wasuke matokeo ili Mkapa aingie Ikulu.
 
Mpaka sasa inatia moyo hatujuwi huko usoni twendako kwani hali ikiendelea kama hivyo sidhani kama wenye dola watafurahia na hali hiyo , kuna hatari ya kumwagwa Janjawidi amabo wapo standby
 
Nilishuhudia uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, nikiwa Moshi, Dar, Morogoro na Arusha. Makundi niliyoona yakiwa kwenye mikutano ya Augustino Lyatonga Mrema yalikuwa yanafanya kila mtu aamini kwamba Mrema angeongoza angalau kwenye hiyo mikoa.

Kilichotoka kwenye majumuisho ya kura huko kulikoitwa ndio ngome ya NCCR-Mageuzi kwa wakati huo ndio CCM na NCCR-Mageuzi waligawana kura. Lakini CCM iliendelea kuwa ndiyo yenye kura nyingi.

Sasa mimi picha huwa kawaida zinaniambia tu kwamba huenda Busanda kuna ushindani lakini haziniiambii kwamba ushindi utakuwa kwa CHADEMA moja kwa moja... mijitu ya CCM haipigi makelele bwana lakini wanajua kupiga kura...

Mnapiga mkutano wenu, makofi mengi etc. kesho yake balozi wa nyumba kumi kumi arudi anasawazisha mambo. kwa kuwa vyama vya upinzani havina viongozi huko kwenye kaya.

Yetu macho, najua kuna watu watasema mbona Tarime iliwezekana... lakini Tarime iliwezekana kwa sababu Tarime ilikuwa ngome ya CHADEMA hata kabla ya kifo cha Mh. Chache Wangwe.

Nawatakia ushabiki mwema.

mkuu sema tu umekosea kidogo.. hiyo mijitu inajua kuiba kura si kupiga kura!
 
Confirmed! CCM WIZI TU HAWANA JIPYA
SOMA HII

Diwani wa CCM anaswa akidaiwa kununua shahada

Na Frederick Katulanda,Busanda

WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Busanda zikiendelea kushika kasi, hali imekuwa mbaya kwa CCM, baada ya diwani na mabalozi wake wawili kunaswa wakidaiwa kuorodhesha majina ya watu wenye shahada kwa lengo la kuzinunua.

Tukio hilo limetokea siku chache baada ya naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na msimamizi wa uchaguzi wa CUF, Maole Kuchilongulo kuituhumu CCM kuwa ilikuwa ikijiandaa kuendesha hujuma ya kununua shahada za wapiga kura kwa lengo la kupunguza kura za upinzani.

Tukio hilo lilitokea juzi katika kijiji cha Shilungule, kata ya Busanda kati ya saa 2:30 na saa 3:00 usiku baada ya mwenyekiti wa Chadema wa kata hiyo kubaini kikao cha siri cha wajumbe wa nyumba kumi kilichokuwa kikiongozwa na diwani wa kata hiyo, Alphonce Matonange (CCM).

Inadaiwa kikao hicho kilikuwa na ajenda ya kuorodhesha shahada za wapiga kura.

Kamanda wa polisi wilayani Geita (OCD), Shabani Kimei alithibitisha kukamatwa kwa watu hao na kusema jeshi lake limewakamata kutokana na malalamiko ya Chadema na kwamba wanalifanyia uchunguzi wa kina tukio hilo.

“Sisi kazi yetu ni kupokea malalamiko kama hivyo tumepokea na sasa tunafanya uchunguzi. Tumewaita watu wa Chadema wametoa maelezo na tunaendelea na uchunguzi ukikamilika tutawasiliana na msimamizi wa uchaguzi kwa ajili ya hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kuangalia sheria za uchaguzi zinasemaje juu ya hatua hiyo,” alieleza.

Akizungumzia tukio hilo, mkurugenzi wa oganaizesheni ya mafunzo wa Chadema ambaye pia ni kamanda wa kampeni za uchaguzi wa Busanda, Singo Benson Kigaila alisema mara baada ya kupata taarifa hiyo, walituma gari na kuwasiliana na polisi ambao walifika na kumtia mbaroni diwani huyo na balozi mmoja huku wengine wakikimbia.

Sambamba na mjumbe huyo kukamatwa na diwani, mjumbe mwingine wa nyumba kumi amekamatwa jana asubuhi katika Kijiji cha Musasa kilicho kata hiyo ya Busanda akidaiwa kuendesha zoezi hilo la kuorodhesha majina ya wananchi wenye shahada pamoja na namba zake.

“Baada ya kupata taarifa hiyo tulipeleka timu yetu, wakati inafika tu diwani na wajumbe wengine ambao walikuwa katika zoezi hilo walikimbia baada ya kuona mwanga wa taa za gari, mjumbe mmoja ambaye alikuwa na shahada alinaswa na baada ya kuhojiwa alikiri kuendesha zoezi hilo,” alieleza.

Alisema akihojiwa na maofisa wa polisi mbele ya viongozi wa Chadema, mjumbe huyo wa nyumba kumi alisema walikuwa wakiorodhesha shahada hizo kutokana na maelekezo ya wakubwa wake ndani ya CCM ambao waliyatoa kupitia msimamizi wa chama chao ambaye alimweleza kuwa ni mwanamke kutoka wilayani Magu mkoani Mwanza.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Diwani Alphonce Matonange wa kata ya Busanda ambaye inadaiwa baada ya kukimbia usiku huo aliwahi kupiga simu polisi akidai kulikuwa na gari la Chadema ambalo lilikuwa limeenda kijijini hapo kwa nia mbaya na kwamba lilitaka kumgonga.

Mwingine ni mjumbe wa nyumba kumi aliyefahamika kwa jina la Abdalah Ibrahimu ambaye inadaiwa alikutwa akiwa na karatasi iliyokuwa imeshaorodheshwa watu 20, ikionyesha majina na namba zao za shahada za kupigia kura.

Kigaila alisema kuwa hatua hiyo ni kosa la jinai kwa vile sheria inaeleza wazi kuwa ni kosa la jinai kuorodhesha namba ya shahada ya kupigia kura ya mtu mwingine awe mwanachama wako ama wa chama kingine na kusema hatua yao ya kwanza imekuwa ni kuwakamata na kuwakabidhi mikononi mwa polisi kuthibitisha walichokuwa wakieleza katika mikutano yao.

Alisema sasa wanasubiri kuona polisi itawafanya nini ikiwa ni pamoja na viongozi wao waliowatuma kuendesha zoezi hilo.

Wakati huo huo, wanafunzi wa shule ya sekondari ya Butundwe iliyopo katika kata ya Nyakagomba wameadhibiwa kwa viboko sita kila mmoja baada ya kuzomea msafara wa mgombea ubunge wa CCM, Lolencia Bukwimba wakati ulipokuwa ukipita eneo la shule yao kutoka kwenye kampeni.

Tukio hilo hilo limetokea Ijumaa majira ya saa 10:00 jioni wakati wanafunzi hao walipoona msafara wa mgombea huyo ukipita eneo la shule na kuzomea, kitendo ambacho kiliwaudhi baadhi ya viongozi wa CCM na kuwaagiza viongozi wa kata kufuatilia shule hiyo.

Habari toka Nyakagomba zinaeleza kuwa katika maagizo hayo katibu mwenezi wa kata hiyo, Oscar Magori, ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Msingi Nyakagomba, ndiye aliyekwenda kulalamika kwa mwalimu mmoja wa zamu ambaye aliamua kuwaadhibu wanafunzi wote wa kidato cha kwanza lakini baadhi ya wanafunzi waligoma na hivyo kuwaadhibu sita tu.

Mkuu wa shule hiyo Monika Mzungu alisema wanafunzi hao wameadhibiwa na mwalimu huyo kwa sababu binafsi na kwamba yeye kama mkuu wa shule hiyo hakutoa amri hiyo ya kuwachapa viboko wanafunzi.

“Mimi sikuagiza watoto hao waadhibiwe. Nilishauri wasijiingize katika siasa na waepuke kushabikia vyama bali wajitahidi katika masomo. Kama kuna mwalimu amewaadhibu amewaadhibu yeye kama yeye na sina habari na hilo,” alieleza mkuu huyo. 

Back
Top Bottom