Uchafu uliokithiri Chefs Pride na K-Tea Shop

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,545
833
Hivi owners wa hii migahawa wamelewa wateja au kitu gani?

au ndio washawaweka watu wa Afya wa JIJI kwenye payroll?
 
yote mawili yanawezekana!! afu hao the so called maafisa wa afya ni wapuuzi sana, hawafanya kazi yao vizuri pesa mbele na wanawaonea wengine amabo hawana makosa ya kutozwa faini!!! (lakini ndo style yetu anyway, ona tfda na tbs)
 
Hapo mahali watu wastaarabu waliacha kwenda siku nyingi.
Kwa hela ya mlo mmoja unawezan kuondoka na tatizo kubwa la afya!!
 
Mara nyingi sana tunajisahau kumaintain na naona yamewakuta hawa wenzetu!!! kulewa misifa...
 
yote mawili yanawezekana!! afu hao the so called maafisa wa afya ni wapuuzi sana, hawafanya kazi yao vizuri pesa mbele na wanawaonea wengine amabo hawana makosa ya kutozwa faini!!! (lakini ndo style yetu anyway, ona tfda na tbs)
Na mifumo yetu ina matatizo, mtu kama bwana afya kama tunavyomuita pesa anazolipwa kama mshahara wake vina dhalilisha hata hiyo taaluma yenyewe ya afya. Matokeo ya hiyo pesa mbuzi anayolipwa kazini ndiyo inayo mfanya akubali kirahisi kuingizwa kwenye payroll isiyo rasmi na matokeo yake madhara yanarudi kwa wateja.

Mfumo huu wa kutojali wataalamu mbalimbali tulionao ni sehemu kubwa ya matatizo tuliyo nayo kama nchi, na hii ndiyo imefanya wataalamu wote kukimbilia kwenye siasa na kuacha field zao zikiwa na watu wasiostahili.

Mungu ibariki TZ.
 
jamani jamani jamani chefs pride sio mahali pa kwenda kula,kuna siku nimetoka na familia yangu tumeenda pale kupata lunch kwenye mchuzi nilikuta mende mkubwa ameiva na kuiva.kwa hasira hatukulipa chakula na ndo mwisho wa mimi kukanyaga pale.
 
lol! kuna siku nilikuwa napata msosi flamingo restaurant pale jnia, mende akawa anapanda ukuta pembeni yangu. nikamuita mhindi,nikamuambia thanks for this bonus! lilimshuka shuuu! namuonesha jinsi chini ya meza (kitako cha round) kulivyogina uchafu, na waitresses wakitoa uchafu mezani wanaweka kwenye ornamental plants! bongo ndo tunapata immunity kwa huu uchafu aisee!
 
<br />
<br />
Yaani...heri tule chipsi vumbi kwa Edo tujue moja...
 
Maafisa wa Afya wangekuwa wanafanya kazi zao ipasavyo, mji mzima wa Dar ungefungiwa na si hizo restaurants pekee.
 
Chef's pride hii hii ninayo ijuwa mimi, dah! Itabidi niwasiliane na Salim... Kulikoni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom