KERO Responded BRELA na Mfumo wa Beneficial Ownership kutokutoa Control Numbers

KERO Responded BRELA na Mfumo wa Beneficial Ownership kutokutoa Control Numbers

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,351
Reaction score
4,616
Habari za wakti huu ndugu zangu wa BRELA

Kwanza kabisa niwaulize hivi Call centre yenu iko Busy sana au wafanyakazi wachache au vyote kwa pamoja maana kasi yenu ya kupokea simu na kushughulikia masuala yanayoletwa kwenu haundani na zama hizi.

Litazameni hilo maana haiwezekani nipige simu Call centre siku nzima nisipate line.Its either huduma zenu ni Mbovu kiasi kwamba kila mtu analalamika na hapo inabidi mtafute namna ya kuongeza channels za mawasiliano

Sasa kuna swala la hii kitu mnaita Beneficial Owner? Hii ni kitu gani mbaona kama ni namna za kuongeza tu Gharama za kufanya Biashara maana nimeingia kwenye mfumo wenu wa BO nashangaa naletewa Bili kubwa mpaka najiuliza hawa jamaa kwani hii issue ya Benficial

Mwisho kwenye huo mfumo wa benficial owner ile hatua ya kutoa control number haifanya kazi sasa sijajua kama ni BY design au mfumo wenu una shida?

Maoni yangu.Hiyo BO ama muifanye iwe sehemu ya USAJILI kwa maana ya kwamba mteja awe na uwezo wa kuweka benficial owners wakati anafanya usajili ili uondoe utaratibu wa kuwa na mifumo mingi bila sababu.

Litazameni hilo la Control number haya mengine muyafanyie kazi kwa kadiri ya uwezo wenu.

Soma pia: KERO - Mfumo mpya wa BRELA BOS una changamoto.




========================​
Majibu ya BRELA

 
Habari, pole kwa changamoto uliyokutana nayo, watoa huduma wetu walikua wanahudumia wateja wengine, Mmiliki manufaa (beneficial owner) ni mtu ambaye anamiliki moja kwa moja au kupitia mtu mwingine asilimia 5% au zaidi ya uwekezaji au ufanyaji maamuzi kwenye kampuni.

Tunaomba tutumie namba ya ombi lako pamoja na namba ya usajili wa kampuni yako kupitia DM kwa ajili ya msaada zaidi.
 
BRELA, hakuna haja ya Brela kuwa mfumo pekee ya Business formation, inabidi Serikali iruhusu vijana waunde mifumo ambayo itaruhusu watu kuunda na kufungua kampuni.

Brela iwe ni repository/directory ambayo watu wanapublish biashara ngapi wameanzisha
 
MlimaSayuni,

Habari, tunaomba kufahamu changamoto uliyokutana nayo katika mfumo wetu kwa ajili ya msaada zaidi.
 
Habari, tunaomba kufahamu changamoto uliyokutana nayo katika mfumo wetu kwa ajili ya msaada zaidi.
Sitaki masada wenu natoa ushauri.

Njia ya kwanza ya kufanya biashara Nchi yoyote Duniani ni company/business formation.

Ili kuwe na ushindani na Urahisi inabidi third parties siruhusiwe kuwa na portals watu wawe wanatumia hizo badala ya kulazimika kutumia BRELA peke yake.

Mataifa kama Uingereza, USA, Hongkong, Indonesia yameweza
 
Sitaki masada wenu natoa ushauri.

Njia ya kwanza ya kufanya biashara Nchi yoyote Duniani ni company/business formation.

Ili kuwe na ushindani na Urahisi inabidi third parties siruhusiwe kuwa na portals watu wawe wanatumia hizo badala ya kulazimika kutumia BRELA peke yake.

Mataifa kama Uingereza, USA, Hongkong, Indonesia yameweza
Tunaomba kufahamu umekutana na changamoto gani kwa ajili ya maelezo zaidi.
 
Inachukua siku ngapi, kupata majibu ya BO ?
 
Back
Top Bottom